Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2011

NAF BLUE VIEW HOTEL MTWARA INAKUTAKIA HERY YA MWAKA MPYA 2012

Karibuni wageni Manispaa ya Mtwara /Mikindani mkoani Mtwara kumbuka uwapo Manispaa ya Mtwara usisumbuke kuuliza Hotel nzuri ya kujipumzisha uliza NAF BLUE VIEW ni Hotel ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora ipo mtaa wa Sinani Manispa ya Mtwara jirani kabisa na stendi kuu ya mkoa wa Mtwara
Vyumba ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW,Mtwara /Mikindani
Kila chumba kuna mawasiliano ya kutosha kama simu , TV n.k
NAF BLUE VIEW inaongoza kwa usafiri na uwapo ndani ya Hotel utafurahia kufika Mtwara
Vyoo na bafu za kisasa zaidi uwapo ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW Mtwara
Mazingira yanapendeza zaidi ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW Mtwara mkoani Lindi
Vitanda vyetu ni vya kisasa zaidi na utapenda kuendelea kutembelea Mtwara kila wakati iwapo utalala ndani ya Hotel yetu ya NAF BLUE VIEW
Hii ndio HOTEL YA NAF BLUE VIEW Mtwara

IPO JIRANI NA STAND KUU YA MKOA WA MTWARA

NAF BLUE VIEW HOTEL

KWA MAWASILIANO ZAIDI

P. o Box 179 Mtwara

Tel. 0232334465 Fax 0232334466

mobile;0776467066/ 0683467066

Email; nafblueviewhotel@gmail.com

KARIBUNI WAGENI MANISPAA YA MTWARA ,KARIBUNI SANA NAF BLUE VIEW HOTEL

BREAKING NEWS LUHANJO AUT UKATIBU MKUU KIONGOZI APOKELEWA NA BALOZI SEFUE


Rais Jakaya Kikwete akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Mh Philemon Luhanjo (kulia) na Katibu Mkuu kiongozi mteule Balozi Ombeni Sefue ofisini kwake Ikulu Dar es salaam Ijumaa usiku mara baada ya kufanya uteuzi huo(picha na Ikulu)
Rais Jakaya Kikwete amemteua Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, kuchukua nafasi inayoachwa wazi na Phillemon Luhanjo ambaye anahitimisha mkataba wake leo Desemba 31.

Balozi Sefue alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani (Washington DC) na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tangu Oktoba 2005.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Balozi Sefue anataraji kuapishwa leo Jumamosi, Ikulu ya Dar es Salaam

December 30, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA TASWA

Mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma Pinto katikati akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Taifa wa TASWA
(A) MAREKEBISHO YA KATIBA

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ilikutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ilikubaliana kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho ili iendane na wakati wa sasa.

Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji inemteua mwanamichezo maarufu ambaye pia ni mwanasheria na wakala wa wachezaji wa soka Damas Ndumbaro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA.

Wajumbe wengine kwenye kamati hiyo ni George John ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa TASWA,Alfred Lucas ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA na atakuwa Katibu wa kamati hiyo na Mwani Nyangasa ambaye ni mwanachama.

Kamati hiyo itasimamia mchakato wa marekebisho hayo, kisha utaitishwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama wote kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo na ni imani ya Kamati ya Utendaji kuwa marekebisho hayo ya Katiba hayatachukua muda mrefu, ili mkutano Mkuu wa TASWA ufanyike kabla ya kumalizika robo ya kwanza ya mwaka 2012.

(B) SEMINA, MAFUNZO MWAKA 2012

Kikao hicho pia kilipanga kuhusiana na masuala mbalimbali ya mafunzo kwa wanachama wake mwaka 2012, ambapo Sekretarieti ya TASWA imepewa jukumu la kuratibu tarehe ya mafunzo yote na italitolea taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili Januari mosi, 2012 kwa kuanzia na mafunzo ya Kanda ya Kaskazini, ambayo awali ilikuwa yafanyike Novemba mwaka huu.

