December 14, 2011

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA TAIFA,UFAULU WAONGEZEKA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi leo imetangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba huku matokeo hayo yakionesha kuwa ufaulu wa wanafunzi umeongozeka na kufikia asilimia 58.28 kutoka asilimia 53.52 ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa Radio Uhuru FM kuwa Pamoja na ongezeko la ufaulu huo pia udanganyifu katika shule mbalimbali umeongezeka kutoka wanafunzi 124 mwaka jana hadi kufikia zaidi ya wanafunzi Elfu-9 kwa mwaka huu sawa na asilimia 1 Nukta 0 ambapo wanafunzi hao wamefutiwa mitihani.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa PHILIPO MULUGO akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam amesema wakati wa zoezi la usahisaji wa mitihani kumebainika udanganyifu kwa baadhi ya shule.

Moja ya udanganyifu uliobanika ni pamoja na wanafunzi kukutwa na Karatasi za majibu ndani ya Chumba cha Mtihani zikiwa na miandiko zaidi ya mmoja.

Kuhusu ufaulu Mheshimiwa MULUGO amesema mwaka huu katika somo la Hisabati wanatahiniwa wamefanya vizuri na kufikia asilimia 39.36 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambao ulikuwa kwa asilimia 24.70.

Somo la Kiswahili ufaulu umeshuka na kufikia asilimia 68.58 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka uliopita ambao ulikuwa ni asilimia 71.02.

Katika hatua nyingine Wizara hiyo imeliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kuwachukulia hatua kali wanafunzi waliohusika katika udanganyifu pamoja na wasimamizi wa mitihani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE