Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2011

BAADA YA RAIS KIKWETE KUTIA SAINI MUSWAADA WA KATABA KUWA SHERIA ,CHADEMA WAIBUKA UPYA

Mbunge John Mnyika

Chadema waweka msimamo wao kuhusi Rais kusaini muswada wa katiba kuwa sheria

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Neema Kishebuka anaripoti kuwa ,Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka bayana msimamo wake kuhusina na muswada ambao umesaini wa Rais kuwa sheria ambayo itaanza kutumika Desemba Mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama Hicho John Mnyika amesema kuwa pamoja na Rais kutia saini muswada huo kuwa sheria bado chama chake kiko katika msimamo huo huo kuwa hakitashiriki katika mchakato wowote wa kuhusian na katiba mpya hadi pale serikali itakapo kubali kurekebisha masuala kadhaa ambayo yameonekana kuwa mabovu ndani ya muswada wa sheria Hiyo.

Mnyika amewatoa hofu watanzania wote na kusema kuwa wao kama kamati iliyoundwa kutoka ndani ya chama Hicho walikwenda kumuoan Rais ili kumshauri asisaini muswada wa heria Hiyo hadi pale utakapo fanyia warekebisho ushauri ambao Rais kikwete amekiuka na kuusaini na badala yke kudai kuwa marekebisho yatafanyiwa kazi .

‘’ Watanzania watuelewe kuwa hatujakubalian na Rais Jk na serikali yake kuwa apitishwa Muswada wa Sheria ya katiba Mpya sisi tulimfuata na mapendekezo yetu tuliyaweka katika waraka tuliompatia kuwa msimamo wetu upo pale pale kwamba asisaini , na kama atasaini basi sisi hatupo tayari kushiriki kwa njia yoyote kwani tupo kwa ajili ya haki za watanzania hatuwezi kukubali katiba Mbovu ‘’ alisema Mnyika

Hata Hivyo Mnyika ameongeza kusema kuwa pamoja na kuwa wao walikubaliana kuboreshwa kwa maeneo ambayo yanaonyesha hayana faida kwa wananchi yaboreshwe ili kuleta katiba iliyo Bora na kwamba hata saini walizowekeana baina yao na serikali si Rais asaini muswada huo wala si Rais asisaini muswada Huo, bali yafanyike maboresho.

Amesema wao kama chadema wamesitisha maandamano ila amewataka viongozi wote wa chama Hicho kuelekea kwa wananchi kuwaeleza muswada aliosaini Rais ulivyo Mbovu.

Ameleeni baadhi ya watu wanaodhani Chadema imenunuliwa na ccm na kusema kuwa hawaungi mkono sheria Hiyo inayotarajiwa kutumika wakati wowote kuanzia sasa na kwamba rais anayo nafasi ya kuzuia sheria hiyo isianze kutumika kwa manufaa ya watanzania ili kuleta katiba Boiiora na si Bora katiba.

Hivi karibuni kamati ndogo ya watu saba iliyoundwa na chadema ilikutana na kufanya mazungumzo yaliyodumu kwa takribani siku mbili , huku chadema wakipeleka mapendekezo yao kwa Rais Kikwete ili kuhusian na muswada wa sheria ya mchakato wa katiba mpya ambapo mnyika kwa niaba ya CHADEMA Na Enanuel Nchimbi kwa niaba ya serikali wote kwa pamoja walitia saini makubaliano ya kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya serika,li na wadau mbali mbali juu ya kuboresha sheria Hiyo kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa sheria mpya.

Kingine walichokubaliana na chadema na serikali ya Jk kuwepo kwa haja ya sheria Hiyo kuendelea kuboreshwa pamoja na kwamba imepitishwa na Bunge ili kujenga hali ya kuaminiana na mwafaka wa kitaifa.

Hata Hivyo kurugenzi ya mawasilino ya Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais Jk amesaini muswada wa sheria ya mabadiriko la katiba 2011.

SAKATA LA VURUGU ZA MBEYA ,MEYA ARUKA KIMANGA KUCHOCHEA VURUGU ZA WAMACHINGA MBEYA.

.Ashangaa chama chake kumgeuza mnyamwezi wa mizigo.

MEYA wa Jiji la Mbeya,Athanas Kapunga,ameibuka na kuwatupia lawama viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani hapa,kuwa wamekiuka taratibu na utamaduni wa chama, kwa kumhukumu bila kumpatia muda wa kujitetea,kufuatia chama hicho kutoa tamko linalowataja viopngozi waandamizi wa halmashauri hiyo kuwa ndio chanzo cha vurugu za wamachinga na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 17 kujeruhiwa kwa risasi na Mabomu ya machozi.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa meya huyo Amesema badala yake viongozi hao wa CCM,ambaye yeye pamoja na nafasi yake ya umeya ni katibu mwenezi na Itikadi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya Mbeya Mjini,walisukumwa zaidi na hisia binafsi za kisiasa na kuamua kumuhukumu bila kuwapatia nafasi.

Kapunga alitoa tamko hilo jana Jijini hapa,katika mkutano wa waandishi alioutisha kwa lengo la kujibu matamnko na tuhuma mbalimbali zilizotolewa na taasisi mbalimbali,ikiwemo CCM kulaani vurugu za wamachinga na polisi zilizoibuka Novemba 11 hadi 12 katika eneo la Mwanjelwa Jijini hapa.

Wiki mbili zilizopita halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mbeya ilikutana kwa dharura na kutoa tamko kali la kulaani vurugu zilizoibuka na bila kificho iliwatupia lawama viongozi waandamizi wa Halmashauri ya Jiji kuwa ndio chanzo cha vurugu kwa kuwalazimisha wamachinga kuondoka eneo hilo la Mwanjelwa bila kuwapa eneo mbadala.