(C) MSIBA WA WANAHABARI

TASWA inatoa pole kutokana na misiba ya wanahabari ambao pia ni wanamichezo Halima Mchuka aliyefariki dunia jana na John Ngahyoma aliyefariki dunia leo.

TASWA imeshtushwa taarifa za vifo hivyo na inatoa pole kwa familia za wafiwa, wanahabari na wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wetu. Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wafiwa. Amin

Amir Mhando

Katibu Mkuu TASWA

WADAU WASAIDIE TWIGA STARS


Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia baadaye mwezi ujao.
Mechi hiyo ya kwanza itachezwa ugenini Januari 14 mwakani jijini Windhoek. Timu hiyo ambayo sasa inafanya mazoezi kwa wachezaji kutokea majumbani (off camp) inatarajia kuingia kambini Januari Mosi mwakani.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linahitaji zaidi ya sh. milioni 50 ikiwa ni gharama za safari, kambi na posho kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya mechi hiyo moja tu. Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tunatoa mwito kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi, kampuni na watu binafsi kusaidia ushiriki wa Twiga Stars kwenye mechi hiyo na michuano hiyo kwa ujumla. Twiga Stars kama ilivyo kwa timu nyingine za Taifa ukiondoa Taifa Stars bado haina mdhamini.
WAAMUZI 14 WAPATA BEJI ZA FIFA
Waamuzi 14 wakiwemo wawili wapya wamefanikiwa kupata beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2012 baada ya kufaulu mtihani wa waamuzi uliofanyika mwaka huu na kusimamiwa na shirikisho hilo.
Ferdinand Chacha na Ali Kinduli ambao ni waamuzi wasaidizi ndiyo wapya katika jopo hilo la waamuzi wa FIFA kwa Tanzania. Waamuzi wa kati waliopata tena beji hizo ni Ramadhan Ibada, Orden Mbaga, Israel Mujuni na Sheha Waziri.
Mbali ya Chacha na Kinduli, waamuzi wengine wasaidizi kwa upande wa wanaume ni Josephat Bulali, Hamis Changwalu, Erasmo Clemence, Khamis Maswa na Samuel Mpenzu. Kwa upande wa wanawake, mwamuzi wa kati ni Judith Gamba wakati wasaidizi ni Mwanahija Makame na Saada Tibabimale.
Mwamuzi pekee wa FIFA 2011 ambaye jina lake halikurudi ni John Kanyenye ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi.
TAIFA STARS, DRC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI
Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeomba kucheza mechi moja ya kirafiki na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Mechi hiyo itafanyika Februari 23 mwakani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
DRC inatarajia kuwasili nchini Februari 18 mwaka huu ambapo itaweka kambi yake ya mazoezi hadi Februari 25 mwaka huu kujiandaa kwa mechi yao ya mchujo ya Kombe la Afrika (CAN) dhidi ya Mauritius.
Mechi ya DRC na Mauritius itachezwa Februari 29 mwakani nchini Mauritius. Stars yenyewe itacheza mechi ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya fainali hizo za 2012 zitakazofanyika Afrika Kusini dhidi ya Msumbiji. Mechi hiyo itachezwa Februari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
13 WASHIRIKI KOZI YA UKAMISHNA
Kozi ya siku mbili ya ukamishna iliyomalizika Desemba 29 mwaka huu imeshirikisha washiriki 13 chini ya ukufunzi wa Stanley Lugenge, Leslie Liunda na Sunday Kayuni.
Walioshiriki kozi hiyo ni Abdallah Zungo, Ally Mkomwa, Ally Mozi, Army Sentimea, Awadi Nchimbi, Beatus Manga, Christopher Mpangala, Hakim Byemba, Josephat Magazi, Juma Mgunda, Juma Mpuya, Mugisha Galibona, Ramadhan Mahano, Robert Kalyahe na Said Nassoro.
Wakufunzi wanaendelea kusahihisha mitihani ya washiriki na baada ya kazi hiyo kwa ambao watakuwa wamefanya vizuri majina yao yataingizwa katika orodha ya makamishna kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano mengine yanayosimamiwa moja kwa moja na TFF.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MCHUKA, NGAHYOMA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Halima Mchuka wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na John Ngahyoma wa Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) vilivyotokea Desemba 29 na 30 mwaka huu.
Misiba hiyo ni mikubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Ngahyoma na Mchuka walishafanya kazi na TFF, hivyo mchango wao katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima. Ngahyoma baada ya kumaliza chuo cha uandishi wa habari mwishoni mwa miaka ya 80 alijiunga na Daily News ambapo alianza kwa kuripoti habari za michezo, hasa mpira wa miguu.
Mchuka naye tutamkumbuka kama mtangazaji wa mpira wa miguu ambapo mara ya mwisho tulifanya naye kazi kwa karibu mwaka 2005 ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Habari ya TFF kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika jijini Mwanza.
TFF inatoa pole kwa familia za marehemu Ngahyoma, Mchuka, BBC na TBC na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito.
Mungu aziweke roho za marehemu Ngahyoma na Mchuka mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

