Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 31, 2012

WAFIWA WALIOKUWA WAKISAFIRISHA MAITI YA MKE WA DKT AHMED LUGELO NUSURU WATEKWE MLIMA KITONGA


Marehemu Joyline Ahmed Lugelo enzi za uhai wake
Mazishi yakiendelea leo
Wananchi wa kijiji cha Kibao wakienda kushiriki mazishi leo,maduka yote yalifungwa katika kijiji hicho cha Kibao
Dkt Ahmed Lugelo akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake mpendwa Joyline Lugelo
Wadau wakiwa wamebeba jeneza la Joyline A.Lugalo leo
Tutakukumbuka dada yetu mpendwa wetu daima
Dkt Ahmed Lugelo akiwa katika majonzi
Baba mzazi wa Dkt Ahmed Lulego na mkewe wakiweka shada maua
Mliki wa mtandao huu Bw.Francis Godwin (kushoto) akiwa na Dkt Ahmed Lugelo ambayo rafiki yake mkubwa toka wakiwa shule ya Kibao Bw.Baraka Mikodela ambao wote ni marafiki toka shule wakiwa katika kaburi la mke wa Dkt Lugelo aliyezikwa leo kijiji cha Kibao Mufindi
Carlolina Sanga na Neema Sanga ambao pia ni rafiki marafiki wa mmiliki wa mtandao huu kutoka shule enzi hizo
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wametenga magogo katika mlima wa kitonga wilaya ya Kilolo katika barabara ya Iringa -Dar es Salaam na kutaka kuwateka wafiwa waliokuwa wakisafirisha mwili wa marehemu Joyline Ahmed Lugelo kutoka jijini Dar es Salaam kwenda kijiji cha Kibao wilaya ya Mufindi kwa mazishi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika milima hiyo ya Kitonga wakati wafiwa hao wakitoka jijini Dar es Salaam kwenda wilayani Mufindi .


Wakizungumzia tukio hilo wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Kibao Mufindi leo waombolezaji hao walisema kuwa watu hao walitega magogo katika mlima huo kwa lengo la kuwateka na kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 za usiku.

Hata hivyo walisema kuwa pona yao ilitokana na maombi pamoja na magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo na kupelekea watekaji hao kutoweka porini.

BREAKING NEWS ....KIWILA KWACHAFUKA MABOMU YATUMIKA KUTAWANYA WANA CCM NA CHADEMA

Taarifa kutoka Kata ya Kiwila mkoani Mbeya ambako kuna kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani zinadai kuwa hari si shwari baada ya kikosi cha kutuliza ghasi ( FFU) kutumia mabomu ya machozi kwa zaidi ya masa a Mawili sasa kutawanya wafuasi wa CCM na Chadema baada ya viongozi wa Chadema kuwazingira katika kikao chao cha faraga wafuasi wa CCM zaidi ya 50 kwa Madai kuwa wanapokea Rushwa.

Kutokana na Hali hiyo FFU wsmeingia kazini na kuwatawanya wafuasi hao wa CHADEMA ambao walionekana kuwashikilia wan a CCM hao ambao walikuwa katika mwandamizi ya kuhitimisha kampeni zao kwa mjumbe wa NEC Anne Malicela kufunga kampeni hizo.

Habari kamili yaja japo kwa sasa naweza kusema habari ndogo hiyo.

March 30, 2012

UCHIMBAJI HUU WA KOKOTO UNACHANGIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA IRINGA

Wanawake wakazi wa Njiapanda ya Mlolo katika Manispaa ya Iringa wakigonga kokoto kwa ajili ya kuuza japo katika eneo hilo kuna uharibifu mkubwa wa mazingira
Hivi ndivyo mazingira yanavyoharibiwa katika eneo hilo na hakuna mpango wowote wa serikali ya manispaa ya Iringa kuthibiti hali hiyo

NEVELEN MEENA AULA USIKU WA TUZO KWA WANAHABARI BORA TANZANIA -LIVE TBC 1

Rais Dk. Jakaya Rais wa T-anzania Jakaya Kikwete akiwa amewasili ukumbini tayari kwa kukabidhi tuzo hizo za waandishi Ijumaa usiku hapa katika picha akionekana kufuatilia ngoma ya asili kutoka kundi la Simba Theatre la jijini Dar es salaam. kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Chande Omar na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga nao wakifuatilia burudani hiyo.

