Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 29, 2012

BAADA YA UONGOZI WA MKOA KUWANYANYASA ,WANAHABARI IRINGA WASUSA KURIPOTI HABARI ZA ZIARA YA MAKAMU WA RAIS DK BILAL

Wanahabari mkoani Iringa wameeleza kusikitishwa na unyanyasaji mkubwa uliofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kushindwa kuwapatia malazi wakati wa ziara ya makamu wa Rais Dr Mohamed G. Bilal na kutokana na unyanyasaji huo wanahabari hao wamefanya mgomo baridi na kukusudia kukutana siku ya jumamosi kwa ajili ya kuitisha maandamano makubwa ya kupinga hatua ya mkoa kutovidhamini vyombo vya habari.

Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard amesema kuwa kutokana na hali iliyojitokeza katika ziara hiyo kwa wanahabari kuteseka kwa kukosa sehemu za kulala kwa kipindi chote cha siku mbili ambacho walikuwa katika ziara hiyo katika wilaya za Makete ,Njombe na Mufindi .


Mtandao huu umeshuhudia wanahabrai hao wakiwa katika mgomo baridi na wakati wote makamu wa Rais akiwa anahotubia wananchi AMA Kutembelea miradi hakuna mwanahabari ambaye alikuwa akijihusisha kupiga picha AMA kuchukua taarifa hizo zaidi ya kujikusanya makundi na kuendelea na kupiga stori binafsi.

February 28, 2012

SHULE YA MSINGI MUUNGANO MJINI IRINGA YAFUKUZWA WANAFUNZI WASIOTOA MICHANGO

Wanafunzi wa shule ya msingi Muungano mjini Iringa wakizunguka mitaani baada ya kufukuzwa na walimu wao leo asubuhi kwa kukosa michango ya mitihani ya majiribio kwa kila mmoja shilingi 3,000
Wanafunzi hawa wakiwa wamejipumzisha katika moja kati ya mtaa baada ya wazazi wao kushindwa kuwapa mchango huo wa mtihani wa majaribio wa kila mwezi kwa darasa la nne katika shule hiyo
Wanafunzi wa shule ya Msingi Muugano mjini Iringa wakirudi nyumbani leo asubuhi baada ya kufukuzwa na uongozi wa shule hiyo kwa kushindwa kulipa mchango wa mitahani wa majaribio wa kila mwezi kwa wanafunzi hao wa darasa la nne.

SIRI YA SPIKA MAKINDA KUKWEPA KUGOMBEA UBUNGE YAANIKWA

Spika Anne Makinda
ZIKIWA zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Njombe kusini Anne Makinda ambaye ni spika wa bunge kutangaza kutogombea ubunge tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015,mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com waibuka na siri nzito za mbunge huyo kuiogopa nafasi hiyo tena.

Baadhi ya wana CCM na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) wameanika siri hiyo ya Makinda kutangazwa kuto gombea kuwa ni kutokana na kuogopa kuja kung'olewa kwa aibu katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake mdogo wa kuwatumikia wapiga kura wake .

Huku wana chama wa CCM wa jimbo la Njombe kusini wakidai kuwa Makinda walianza kumchoka kutokana na kushindwa kufanya mambo ya kimaendeleo katika jimbo hilo na hivyo kusababisha jimbo hilo kuwa ngome ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Kwani wamedai kuwa pamoja na jimbo hilo kuongozwa na mbunge Makinda ambaye pia ni spika wa bunge ila kasi ya maendeleo katika jimbo hilo haipo na kama jimbo halina mbunge kutokana na mbunge wao huyo kuonekana kuegemea mambo ya kitaifa zaidi huku jimboni kwake mambo yanakwenda kombo .