AURIC AIR YAJITOSA TABORA LIVINGSTONE MARATHON

Wadhamini waanza kujitosa Tabora Livingstone Marathon

Na mwandishi maalum wa mtandao huu.

KAMPUNI ya Ndege ya Auric Air ya jijini Dar es Salaam imejitosa kusapoti mashindano ya Mbio ya Tabora Livingstone Marathon yanayotarajiwa kufanyika mjini Tabora Machi mwakani.

Mbio hizo za kwanza katika historia ya Mkoa wa Tabora, zitakuwa za Nusu Marathon Kilomita 21 na zile za kujifurahisha za Kilomita 5.

Akikabidhi msaada wa fulana kwa Mratibu wa mbio hizo, Ramadhani Makula jijini Dar es Salaam jana, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Auric Air, Deepesh Gupta, alisema, wamesukumwa kutoa msaada hyo ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu nne chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuendeleza na kuhamasisha michezo hapa nchini.

Gupta alisema, kwa kuzingatia malengo na madhumuni yam bio hizo, wameona japo watoe msaada huo mdogo wa fulana zitakazotumiwa na waratibu na wasimamizi wa mbio hizo ili kusaidia kufanikisha tukio hilo muhimu.

Akipokea msaada huo, Mratibu wa Tabora Livingstone Marathon, Makula, aliishukuru kampuni hiyo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwaunga mkono katika kufanikisha mbio hizo za kihistoria.

Makula alisema, hafla ya uzinduzi rasmi wa mbio hizo ambao utawashirikisha wadau na wafadhili mbalimbali utafanyika jijini Dar es Salaam Januari 10.

Aliwataka vijana wenye vipaji mbalimbali wa Mkoa wa Tabora na maeneo ya jirani kujiandaa na mbio hizo, huku akitoa pongezi kwa ushirikiano unaotolewa na Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora.

JOHN NGAHYOMA AFARIKI DUNIA

Habari za leo Wakuu,
Tumepata taarifa kwamba Mwandishi wa Habari mkongwe nchini ambaye alikuwa akifanya kazi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), John Ngahyoma amefariki dunia leo asubuhi.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata, karibu na nyumbani kwa Marehemu Danny Mwakiteleko. Mwenye taarifa zaidi atufahamishe.
Tunaitakia moyo wa subira na Mungu awafariji wanafamilia wa Ngahyoma katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
RIP John Ngahyoma, umetangulia na wengine tutafuata.


Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors' Forum (TEF),
Dar es Salaam -Tanzania.
Cell: +255 - 715 -339090
+255 - 787 - 675555

RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

mwanahabari Halima Mchuka enzi za uhai wake
Rais Kikwete akisalimiana na wafiwa leo
Rais Kikwete akishiriki kuombea mwili wa mwanahabari Halima Mchuka kabla ya mazishi
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa(picha na Ikulu)


VIONGOZI JIJINI DAR ES SALAAM WAKARIBISHA KIPINDUPINDU?