Leo ndiyo leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kunafanyika hafla kubwa ya utoaji wa tuzo ya Umahili wa uandishi wa habari kwa mwaka wa 2012 zinazoandaliwa na Baraza la Habari MCT na washirika wake ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete.


Wamejitokeza wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wasomi na waandishi wa habari wakongwe kama picha ya kwanza inavyoonekana kutoka kulia ni Profesa Aisha Yahya Othman mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Jenrrali Ulimwengu, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliyesimama na Profesa Shivji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika hafla hiyo usiku huu.
Hawa ni miongoni mwa majaji kulia ni Itillio Tagalile, Afisa Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud na Wenceslaus Mushi wakijadili jambo.
Kushoto ni Awaichi Mawala kutoka Zantel na Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala
Wageni waalikwa kutoka mashirika mbalimbali nao wamehudhuria katika hafla hiyo.
Majaji wakiwa katika meza yao.
Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA Modestus Lilungulu kushoto na mjiumbe wa bodi Dk.Marcelina Chijoriga kulia wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga.
Mhariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo Jaquiline Liana akizungumza na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo Juma Pinto kulia.
Clement Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji TBC akizungumza na Profesa Helmasi Mwansoko Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wadau kutoka Shelutete kutoka TANAPA na Geofrey Tengeneza kutoka TTB nao wapo katika hafla hiyo.

Wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nao wamejongea katika hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Mbunge wa Kondoa Kusini akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws
Bendi ya Msondo ikitumnuiza katika hafla hiyo.
Mzee wa Kammbi popote Antonio Lugas akiwa na mdau Abel Onesmo kutoka Clouds FM(picha zote na FullShangwe )


Katibu wa jukwaa la wahariri Tanzania Nevelin Meena aula tuzo ya habari za utawala bora ,gazeti la Uhuru latoa mpiga picha bora , majira mchora katuni bora , ITV yachukua tuzo ya habari utawala bora upande wa radio Noel Thomson aula, wateule wa magazeti habari za Maralia ni gazeti la Rai ,upande wa radio katika Maralia ni TBC ,upande wa magazeti ni IMani Imani .

Tuzo za michezo ni radio ni Abdala Machura kwa upande wa TV KIbanda amtabiria Bw.Annual Mkama afuta matokeo

Upande wa magazeti ni David Azaria wa gazeti la Habari leo kaibuka Mshindi wa habari za walemavu upande wa TV ni Lekoko Livilala upande wa Radio ni walioshindana ni Mliamani Radio na TBC one Tuma Dandi aibuka kidedea kutetea walemavu wenzake ,Nasra Abdala Kutoka gazeti la Tanzania Daima kashinda tuzo ya habari ya jinsia

Tuzo habari ZA UKIMWI katika magazeti imechuliwa na Elias Msuya kutoka gazeti la Mwananchi ,katika radio ni Betrice Nangawe kutoka radio Sun ,upande wa tuzo ya afya upande wa magazeti tuzo imekwenda kwa Sharifa Kalokola kwa upande wa radio ni Secelia Ndamakigezi ,tuzo ya mazingira kwa upande wa magazeti imechukuliwa na Lukas Liganga tuzo ya habari uchumi na biashara imekwenda kwa Bw Mashira upande wa TV ni zawadi imekwenda TBC kwa kuchukuliwa na Aneth Andwer .

