Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

January 31, 2012

DAKIKA 45 ZA ITV NA CHANGAMOTO ZAKE......

Wanahabari wa radio Fm za kijamii na vituo vya TV za kijamii katika Halmashauri za wilaya za mikoa ya nyanda za juu kusini wamekosoa mwenendo wa kipindi cha dakika 45 za ITV kuwa umeanza kuyumba tofauti na mwanzo ambapo kipindi cha Dakika 45 kilikuwa kikivutia wengi zaidi kutokana na kuibua mambo mazito yanayogusa Taifa kwa ujumla hivyo wamtaka mwendeshaji wa kituo hicho kubadilika kwa kupokea maoni ya wadau na kujiuliza juu ya Hali ya kipindi kwa sasa na Mwanzo.

wataka mwendeshaji wa kipindi kuangalia mambo ya kuyafanyia kazi kwa wakati ili jamii kuweza kuendelea kukipenda zaidi kipindi cha Dakika 45 ambacho kwa sasa kinapoteza mwelekeo

JESHI LA POLISI NA BASATA WAUNGANA KUWABANA WEZI WA KAZI ZA SANAA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Jeshi la Polisi nchini wameunda kikosikazi maalum kitakachokuwa kikifuatilia uharamia na maovu mbalimbali katika shughuli za Sanaa na Burudani.

Kukosi kazi hicho kimeundwa baada ya Jeshi la Polisi nchini kutumia Sanaa shirikishi katika kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa kuhusu dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.

Akizungumza kuhusu kikosikazi hicho, Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, BASATA Bi. Vivian Shalua alisema kuwa, kazi kubwa ya kikosi hiki itakuwa ni kufuatilia maonesho yasiyokuwa na vibali, uharamia kwenye kazi za wasanii na wasanii kutoka nje wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

Aliyataja majukumu mengine ya kikosikazi hicho kuwa ni pamoja na kudhibiti maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania, kusimamia utoaji vibali kwa wasanii wa kitanzania wanaoenda kufanya maonesho nje ya nchi na majukumu mengine yatakayojitokeza.

“Kikosikazi hiki kitakuwa tayari kufuatilia taarifa yoyote ya uharamia kwenye kazi za wasanii, maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania na wasanii wanaoingia ndani ya nchi na kufanya maonesho bila vibali” alisisitiza Shalua.

Kikosikazi hicho kinaundwa na Shani Kitogo (Afisa Utamaduni Ilala), Tatia Ramadhan (Polisi, TAZARA), Afande Jeremiah (Polisi Kati), Koplo Juma Mashauri (Polisi Airport), Michael Kagondela (Idara ya Utamaduni), Afande Deus Matoro (Reli) na Afande Swai (Traffic),
Wengine ni Vivian Shalua (BASATA), Jonathan Abel na Tatu Burhan (Uhamiaji), Deus Kessy (Polisi Reli), Koplo Josephat Syllively (Polisi – Maji), Masanja Nyalali (Polisi – Airport) na PC Mwakajaby (Polisi – TAZARA)

WATANGAZAJI WA RADIO FM MIKOANI WAONYWA KUACHA KUIGA CLAUDS FM WATAKIWA KUBUNI VYAO.

Wadau wa mtandao huu kutoka Rukwa na Mbeya wakiwa na mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin (katika) baada ya kukutana katika semina ya mafunzo ya tume ya Taifa ya kuthibiti UKIMWI (TACAIDS) iliyoandaliwa maalum kwa waandaaji wa vipindi vya radio za kijamii mikoa ya kusini na waendeshaji wa vipindi ,semina inayofanyika jijini Mbeya

Wakati vituo mbali mbali vya radio Fm nchini Zikiwemo vile vya mikoani vikionyesha kujikita zaidi katika kuiga sauti na vipindi na sauti za watangazaji wa kituo cha radio Clauds Fm ,Tume ya taifa ya kuthibiti Ukimwi (TACAIDs) imetaka watangazaji hao kuepuka kuiga mazuri ya radio Clauds Fm na badala yake kuanzisha ubunifu wao ili nao waweze kutambulika kwa kazi zao badala ya kuiga hadi sauti za wengine.

Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya wakati wa mafunzo ya siku mbili ya watarayishaji na waendeshaji wa vipindi katika vituo vya radio za jamii kwa mikoa ya Mbeya ,Ruvuma, Rukwa na Iringa ,semina inayoendelea katika ukumbi wa chuo cha madaktari mkoani Mbeya.

