Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2012

DC LUDEWA JUMA MADAHA AWAPA SOMO LUDEWA

Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa  Juma Madaha  amewataka  watumishi  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  kufanya  kazi kwa upendo na mshikamano kama njia ya kuuanza mwaka mpya  wa 2013 kwa upendo na ufanisi zaidi.

Mkuu  huyo  wa  wilaya ametoa kauli  hiyo leo wakati wa kuwaaga watumishi wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa na kuwakaribisha  watumishi wapya pamoja na kuaga na kukaribisha mwaka mpya  wa 2013 ,sherehe  zilizofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa .

 Asema kuwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ni watumishi ambao wanaweza kulikomboa Taifa katika dimbwi la umasikini iwapo kama kila mtumishi atadumisha umoja na mshikamano .

 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kila mtumishi ni lazima kujuwa wajibu wake na kutambua malengo yake katika kuitumikia Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa na kudai kuwa baada ya kugawanywa mkoa wa Iringa na Njombe hivi sasa mkoa wa Njombe ndio unapiga hatua zaidi katika maendeleo ukilinganisha na mkoa wa Iringa.

Aidha awataka watumishi wa Halmashauri ya Ludewa kuhakikisha wanafika kazini saa mmoja asubuhi na saa 1.30 kuanza kazi ya serikali badala ya kufika kazini kwa kuchelewa .

 Madaha alisema kuwa hakuna haki bila kutimiza wajibu na kuwataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutimiza wajibu kwanza katika kazi badala ya kudai haki bila kutimiza wajibu .

 Amtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Fidelis Lumato kuhakikisha anawabana watumishi wasiowajibika huku akiwataka watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuzingatia sheria ,kanuni na utaratibu huku kuonyesha mfano mwema katika maeneo yao ya kazi.

 Madaha alisema kuwa hatakuwa na huruma kwa mtumishi wa Halmashauri hiyo atakayeshindwa kutimiza wajibu wake na kuwa kwa mwaka 2013 nyaraka zote za sheria za utumishi wa umma zitawekwa mahali ambapo kila mtumishi ataweza kusoma na kuzitambua zaidi ili pale anapokiuka kuwajibika kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu.

 Akemea vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi na kutaka watumishi kuchukua hatua ya kupambana na rushwa na kuwa rushwa katika wilaya ya Ludewa inapaswa kupigwa viti na kila mmoja .

 Mkuu huyo wilaya amesema kuwa iwapo kila mtumishi wa wilaya hiyo atafanya kazi kwa uaminifu na kuchukia vitendo vya rushwa wilaya hiyo itaendelea kupiga hatua katika maendeleo.

Kuhusu wastaafu mkuu huyo wa wilaya alitaka Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuweka utaratibu wa kuwasaidia wastaafu ili nao waweze kuendelea na kunufaika na matunda ya Taifa

 Alisema kuwa pamoja na wazee wastaafu kulitumikia vema Taifa ila bado maadili ya Taifa yameendelea kumomonyoka kutokana na wazee kushindwa kuwafunza vema vijana katika maadili mema na kuwa wazee waliowengi wanashindwa kuwalea watoto wao katika maadili kutokana na hali ya umasikini inayowakabili.

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akitoa  salam zake katika sherehe hizo alisema kuwa kwa upande  wake  amefarijika kufika katika sherehe  hizo na  kufanya  sherehe  hiyo ya kufunga mwaka na watumishi hao huku akieleza matumaini yake makubwa katika  kuwatumikia  wananchi wa jimbo la Ludewa .

SHEREHE ZA KUAGA MWAKA 2012 NA KUAGA WATUMISHI LUDEWA ZAFANA -LIVE


Aliyekuwa kaimu mkurugenzi  

Sherehe za kuwaaga na kuwakaribisha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa zafana usiku huu katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa . Katika sherehe hizo ambazo pia zimeambatana na kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 zinafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Ludewa huku viongozi mbali mbali wa Wilaya na Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa wakiwa wamepamba sherehe hiyo.

