Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

October 31, 2011

HOT NEWZ...............UNYAMA UNYAMA MZEE WA MIAKA 60 LUDEWA ACHOMWA MOTO KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

Umati wa Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakiwa wamemshikilia dada wa marehemu aliyekuwa akilia huku akimlaumu marehemu kaka yake kwa kujihisisha na uchawi na kukataa ushauri wake.

MTU MMOJA aitwaye Laurance Nkwera 60 mkazi wa Kijiji cha Ibani Ludewa katika Mkoa mpya wa Njombe amekufa kwa kuchomwa moto na kuungua vibaya kwa imani za kishirikina, huku nyumba yake ikiteketea, na familia yake kunusulika kifo kwa kutoboa nyumba.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Ludewa Basil Makungu anaripoti kuwa tukio hilo limetokea usiku wa octoba 01 mwaka huu majira ya saa nane alfajili baada ya mlango wa Nyumba yake kufungwa nje na watu wasiojulika kutokana na mvutano uliotokea kati yake na wauaji kabla ya wauaji hao kumzidi nguvu na hatimaye kuchoma nyumba yake.

Akizungumza katika eneo la tukio Cesilia Haule ambaye ni mke wa marehemu Laurance alisema kuwa yeye na mumewe walikuwa wamelala chumbani na watoto wao wawili wakiwa wamelala sebuleni na kwamba ilipofika saa nane za usiku watu wasiojulikana waligonga mlango na kutoa masharti ya kutokutoka nje.

Ester Nkwera ni mtoto wa marehemu na Mwanafunzi wa darasa la nne
katika shule ya msingi Kimbila anasema yeye alikuwemo ndani wakati Nyumba ikiunguzwa moto na kwamba yeye na mama yake walifanikiwa kujiokoa kwa kutoboa nyumba yao ya miti lakini Baba yake alibaki pamoja na mdogo wake Laurance.

Laurance ni mtoto wa marehemu mwenye miaka mitano tu, yeye alinusurika kifo kwa kupita katika mikono ya wauaji ambao walikuwa wamezingira nyumba hiyo ya miti huku wakiwa wamesimama pembeni kuhakikisha Nyumba na vyote vilivyomo vinateketea.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Ibani Philipo Haule, Afisa Mtendaji Kata Onesmo Haule wamesema kuwa marehemu pamoja na watu wengine wanne ni muda mrefu walikuwa wakituhumiwa kujihusisha na kuwatesa watu kwa uchawi ikiwemo kubaka wake za watu kiuchawi, kuua watu na kuwafanyisha kazi usiku kwa uchawi.

Wakizungumza kwa masharti ya kutoandika majina kwa kuhofia usalama wao wakazi wa kitongoji cha Ibani Ludewa walisema wamechoshwa na udhalilishwaji unaofanywa na wachawi ikiwemo kuwabaka wake zao kiuchawi,kuwauwa na kuwatumikisha kazi usiku na kwamba watahakikisha wanaikomesha tabia hiyo kwa kila anayehusika kwa kuwa wananfahamika.

Aidha Monica Mchiro Diwani wa Kata ya Ludewa alikiri kufanyika kwa
mkutano wa hadhara octoba 11 mwaka huu unaowahusu watu watano wanaotuhumiwa na Wananchi kuwatesa kwa nguvu za uchawi hata hivyo watuhumiwa akiwemo marehemu walikana kuhusika na matukio hayo.

Bi
Monica aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa polisi na ofisi za vijiji na Kata kuhusu uhalifu wowote uanotokea katika maeneo yao.

Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundala amemwagiza mkuu wa polisi wilaya kuhakikisha wale wote waliohusika na ukatili huo wanakamatwa haraka na kupelekwa mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

Aidha Bundala amekemea vikali tabia hiyo na kusema kuwa kwa jamii iliyoelimika haiwezi kufanya mambo kama hayo, na kuongeza kuwa kuna haja ya kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa namna ya kukabiliana na matukio kama hayo kwa kufuata sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Iringa Kamishna Msaidizi wa polisi Evarist Mangala alikiri kutokea kwa mauaji hayo na kwamba taarifa kamili atatoa baada ya kupata taarifa kamili ingawa alikiri kuwa chanzo cha
mauaji ni imani za kishirikina.

Mtandao huu unalaani kwa nguvu zote kitendo hicho cha wananchi wa Ibani Ludewa kujichukulia sheria mkononi hata kuamua kupoteza maisha ya mzee Nkwera eti kwa imani za kishirikina,ni vema wananchi kuacha kufanya maamuzi mazito kama haya kwa wazee wetu kwani inapendeza kuona wananchi wanatumia vyombo vya sheria zaidi katika kuondoa tafauti zao badala ya kujigeuza wao ni Mahakama

MIRADI YA TASAF MUFINDI; WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI YA KIKWETE

Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania (TASAF) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Chamila Bidya ( wa tatu kushoto) na diwani wa kata ya Rungemba Patrick Mwihava (wa kwanza kushoto) wakishirikiana leo na viongozi na wananchi mbali mbali wa kijiji cha Rungemba kusogeza tofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho iliyojengwa kwa ufadhili wa asilimia 80 na TASAF na asilimia 20 nguvu za wananchi

WANANCHI wa kata ya Rungemba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wapongeza mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa kusaidia miradi yenye thamani ya shilingi milioni 245,549,790.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu wakati wa kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo na jinsi ambavyo wananchi wa pembezoni wanavyonufaika na fursa za kimaendeleo zinazotolewa na serikali, iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya kikwete.