Hii ni stendi ya kitaifa ya Ubunge jijini Dar es Salaam ikiwa imezungukwa na uchafu kila kona

KWAHERI MWAKA 2011 WENYE MACHUNGU TELE KARIBU MWAKA 2012

Mtoto wa mmiliki wa mtandao huu Fraviana Francis Godwin akiwa amejipumzisha

Mwaka 2011 ulikuwa ni mwaka wenye changamoto tele za kimaisha na ni mwaka ambao watanzania tumejikuta kukiomboleza vifo vya watanzania wenzitu katika ajali ya meli bahari ya Hindi ,ajali za barabarani ,pamoja na maafa ya mvua jijini Dar es Salaam ,tunaamini kuwa yote ni mapenzi na mipango ya mwenyezi Mungu mweweza na mtoaji wa yote .

Hivyo kama ndivyo hatuna budi kumshukuru yeye aliyetuleta duniani japo wenzetu wametangulia sisi tutafuata pia.

Pia tumeshuhudia misukosuko ya kisiasa hapa nchini wapo wanasiasa ambao wamejiweka pazuri kwa mwaka 2011 kwa kutimiza sehemu ya ahadi zao kwa wapiga kura wao na wapo ambao kwa mwaka huu wameonyesha uwezo wao mdogo katika utendaji .

kama hivyo ndivyo kwa wana siasa waliofanya vema tuwapongeze zaidi na waliofanya chini ya kiwango wajipange kwa mwaka 2012 na huku wakitambua miaka mitano si mbali sana.

Katika maandamano kwenye siasa yapo maandamano yenye tija kwa Taifa na yasiyo ya tija kwa Taifa hivyo kwa wana siasa wanapaswa kujiuliza maswali zaidi kwa mwaka 2011walipohamasisha watanzania kuandamana kuna mabadiliko ama hakuna na kama ndivyo hongereni na kama sivyo tutafute njia nyingine za kufikisha ujumbe.

Katika dini pia tumepata kushuhudia mambo mazuri kwa viongozi wetu wa dini na mambo mabaya hivyo lazima viongozi wa dini pia kujitathimini utendaji wetu ni ule wa kumpendeza Mungu ama wa kujipendeza sisi.

Ulizi na usalama kwa taifa letu tumepata kushuhudia utendaji mzuri wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kiasi cha Tanzania kuenedelea kuwa nchi ya amani na kama kuna mapungufu basi ya kibinadamu hatuna budi kusamehe na kujipanga kwa mwaka 2012.

Wakulima wetu pia wameongeza uzalishaji ila masoko bado ni kikwazo huku wananchi wa pembezoni wakiendelea kulia na maisha na kukosa kunufaika na fursa za Taifa hili.

Mdau wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com una lipi la kujivunia kwa mwaka 2011? ama kuna jambo gani la kujutia kwa mwaka 2011 na umejipanga vipi kwa mwaka 2012?

Mtandao huu unapenda kuwashukuru wadau wote kwa kufanikisha mtandao huu kuendelea kupiga hatua na kuzidi kuwa maarufu hapa nchini kwa kuwa na idadi ya wasomai zaidi ya milioni 4 naamini si kazi yangu pekee bali ni kazi yetu sote ,pia nawashukuru wote wanaotangaza biashara zao katika mtandao huu kwa nafasi ya pekee sitaacha kulishukuru kampuni ya FM Abri ,Maziwa ya Asas Iringa ,Famari Store kwa kuwa waanzilishi wa kujingaza katika mtandao huu toka ulipoanzishwa miaka miwili sasa.

Pia napenda kuwashukuru wafanyabiashara wengine na makampuni kwa kuendelea kutumia mtandao huu kutangaza biashara zao kama maji Afrika, Radio Overcomes FM, Ruaha Hilltop Lodge, Naf Blue View Hotel Mtwara na wengine wote ambao wameendelea kujitangaza na mtandao huu ambao unapenda kuwakaribisha wengine pia kujitangaza ili kujulikana zaidi.