 Akizungumza katika sherehe hiyo mratibu wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Gladness Mwano amesema kuwa katika sherehe hiyo jumla ya watumishi 6 wanaagwa rasmi baada ya kustaafu na watumishi 14 wanahama huku watumishi 5 wakikaribishwa katika Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa .

Watumishi wanaostaafu katika Halmashauri hiyo ni pamoja na Augusta Kayombo ( Idara ya afya), Gerold Kayombo ( katibu TSD), Ignas Mkechi (ukaguzi wa shule), Beneth Nzalamoto ( Idara ya afya) , Edwird Masangula (idara ya fedha) na Ireen Mtetemela ( idara ya utawala).

Wakati watumishi waliohama ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Hilda Lauwo aliyehamia Maswa , Juma ,Ally (afisa utumishi na utawala aliyehamia Mbinga, Advery Dallu Afisa utumishi na utawala amehamia TAMISEMI Dodoma, Alto Liwolelu (Mwanasheria aliyehamia Kilolo), Emmanuel Mlelwa (afisa elimu sekondari aliyekwenda Pangani ,Christopher Nyandiga (mhandisi aliyehamia RAS Njombe), Rashid Mtamila ( Mhandisi wa ujenzi aliyehamia Sumbawanga),Gumbo Mvanda ( afisa misitu anahamia Ras Njombe),Daud Kumburu (afisa ufugaji nyuki anahamia Ras Njombe ), Mussa Sechonge (Afisa kilimo wadudu anakwenda Morogoro),Rose Lutambi (muunguzi mifumo ya kompyuta anakwenda Njombe mji) na Mariam Kinyamagoha (afisa muuguzi anahamia Mufindi).

 Aidha Halmashauri ya wilaya ya Ludewa imepokea watumishi wapya ambao wanachukua nafasi ya waliohama na kustaafu ikiwemo nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo inayochukuliwa na Fidelis Lumato aliyehamia kutoka Tarime, Mathan Chalamila (mwanasheria anayehamia kutoka Njombe DC ,Maternus Ndumbaro (afisa elimu sekondari anayehamia kutoka Makete , Baraka Mkuya (mahandisi ujenzi anayehamia kutoka Sumbawanga MC na Antony Mbi
nda (katibu TSD anayehamia kutoka Mufindi)

Akizungumza katika sherehe hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mateo Kongo alisema kuwa Halmashauri hiyo imefarijika kwa utendaji wa watumishi waliopita na kuwakaribisha wapya huku akiahidi kuwapa ushirikiano zaidi.

WANANCHI WA KATA YA WASA WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MDAHALO WA MABADILIKO YA TABIANCHI


Wakazi wa kata ya wasa na vitongoji vyake wakiwa wamehudhuria katika mdahalo wa mabadiliko ya Tabianchi yaliyoandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Iringa (ICISO-UMBRELLA)


Afisa uhusiano wa ICISO-UMBRELLA Iringa Mwabulala akifungua mdahalo katika ukumbi wa Katoliki Wasa

Baadhi ya wananchi walioshiriki wakiandika taarifa muhimu zilizokuwa zikitolewa na mtoa mada wa mabadiliko ya TabianchiMkazi wa wasa Albert Gowola akichangia katika mdahalo wa Mabadilio ya Tabianchi

Diwani wa kata ya Wasa Masumbuko Choga akitoa maoni yake baada ya mdahalo huo.

KOCHA MPYA WA SIMBA PATRICK LIEWING ATUA JIJINI DARNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kocha mpya wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa saba za mchana kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba.

 Uongozi wa Simba, kwa kupitia Katibu Mkuu wao, Evodius Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Kocha huyo anawasili huku akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo Julio, kocha ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa kitendo chake cha kukubali kuinoa timu hiyo.

Mengi juu ya ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo ya mwisho na kuingia makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa cha kurudisha imani kwa wapenzi na wanachama wao.

Simba ilimaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu, nyuma ya timu ya Yanga na Azam FC.

MBUNGE ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI HUKU AKINYESHEWA NA MVUA


Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe (pichani)akubali kunyeshewa na mvua kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Chanjale wilayani Ludewa ambao walikuwa wakilalamikia ufisadi unaofanywa na viongozi wao wa kijiji na kata.

Mbunge huyo ambae awali kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi alipewa mwamvuli kwa ajili ya kujikinga na mvua iliyoanza kunyesha muda mfupi kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi hao ,baadae alikataa kujifunika mwamvuli huo kwa madai kuwa hawezi kujifunika mwamvuli kula starehe wakati wananchi wake wanakero na wananyeshewa na mvua.

 Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliendelea kusikiliza na kujibu maswali mbali mbali ya wananchi juu ya ufisadi unaofanywa na viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi wala kuitisha mkutano kijijini hapo.

 Wananchi hao mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha mfano kwa viongozi wengine kwa kufika kulala katika kijiji hicho na kusikiliza kero zao ,bado walisema kuwa viongozi wa kijiji hicho na kata wamekuwa ni tatizo kubwa na wao kama wananchi wameonyesha kuwachoka viongozi hao.

 Akizungumza katika mkutano huo mbunge Filikunjombe alisema kuwa anasikitishwa na utendaji wa viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kufanyia kazi matatizo ya wananchi wa kijiji hicho hata kwa kushindwa  kujenga  choo cha wanafunzi .

Hata  hivyo alisema kuwa ofisi yake anachukua hatua ya kuchangia  kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya  kusaidia ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya Msingi Chanjale

DIWANI WA CCM LUDEWA AKICHAMBUA CHADEMA ,MBUNGE APOZA

                                                                              Dkt Slaa

DIWANI wa kata ya Lumbila wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Justine Mwakila akishukia Chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) kuwa ni Chama chenye ubinafsi hivyo kuwataka wananchi kuacha kuyumbishwa na Chama hicho na badala yake kutulia Chama cha mapinduzi ( CCM)

Diwani huyo Mwakila alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe katika Kijiji cha Nkanda mwambao mwa ziwa Nyasa.

Alisema kuwa anashangazwa na tabia ya baadhi ya vijana wa kata hiyo kuiga siasa ya uchadema Kutoka mkoa wa Mbeya ambako ni mpakani mwa Kijiji hicho Kutoka jimbo la Kyela na Ludewa na kuacha kutulia na CCM .

Mwakila alisema vijana wengi washabikia Chadema bila kujua mambo ya ndani ya Chadema na kuwa  Chadema kimekuwa kikiendeshwa kibinafsi zaidi ukilinganisha na CCM .

" Nawaomba sana wananchi wa Kijiji cha Nkanda tusiigize maisha yake kwa kushabikia vyama vya upinzani wakati mbunge wetu Filikunjombe amekuwa mbele kutupigania wananchi....hivyo kuendelea kushabikia upinzani ambao hata siku moja hawajapata kufika hapa kwetu"

Hivyo alisema hatua ya vijana kuendelea kushinda katika vijiwe na kushabikia upinzani bila kufanya kazi.

Kwa Upande wake wananchi wa Kijiji hicho katika risala yao iliyosomwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho Abel Mwakirambo kwa mbunge huyo walisema kuwa katika Kijiji hicho awali kulikuwa hakuna huduma ya afya ila sasa kuna mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba ya mganga utakaotumia zaidi ya shillingi milioni 60 ujenzi unaojengwa kupitia mradi wa TASAF

Walisema kuwa ili kukamilisha mradi huo kiasi cha zaidi ya shillingi milioni 23.9 zinahitajika ikiwa ni pamoja na kumuomba mbunge huyo kuwa mlezi wa Kijiji na kusaidia kuwaletea mganga japo mmoja.