"Hatukutegemea jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Deo Filikunjombe ni kijana mchanga katika siasa kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo kwa kipindi kifupi toka alipoingia madarakani uchaguzi wa mwaka 2010 .....huku mbunge wetu spika Makinda akishindwa hata kutengeneza barabara za jimboni kwake na kuwa barabara mbovu kuliko hata za wilaya ya Ludewa na zile za wilaya ya Makete" alisema John Sanga mkazi wa Njombe mjini

Alisema kuwa zamani jimbo la hilo la Njombe kusini bendera za vyama vya upinzani zilikuwa za kutafuta ila ukipita leo katika jimbo hilo la Makinda utitiri wa benderea za Chadema vijijini na mjini unaweza kufikiri ni ngome ya Chadema.

Sanga alisema kuwa hatua ya mbunge wao huyo kuwa mbunge wa kwanza wa CCM kutangaza kutogombea ni baada ya kuona hali ya upepo wa kisiasa kwake kuwa mbaya zaidi na hata akiwa katika ziara zake jimboni wananchi wamekuwa hawamkubali kivile.

Hata hivyo alisema jimbo la Njombe kusini ambalo mbunge wake Makinda limeendelea kuwa nyuma kimaendeleo na kupitwa na jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Fikunjombe ameendelea kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo ukilinganisha na mbunge wao Makinda ambaye amekuwa ni mtalii katika jimbo hilo .

"Tunamshangaa sana mbunge wetu Makinda kwa uamuzi wake wa kutangaza kutogombea .... kiukweli hata asingetangaza msimamo wetu wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini japo hatukuweka wazi ila ilikuwa ni kumpiga chini katika kura za maoni sisi kwa sasa mbunge wetu ni kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe Deo Mwanyika ambaye amekuwa akiendelea kuhamasisha maendeleo jimboni "

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchugaji Msigwa alisema kuwa Makinda ni sawa na mfa maji ambaye kimsingi haishi kutapa tapa kwani kauli yake ya kuwa wabunge nusu walitaka kujiuzulu kwa sakata la posho ni uongo mtupu na kuwa yeye ametumia kisingizio cha posho kuweza kueleza nia yake ya kutogombea ubunge ila ukweli Makinda amebanwa sana na Chadema katika jimbo lake.

Mbunge Msigwa alisema moja kati ya mikakati ya Chadema ni kuhakikisha inachukua majimbo mengi zaidi katika mkoa wa Iringa na moja kati ya majimbo ambayo ni rahisi zaidi kwa Chadema kushinda ni pamoja na jimbo hilo la Makinda ambalo wapiga kura wa jimbo hilo hawataki kabisa kusikia Makinda wala CCM.

"Makinda asijitetee kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kupisha wanachama wengine kuongoza ama kwa ajili ya posho ya wabunge ....anapaswa kusema wazi kuwa jimbo hilo limemshinda kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wapiga kura wake"

UREMBO IRINGA NI KWA MAMA WEEK-END SHOP PEKEE


Tembelea Mama Week-End Urembo Shop Iringa leo ujipatia urembo kwa ofa maalum ya Pasaka
Usisumbuke kuuliza ama kutafuta duka la urembo ndani ya mji wa Iringa fika leo Mama Week-End Urembo Shop lipo eneo la Miyombini jirani na Famari Store karibu kabisa na Zebra ya Msitiki wa Ijumaa
Pete na mapambo ya kila aina ndani ya Mama Week - End urembo shop
Cheni za aina mbali mbali kwa wanawake na wanaume zipo
Ama kweli mama Week- End Urembo Shop ni jibu kwa swali lake kwako unayependa kupendezaUsisumbuke kutafuta ama kuuliza duka la urembo wa ukweli uwapo mjini Iringa uliza mama week-End Urembo Shop ni jibu la swali lako ,tupo jirani na Famari Store mkono wa kushoto barabara kuu ya Uhuru kabla ya kufika Zebra ya Msikiti wa Ijumaa kama watokea Stendi kuu na kama watokea Mshindo ni baada ya kuvuka Zebra ya mtikiti wa Ijumaa ng'ambo ya pili yaani mkono wa kulia utaona bango letu hapa juu .

Tupigie simu 0715 961433 Tutakusikia tutakufikia
GLORY LODGE IRINGA NI SEHEMU TULIVU PA KUJIPUMZISHA
Muonekano wa nje kabla ya kuingia ndani ya Lodge na eneo kubwa la parking ya magari na ulinzi thabiti.
Huduma safi ya maliwato/choo
Huduma bora ya malazi
Muonekano wa Glory Lodge kwa nje


Mandhari safi uingiapo mapokezi

HUDUMA ZINAZOTOLEWA:
Malazi,Chakula,Vinyaji,Breakfast bure
Vyumba:
Self Contain,Flat Screen zenye DSTV vyumba vyote,Simu kila chumba,heater vyumba vyote vitanda vikubwa na vyenye ubora
Bei ya chumba:30000
CONTACTS
0762967626/0717706441
Huduma za semina/works shops pia zipo

Glory Lodge Ipo Kihesa jinani na uwanja wa mpira wa shule ya msingi Kihesa


GLORY LODGE
The best lodge in town

February 27, 2012

HUU NI UNYANYASAJI WA KIJINSIA ,MFANYABIASHARA AMPACHIKA MIMBA BINTI AMTELEKEZA NA MTOTO

Binti Mary Protas (22) mkazi wa mtaa wa Kagera wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwa na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi miwili na nusu baada ya binti huyo na mwanae kutelelezwa na mfanyabiashara wa kukodisha mikanda mjini Iringa
Hapa akiwa amekaa katika bustani ya manispaa ya Iringa akisubiri kusaidiwa baada ya maisha yake na mtoto kuwa machungu zaidi
Msamaria mwema Victor Kayombo waziri wa burudani katika chuo cha Ruco Iringa akiwa na binti huyo

Binti Mary Protas (22) mkazi wa mtaa wa Kagera wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam amejikuta akiishi maisha ya kuomba omba katika manispaa ya Iringa baada ya kudaiwa kutelekezwa na mzazi mwenzeke ambae ni mfanyabiashara wa kukodisha mikanda katika manispaa ya Iringa.

Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com binti huyo alisema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na mfanyabiashara huyo wa kukodisha mikanda jijini Dar es salaam wakati yeye akiwa katika kazi ya kuuza chakula katika moja kati ya Hoteli jijini D,Salaam.

Alisema kuwa makubaliano yao yalikuwa ni kuja kuishi kama mke na mume na hivyo kutokana na ahadi hiyo ya kuja kuoana walikubaliana kuzaa mtoto ila baada ya kufanikiwa kumjaza mimba kijana huyo mfanyabiashara alikata mawaliliano hadi alipoamua kumfuata mjini Iringa.

Hata hivyo baada ya kufika mjini Iringa alifukuzwa na mfanyabiashara huyo akihofu mke wake wa ndoa kuja kumfumania .

Alisema kuwa siku alipofika kwa mara ya kwanza mjini Iringa baada ya kufukuzwa kwao D,Salaam na familia yake hadi atakapomfuata aliyempa mimba huyo kijana huyo aligeuka mbongo na kumfukuza nyumbani na hivyo kuhifadhiwa na waziri huyo wa burudani chuo cha Ruco .

Hivyo alisema kuwa hadi sasa suala hilo limefikishwa polisi Iringa pamoja na ustawi wa jamii na kusubiri kijana huyo kuitwa.

kwa sasa ameomba wasamaria wema kumsaidia kupata mtaji na sehemu ya kuishi kwa muda wote atakaokuwepo mjini Iringa ,waweza kuwasiliana na binti huyo kwa ushauri na msaada kwa namba 0755 885218 ama waweza kuwasiliana na mkurugenzi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa namba 0754 026299/0712 750199