Mungu awabariki daima ,kwaheri mwaka 2011 karibu mwaka 2012

BREAKING NEWS......ABIRIA ZAIDI YA 2000 NA JAJI MKUU WA TANZANIA WAKWAMA KWA MASAA ZAIDI YA. MATATU RUVU DARAJANI

Foleni ya mabari ya abiria na mizigo pamoja na magari ya serikali leo baada ya barabara kuu ya Dar -morogoro kufungwa kwa muda kutoka na ajali iliyotokea eneo la Ruvu
Mdau wa mtandao huu kutoka mkoani Morogoro akiwa amekwama pia
Dc Norman Sigala akiwa na mdau wa Morogoro
Hata kupenya kwa Taxi ilikuwa vigumu

Msafara wa jaji mkuu wa Tanzania ukiwa umekwama pia
Hapa gari lake likijaribu kupenya
Jitihada za askari wa kikosi cha usalama barabarani ndizo ziliepusha msongamano huu
Abiria wakitembea kwa miguu kwenda kutafuta chochote cha kutafuna kijijini umbali wa km 7 toka eneo la ajali

Askari wakiendelea na jitihada za kuomba msaada wa kuvutwa kwa lori hilo
Lori lililopata ajali na kuziba barabara hili hapa

Foleni kubwa eneo la Ruvu darajani asubuhi hii kuna ajali mbaya katika eneo Hilo madereva kuchueni tahadhari kubwa katika tukio hili abiria zaidi ya 2000 Pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali ukiwemo mascara wa jaji mkuu wa Tanzania na wakuu wa wilaya na wabunge pia wameonja adha hiyo.

Chanzo cha kukwama kwa abira hao na malori zaidi ya 200 ,mabasi zaidi ya 100 ni katakana na Lori lenye namba za usajili T 293 AFV scania kugongwa na kuziba barabara hiyo .

Mbali ya ABIRIA hao kukwama kutoka saa 12 asubuhi hadi saa 3.45 asubuhi Lori Hilo lililopata ajali usiku wa Leo bado dereva wa gari lenye namba zakibalozi likiwa na namba T 116 CD 1123 alipana uchapwa na abiria hao waliokwamaMA baada ya kugoma kupisha Lori lililofika kuvuta Lori Hilo lililozoba njia.

Barabara hiyo pia hutumiwa abiria wa Dodoma,Kilimanjaro,Arusha,Mwanza,Tanga pia nchi za Zambia,Malawi,Msumbiji ,Kenya na nyingine nyingi.

Ajali hiyo imesababisha foleni kubwa kutoka bongo hadi Chalinze kwa magari kukwama kwenda mikoani wala kuingia jijini Dar

December 29, 2011

KLABU YA SIMBA KUUAGA MWAKA 2011 NA KUUKARIBISHA 2012 KWA KUCHEZA NA MTIBWA SUGARKLABU ya soka ya Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika pambano litakalofanyika katika Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam JIONI ya Jumamosi, Desemba 31 mwaka huu.

Pambano hilo litakuwa la mwisho kwa Simba kucheza jijini Dar es Salaam mwaka huu. Pambano hilo pia litakuwa la mwisho kwa Simba kabla haijakwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopangwa kuanza Januari 2 mwakani.

Simba itaondoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar Januari Mosi mwaka huu (Jumapili).

Pambano dhidi ya Mtibwa litakuwa sehemu ya maandalizi ya michuano ya Mapinduzi, Ligi Kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa ambayo Simba itashiriki mwakani.

Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic, kukaa kwenye benchi la ufundi na kuiongoza klabu yake hiyo ambayo ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

Viingilio katika pambano hilo vitakuwa ni Sh 5,000 kwa VIP na 2,000 kwa majukwaa mengine. Simba imeweka kiingilio hicho ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuhudhuria pambano hilo na kusherehekea kumaliza mwaka salama huku wakiitazama soka la uhakika.

Profesa Cirkovic ameahidi kwamba kwenye pambano hilo atashusha kikosi kamili cha wachezaji wa Simba ili kubaini ni kwa namna gani wachezaji wake wameyaelewa mafunzo yake.

“Nawakaribisha wapenzi na wanachama wa Simba na wapenda soka kwa ujumla waje kwa wingi kuiona Simba ikicheza. Nimesikia kwamba uwanja wa Azam ni mzuri na utaendana na aina ya mchezo ambao Simba itakuwa ikiucheza chini yangu. Nataka kuonyesha soka la asili la Simba,” alisema.