Alisema kuwa Kijiji hicho kina vitongoji vitatu na wakazi 495 Kati yao wanawake 251 na wanaume 244

Mtendaji huyo alisema katakana na idadi kubwa ya wananchi na kukosa huduma ya afya kwa wanawake wajawazito ambao walikuwa wakipoteza maisha pindi wanapokwenda kupata huduma hiyo nje ya Kijiji kwa kupitia usafiri wa maji na pindi ziwa linapochafuka wamekuwa wakifia ziwani.

Alisema mradi huo wa Zahanati ulibuniwa na wananchi na kuanza mwaka 2008 kupitiwa mfumo  wa maendeleo ya jamii ( TASAF).

Kuwa hadi sasa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 60.3 ambazo zimetolewa na TASAF wakati ofisi ya mbunge kupitia mfuko wa jimbo zimetolewa kiasi cha shilingi milioni 1.6 wakati fedha zilizopo kwa ajili ya kumalizia mradi huo ni shilingi milioni 23.9

Kwa Upande wake mbunge Filikunjombe aliwataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kufanya kwa ushirikiano zaidi ili kulifanya jimbo hilo kuwa mbele katika maendeleo.

Alisema kuwa anaamini kuwa wananchi wa Nkanda na jimbo hilo wanataka maendeleo na sio vyama vya siasa na kuwa yeye ni mbunge wa vyama vyote kwa wakiomchagua na wasio mchagua.

" Mimi sasa ni mbunge wa wote CUF, Chadema, TLP na CCM pamoja na wote wasio kuwa na vyama ...ila rai yangu kwenu kuacha ubishani wa kisiasa na kufanya kazi siasa za mabishano ya kisiasa kwani hatutatufikisha pote ila maendeleo yatatufikisha mbele zaidi"

Filikunjombe alisema bungeni kuna wabunge zaidi ya 300 na wapo baadhi ya wabunge ambao wanawakilisha wananchi kwa staili ya kuzinzia ila kwa Upande wake kamwe hataenda bungeni kwa kuwajulisha wananchi kwa kuzinzia bali atakuwa macho na kupambana na ufisadi na kupigania maendeleo ya jimbo lake la Ludewa muda wote.

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI TUNAWATAKIA WOTE HERI MWAKA MPYA 2013


SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
  TUNAWATAKIA WOTE HERI  MWAKA MPYA 2013

RATIBA YA MELI MPYA JANUARY 2013
 
FROM TILBURY 15/01/2013
FROM SHEERNESS 18/01/2013
BOOKINGS ZOTE SASA ZINAFANYIKA ONLINE
PLEASE VISIT OUR IMPROVED WEBSITE

VEHICLE INSPECTION FOR KENYA AND UGANDA NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES
JUST DROP YOUR  CAR IN OUR OFFICE AND WE WILL INSPECT IT AND DELIVER IT TO THE PORT FOR YOU
MITUMBA £65 KWA BALLE LA 45KGS AGIZA SASA
 
kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;

CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
HASSAN (RICHARD) +44 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477
                       

BREAKING NEWSS MBUNGE FILIKUNJOMBE NA MSAFARA WAKE WANUSURIKA ZIWA NYASA , BOTI YAZIMA GAFLA KATIKATI YA ZIWA

Boti  iliyobeba msafara  wa mbunge Filikunjombe ikianza safari baada ya  kuzima na kuwashwa tena ndani ya  ziwa nyasa ,kutoka  kushoto ni mimiliki wa mtandao huu mzee wa matukio  daima, Filikunjombe Felix Haule na dereva wa boti  hiyo
  Mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  (wa  kwanza  kushoto) akimtazama dereva  wa boti ya Halmashauri ambae alikuwa akihangaika  kuiwasha boti  hiyo baada ya kuzima ghafla katikati ya  ziwa nyasa  alfajiri ya  leo wakati mbunge  huyo na msafara  wake akitoka kufanya mkutano kijiji cha Nsisi  ukanda wa Mwamba
 Msafara  wa mbunge  ukiingia ndani ya  boti  hiyo leo alfajiri tayari kwa kuanza  safari hiyo
MSAFARA  wa mbunge  wa  jimbo la Ludewa  mkoani Njombe  Deo  Filikunjombe wenye  watu zaidi ya 16  wanusurika  kukwama katikakati ya  ziwa  nyasa baada ya  boti ya Halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  waliyokuwa  wakisafiri  kutoka kijiji ch Nsisi kwenda kata ya  Lupingu  kuzimika ghafla.