DIWANI WA CCM IRINGA NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Diwani wa kata ya Maboga CCM Flugence Lutego (kulia ) akiwa na mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya kijana Denis Kiluka ,kushoto ni mtuhumiwa namba moja Benison Mdongwe
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya kijana Denis Kiluka akiwemo diwani wa kata ya Maboga Flugence Lutego (CCM) wakiingizwa mahakamani leo
Watuhumiwa watatu wa mauaji ya kijana Kiluka wakiwa na watuhumiwa wengine wakifikishwa mahakamani leo na askari polisi
Diwani wa kata ya Mabonga Flugence Lutego (CCM) akiwa amejifichwa kukwepa kamera za waandishi wa habari leo baada ya kusomewa shitaka la mauaji na kunyimwa dhamana
Mtuhumiwa namba tatu katika kesi hiyo ya mauaji Joel Kihwele akitoka mahabusu ya mahakama kwenda kupanda gari la mahabusu
Watuhumiwa wa mauaji wakifikishwa mahakamani leo
Diwani Lutego(kulia) na mtuhumiwa namba tatu wakipanda karandinga la polisi tayari kwa kwenda mahabusu mtuhumiwa namba moja wa kesi ya mauaji Bw.Benison Mdongwe akitoka mahabusu kwenda kupanda karandinga la polisi

DIWANI wa kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini Flugence Lutego (41) na wananchi wake wawili wapandishwa kizimbani leo kwa tuhuma za mauaji ya mwendesha piki piki Denis Kiluka mkazi wa Isoka kata ya Mwangata katika manispaa ya Iringa .

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakamani ya wilaya ya Iringa Mary Senapee leo majira ya saa 5.20 leo asubuhi na kusomewa shitaka hilo la mauwaji hukuwa wakitakiwa wasijibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya mauwaji.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu Senapee wakili wa serikali Lilian Ngilangwa alisema kuwa mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo ya mauaji kesi namba 8 ya mwaka 2012 ni Benisony Mdongwe (30) ,Flugence Lutego (41) na Joel KIhwele (39) ambaye ni mtuhumiwa namba tatu katika kesi hiyo.

Alisema kuwa watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Makombwe kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini na ni wakulima wa kijiji hicho ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kumuua kijana Denis Kiluka siku ya Februari 12 mwaka huu katika kijiji hicho cha Makombwe Iringa vijijini.

Wakili huyo wa serikali Ngilangwa alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo la mauwaji na hivyo kwa pamoja wanashitakiwa kwa kesi ya mauaji namba 8 ya mwaka 2012 kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo baada ya kusomwa kwa shitaka hilo hakimu Senapee alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu namba 148 cha sheria kesi hiyo haina dhamana kwa watuhumiwa na hivyo watuhumiwa wote watatu mbali ya kutotakiwa kujibu chochote kutokana na mahakamani hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo watakwenda mahabusu hadi kesi hiyo itakapotajwa tena machi 13 mwaka huu.

DIWANI WA CCM ANAYETUHUMIWA KWA MAUAJI APANDISHWA KIZIMBANI ATUPWA MAHABUSU

Watuhumiwa watatu wa mauaji ya kijana Denisi Kiluka mkazi wa Isoka kata ya Mwangata mjini Iringa akiwemo diwani wa CCM kata ya Maboga Flugence Lutego wamepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauwaji hayo.


Waliopandishwa Kizimbani ni mtuhumiwa namba moja Bensony Mdongwe (30) diwani Flugence Lutego (41) na Joel Kihwelo (39) wote watatu wanatuhumiwa kumuua kijana mwendesha Piki piki Denis Kiluka na hawakutakiwa mujibu chochote kutokana na mahatma hiyo ya wilaya kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa wote wanadaiwa kufanya mauaji hayo ya kinyama katika kijiji cha Makombwe kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.

Hivyo imesogwezwa hadi machi 13 mwaka huu itakapotajwa kwa Mara ya pili mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mary Senapee

Picha zinakuja hivi punde

' LIVE' DIWANI WA CCM ANAYETUHUMIWA KWA MAUWAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI

Umati mkubwa wa wananchi wamejitokeza kumshuhudia diwani wa CCM kata ya Maboga Flgence Lutego ANAYETUHUMIWA kwa mauwaji ya kijana Denisi Kiluka zaidi sikiliza Radio country fm

DIWANI WA CCM KATA YA MABOGA ANAYETUHUMIWA KUUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO IRINGA

SAKATA la mauwaji ya kijana Denis Kiluka mwendesha piki piki mkazi wa Isoka kata ya Mwangata limezidi kuchukua sura mpya zaidi ambapo Leo jeshi la polisi mkoani Iringa asubuhi hii litawapandisha mahakamani watuhumiwa wa mauwaji hayo akiwemo diwani wa kata ya Maboga kupitia Chama cha mapinduzi ( CCM) diwani Fulgence Lutego.