Tuzo ya habari za Elimu kwa magazeti kwa Erick Kabembera upande wa TV imekwenda kwa TBC Dodoma kwa Bi. Victoria Patrick kwa upande wa radio tuzo imekwenda kwa Grece Kihondo ,tuzo ya habari wa watoto katika magazeti imekwenda kwa Nashon Kenedy ,upande wa TV ni Anganile Mwakanjala wa TBC amekuwa pekee.
Upande wa Radio tuzo ya watoto imekwenda kwa Sempaka Mchome

Tuzo ya hifadhi ZA Taifa katika magazeti imekwenda kwa Paul Jems kwa upande wa Radio imekwenda kwa TBC Taifa kwa Alex Magwesa ,huku tuzo ya utalii wa ndani upande wa magazeti imekwenda kwa Monica LUhondo awapiku Kalulunga na Midelo ,upande wa TV ni Juma Lugasi upande wa radio hakuna mshindi.

Tuzo ya maafa na migogoro katika magazeti ni Daniel Mbega ,katika TV ni Joseph Bula ambaye habari zake mbili zote ziliingia katika shindano hilo tuzo ya sayansi na Teknolojia imekwenda kwa Benard Lugongo kwa upande wa gazeti na radio ni Abel Mwende wa Claus Fm akosa mpinzani na kwa magazeti ni Nevelin Meena kwa TV hakuna Mshindi .

Tuzo ya habari zanye mvuto kwa watu upande wa magazeti ni P. Machira kwa upande wa habari za michezo na burudani upande wa TV ni Anual Mkama wa Mlimani TV akosa mpinzani ,

Kwa upande wa washindi wa jumla tuzo imechukuliwa na Nevelin Meena wa Mwananchi akabidhiwa tuzo na Rais Jakaya Kikwete aibuka na kitita cha kufa mtu dola kasha za kujiendeleza Masomo zatolewa kwake .wakati tuzo ya maisha ya mafanikio katika maisha katika tasinia ya habari imechukuliwa na Philip Karashan aliyejipatia shilingi milioni 10

TANZIA ,MDAU AHMED LUGELO AFIWA NA MKEWEBwana Ahmed Lugelo akiwa na mkewe Joyline Assenga ambaye amefariki dunia juzi na anataraji kuzikwa kesho katika kijiji cha Kibao wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na mtandao huu utakuwezesha kupata matukio ya mazishi hayo .

Ahmed Lugelo nimepata kusoma naye na mbali ya kusoma naye pia ni jirani yangu mkubwa na wazazi wake ni walimu ambao wamepata kunifundisha .

Harusi ya Ahmed na Joyline alifanyika Septemba 12 mwaka 2010 na harusi hiyo kufanyika katika ukumbi wa RC KibaoLOWASSA AIVURUGA CHADEMA ARUMERU ,APOKELEWA KAMA SHUJAA AMNADI KWA KISHINDO MGOMBEA WA CCM

Mh.Edward Lowasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukam mara baada ya kutua jimbo la Arumeru kumnadi mgombea wa CCM
Mhe.Lowassa akipokelewa kama shujaa jimboni Arumeru leo
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe,Benjamin Wiliam Mkapa akionyesha dole kuashiria ushindi mtupu kwa CCM jimbo la Arumeru
Mapokezi makubwa ya Mhe,Lowassa leo jimboni Arumeru haijapata kutokea
Mh. Lowasa akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashari,Sioi Sumari.

Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki wa Tiketi ya CCM,Sioi Sumari akiingia viwanja vya mkutano leo
Wasanii marufu wa mziki wa kizazi kipya nao walipagawisha
Morani wa Kimasai nao walikuwepo kupamba mapokezi ya Lowassa na kampeni za CCM
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowasa akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Mashariki leo kwenye viwanja vya Kikatiti,Wilayani Arumeru.(picha na na habari na Othman Michuzi Jr )

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli mh Edward Lowasa amewaasa wananchi wa arumeru mashariki kutofanya makosa ya kujaribu sumu kwa kutoichagua ccm.