Akitoa Elimu kwa wanahabari hao kuhusiana na mtayarishaji na mwendeshaji mzuri wa kipindi katika radio hizo za kijamii na radio nyingine hap a nchini ,mtaalam kutoka chuo kikuu cha Tumaini D,Salaam Richard Ngaiza alisema kuwa utamaduni wa watarayishaji hao wa vipindi ama waendeshaji kuiga mazuri yaliyoanzishwa na radio Clauds Fm na kusahau kubuni mazuri ya Kwao ni kuzidi kumuua kitaaluma na kuwa mafanikio ya radio Clauds Fm na kutokea kuwa radio pendwa katika Tanzania ni kutokana na ujuzi wa kweli wa watangazaji wake .

"Lazima watarayishaji wa vipindi na watangazaji kujaribu kuwa makini zaidi na kabuni vipindi vyenu na kutangaza kwa sauti yako bila kuiga kna siku wasikilizaji wakibaini kuwa umekopi kila kitu watakushusha na kukuona si chochote katika fani"

Hivyo aliwataka watangazaji kujifunza kabuni mambo ya Kwao kuliko kuiga kila jambo na kuwa utangazaji wa kukopi kwa mwingine ni utangazaji usio na tija katika tasnia ya habari .

Alisema kuwa wasikilizaji wanapenda kusikia mambo mbali mbali yanayoendelea katika mikoa Yao Hata Kama mtamgazaji atatangaza kwa sauti yake bila kuiga ya mtu mwingine ama kuwa na vipindi binafsi kuliko kukopi vipindi vya radio Clauds Fm .

Hivyo aliwataka watarayishaji wa vipindi kwa radio hizo za jamii mikoa ya kusini kuanza kuandaa vipindi vya UKIMWI ili kusaidia jamii ya mikoa hiyo kupunguza kasi mpya ya maambukizi ya VVU.

Kwa upande wao wanahabari washiriki wa warsha hiyo wamempongeza mwendeshaji huyo wa mafunzo kwa kuliona hilo na kudai kuwa baadhi ya radio zimezidi kukopi kazi za wengine na kuwa sehemu kubwa ya watangazaji hao wamekuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kuwa baadhi ya radio wamekuwa wakikopi hadi ratiba za vipindi vya radio nyingine ikiwemo Clauds Fm na kumfanya msikilizaji kushindwa kutofautisha stesheni hizo.

TAARIFA MBALI MBALI TOKA TFF LEO

MECHI YA TWIGA STARS YAINGIZA MIL 38/-
Mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia (Brave Gladiators) imeingiza sh. 38,220,000.
Kiasi hicho ni kutokana na watazamaji 16,334 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa juzi (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Twiga Stars kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 1,000 (watoto), sh. 2,000 (viti vya kijani na bluu), sh. 3,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 5,000 (VIP C na B) na sh. 10,000 kwa VIP A.
Watoto waliokata tiketi kuingia uwanja ni 634, viti vya rangi ya kijani na bluu 13,238, viti vya rangi ya chungwa 1,040, VIP B na C 1,246 na VIP A watazamaji 176.
Vilevile Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki na wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha mechi hiyo kati ya Twiga Stars na Namibia.
WAMISRI KUICHEZESHA STARS FEB 29
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo namba 25 itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Farouk Mohamed atakayekuwa mwamuzi wa kati. Wasaidizi wake ni Ayman Degaish na B.T Abo El Sadat wakati mwamuzi wa akiba ni Ghead Grisha.
Kamishna wa mechi hiyo ni Loed Mc Ian wa Afrika Kusini. Mchezo wa marudiano kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini utafanyika jijini Maputo baadaye mwaka huu.
NAHODHA TWIGA STARS KUCHEZA UTURUKI
Nahodha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia Mwasikili ameondoka jana alfajiri (Januari 30 mwaka huu) kwa ndege ya Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza mpira wa kulipwa.
Mwasikili amekwenda kujiunga na Luleburgazgucu Spor Kulubu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo.
Beki huyo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa mkataba wa miaka miwili.
Awali Mwasikili alitakiwa kujiunga mapema na timu hiyo lakini alilazimika kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave Gladiators) iliyochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TACAIDS YAJIPANGA KUTUMIA RADIO ZA JAMII KUTOA ELIMU YA UKIMWI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Iringa OWENI WIMBO akiwasilisha mikakati ya mkoa wa Iringa
mtaalam wa mawasiliano ambaye ni mhadhiri msaidizi wa chuo kikuu cha Tumaini D,Salaam Bw. Richard Ngaiza
afisa uhusiano wa TACAIDS Glory Mziray
Baadhi ya wanahabari wa vituo vya utangazaji vya kijamii mikoa ya nyanda za juu kusini wakiwa katika mafunzo