watuhumiwa hao watapandishwa mahakamani asubuhi ya Leo katika mahakama ya Wilaya ya Iringa na mtandao huu utakuwezesha kupata kila kinachojiri katika mahakama hiyo kwa maana matukio yote yatakuwa Live

February 26, 2012

MKALI WA WIKI KTK MTANDAO HUU NI ASKOFU BOAZ SOLLO

Askofu Boaz Sollo wa kanisa la Overcomers mjini Iringa ameibuka mkali wa wiki katika safu hii ya mkali wa wiki inayorushwa katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kila jumapili .

Jina la askofu Sollo limeendelea kutikisa katika mkoa wa Iringa na mikoa mbali mbali ya Tanzania kutokana na kukubalika zaidi katika huduma zake za kiroho ambazo ameendelea kuzitoa katika mikoa mbali mbali na kujizolea umaarufu mkubwa .

Na umaarufu wake si umetokana na jina lake lah!hasha ni kutokana na uponyaji wagonjwa ambao wamekuwa wakifika kupatiwa huduma ya maombezi katika mikutano yake ya injili iliyopata kufanyika katika mkoa wa Iringa ,Dodoma na safari hii kuanzia tarehe 9 mwezi ujao ataliteka jiji la Mbeya

Iwapo wewe ni mkali unaweza kuleta picha yako hapa pamoja na maelezo mafupi tuma kwa email .francisgodwin.blogspot.com

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI UPENDO NKONE KUPAMBA UZINDUZI WA ALBAMU YA HASHIMU KIPONDA LEO

Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini Upendo Nkone mchana wa leo kuanzia mida ya saa 8 hadi saa 12 jioni atakuwa akiwasha moto wa nyimbo za injili katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa .

Waimbaji mbali mbali watakuwepo kupamba tamasha hilo la uzinduzi wa Albamu ya mwimbaji Hashimu Kiponda

NAF BLUE VIEW HOTEL NI HOTEL BORA MTWARA NZIMA

Karibuni wageni Manispaa ya Mtwara /Mikindani mkoani Mtwara kumbuka uwapo Manispaa ya Mtwara usisumbuke kuuliza Hotel nzuri ya kujipumzisha uliza NAF BLUE VIEW ni Hotel ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora ipo mtaa wa Sinani Manispa ya Mtwara jirani kabisa na stendi kuu ya mkoa wa Mtwara
Hii ndio HOTEL YA NAF BLUE VIEW Mtwara
Choo na bafu ni vya kisasa zaidi na ukichangua kujipumzisha kwetu ni sawa na kuchagua afya bora
Vitanda vyetu ni vya kisasa zaidi na utapenda kuendelea kutembelea Mtwara kila wakati iwapo utalala ndani ya Hotel yetu ya NAF BLUE VIEW

IPO JIRANI NA STAND KUU YA MKOA WA MTWARA

NAF BLUE VIEW HOTEL

KWA MAWASILIANO ZAIDI

P. o Box 179 Mtwara

Tel. 0232334465 Fax 0232334466

mobile;0776467066/ 0683467066

Email; nafblueviewhotel@gmail.com

KARIBUNI WAGENI MANISPAA YA MTWARA ,KARIBUNI SANA NAF BLUE VIEW HOTEL

UFISADI WAIKUMBWA HALMASHAURI YA MISUNGWI

Naibu waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri

JINAMIZI la tuhuma za ufisadi zinazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, limeanza kuchukuwa sura mpya, baada ya Mkuu wa Mkoa huo kutangaza vita dhidi ya mafisadi hao, na kusema atamshauri Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aivunje halmashauri hiyo ili ianze upya.

Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Mwanza Bw.Sitta Tumma anaripoti kuwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist Welle Ndikilo amesema ubadhilifu mkubwa wa fedha za miradi unaoonekana kukithiri ndani ya halmashauri hiyo ya Misungwi ni sawa na ugonjwa wa kansa, hivyo ni vema halmashauri hiyo ikavunjwa na wahusika wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kisheria.

Mbali na hayo, Ndikilo ameviagiza vyombo vyote vya dola, ikiwemo Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Usalama wa Taifa, pamoja na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuanza mara moja kuwashughulikia vigogo wa halmashauri hiyo, wanaotuhumiwa na ufisadi huo wa kutisha.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza, Ndikilo ameyasema hayo jana wilayani Misungwi, wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, katika ziara yake ya siku moja katika kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo.

Ndikilo alilazimika kuyasema hayo kufuatia kuwepo kwa ripoti za wakaguzi mbali mbali, akiwemo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye ripoti yake imebaini madudu mengi ya kuliwa kwa mamilioni ya fedha za miradi katika halmashauri hiyo.

“Tume tatu za ukaguzi ikiwemo ya Tamisemi na CAG ripoti zao zinasema ubadhilifu hapa Misungwi unatisha. Fedha nyingi za maendeleo mnakula tu, hamuwaonei huruma wananchi wetu?.

“Ripoti hizi zinasema sh. Milioni 336.7 za manunuzi zimeliwa maanamatumizi yake hayakufuata utaratibu. Chanzo ni idara ya fedha, afya na wahusika wapo 12 na wametajwa kwa majina.

“Ripoti hizi zinasema sh. Milioni 242 zimeliwa na watumishi wetu hawa. Ripoti inataja chanzo ni idara ya fedha, afya. Kwa hali hii nitamshauri Waziri Mkuu tuanze upya hapa Misungwi”, alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza, Ndikilo.

Kauli hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, imekuja siku chache baada ya vyombo kadhaa vya habari likiwemo gazeti hili kuripoti tuhuma hizo za ubadhilifu wa fedha za maendeleo wilayani humo.

Ndikilo ambaye alikuwa akiwataja hadi majina ya watumishi wanaotuhumiwa kwa ufisadi huo kupitia ripoti za wakaguzi alizokuwa nazo kikaoni hapo, watumishi hao mafisadi watalaani na wananchi, na kwamba kwa sasa Misungwi nayoongozwa na Mkurugenzi wake, Exavieri Tilweselekwa ipo kwenye ICU na inasumbuliwa na ugonjwa hatari wa kansa.

Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa mkoa aliambatana na waandishi wa habari, Ofisa Usalama wa Taifa wa Mkoa wa Mwanza, Meja Mutashi, Katibu Tawala wa Mkoa, Doroth Mwanyika, Mkuu wa wilaya hiyo ya Misungwi, Mariam Seif Lugailla, Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo, Mkurugenzi wa halmashaurio hiyo Exaviery Tilweselekwa na wakuu wa idara mbali mbali wa halmashauri ya Misungwi.

Katika hotuba yake hiyo ya machungu, Ndikilo ambaye alitumia muda wa dakika 57 kurusha makombora kwa viongozi wa halmashauri hiyo alisema, zaidi ripoti za wakaguzi zinaonesha zaidi ya sh. Milioni 60.3 zimeliwa kupitia malipo yenye mashaka (malipo hewa), na kwamba watumishi 23 wamehusika.

Kana kwamba hiyo haitoshi, alisema zaidi ya sh. Milioni 56 za manunuzi hazijulikani zilipo kwani matumizi yake hayajaoneshwa kwenye taarifa, huku sh. Milioni 36 za DASIP nazo zimeliwa kwa njia ya udanganyifu na baadhi ya vigogo wa halmashauri hiyo ya Misungwi.

Katika hilo, alionesha wasiwasi na umakini wa baraza la madiwani wa Misungwi lililopo chini ya mwenyekiti wake, Benard Polcarp, na kusema: “Hivi Misungwi hakuna baraza la madiwani?. Au baraza hili ni sehemu ya tatizo?”.