Akizungumza katika mkutano wa kampnei kumnadi mgombea wa ccm jimbola arumeru mashariki Sioi Sumari leokatika eneo la kikatiti, Mh Lowassa amesema kwa kuichagua ccm wananchi wa arumeru wataondokana na vureugu na fujio ambazo hivi sasa jimbo la arusha mjini limeshuhudia kila uchao.

''Nawaomba wananchi wa arumeru, msijaaribu kuinywa sumu, sumu haijaribiwi..hivi tujiulize Chadema wameshinda Moshi, Hai, Karatu, lakini kote huko hatujasikia fujo maandamano na vurugu kama tunazoziona Arusha''alitahadharisha Lowassa huku akishangiliwa na kuongeza kuwa ni CCM pekee ndicho chama chenye sera za amani.

Aidha Mh Lowassa amewaomba wananchi wa Arumeru kuingia nao mkataba wa kutatua matatizo yao kwa kumchagua mgombea wa huyo wa CCM.''Ndugu zangu napenda kuwaambia kwamba kwa kuichagua ccm tutafunga ajenda za matatizo ya umeme, ardhi na maji..Mimi nikiwa kwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Arusha nitahakikisha kuwa matatizo haya yanatatuliwa haraka''alisema.

''Mimi si mtu wa kupiga porojo, mimi ni mtu wa vitendo.kwahiyo tarehe 10 April mkichagua Sioi ataapa na saa 7.30 mimi na wabunge wenzangu wa Arusha tutamwita waziri wa ardhi mama Tibaijuka kumuelezea tatizo la ardhi hapa arumeru mashariki''alisema Lowassa ambaye amebatizwa jina na washabiki wake la mzee wa maamuzi magumu.

Huku akichombeza na maneno ya ''hapo vipi'' na kuitijkiwa ''hapo sawa'' Mh Lowassa alisema kuwa Sioi Sumaru ana uwezo wa kushughulikia na kutatua kero za arumeru mashariki.Amesema kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo katika jimbo hilo la arumeru mashahriki, kumeisadia serikali na ccm kwa ujumla kubaini kero zilizoko katika jimbo hilo.

Kwa upande wake Sioi alisema akipewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, atamshika shati Mh Lowassa pamoja na wabunge wengine kutatua kero za jimbo hilo.

VITUO VYA MAFUTA VYAFUNGWA IRINGA KWA KUKOSA MAFUTA -LIVE

Kituo pekee cha Iringa Servece stition ambacho kilikuwa kikiuza mafuta leo
foleni ya mafuta usiku huu mjini Iringa
Kituo cha Gapco kikiwa kimefungwa
Kituo cha Eso nacho kikiwa kimefungwa
Hali ya upatikanaji wa mafuta aina ya Petrol na Dizel katika mji wa Iringa imekuwa ya utata zaidi baada ya vituo vyote kufungwa kwa kukosa nishati hiyo na kupelekea baadhi ya magari kuegeshwa kwa kukosa mafuta.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya madereva wamesema kuwa hali ya upatikanaji wa mafuta hayo imeanza kuwa ngumu kati ya mida ya saa 12 za jioni baada ya vituo zaidi ya vinne katika mji wa Iringa kufungwa kwa mpigo na kuacha kituo kimoja pekee cha Iringa Service Station ambacho kilikuwa kikiuza nishati hiyo na kufanya foleni katika kituo hicho kuwa kubwa zaidi na polisi wa kikosi cha usalama barabarani kufika kusaidia kuongoza magari eneo hilo.

Hata hivyo wamedai kuwa yawezekana uhaba huo wa mafuta ni njama za wafanyabiashara wa vituo hivyo vya mafuta mjini Iringa ili kutaka kupandisha bei ya mafuta ama wamesikia serikali kupitia EWURA inataka kushusha bei ya mafuta hayo.

Kwa upande wake wafanyabiashara wa mafuta mjini Iringa wamesema kuwa kufungwa kwa vituo hivyo ni kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo katika vituo vyao na kuwa yawezekana usiku wa leo magari ya mafuta kushusha mafuta katika vituo hivyo.