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba Sports Club
0772 01 72 47


HALMASHAURIYA MISUNGWI YAONYESHA UBABE KWA WAZIRI MAGUFULIHALMASHAURI ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imemtunishia 'misuri' Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli(pichani) baada ya uongozi huo kupuuza na kukataa kutekeleza agizo lililotolewa na Waziri huyo, juu ya Kivuko cha Serikali cha Mv. Kigongo.


Uongozi wa halmashauri hiyo umesema, kamwe hautatekeleza agizo la Waziri Magufuli alilolitoa kwa kuitaka halmashauri hiyo ikome mara moja kukusanya ushuru katika kivuko hicho cha Kigongo Ferri, kinachosafirisha abiria ndani ya Ziwa Victoria kutoka Misungwi kwenda Wilayani Sengerema mkoani hapa.


Mwandishi wa mtandao huu, Sitta Tumma anaripoti kutoka Misungwi kuwa; Kauli hiyo ya kupuuza agizo la Waziri Magufuli, imetolewa jana na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo ya Misungwi, Benard Porcarp, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya hospitalini iliyofanyika katika hospitali ya wilaya hiyo.


Desemba 16 mwaka huu, Waziri Magufuli alipokuwa akizindua Kivuko cha Mv. Kome II Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema, aliagiza halmashauri ya wilaya ya Misungwi kuacha mara moja kutoza ushuru kwenye kivuko cha Mv. Kigongo, kwa kile alichodai kwamba kivuko hicho ni cha Serikali kuu.


Waziri Magufuli ambaye alitoa agizo hilo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Mariam Seif Lugailla aliitaka halmashauri hiyo kukoma kukusanya ushuru kivukoni hapo, la sivyo Misungwi wajenge kivuko chao cha kukusanya ushuru huo, na si hicho kilichojengwa na Serikali kuu.


Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa halmashauri ya Misungwi, Waziri Magufuli hana mamlaka yoyote ya kuzuia ukusanywaji wa ushuru katika kivuko hicho, na kwamba kamwe agizo hilo hawatalitekeleza, badala yake wataendelea kutoza ushuru huo kwa ajili ya mapato ya halmashauri."Waziri Magufuli hana mamlaka hayo ya kutuzuia sisi tusikusanye mapato hapo Kigongo Ferri.


Tulimshangaa sana alipotoa agizo lake hilo kwetu."Yeye anasimamia sheria, halafu anakuwa wa kwanza kuvunja sheria. Sisi siyo mbumbumbu, ndiyo maana nasema Misungwi tutaendelea kukusanya ushuru Kigongo Ferri, bila kuogopa agizo la Magufuli", alisema mwenyekiti Porcarp kwa kujiamini mbele ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Xavier Tilweselekwa.


Alisema, halmashauri hiyo inatumia sheria GN 198 ya mwaka 2002 katika kukusanya ushuru kivukoni hapo, ndiyo maana wana jeuri ya kukataa agizo la kiongozi yeyote

KLABU YA SIMBA YAMLILIA MTANGAZAJI WA MICHEZO HALIMA MCHUKA WA TBC

Rais Jakaya kikwete akimjulia hali mtangazaji wa TBC michezo Halima Mchuka wakati alipolazwa kabla ya kifo chake


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KLABU ya soka ya Simba ya Dar es Salaam inatoa salamu za rambirambi kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na tasnia ya habari kwa ujumla kufuatia kifo cha aliyekuwa mtangazaji maarufu wa michezo nchini, Halima Mchuka, aliyefariki usiku wa kuamkia leo


Jina la Halima Mchuka ni maarufu kwa wanamichezo si Tanzania pekee bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati kwa vile yeye aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutangaza mchezo wa soka redioni.


Katika enzi za uhai wake, Halima alifanya kazi kwa karibu na klabu ya Simba, akitembelea ofisi za makao makuu mtaa wa Msimbazi kwa ajili ya kutafuta taarifa mbalimbali za kimichezo.