Tamko hilo pia liliwataka viongozi hao wa Jiji kuhakikisha wanawadhibiti mgambo wa wake kwa kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa wafanyabiashara hao kutokana na kuendesha uparesheni zisizo na mpangilio huku wakipora mali na bidhaa za wafanyabiashara hao.

Kapunga alisema “ mimi hapa Halmashauri ndio Kamisaa wa chama changu,wasingepaswa kunilaumu bali walitakiwa kuniuliza ,…CCM ni vikao ingeniita ,halmashauri kuu ni chombo kikubwa Mkuu wa wilaya ni mjumbe angeniita tu,Mkuu wa mkoa ni mjumbe na ndio kada mkuu wa chama alishatoa tamko juu ya kilichotokea,yeye alitosha kutubeba wote si wengine kuibuka kwa hisia zao tu ” .

Hivyo alisema anamini kuwa matamko hayo yalikuwa yawatu binafsi ndani ya chama chake kwa kuwa hayakuzingatia utaratibu wa chama wa kutoa adhabu bila kumpatia mtuhumiwa nafasi ya kujitetea.

Akiendelea kujibu maswali ya waandishi wa habari Meya Kapunga alishikwa na kigugumizi kwa kushindwa kumtaja mtu aliyetoa amri ya mgambo kwenda kufanya oparesheni ya kuwaondoa wamachinga ilihali tayari kulikuwa na mazungumzo baina yao na viongozi wa wamachinga.

“Waandishi wa habari kama hamjui mipaka ya utendaji ndani ya halmashauri ngoja niwaelimishe mimi kama Meya huwa natoa maelekezo tu kwa Mkurugenzi baada ya maamuzi kutoka ndani ya vikao vya baraza la madiwanisiwezi kwenda kuamuru mgambo wakafanye vurugu ” alisema .

Hata hivyo alitolea ufafanuzi kuwa maamuzi ya wamachinga kuondolewa katika eneo hilo la Mwanjelwa, lilifikiwa kwenye vikao vya baraza la madiwani,ambapo madiwani hao walipendekeza maeneo ya kuhamia wamachinga hao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Musa Mapunda,alipotakiwa kutaja kiongozi aliyeamuru mgambo hao kuendesha oparesheni ya kuwatoa machinga wakati mazungumzo yalikuwa mezani kati ya viongozi wa wafanyabiashara hao,alisema mgambo hao hawakutumwa bali walikuwa kwenye utekelezaji wa kawaida wa majukumu yao .

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA EAC


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilish Tanzania katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika mjini Bujumbura, Burundi Novemba 29 - 30, 2011. Makamu wa Rais alifika mjini hapa jana ambapo aliwakuta Mawaziri kadhaa wa Tanzania waliotangulia kuhudhuria mikutano ya ngazi za Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Manaibu Waziri Deo Mfutakamba, Lazaro Nyalandu na Adam Malima.

Katika mikutano ya awali katika ngazi ya Mawaziri, Tanzania ilijumuika na nchi nyingine za ukanda huu kutazama namna ya kusaini Protokali ya Ulinzi wa pamoja, protokali inayotaka nchi wanachama wa Jumuiya hii kushirikiana kijeshi pale inapokubalika ama inapoonekana kufaa baada ya nchi mwanachama kuwa katika hatari ya vita.

Hata hivyo mjadala huu ulikuwa ni mkali huku Tanzania ikitaka protokali hii isainiwe mara tu pale itakapokuwa na kipengele kinachobainisha kuwa, nchi wanachama watatakiwa kushirikiana ama kusaidiana baada ya kila nchi mwanachama kupima aina ya hatari na mchango wa hatari hiyo kwa nchi mshiriki ambaye ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pia, mkutano huu ulikuwa na kazi ya kupitisha maelekezo ya wataalam yanayolenga kuongeza kasi ya kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki. Msimamo wa Tanzania katika agenda hii ni kuwa zoezi hili halijafikia muda muafaka na kwamba kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika kabla ya Jumuiya hii kuunda shirikisho.

Hata hivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki zimekuwa zikishirikiana kwa lengo la kuongeza kasi na kuishinikiza Tanzania kukubali kuundwa kwa shirikisho, jambo ambalo linapingana na taratibu na kanuni za Jumuiya hii, zinazotokana maamuzi yote yafanyike kwa makubaliano yanayotoka kwa wananchi wa jumuiya hii na kwa kila taifa husika. Kwa mujibu wa ujumbe wa Tanzania, suala la shirikisho lilipingwa katika kamati ya Wangwe na hadi wakati Tume hiyo ilipokusanya maoni, hadi sasa hakujawa na tofauti ya mtazamo.

Tanzania inahitaji kufanyika kwanza maafikiano katika soko la pamoja na mataifa ya jumuiya hii kutazama namna yatakavyoweza kunufaika kabla ya kukimbilia ushirikiano wa kisiasa ambao kama utakimbiliwa bila mazingira kujengwa, ni rahisi kwa jumuiya hii kuvunjika kama ilivyowahi kufanyika huko nyuma.

Makamu wa Rais pia alikuwa na kazi ya kufunga mkutano wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukijadili mahusiano na uendelezaji wa Ukanda za Ziwa Tanganyika ambapo katika mkutano huo, alifafanua namna Tanzania inavyoshiriki kwa ukamilifu kuunganisha mikoa yake na nchi za mipakani hasa katika ujenzi wa barabara za lami, na namna ushirikiano kati ya nchi za SADC, EAC na COMESA unavyolenga kukuza biashara sambmba na uchumi kwa nchi wanachama.

Makamu wa Rais anarejea nyumbani kesho Desemba Mosi ambapo atakuwa na kazi ya ufunguzi wa barabara jijini Dar es Salaam Desemba pili, 2011.