Aeleza  kusikitishwa na tatizo la  mawasiliano katika eneo  hilo la ziwa nyasa Filikunjombe  alisema kuwa  hatari  sana  kwa usalama  wa maisha ya  watanzania wanaotegemea  usafiri wa ziwa nyasa kusafiri katika ziwa  hilo bila ya kuwa na mawasiliano ya mtandao hata mmoja  na kuitaka  serikali  kuangalia uwezekano  wa kuboresha mawasiliano ya  simu katika maeneo hayo ya Ziwa Nyasa  upande wa Tanzania.

Tukio  hilo ambalo ni la pili kwa mbunge  Filikunjombe  kunusurika katika  ziwa  hilo  lilitokea majira ya saa 11.40 asubuhi ya  leo   wakati boti  hiyo ya msafara  wa mbunge  huyo iliyokuwa na mkewe  na viongozi mbali mbali ya  Chama cha mapinduzi (CCM)  wilaya ya Ludewa  wakiongozwa na mwenyekiti  wao Stanley Kolimba  pamoja na  wakuu  wa idara  na  wapiga  kura  wake  .

Boti  hiyo ambayo  iliondoka kijiji  cha Nsisi kata ya Lifuma  majira ya saa 10 alfajiri   baada ya   kumaliza  kupita  eneo  lenye mkondo mrefu na maji katika ziwa  hilo nyasa umbala  wa mwendo wa dakika  20 kabla ya  kufika kijiji bandari  ya Lupingu  ghafla boti  hiyo  ilionyesha kupunguza mlio wake na  kuzimika na kupelekea  viongozi  waliokuwemo katika boti  hiyo kutaharuki na mbunge kulazimika  kumpunguza  sauti ya muziki  nyimbo  za injili  uliokuwa ukipigwa katika boti hiyo na kuwaeleza  kuwa  kuna  tatizo boti  imezimika.

Tangazo  hilo na hatua ya mbunge  kuwaeleza abiria  waliokuwemo katika boti  hiyo juu ya tatizo  hilo na  kuwataka  kutulia bila  kuchukua hatua  yoyote ya kujirusha katika maji  iliwafanya viongozi waliokuwa wamejipumzisha kwa  kuuchapa usingizi kama katibu mwenezi  wa CCM mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya kuamka  kutulia kimya.

“Jamani  kuna tatizo  limejitokeza boti  imezima ghafla  sasa  nawaombeni  wote  kutulie tusifanye  chochote Mungu  yupo nasi “ alisikika akiongea mbunge  Filikunjombe huku  kila mmoja akiwa na hofu kubwa .

Hata  hivyo  jitihada  mbali mbali  ziliweza kufanyika na madereva wa boti  hiyo kwa  kuhangaika huku na  kule na  kubaini  tatizo la boti hiyo kuzima kuwa ni mafuta  kukata katika paipu ya  kupeleka mafuta kwenye injili ya boti hiyo tatibu ambalo  lilishughulikiwa ndani ya dakika kama 5  hivi na boti  hiyo  kuendelea na  safari.