TUME ya Taifa ya kuthibiti UKIMWI (TACAIDS) imewataka watayarishaji wa vipindi na watangazaji katika radio za jamii mikoa ya nyanda za juu kusini kutumia nafasi yao kwa kuelimisha na kutoa elimu kwa juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na changamoto za UKIMWI Katika mikoa ya Iringa ,Ruvuma ,Rukwa na Mbeya kama njia ya kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya VVU.

Changamoto hiyo imetolewa leo afisa uhusiano wa TACAIDS Glory Mziray wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa watayarishaji wa vipindi na wawakilishi zaidi ya 40 wa radio hizo za jamii katika mikoa ya nyanda za juu kusini ,mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa chuo cha madaktari jijini Mbeya.

Alisema kuwa lengo la TACAIDS kutoa mafunzo hayo kwa wanahabari ni kutaka kuzitumia Radio hizo za jamii katika mikoa ya kusini ili kuweza kusaidia kampeni za mapambano dhidi ya UKIMWI katika mikoa hiyo .

Mziray alisema kuwa kwa kuwa zipo baadhi ya kampeni ambazo zimepata kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kupitia nguvu ya vyombo vya habari ni wazi kampeni hiyo ya TACAIDS kutaka kuzitumia radio za jamii katika mikoa ya kusini katika mapambano dhidi ya Ukimwi inaweza kufanikiwa kwa kupindi kifupi zaidi na hivyo kuwataka wanahabari wa mikoa hiyo ya kusini kubuni vipindi bora za elimu ya UKIMWI kwa jamii ili kusaidia kufikisha elimu hiyo.

Alisema kuwa kasi ya mambukizi ya VVU katika mikoa ya nyanda za juu kusini imeendelea kuongezeka na japo elimu ya UKIMWI imekuwa ikitolewa kupitia asasi mbali mbali na ndio sababu ya sasa TACAIDS kulazimika kuelekea mkakati wake katika radio hizo za jamii ili kusaidia kufikisha elimu zaidi.

Kwa upande wake Afisa uraghabishi wa TACAIDs Simon Keraryo alisema kuwa matumizi sahihi ya radio za kijamii katika kufikisha elimu ya UKIMWI kwa UKIMWI kwa wasikilizaji wa radio hizo.

Alisema sehemu kubwa wananchi wamekuwa na imani kubwa na radio hizo za jamii na kuwa kutokana na imani hiyo ndio sababu ya TACAIDS kuelekeza nguvu zake katika mapambano ya UKIMWI kupitia vituo hivyo .

Huku mtaalam wa mawasiliano ambaye ni mhadhiri msaidizi wa chuo kikuu cha Tumaini Ricard Ngaiza alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa radio za jamii ila sehemu kubwa ya radio hizo zimekuwa hazifanyi mambo ya kijamii.

Kwani alisema kuwa iwapo radio hizo zitaweza kufanya kazi kwa kutoa elimu kwa jamii ikiwemo elimu ya UKIMWI upo uwezekano mkubwa wa radio hizo kuchangia kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya VVU.

Huku kwa upande wake wanahabari washiriki wa mafunzo hayo walionyesha kutofautiana juu ya mwenendo wa baadhi ya radio FM hapa nchini ambazo zimekuwa zikiongoza kwa kuiharibu jamii kwa kuhamasisha ngono zaidi badala ya kuelimisha madhara ya ngono kwa jamii.

Kwani walisema kuwa sehemu kubwa ya Radio FM zimekuwa zikijikita katika burudani na kuzungumza udaku badala ya kusaidia kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa UKIMWI.

MWISHO

SERIKALI RUVUMA YAWATAKA WAKULIMA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu (mwenye kaunda suti nyeusi wa tatu kulia ) akisikiliza maelezo ya kilimo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya (kulia) wakati wa ziara ya kukagua usambazaji wa pembejeo kijiji cha Lugagara wilaya ya Songea

Serikali imewataka wakulima mkoani Ruvuma kulima kwa wingi mahindi katika msimu huu kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo licha ya changamoto za soko lililowakabiri msimu wa kilimo uliopita.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakati wa ziara yake katika vijiji vya Magagula, Lugagala na Muungano Zomba vilivyopo wilaya ya Songea .