Imetolewa na: Idara ya Habari Ofisi ya Makamu wa Rais

Novemba 30, 2011

MDAHALO WA KATIBA IRINGA MOTO,WATAKA WABUNGE WASIWE MAWAZIRI AMA WAKUU WA MIKOA

Mwanahabari Mawazo Marembeka wa Star Tv akichukua matukio katika madahalo huo

Mwenyekiti wa Asasi za kiraia Iringa Alexzander Kisinini akifunga mdahalo huo
Mratibu wa midahalo hii mkoa wa Iringa Raphael Mtitu kushoto akifanya maandalizi ya mdahalo leo na timu yake
Watoa mada mbali mbali juu ya katiba wakisikiliza michango ya wananchi wa jimbo la Iringa mjini

WANANCHI jimbo la Iringa mjini wajitokeza kwa wingi katika madahalo wa katiba washauri katiba mpya ijayo wabunge wasiteuliwe kuwa mawaziri ama wakuu wa mikoa.
Wakichangia katika madahalo huo wa katiba ulioratibiwa na Mwavuli wa Mashirika Yasio ya Kiserikali Mkoani Iringa (Iciso) kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society na kufanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa .

Mdahalo ambalo ulikuwa ukirushwa moja kwa moja na kituo cha Radio Overcomers Fm na mtandao huu wananchi hao walisema kuwa pamoja na kuwakatiba ya sasa ambayo inamruhusu Rais kuwateua wabunge kuwa mawaziri ama wakuu wa mikoa katika katiba ijayo ni vema utaratibu huo ukifutwa ili wabunge wabaki kuwatumikia wananchi wa jimbo kama walivyoomba.
Katika madhalo huo ulioanyesha kuvunja rekodi kwa kuhudhuriwa na makundi yote likiwemo la vijana na wazee ,wasomi wa vyuo na sekondarti pamoja na walemavu , wananchi hao wametaka Katiba Mpya iwe na sheria inayoruhusu uundwaji wa serikali mseto.

Pia walisema ni vema kwa Katiba Mpya kukawepo na sheria ya ukomo wa ubunge ili kutoa nafasi kwa watanzani wengi wenye uwezo kuwawakilisha wanannchi b kuongoza nafasi hiyo na pia wabunge kubaki kuwa wawakilisha wa wananchi jimboni badala ya kupewa majukumu mengine ya kimkoa ama kitaifa .

Walisema kama ilivyo kwa Rais kuwa na kikomo cha vipindi viwili hata wabunge na madiwani nao wawe na kikomo cha vipindi viwili pekee isiwe zaidi ya hapo.


Akichangia kuhusu uundwaji wa serikali ya mseto Daudi Mwangosi alisema mgombea urais anayeshika nafasi ya pili, Katiba itamke wazi kwamba ndiye atakeyakuwa Waziri Mkuu wa nchi.
Hoja nyingine zilizotolewa katika mdahalo ni pamoja na ile ya kupunguza madaraka ya Rais likiwemo suala la uteuzi wa watendaji katika mihimili mingine.
Hakim Mstaafu wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Angundile Nyingi alisema mihimi mitatu ya nchi haijitegemei kwasababu kwa uteuzi wa watendaji wa mihimili mingine umekuwa ukifanywa na kiongozi wa muhimili mwingine ambao ni serikali.

Aidha Nyingi alisema katika Katiba Mpya lazima kuwepo na chombo maalumu kitakachokuwa kinafanya kazi ya kumteua Jaji Mkuu na majaji wengine ili ile dhana ya mihimili ya nchi kujitegemea iwe na maana.

Akizungumza baada ya mdahalo huo mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa pamoja na serikali awali kuzuia kufanyika kwa midahalo hiyo ila kwa sasa kaimu mkuu wa wilaya ya Iringa Evarita Kalalu ameruhusu midahalo hiyo kufanyika na kuwa kesho kutwa jumapili mdahalo kama huo utaendelea katika jimbo la Kalenga kwenye ukumbi wa karakana Tanangozi na mdahalo utakaofuata utakuwa jimbo la Isimani na mwisho itakuwa ni jimbo la Kilolo.

BREAKINGEWS....MUNGU YU MWEMA , JERY MURO HURU .....

Hakika Mungu mkubwa amesikia maombi yetu ni ,aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.

'LIVE' MDAHALO WA KATIBA IRINGA UMENZA UKUMBI WA MWEMBETOGWA SEKONDARI

Wananchi wa jimbo la Iringa wakiwa katika mdahalo wa katiba
Diwani wa kata ya Makongoni Mhe.Tenga akiwa katika mdahalo huo
Wanachama wa vyama vya Chadema na CCM na vyama mbali mbali na wasio na vyama wapamba mdahalo wa katiba Iringa

Mdahalo wa katiba umeanza katika ukumbi wa sekondari ya Mwembetogwa mjini Iringa sasa wananchi wafurika.

Mdahalo huo ulioratibiwa na Mwavuli wa Mashirika Yasio ya Kiserikali Mkoani Iringa (Iciso) kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society ulifanyika jana katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa ikiwa ni siku chache baada ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Evarista Kalalu kuizuia asasi hiyo kufanya midahalo hiyo.
Alikuwa Stani Chilowoko mwanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Mwembetogwa aliyeibua hoja hiyo iliyoungwa mkono wa wananchi wengi walioshiriki mdahalo huo.
Chilowoko alisema litakuwa jambo la kushangaza kama katika Katiba Mpya hakutakuwa na sheria inayoweka ukomo wa ubunge ili kuongeza uwajibikaji kwa wanaochaguliwa kushika nafasi hiyo nyeti.
Kuhusu sheria ya uundwaji wa serikali ya mseto, Daudi Mwangosi alisema mgombea urais anayeshika nafasi ya pili, Katiba itamke wazi kwamba ndiye atakeyakuwa Waziri Mkuu wa nchi.
Hoja nyingine zilizotolewa katika mdahalo ni pamoja na ile ya kupunguza madaraka ya Rais likiwemo suala la uteuzi wa watendaji katika mihimili mingine.
Hakim Mstaafu wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Angundile Nyingi alisema mihimi mitatu ya nchi haijitegemei kwasababu kwa uteuzi wa watendaji wa mihimili mingine umekuwa ukifanywa na kiongozi wa muhimili mwingine ambao ni serikali.