Hii  ni mara ya  pili kwa  mbunge Filikunjombe  kunusurika katika ziwa  hilo ambapo awamu ya kwanza  ilikuwa mwaka jana mwezi  wa saba ambapo  yeye na motto  wake  wa miaka 13 pamoja na mwenyekiti  wa CCM  mstaafu  wa CCM wilaya  hiyo  walitumbukia katika  ziwa  hilo na kuokolewa  wakati  wakitumia usafiri wa mtumbwi kutaka kuingia katika boti  iliyokuwa  imeegeshwa katika  kina kirefu cha maji  eneo la Makonde.
Awali akizungumza na  wananchi  wa  kijiji cha Nsisi , Lifuma na  wananchi  wa vijiji  vya Makonde , Ndowa , Chanjale na Lumbila  kwa nyakati  tofauti katika mikutano yake ya hadhara  mbunge  Filikunjombe  alisema  kuwa wakati akiendelea  kuiomba  serikali  kuangalia uwezekano wa kuboresha mawasiliano katika  maeneo hayo ya Mwambao tayari amekuwa akifanya jitihada za  kutatua tatizo la mawasiliano katika ukanda  huo wa Mwambao na  kuwa  upo  uwezekano  wa  kupatiwa minala mitatu  ya  simu eneo  hilo .

Waliokuwemo katika boti  hiyo ni pamoja na  wanahabari  zaidi ya  wanne akiwemo mwandishi  wa habari hizi , baba mzazi  wa mbunge Filikunjombe ,mke wa mbunge  huyo , katibu  wa mbunge  huyo , katibu mwenyezi  wa  CCM wilaya ya Ludewa  Filix Haule , katibu mwenezi  wa CCM mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe Stanley Kolimba, pamoja na wakuu wa idara wa wilaya ya Ludewa 

Wakati  huo  huo  mbunge Filikunjombe  aliwataka  wananchi  wa Mwambao  kuhakikisha   wanashiriki katika shughuli za kimaendeleo ya  kuepuka kuendelea kuvuta kisiasa kama ilivyo kwa wananchi  wa kijiji cha Makonde ambao  wao  wakati  wote  wanashindwa kufanya kazi za uzalishaji mali  na badala yake  wanaendelea  kufanya maandamano kila wanapofika  viongozi kwa ajili ya kumpinga  diwani  wao Chrispine Mwakasungura .

MMOJA AJERUHIWA NA MADARASA SITA YAEZULIWA NA UPEPO MKALI WILAYANI RUANGWA


Na Abdulaziz,Lindi

UPEPO mkali uliombatana na mvua kubwa umeziathiri baadhi ya nyumba huku shule ya sekondari ya Mnacho wilayani Ruangwa ikipata athari kwa kiasi kikubwa baada ya madarasa sita kuezuliwa mabati na baadhi ya wanakijiji kupata majeraha na kusababisha wakazi wengine kukosa mahali pa kuishi.

Upepo huo uliotokea jana ni mfufulizo wa matukio hayo kwa vijiji vya kata hiyo ambapo awali mwanzoni mwa mwaka huu uliezua madarasa mawili ya shule hiyo.

Akitoa taarifa ya maafa hayo ya jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa leo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,Bw Reubern Mfune alieleza kuwa Kufuatia kuwepo kwa tukio hilo lilitokea jana jioni Ofisi yake ilifika eneo la tukio akiwemo na mkuu wa wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira na tayari wamepelekwa wataalamu kutathimini athari hizo ili shule hiyo inayotarajiwa kuanza muhula jan 14 Halmashauri yake itashirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha hali ya shule inakamilishwa.

Aidha Mkurugenzi alibainisha katika kikao hicho cha baraza la madiwani kuwa Katika maafa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliathiri shule hiyo bado ni changamoto katika Halmashauri yake kufuatia kupangawa kupokea wanafunzi 92 wa kidato cha kwanza na inatarajiwa kufunguliwa jan 14,2013 Katika maafa hayo Mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini

December 30, 2012

ZAIDI YA ABIRIA 20 WANUSURIKA KUFA


gari likizimwa moto na kikosi cha moto iringa
daladala yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ikiwaka moto eneo la mshindo. Na Denis Mlowe - Iringa

Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayofanya shughuli za kusafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.

Ajali hiyo iliyotokea mida ya saa saba mchana ilihusisha daladala aina ya kipanya yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ilitokea katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo mkoani hapa.

Shuhuda ya ajali hiyo Anthony Zamilinga amesema kwamba gari hiyo ilikuwa ikitokea maeneo ya Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa.