Mwambungu aliwaeleza wananchi kuwa serikali inatambua kero ya ununuzi wa mahindi iliyotokea msimu wa 2011/2012 ambapo wakulima wengi walichelewa kupokea fedha zao kutoka Wakala wa Hifadhi za Chakula (NFRA).

Aliongeza kusema kuwa changamoto ya fedha za wakulima hazitajitokeza tena msimu ujao kwani tayari serikali imejiandaa kwa kutengwa fedha katika bajeti ili kuhakikisha mahindi yote yatanunuliwa kwa wakati.

“Limeni kuliko mwaka jana kwani serikali imejipanga kununua kwa wakati na kuhakikisha kuwa hakuna mkulima atakayecheleweshewa malipo na serikali” alisema Mwambungu na kuongeza kuwa hakuna mkulima sasa anayeidai serikali wote wamelipwa.

Mkuu wa mkoa Mwambungu alisisitiza kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuondoa kero ya kukopa mahindi ya wakulima hivyo ni vema wakulima wakaendelea kuunga mkono juhudi hizi za serikali kwa kuongeza uzalishaji.

Katika msimu 2011/2012 wa kilimo kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Hifadhi ya Chakula jumla ya tani 50,018 za mahindi zimenunuliwa kutoka kwa wakulima mkoani Ruvuma zenye thamani ya shilingi bilioni 17.5 ambapo kilo ilinunuliwa kwa shilingi 350.

Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wakulima wa vijiji hivyo alivyovitembelea kwa kutumia vema pembejeo za ruzuku kwa mfumo wa vocha kwani wameongeza uzalishaji wa mahindi na kuifanya wilaya ya Songea kuongoza katika kuzalisha mahindi mkoani.

Ziara ya Mkuu wa mkoa ilihusisha pia kukagua zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo ambapo kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya alisema wilaya imepata mgao wa vocha 64,417 ambazo zimesambazwa kwa wakulima.

Sabaya alisema vocha hizo zinahusisha mbegu bora za mahindi, mbolea ya kupandia na mbolea ya kukuzia ambapo bei ya mfuko wa mbolea ya kupandia (DAP) inauzwa shilingi 80,000/=huku mkulima akichangia shilingi 52,000/=.

Kuhusu mbolea ya kukuzia (UREA) mfuko unauzwa shilingi 72,000/= na mkulima anachangia shilingi 52,000/= huku serikali ikilipia zinazobaki na kwa mbegu bora mfuko unauzwa shilingi 40,000/= huku mkulima akichangia 20,000/= na serikali zinazobakia.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Lugagara Bi Taifa Mahundi katika risala yake alisema wakulima wana changamoto kubwa ya upungufu wa vocha za ruzuku hivyo akaiomba serikali kuongeza mgao kwa kijiji.

Mkuu wa mkoa akijibu hoja hiyo aliwafahamisha wananchi kuwa vocha zinazotolewa ni vigumu kufanana na idadi ya wakulima kwani hiyo ni ruzuku itolewayo na serikali kuwasaidia wakulima kujenga uwezo wa kujitegemea.

Katika msimu huu wa kilimo mkoa wa Ruvuma umepatiwa vocha za ruzuku ya pembejeo za kilimo 192,000 ambapo kwa mwaka uliopita ulipatiwa vocha 204,000 hivyo kuwa na upungufu wa vocha 12,000/=.

Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa sita maarufu kwa uzalishaji wa mahindi nchini ambapo mikoa mingine ni Iringa, Mbeya, Rukwa, Kigoma na Morogoro.
…………………………………………………………………………………………………
Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma

DARASA ELIMU YA UKIMWI KWA WANAHABARI LAENDELEA UKUMBI WA MADAKTARI MBEYA -LIVE
Wawezeshaji wa kitaifa wakiwa katika harakati za semina
wanahabari wakiwa katika semina


waratibu wa TACAIDS kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Ruvuma akieleza hali halisi ya UKIMWI mkoani kwake
Wawezeshaji wa TACAIDS Taifa wakifuatilia mrejesho wa UKIMWI kutoka kwa waratibu wa TACAIDS
Darasa linaendelea kwa wanahabari kunolewa
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya utangazaji mikoa ya Iringa,Mbeya,Rukwa na Ruvuma wakiwa darasani