November 29, 2011

WANANCHI JIMBO LA IRINGA MJINI KUSHIRIKI MDAHALO WA KATIBA BILA MBUNGE WAO

Wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambalo ni jimbo pekee kwa mkoa wa Iringa kuongozwa na upinzani kesho wanataraji kushiriki katika mdahalo wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembdetogwa bila ya ushiriki wa mbunge wao Mchungaji Peter Msigwa (chadema).

Mbunge Msigwa ambaye alitegemewa kuwa chachu kubwa katika mdahalo huo hataweza kufika katika madahalo huo kutokana na kuwa nje ya jimbo la Iringa mjini kwa shughuli za bunge.

Mchungaji Msigwa ameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa alipenda sana kufika katika mdahalo huo ila ameshindwa kutokana na kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa japo amewaomba wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini kujitokeza katika madahalo huo ili kuifahamu vema katiba .

Mdahalo huo unategemea pia kuwashirikisha wananchi zaidi ya 10000 wa jimbo la Iringa mjini kutoka vyama vyote na wale wasio na vyama vya siasa mdahalo unaotegemewa kuanza majira ya saa 4 asubuhi katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini hapa.

Mratibu wa midahalo hiyo kutoka asasi za kirai Tanzania Raphael Mtitu ambaye ni katibu wa ICiso ambao ni waratibu wa mdahalo huo amewataka wananchi wote kufika bila kukosa katika mdahalo huo utakaorushwa katika mtandao huu LIVE na radio Overcomers Fm 98.6 .

Mbali ya mdahalo huo mjini Iringa mdahalo mwingine utafanyika kesho kutwa Alhamisi katika mji wa Ilula wilaya ya Kilolo baada ya ule ya Luganga wilayani Kilolo kufutwa .

YAMETIMIA RAIS JAKAYA KIKWETE ATIA SAHII MUSWAADA WA KATIBA MPYA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari
ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge
kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu
katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na
Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi
Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria
hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
*DAR ES SALAAM*.
29 Novemba, 2011

SIMANZI YATANDA IRINGA KIFO CHA VERONICA MTATIFIKOLO AMETUTOKA

Taarifa zilizotua katika mtandao huu jioni hii kutoka katika Manispaa ya Iringa zinadai kuwa mfanyakazi wa Saloon iliyopo eneo la ukumbi wa IDYDC Veronica Mtatifikolo (pichani) amefariki dunia ghafla baada ya kuugua kichwa.

Kifo cha Veronica kimewaliza wengi mjini Iringa kutoka na ucheshi na kujichanganya katika shughuli mbali mbali ziwe za shida na faraja katika mji wa Iringa .

Taarifa za mazishi yake zitakujia katika mtandao huu endelea kutembelea

BREAKING NEWSSsssss WATU 34 WALAZWA IRINGA KWA KUNYWA TOGWA YENYE SUMU

Watu waliokunywa togwa wakati wa sherehe wakiwa wamelazwa hospital wakipatiwa matibabu

WATU 34 wa kijiji cha mtitu wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwemo familia moja ya watu sita wamenusurika kifo na kulazwa katika hospital teule ya wilaya ya Iringa (Hospital ya Ipamba) baada ya kunywa togwa katika sherehe ya kipaimara inayosadikika kuwa na sumu.

Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika kijiji hicho cha Mtitu wilaya ya Kilolo wakati watu hao walipofika kusherekea sherehe ya kipaimara cha mtoto Hotmary Mpogole na kupewa kinywaji hicho cha asili kilichotengenezwa kwa unga wa nafaka ya mahindi (togwa)

Akielezea juu ya tukio mhanga wa tukio hilo Geofrey Chavala alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na rafiki yake wakati akitokea msibani kuwa waelekee katika nyumba hiyo kwa ajili ya kula wali wa sherehe na baada ya kufika walipewa chakula hicho na baada ya hapo walipewa togwa kama kisushio .

Hata hivyo alisema wakati akiendelea kunywa alibaini radha tofauti na ile ambayo amepata kuizoea kwa kinywaji kama hicho na hivyo kuonyesha kusitasita katika kuendelea kunywa japo alijitahidi kunywa hadi anamaliza lita moja peke yake.

Alisema baada ya kumaliza hali ya hewa tumboni ilibadilika na kujikuta akianza kutapika na kuhara damu hali iliyopelekea kurudi nyumbani na baada ya kufika huo alikutana na bibi yake na kuelezwa kuwa kama amekunywa togwa wenzake wanakusanywa kwa ajili ya kwenda Hospital ndipo alipoungana na wenzake hao.


Fedelika Chaula (40) ambaye ni mzazi wa watoto waliokuwa wakifanyiwa sherehe hiyo ya Kipaimara alisema kuwa aliandaa sherehe hiyo kwa ajili ya kuwapongeza watoto wake wawili na kuandaa togwa hiyo kwa ajili ya kunywaji kwa watu walioalikwa katika sherehe hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa mahindi yaliyotumika kwa ajili ya kuandaa togwa hiyo ni mahindi ambayo wamekuwa wakiyatumia siku zote kwa ajili ya chakula na kuwa anashangazwa na kutumia nafaka hiyo kwa kutengeneza togwa na kupatwa na madhara hayo.