Alisisitiza kwamba, kufuatia hali hiyo mbaya, yeye na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, wataishauri Serikali Kuu kupitia kwa Waziri Mkuu na mwenye dhamana ya halmashauri kuwachukulia hatua kali vigogo hao, ikiwa ni pamoja na kuivunja ili halmashauri hiyo ianze upya na watumishi wenye damu mpya.

“Mimi na RAS tutaishauri Serikali ianze mara moja kuchukuwa hatua kali dhidi ya halmashauri hii ya Misungwi. Tunahitaji Misungwi tuanze na damu nyingine mpya, maana bila hivyo hatutaenda.

“Halmashauri nyingi tu huwa zinavunjwa zikionekana kuboronga. Hata hule Dar es Salaam iliwahi kuvunjwa kwa sababu kama hizi hizi. Hatutaki mambo haya na ninataka tutoke kwenye ICU na ugonjwa huu mbaya wa kansa”, alifoka Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza, Ndikilo.

Akihitimisha hotuba yake hiyo kwa watumishi wa halmashauri ya Misungwi, RC Ndikilo aliagiza watumishi wote wanautuhumiwa kwa ufisadi huo kupeleka maelezo juu ya tuhuma hizo nzito za ubadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao hicho, walimtaka Mkuu huyo wa mkoa awafukuze kazi mara moja watumishi hao, na kwamba walimtaka aondoke na watuhumiwa hao na wala asiwahamishie halmashauri nyingine bali awafukuze kazi mara moja.

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHAMA TAWALA CHA BOTSWANA - BOTSWAN DEMOCRATIC PARTY (BDP) MJINI GABORONE YAFANA

.Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama, Makamuw a rais wa Afrika Kusini Bw Kgalema Nontlanthe,
na Marais Wastaafu wa Botswana Sir Ketumile Masire ( wa pili shoto) na Bw Festus Mogae,
wakiwa chini ya mti wa Marula ambako miaka 50 ilopita BDP ilizaliwa.

Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama,
wakimshangilia Rais wa Zamani wa Botswana Sir Kitumile Masire akifunua kitambaa kuweka
bango la mahali ilipozaliwa BDP

Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama,
Makamu wa rais wa Afrika Kusini Bw Kgalema Nontlanthe,
na Marais Wastaafu wa Botswana Sir Ketumile Masire ( wa pili shoto) na Bw Festus Mogae,
wakijiandaa kukata keki ya sherehe hizo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana jana February 25, 2012
(Picha zote na Ikulu )

MKOA WA IRINGA KUTUMIA ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KUNYANYASA WANAHABARI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr. ii au Sugu’, wakati akiondoka eneo la Uyole, baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la SACCOS-UWAMU lililopo Mbeya mjini, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

WAKATI makamu wa Rais Dk Gharib Bilal anayetaraji kuanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika wilaya nne za mkoa wa Iringa kesho ( Februari 27) wanahabari mkoa wa Iringa wasikitishwa na hatua ya uongozi wa mkoa huo kunyanyasa wanahabari watakaoshiriki ziara hiyo kwa kuwanyima posho za kijikimu na kuwataka kuchangia gharama za ziara hiyo kwa wale watakao kuwa tayari kushiriki .

Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa(IPC) Frank Leonard alisema kuwa kilichofanywa na uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kutoa gari bila ya kuwapa posho kwa ajili ya malazi na chakula wanahabari hao ni sawa na unyanyasaji kwa wanahabari hao .

Kwani alisema kuwa inakuweje mkoa kushindwa kutenga bajeti kwa ajili ya wanahabari 7 walioteuliwa kwa ajili ya kushiriki ziara hiyo na kuishia kutoa usafiri huku wakitambua kuwa wanahabari hao wanahitaji pia kulala na kula .