Simba itaukumbuka daima mchango wa Halima Mchuka kama mwanahabari, mwanamichezo na mtu ambaye alivutia wanawake wengi kupenda mchezo wa soka na pia kazi ya utangazaji na uandishi wa habari kwa ujumla.


Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.


Imetolewa na


Ezekiel Kamwaga


Ofisa Habari


Simba Sports Club


0772 01 72 47

TFF YATOA RAMBI RAMBI KIFO CHA MCHEZAJI RASHID MOYO

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Rashid Moyo kilichotokea usiku wa Desemba 25 mwaka huu kwao Msambweni, Tanga.

Moyo ambaye aliichezea timu ya Taifa kwenye miaka ya 70 alizikwa Desemba 26 mwaka huu kwenye makaburi ya Mabawa mkoani Tanga. Pia alikuwa mchezaji wa timu ya Coastal Union ya mkoa wa Tanga.

Msiba huo ni pigo kwa familia ya Moyo, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa wakati akiwa mchezaji.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Moyo, Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA) na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.

Mungu aiweke roho ya marehemu Rashid Moyo mahali pema peponi. Amina


Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MBUNGE FILIKUNJOMBE AMWAGA MISAADA KWA WAGONJWA NA HOSPITALI YA LUDEWAMbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (pichani anayembusu mgonjwa ) ameendelea kuteta kwa vitendo katika kuwatumikia wapiga kura wake ,baada ya safari hii kuamua kuwatembelea wagonjwa wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa na kuwapa misaada mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukabidhi misaada ya mashuka ,magodoro ,kandambili na mablanketi kwa uongozi wa Hospitali hiyo .

Mbunge huyo alikabidhi msaada huyo pamoja na fedha za matumizi kwa wagonjwa hao kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Mwaka mpya.

Akikabidhi msaada huo kwa wagonjwa na mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa Happines Ndosa ,mbunge Filikunjombe alisema kuwa amelazimika kuwafariji wagonjwa hao kama njia ya kuwakumbuka na kuwapa faraja zaidi.


Alisema kuwa misaada hiyo ambayo imeikabidhi kwa wagonjwa na Hospitali hiyo inagharimu zaidi ya shilingi milioni 2 na kuwa amefanya hivyo ili kuwafanya wagonjwa hao kula sikukuu kwa faraja zaidi.

HUU NI MSIMU WA SIKU KUU KARIBUNI WAGENI

NAF BLUE VIEW HOTEL MTWARA

Karibuni wageni Manispaa ya Mtwara /Mikindani mkoani Mtwara kumbuka uwapo Manispaa ya Mtwara usisumbuke kuuliza Hotel nzuri ya kujipumzisha uliza NAF BLUE VIEW ni Hotel ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora ipo mtaa wa Sinani Manispa ya Mtwara jirani kabisa na stendi kuu ya mkoa wa Mtwara
Vyumba ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW,Mtwara /Mikindani
Kila chumba kuna mawasiliano ya kutosha kama simu , TV n.k
NAF BLUE VIEW inaongoza kwa usafiri na uwapo ndani ya Hotel utafurahia kufika Mtwara
Vyoo na bafu za kisasa zaidi uwapo ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW Mtwara
Mazingira yanapendeza zaidi ndani ya Hotel ya NAF BLUE VIEW Mtwara mkoani Lindi
Vitanda vyetu ni vya kisasa zaidi na utapenda kuendelea kutembelea Mtwara kila wakati iwapo utalala ndani ya Hotel yetu ya NAF BLUE VIEW
Hii ndio HOTEL YA NAF BLUE VIEW Mtwara

IPO JIRANI NA STAND KUU YA MKOA WA MTWARA

NAF BLUE VIEW HOTEL

KWA MAWASILIANO ZAIDI

P. o Box 179 Mtwara

Tel. 0232334465 Fax 0232334466

mobile;0776467066/ 0683467066

Email; nafblueviewhotel@gmail.com

KARIBUNI WAGENI MANISPAA YA MTWARA ,KARIBUNI SANA NAF BLUE VIEW HOTEL