Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube

December 2, 2011

MSANII WA KUNDI LA ZE ORIJINO KOMEDY VENGU AZUSHIWA KIFO

Rais Dkt Jakaya Kikwete alipomtembelea Hospital msanii wa kundi la Ze Comedy Joseph Shamba a.k.a Vengu
Msanii Vengu
Msanii JOseph Shamba ama Vengu kulia akiwa na wasanii wenzake wa kundi la Orijino Komedy .

Taarifa zilizozagaa mitaani katika mji wa Iringa na maeneo mengine hapa nchini zinadai kuwa msanii huyo Vengu ambaye hali yake ilikuwa mbaya amefariki dunia.

Taarifa hizi zimeonyesha kuwaliza wengi huku wadau mbali mbali wa mtandao huu wakipiga simu kutaka kujua usahihi wa taarifa hizo ambazo hata hivyo chanzo chake cha kuvumishwa bado kufahamika.

Hata hivyo jitihada za mtandao huu kumtafuta mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji bado zinaendelea ili kujua ukweli wa hali ya afya ya msanii huyo japo chanzo cha uhakika na cha karibu zaidi na familia ya Vengu kimedai kuwa hali ya afya ya Vengu kwa leo ni nzuri zaidi ukilinganisha na siku za nyuma.

Mtandao huu unaendelea kumwombea afya njema Vengu ili apone na kurejea kulitumikia Taifa katika tasnia ya sanaa
Share this article :

1 comments:

JigambeAds said...

Jamani Watanzania tumuombeeni ndugu yetu Vengu apate afya njema!

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE

 
Mzee wa matukio daima © Copyright 2016. All Rights Reserved.

Powered by Mkami Jr.
Back to TOP