Alisema kuwa watoto wake wanne wamelazwa katika hospital hiyo pamoja na yeye mwenyewe kwa kunywa togwa hiyo .

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mtitu Beatus Kivamba akielezea tukio hilo alisema kuwa awali alikutana na watu wawili wakitoka katika sherehe hiyo huku wakitapika na kuraha kutona na kunywa togwa hiyo na baada ya kuwasiliana na muunguzi wa kituo cha afya Mtitu ndipo alipomthibitishia kupokea wagonjwa zaidi wa tukio hilo .

Alisema kutokana na tukio hilo alilazimika kuomba msaada kwa gari kwa Paroko wa Mtitu ambaye alitoa usafiri wa Lori na kuwachukua wagonjwa wote 34 na kuwafikisha katika Hospital hiyo ya Ipamba kwa matibabu.


Muuguzi mkuu wa Hospital hiyo ya Ipamba Sr. Julieta Mzena aliwataja waliofikishwa hospital hapo na kulazwa kuwa ni pamoja na watoto zaidi ya watano ambao ni wanafunzi na watu wazima wanaume na wanawake.

Aliwataja wahanga hao ambao wamelazwa kuwa ni pamoja na Yudita Ndongoro , Onolata Mhangara, Otineli Mpogole, Sekela Mbilingi, Jafarini Mhulila, Faines Mhulila, Agineli Luvinga, Sofia Mhulila, KIlelia CHongolo, Frolida Mgaya, Geofrey Chawala, Vero Kasuga, Meshack Chaula, Nemia Chaula, Baraka Kivale, Edison Kivale, MUstaphar Mhulila, na Gelion Mpogole.

Wengine ni Chelelina Chongolo , Raheli Mgogolo ,Kanisia Chongolo, Diana Chongolo , Chadeta Mlimakizi, Zaina Mpagama, Bile Mtono , Setty Kilave, Nesta Mwofuga,Manwela Mhagala ,Federika Chaula na mtoto Hotmery Mpogole mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi mtitu ambaye ndiye alikuwa ameandaliwa sherehe hiyo ya kipaimara.

Alisema kuwa hali za wagonjwa hao zinaendelea vizuri na kuwa tatizo lao inaonekana kula chakula chenye sumu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alisema kuwa yupo nje ya ofisi na kikazi na kuwa bado hajapata tarifa na kuahidi kufuatilia zaidi.

NGORONGORO HEROES KWENDA BOTSWANA KESHO

Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na viongozi watano kinatarajia kuondoka kesho (novemba 30 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kwenda Gaborone, Botswana.
Ngorongoro Heroes itaondoka saa 20.20 usiku kupitia Johannesburg, Afrika Kusini kwenda huko kushiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano hiyo itafanyika kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama wa COSAFA na Tanzania inayoshiriki kama mwalikwa.
Wachezaji watakaoondoka ni Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga).
Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars).
Ngorongoro Heroes iko kundi C pamoja na Zambia, Afrika Kusini na Mauritius na itacheza mechi yake ya kwanza Desemba 2 mwaka huu dhidi ya Zambia. Mechi ya pili itakuwa Desemba 4 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini wakati ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi ni dhidi ya Mauritius itakayochezwa Desemba 6 mwaka huu.
Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou. Wengine katika msafara huo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kocha Msaidizi Mohamed Rishard, Daktari wa timu Dk. Joakim Mshanga na kocha wa makipa Peter Manyika.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

LOWASSA ;'MUNGU YU PAMOJA NAMI NITAYASHINDA MAJARIBU'

Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kati Mch, Eliufoo Sima akitoa mahubiri katika kanisa hilo usharika wa Amani Sabasaba mjini Singida wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ulioendeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa
Askofu wa KKKT Mchungaji Eliufoo Sima akipokea kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu kutoka kwa Mhe.Lowasa kama mchango wake katika kufanikisha harambee ya ujenzi wa kanisa hilo ( PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO)

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Lowasa amesema kuwa pamoja na kusemwa maneno mengi sana kwenye vyombo vya habari juu yake lakini anamwami mungu kuwa anampigania kila kukicha.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Singida Hillary Shoo anaripoti kuwa Lowasa ameyasema hayo leo mjini Singida wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT usharika wa Amani sabasaba mjini Singida.

“Wale wanaofuatilia siasa za nchi yetu kuna maneno mengi saana lakini bwana ni mwema na mwaminifu hatimae tumeshinda”.Alisema.

Alisema mara baada ya taarifa hizo siku moja akiwa nyumbani kwake na mkewe huku wakiangalia TV na kutaka kujua magazeti yanasemaje asubuhi kulikuwa na maneno mengi yaliyosemwa ya hovyo hovyo juu yake mengine walishindwa kuyasoma.

“Lakini mke wangu alienda chumba cha pili na kuchukua biblia na kunifungulia maneno ya bibilia kitabu cha Isaya 41:10, usiogope kwa maana mimi niko pamoja nawe tusifadhaike kwa maana mimi ni mungu wako nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam nitakushika mkono wa kuume wa haki yangu.” Alisema na kuongeza kwa maneno hayo niliendelea sana lakini baba askofu nisamehe nichukue hadhara hii kuwashukuru watu wengi sana walioniombea na hatimae kufika hapa nilipo.

“Wapo waislamu na mashekhe walifanya dua kwa niaba yangu, nawashukuru sana, pia wapo wakristo walioniombea nao nawashukuru sana, mapadri, mashemasi na watawa, wachungaji na wainjilisti wa madhehebu yote, kwaya bmbalimbali na waimbaji wa nyimbo za injili, wanamaombi wote, wanamtandao wao wa ajabu una nguvu kweli kweli na maaskofu wa makanisa yote ya kikristo pia nawashukuru sana.” Alisema Lowasa.