" Huu utaratibu wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ulioanza nao wa kutaka wanahabari kuchangia gharama za ziara za viongozi ni utaratibu wa kuwanyima haki wananchi kupata habari .....kwani viongozi wanapokuja katika mkoa wananchi wanategemea kupata habari kupitia vyombo vya habari na kila mwaka mkoa umekuwa ukitoa usafiri na posho ya kujikimu kwa wanahabari wanaoteuliwa kuingia katika ziara husika ....sasa leo mkoa kutaka vyombo vya habari kuchangia gharama ili wanahabari wake kuingia katika msafara huo ni sawa na mkoa kuanzisha utaratibu wa kuuza habari kwa wananchi wake "

Alisema kuwa suala hilo halitavumiliwa na wanahabari kwani kinachofanywa na uongozi wa mkoa wa Iringa ni kunyanyasa waandishi kwani haiwezekani mkoa kuwalipa posho madereva ,mafundi na viongozi wengine wanaoshiriki ziara hiyo huku vyombo vya habari vikitakiwa kuchangia gharama.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Denis Gondwe aliwaambia wanahabari hao waliofika kupokea taarifa ya mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma jana ofisini kake kuwa moa hauna hata senti moja ya kuwagharamia wanahabari watakaoshiriki ziara hiyo zaidi ya kutoa usafiri .

Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma kwa njia ya simu ili kutolea ufafanuzi suala hilo hakuweza kueleza chochote zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na katibu tawala wa mkoa wa Iringa Getrude Mpaka ambaye hata hivyo alisema yupo nje ya mkoa wa Iringa na kutaka atafutwe kaimu katibu tawala Barnabas Ndunguru ambaye alikiri kuwa ni kweli mkoa hauna fedha za kuwalipa wanahabari watakaoshiriki ziara ya makamu wa rais .

"Ni kweli mkoa hauna fedha za kuwalipa posho waandishi wa habari hata sisi tunaoingia katika ziara hii tunajilipia wenyewe kutoka katika mifuko yetu ....hivyo tunaomba na ninyi mjigharamie katika ziara hii"
Imekuwa ni kawaida kwa uongozi wa mkoa wa Iringa kubagua wanahabari katika ziara za viongozi wa serikali ila kwa suala la kutaka waandishi kuchangia gharama ni mara ya kwanza kwa mkoa wa Iringa kuanza kujiweka mbali na vyombo vya habari japo awali ofisi hiyo ya mkuu wa mkoa wa Iringa ilikuwa na kawaida ya kuchukua chombo kimoja pekee cha serikali ila safari hii hakuna chombo ambacho kimeingizwa katika utaratibu wa kulipwa posho na ofisi hiyo ya mkuu wa mkoa .
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Ishengoma alisema Makamu wa Rais atapokelewa katika kijiji cha Mfumbi, wilayani Makete Februari 27 na ataweka jiwe la msingi katika mradi wa soko lililojengwa kwa nguvu za wananchi kijijini hapo.
Pia alisema akiwa katika wilaya ya Makete makamu wa Rais atasalimiana na wananchi katika kijiji cha Matamba kabla ya kuelekea shule ya sekondari Kitulo ambako atazindua ujenzi wa nyumba ya walimu na baadaye ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha Veta kilichopo Makete mjini kabla ya kufanya mkutano na wananchi katika uwanja wa Iwawa.
Febrauri 28, Dk Bilal atazindua benki ya wananchi ya Njombe, ataweka jiwe la msingi katika jengo la upasuaji katika kituo cha afya Makambako na kuzungumza na wananchi kabla ya kuelekea wilayani Mufindi.
Akiwa wilayani Mufindi, Dk Ishengoma alisema Dk Bilal ataweka jiwe la msingi katika kiwanda cha Mbao cha Sao Hill Mufindi na hatimaye kuelekea Rungemba ambako atasalimiana na wananchi na kufungua Zahanati ya kijiji.
Februari 29, Makamu wa Rais atakuwa wilayani Iringa ambako ataweka jiwe la msingi katika machinjio ya kisasa Ngelewela yaliyopo mjini Iringa, atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa mwembetogwa na kuhitimiza ziara yake kwa kufanya majumuisho katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Akiwa katika mikoa hiyo atatembelea wilaya za Makete, Njombe kwa mkoa wa Njombe na wilaya za Mufindi na Iringa huku wilaya ya za Ludewa na Kilolo zikiachwa katika ziara hiyo ya Makamu wa Rais .