Msemaji wa Zimamoto Kaimu Mkuu wa Kituo Sajenti Meja John Zakaria amesema chanzo cha ajali hiyo hitalafu ya umeme iliyotokea katika gari hiyo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na tabia ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao. “kikosi cha zimamoto kinatoa elimu kila mara kuhusu elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kuna namba za simu za dharura ambazo ziko wazi wakati wote lakini wananchi hawana tabia ya kutoa taarifa mapema na ndio maana hasara kama hizi zinajitokeza hivyo hatuwezi kuota kama kuna janga la moto hivyo naomba ushirikiano wa wananchi katika majanga ya moto kama haya” alisema Sajenti Meja Zakaria

Mmiliki wa dala dala hiyo Ayubu Kabigi amesema kwamba amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo na amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari yake kwani wakati anapigiwa simu alikuwa anajiandaa na safari ya nje ya mkoa. “nawashukuru sana wananchi wa maeneo ya mshindo na kikosi cha zimamoto kuwahi kufika mara baada ya kupewa habari kuhusu janga hilo licha ya kwamba gari lilikuwa limewaka moto na kuteketea” alisema Kabigi

MBUNGE VITI MAALUMU CHIKU ABWAO AWAKOPESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI IRINGA


Wanakikundi wajasiriamali wa Mafuruto

Mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Chiku Abwao akiongea na wanakikundi Mafuruto

Mmoja wa wanakikundi akipokea mkopo toka kwa mbunge

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD MOHAMED


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishiriki katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012. PICHA NA IKULU.

ICISO-UMBRELLA KUANZA MDAHALO WA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI TAREHE 31/12 WASA


 RAPHAEL MTITU Akizungumza na vyombo vya habari Iringa kuhusu mdahalo.
MTANDAO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI MKOA WA IRINGA (ICISO-UMBRELLA) KWA KUSHIRIKIANA NA MTANDAO WA AZISE WA KILOLO (KIDINGOU), IRINGA VIJIJINI (IRUNGO) NA IRINGA MANISPAA (IMUCISO) WANAKULETEA MDAHALO WA WAZI UTAKAOWAKUTANISHA WANANCHI NA VIONGOZI WAO KWA LENGO LA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI.
 MDAHALO UTAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ROMAN CATHORIC- WASA SIKU YA JUMA TATU TAREHE 31/12/2012 KUANZIA SAA 6:00 MCHANA. JIMBO LA KILOLO TAREHE 3/1/2013 KATIKA UKUMBI WA SOCIAL CENTRE- BOMA LA NG’OMBE SAA 6:00 MCHANA NA JIMBO LA ISIMANI KATIKA UKUMBI WA SHULE YA MSINGI IDODI TAREHE 5/1/2013 SAA 4:00.

WALENGWA: WANANCHI WOTE (WANAWAKE, WANAUME, VIJANA, WAZEE, WANAFUNZI, WAFANYAKAZI, WAFANYABIASHARA, ASASI ZA KIRAIA, VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA, VIONGOZI WA SERIKALI KUANZIA NGAZI YA KITONGOJI HADI WILAYA, WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU, VIONGOZI WA DINI, WANAHABARI N.K.

FIKA USHIRIKI ILI UWE SEHEMU YA MAENDELEO YA JIMBO LA KILOLO, KALENGA, ISIMANI NA IRINGA MANISPAA NA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YANAYOHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI.

KUMBUKA MDAHALO HUU UTARUSHWA MOJA KWA MOJA (LIVE) KATIKA REDIO YA OVERCOMERS FM, REDIO FURAHA FM NA BLOG YA FRANCIS GODWIN.

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRE AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

December 29, 2012

UTAJIRI WA GESI ASILIA: TUWASIKILIZE WATANZANIA WA MTWARA NA LINDI TUSIPUUZE


Mh zitto Kabwe
Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?.
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? 
Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.
Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?
Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.

MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO

Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho. Waandishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika mkutano huo
Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .

December 28, 2012

KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUUTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 28, 2012

Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.

Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.

TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.

OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.

Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)