Aidha Mhe Lowasa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli alisema kuwa maneno mengi ya kisiasa yalisemwa juu yake lakini kimsingi hayakuwa ya kweli ya ukweli na siasa zinazoendelea kwa sasa ni za kuchafuana.

Pia Lowasa alinukuu maandiko mengine ambayo aliyasoma kutoka kitabu kitakatifu cha Warumi ambayo aliyasoma mwenyewe.
“ Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu hataihuisha miili yemu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anakaa ndani yenu” alinukuu Lowasa.

Aidha alisema kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo amekumbana nayo amekuwa akimwona mungu akimtetea na utetezi huo ameupata kutoka kwa mungu, kutokana na maombi ya watakatifu kutoka dini mbalimbali ambao wako pamoja.

Wale wote ambao wamaamini kuwa nafanya kazi kwa kusimamia haki ya mungu na kazi zote kwa ujumla waliniombea usiku na mchana na kwa hilo mungu kawasikia na kanifanya kuendelea tofauti na uchafu ambao mimekuwa nikibambikizwa na siasa za kuchafuana.

Hata hivyo Lowasa alidai kuwa kama kiongozi hana mungu ndani yake hawezi kuhimili mikiki ya kisiasa kwani kinachotakiwa ni kumwomba mungu ili aweze kutetea kazi zinazofanywa na mtu mwenye haki.

“Nimekuja kwenye harambee sio kupiga maneno ya kisiasa, nilimwambia baba askofu tuna utamaduni wa kualikwa haramabee nyingi sana , lakini kabla ya kukubali unauliza kwamba hao unaoshiriki nao wamefanya nini, nyie mmefanya kazi kubwa sana nawashukuru na nafurahi kwenye harambee hii.” Alisistiza na kuongeza.

“Kwa sababu ni njia mojawapo ya kuthibitisha kwamba wananchi wanaweza kufanya mambo yao kwani kanisa kama hili miaka ya nyuma lingeweza kujengwa na wafadhili wa nje lakini leo limejengwa na wananchi wenyewe.

Mapema askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya kati Mchungaji,Eliufoo Sima anaamini utulivu wa viongozi wa nchi hii ni dhahiri kwamba Taifa hili kwa jinsi ya utamaduni na mapokeo yake , na mambo magumu yanayotokea siku hadi siku, litafanikiwa kutengeneza njia thabiti ya mafanikio ya watu wake.

Askofu Sima alisema kumekuwepo na madai mengi kuwa nchi yetu ni maskini lakini angependa viongozi kuyashughulikia kwa umakini mkubwa ili kuondoa manung’uniko miongoni mwao ili yasiharibu tabia njema ya baadhi yao .

Hataa hivyo Askofu Sima alimwagia sifa Mhe.Lowasa na kusema kuwa ni tofauti na viongozi wengine ambao unaweza kuwatafuta kwenye simu kwa muda mwingi na wakawa hawapatikani.

“Kwa kweli wewe ni kiongozi wa pekee,tofauti na wengine,unaweza ukmtafuta kwenye simu hata mara tano na hapatikani,lakini wewe kila ninapokupigia unapokea simu yangu,na hata katika harembee hii nilipokupigia nikakuomba uje Singida ukasema upo njiani unaenda Dodoma,”“Lakini na mimi nikakwambia nipo njiani naenda Morogoro,ukasema basi tukutane njiani,mtu mkubwa kama wewe kukutana njiani hiyo ni ajabu.”alisema AskofuKatika harambee hiyo Mhe.Lowasa amechangia kiasi cha shilingi milioni kumi ambapo makusanyo yote yaliyopatikana katika ujenzi wa kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Amani zilipatikana zaidi ya shilingi milioni 138.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini liliko Kanisa hilo Mohammed Dewji (MO) alichangia shilingi milioni 10, mfanya biashara maarufu hapa nchini aliyemtaja kwa jina moja tu la Patel amechangia mabati ya kuezekea kanisa hilo yenye thamani ya shilingi milioni 50.


Kanisa hilo la usharika wa amani linatarajiwa kukamilika mapema hapo mwakani kwa gharama ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 480.

November 28, 2011

SERIKALI YAKUBALI YAISHE YABARIKI MIDAHALO YA KATIBA

HATIMAYE serikali ya wilaya ya Iringa imekubali yaishe baada ya kuruhusu asasi za kiraia Tanzania chini ya uratibu wa Azaki ya Iciso mkoa wa Iringa kwa kuruhusu MIDAHALO hiyo ya KATIBA kuendelea Kama kawaida.

Zuio hilo ambalo liliwekwa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa limeondolewa na ofisi hiyo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wing katika MIDAHALO hiyo yenye lento la kuwafanya wananchi kujua katiba vema.

Mratibu wa MIDAHALO hiyo Raphael Mtitu amesema kuwa katakana na serikali ya wilaya ya Iringa kuafiki MIDAHALO hiyo kesho jumanne wakazi wa jimbo la kilolo wataanza kunufaika na MIDAHALO hiyo katika ukumbi wa kanisa la Angricana Luganga kill kuanzia majira ya SAA 8 mchana ,huku wakazi wa jimbo la Iringa mjini mdahalo Kama huo utakuwa siku ya Novemba 30 majira ya SAA 4 asubuhi katika ukumbi wa Shule ya sekondari Mwembetogwa na jimbo la Kalenga wao watashiriki mdahalo huo siku ya Desemba 4 katika ukumbi wa karakana Tanangozi mdahalo utakaofanyika kuanzia majira ya SAA 6 mchana na jimbo la Isimani itakuwa ni Desemba 5 majira ya SAA 6 mchana katika ukumbi wa Magabe Migoli

CCM YADAIWA KUKIHUJUA CHADEMA

Imebainika kuwa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kinatumia fedha nyingi ili kuwakodisha mabaunsa 7 kutoka klabu mbali mbali za usiku jijini Arusha kwa lengo la kuwafanyia Fujo wanachama wa chadema mkoani Humo.

Mabaunsa hao ambao kwa mara ya kwanza walionekana katika mahakama Kuu ya Arusha wakiwa wamevaa miwani meusi wakati wa kesi ya Nape Nnauye ambapo hata Hivyo hakufika mahakamani hapo kutokana na kuumwa.

Mwandiahi wa habari hizi aliwashuhudia tena mabaunsa hao muda Mfupi baada ya kesi ya viongozi waandamaizi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema wakiwa katika viwanja vya mahakama Hiyo.

Waliingia kwa makundi ambapo kundi la kwanza liliingia na watu watatu na kwenda kukaa nyuma ya gari la katibu mkuu wa chadema Dk Wilbroad Slaa.

Hata Hivyo baadhi ya watu waliokuwepo mahakamani hapo wamedai kuwa mara Nyingi mabaunsa hao wamekuwa wakionekana katika ofisi za ccm mkoani hapo na kwamba tayari taarifa zinadai kuwa wanalipwa pesa Ndefu kwa ajili ya kushinikiza Fujo za Arusha ili baadae ionekane kuwa zimefanywa na wafuasi wa chadema.

Hat Hivyo muda mfupi baada ya Dk Slaa na viongozi wengine wa chama kuondoka mahakamani hapo mabaunsa hao nao waliondoka na kuelekea Ofisi za CCM Mkoa.

Hata Hivyo kijana mmoja ambaye ni mwanachama wa chadema alidai kuwa mmoja wa mabaunsa hao siku tatu zilizopita alifika katika eneo lake la kazi maeneo ya Unga Limited akiwa na panga na kumtishia maisha.

Taarifa zinadai kuwa mabaunsa hao wameamua kuzisahau kazi zao na kufanya kazi na ccm kwa malipo mazuri ili kuhakikisha kuwa wanachafua na kuvuruga kabisa nguvu ya upinzani Jijini Humo.

Taarifa Hizo zinaendelea kudai kuwa awali watu hao walikuwa walinzi wanaokodiwa na chadema na kwamba wameamua kugeuka baada ya kuahidiwa donge nono la shilingi laki moja kwa siku.

BREAKINGNEWSZzzzz SOKO KUU LA TUNDUMA LINATEKETEA KWA MOTO SASA

Taarifa za uhakika kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa soko kuu la Tunduma kwa sasa linaendelea kuteketea kwa moto uliozuka ndani ya soko hilo.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka eneo la tukio Moses Ng'wat anaripoti kuwa moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 12 za jioni na jitihada za magari ya zimamoto ya mkoa wa Mbeya zimmegonga mwamba na kulazimika kuomba msaada wa magari ya Zimamoto kutoka nchi ya jirani ya Zambia.

Hata hivyo chanzo cha moto huo bado kutajwa na jitihada za kumsaka kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya bado zinaendelea.

HOT NEWS.....CHADEMA WAKUBALIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETEMazungumza kati ya ujumbe wa chadema na serikali yamefikia mwisho huku pande zote mbili zikitoka na makubaliano ya pamoja kuhusian na marekebisho ya sheria ya katiba mpya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho ambazo mtandao huu umezipata zinadai kuwa ,Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu katibu mkuu chadema John Mnyika na waziri wa habari, vijana utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi imebainisha kuwa baada ya vuta Nikuvute ya takribani siku mbili hatimaye maafikiano ya pamoja yamepatikana.
Taarifa Hiyo inasema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge ipo haja ya Rais kuendelea kuiboresha katika vipengele kadhaa ili ikidri mahitaji ya kujenga na kuaminiana na muafaka wa kitaifa.Pia imekubaliana yawepo mawasilano ya karibu na mashauriano ya mara kwa mara kati ya serikali na wadau mbali mbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo kla kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa katiba Mpya.Hata Hivyo habari zinadai kuwa kumekuwa na Vute nikuvute baina ya serikali na chama Hicho chenye nguvu kubwa hali iliyopelekea Rais jana kuahirisha kikao Hicho ambacho kimemalizika novemba 28.
Hata hivyo madai ya chadema ni kumuomba Rais kutosaini mchakato huo hadi kwanza ufanyiwe marekebisho ombi ambalo lilimuweka Jakaya katika wakati Mgumu na kuahidi kulifanya kazi ombi hilo.MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SIKU WA VIONGOZI WA TAKUKURU-TANGA

akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, mara baada ya kufungua ramsi mkutano Mkuu wa mwaka wa siku mbili wa Viongozi wa Takukuru uliofunguliwa leo Novemba 28, mkoani Tanga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Takukuru baada ya kufungua mkutano huo
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo wa Takukuru waliohudhuria Mkutano huo Mkuu wa Mwaka ulioanza leo,Picha na Muhidin Sufiani-OMR

DHI NURENY ISMAMIC FOUNDATION YALETA NEEMA KWA WAGONJWA WA MACHO IRINGA

Mwenyekiti wa Dhi-Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Abri akizungumza na wanahabari leo Madaktari bingwa wa macho wanaotoa tiba bure Iringa ,Dr Fakhruddin Dakhan ,na Dr Arif Shah wakihojiwa na wanahabari leo
sehemu ya dawa za bure za macho Wagonjwa wakiwa katika foleni
Dr Arif Shah kutoka Saud Arabia akitoa tiba ya macho
matibabu kwa wagonjwa wa macho Iringa

ZAIDI ya dola za kimarekani 50,000 zinataraji kutumia kugharamia bure matibabu watu zaidi ya 5000 wenye matatizo ya macho mkoani Iringa .

Akizungumza leo katika viwanja vya Umm Salam Ngangilonga mjini Iringa wakati wa uzinduzi wa zoezi la tiba ya bure kwa watu wenye matatizo ya macho mkoani Iringa ,Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka taasisi hiyo ya Al Basar International Foundation, Fhakruddin Dakhan alisema fedha hizo zimelenga kutoa huduma ya bure kwa wagonjwa wa macho mkoani Iringa.

Alisema kwa kupitia timu ya madakatari waliobobea katika utoaji wa huduma za macho kutoka nchini Pakistan, wanatarajia shughuli hiyo itafanikiwa kama walivyopanga kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwa siku ya kwanza.

Mwenyekiti wa Dhi-Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Abri alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwasaidia watanzania wenye matatizo ya macho kupata kuona

Alisema huduma hiyo inatolewa na taasisi ya kimataifa ya Al Basar International Foundation ya Saud Arabia kwa msaada wa asasi isiyo ya kiserikali ya Dhi Nureyn Islamic Foundation mkoani Iringa.

Pia alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kupunguza ongezeko la watanzania wateseka kwa matatizo ya macho huku wengi wao wakiendelea kuteseka kwa kukosa fedha za matibabu .

Hivyo alitaka wakazi wa mkoa wa Iringa wenye matatizo ya macho kutumia fursa hiyo kufika kupewa matibabu bila malipo na wale wasio na matatizo ya macho pia kujitokeza kupima macho yao bure.

Alisema kuwa wagonjwa hao kutoka maeneo mbalimbali za mkoa wa Iringa wanatarajiwa kufanyiwa upimaji wa macho, kupewa dawa, kupewa miwani na kufanyiwa upasuaji mbalimbali ukiwemo wa kutoa mtoto wa jicho.

Katibu Mtendaji wa Dhi-Nureyn Islamic Foundation, Elm Shamsi alisema taasisi ya Al Basar International Foundation imeleta madaktari bingwa wanne wa huduma za macho watakaoifanya

Shamsi alisema asasi hiyo imewaleta wataalaamu hao katika jitihada zao za kushirikiana na serikali kukabiliana na matatizo ya magonjwa ya macho yanayozidi kuwaandama watanzania walio wengi.

WAHITIMU CHUO CHA VETA IRINGA WATAKIWA KUWAKIMBIA WAAJIRA WAPENDA RUSHWA ZA NGONO

Mhitimu wa fani ya mapishi chuo cha VETA Iringa Perida Erasto akionyesha cheti chake

Mgeni rasimi katika mahafali ya 15 ya chuo cha Veta Iringa Bw.Enock Ndondole akimkabidhi cheti mhitimu Perida Erasto leo ambaye alikuwa akisomea fani ya mapishi
PS wa mkuu wa chuo cha Veta akimpongeza mhitimu wa chuo cha Veta Iringa fani ya upishi Perida Erasto Godwin
Hongera sana Perida Erasto Godwin
Mgeni rasmi Enock Ndondole akimkabidhi cheti mhitimu
Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin akimpongeza mdogo wake Perida baada ya kuhitimu chuo cha Veta leo
Wahitimu walilishana keki leo
Wahitimu wa chuo cha ufundi stadi Veta Iringa wakiimba nyimbo

WAHITIMU wa kike katika chuo cha ufundi stadi VETA mkoa wa Iringa wameaswa kuepukana na waajiri wanaotoa ajira kwa kutaka rushwa ya ngono pia kuepukana kutotegemea ajira kutoka serikalini na badala yake kujiajiri katika sekta zisizo rasimi ili kunufaika na Mafunzo hayo

Pamoja na kupewa Rai hiyo bado wanafunzi wameaswa kuacha kuchagua Masomo ya kujifunza katika vyuo hivyo kwani kufanya hivyo ni kuendelea kupishana na ajira katika fani ambazo wamekuwa wakibagua katika vyuo hivyo.

Rai hiyo imetolewa na mgeni rasimi Enock Ndondole katika mahafali ya 15 ya chuo cha ufundi stadi (VETA) mkoa wa Iringa alisema kuwa mimewepo na tatizo la baadhi ya. Wanafunzi kuendelea kuchagua fani huku baadhi ya watoto wa kike kushindwa kujiunga na fani ya mapishi huku baadhi ya watoto wa kike kukimbia Masomo ya ufundi magari kwa Imani kuwa kazi hiyo ni kwa ajli ya wamzika pekee.

Alisema kuwa hivi sasa Soko la ajira zote lipo kubwa katika fani zote na ndio sababu ya VETA kuanzisha Masomo hayo katika vyuo vyake katakana na kufanya utafiti wa kin a kabla ya kuanzisha fani hizo.

Katika hatua nyingine Ndondole aliwataka wahitimu hao has a watoto wa kike kuachana na kutumia rushwa na ngono kwa ajili ya kuomba kazi kwani kufanya hivyo ni kujitafutia kifo kwa ugonjwa wa UKIMWI.

Alisema kuwa elimu hiyo ambayo wameipata chuoni hapo ni elimu kwa ajili ya kujinasua katika dimbwi la ajara na sio sehemu ya kutafuta mauti kwa kuendekeza rushwa za ngono ambazo mwisho wa siku ni kufukuzia mauti .

Aidha aliwataka wahitimu hao kuendelea kukitangaza chuo hicho kwa kufanya kazi kwa bidi na kujiheshimu zaidi katika kazi badala ya kueneza picha mbaya ya kutumia rushwa ya ngono wakati wa kuomba kazi.