Wakazi wa kata ya Rungemba Sophia Mlishoyo mjumbe wa mradi wa Zahanati uliopo chini ya TASAF na Yustinus Mkanyipelele ambaye ni katibu wa mradi huo kijiji cha Rungemba ,walisema kuwa kusaidia kujengewa zahanati katika kijiji hicho ni ukombozi mkubwa na hivyo hawana budi kuipongeza serikali kupitia mradi huo wa TASAF.

Mlishoyo alisema kuwa wanawake wa watoto ndio ambao walikuwa wakipata shida kubwa ya kwenda kijiji cha Rungemba Mnadani katika wilaya ya Iringa vijijini kupatiwa huduma ya afya kwa foleni kutokana na kijiji hicho kukosa huduma ya afya ama kwenda Mafinga .

Hata hivyo alishauri serikali kuweza kuendelea kusaidia miradi mingine katika kijiji hicho pamoja na kuharakisha zoezi la kusogeza umeme wa gridi ya Taifa ili kusaidia Zahanati hiyo kutumia vifaa vya kisasa zaidi.

Diwani wa kata hiyo Patrick Mwihava mbali ya kuishukuru serikali kwa kuanzisha mfuko huo wa TASAF bado alipongeza ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi wa kijiji cha Rungemba kwa kujitolea nguvu zaidi asilimia 20 ili kuunga mkono uwezeshwaji wa TASAF wa asilimia 80.

Aidha alisema kuwa kata yake bado ina changamoto mbali mbali na kuomba mfuko huo wa TASAF kuendelea kuwa mkombozi zaidi kwa wananchi wa vijijini ambao wanatamani sana kuwa na maisha bora kama wale wa mijini.

Mratibu wa TASAF wilaya ya Mufindi Chamila Bidya alisema kuwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wananchi na TASAF wilaya ya Mufindi ndio ambao umeendelea kusogeza maendeleo zaidi kwa wananchi hao.

Hata hivyo alisema kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya milioni 245 zilizotolewa na TASAF katika kipindi cha mwaka 2010-2011 zilipata kutumika katika kukamilisha na kufanya ukarabati wa mkiradi mbali mbali iliyofadhiliwa na TASAF baada ya kuibuliwa na wananchi wenyewe.

Alisema kuwa katika kipindi hicho TASAF –Mufindi ilifanya ukarabati na ukamilishaji wa nyumba na vyumba vya madarasa 44 katika shule mbali mbali za sekondari ,bweni moja , nyumba za waganga tano ,nyumba moja ya mwalimu, majengo ya utawala matatu , Zahanati moja, kituo cha afya kimoja, pamoja na kufanya ukarabati na ujenzi wa kituo cha kulelea watoto kimoja na ukarabati wan a ujenzi kwenye miradi ya mifumo ya maji 32.

Bidya alisema kuwa TASAF –Mufindi imefadhili ujenzi wa vyoo 27 na ukarabati wa vyoo 15 pamoja na ujenzi wa mabafu nane na shughuli nyingine mbali mbali za kijamii.

WEMA UMENIPONZA ......

Fundi radio katika eneo la Tulivu Klabu katika Manispaa ya Iringa akiwa anavuja damu baada ya kuambulia kipigo wakati akiamua ugomvi uliozuka kazini kwake

Fundi radio huyo akielezea tukio lilivyotokea kwa baadhi ya wananchi jana

JAQUELINE SIKAMWA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ANAYEKUJA JUU NCHINI

Mwimbaji wa nyimbo za injili Jaqueline Sikamwa akizindua albamu yake ya USIJALI katika ukumbi wa sekondari ya Mwembetogwa,mwimbaji huyu amekuwa akifanya vema katika tasnia hiyo na juhudi zake zimekuwa zikizidi hata zile za Rose Mhando pindi akiwa jukwaani

Hapa akiwajibika jukwaani

Baadhi wa waimbaji waliosindikiza sherehe hii

Wadau wa nyimbo za injili ambao walifika kushuhudia sherehe hiyo

Mtangazaji wa Radio Overcomers Fm Denis Nyali ambaye amekuwa msaada mkubwa wa kupromoti wasanii wa nyimbo za injili katika hapa nchini,


Iwapo umeandaa tamasha ama unataka kumpata msanii Jaqueline Sikamwa kwa ajili ya kufanya tamasha la uimbaji waweza mtafuta kwa namba 075621 264 au 0654b540495

October 30, 2011

WAANDISHI IRINGA WAITOLEWA MACHO OFISI YA MAJI BONDE LA RUFIJI

Wafanyakazi wa maji bonde la Rufiji Iringa wakiwa katika sherehe
Hatua ya uongozi wa bodi ya maji bonde la Rufiji mkoani Iringa kuamua kukutana na wadau wa bonde hilo katika kikao cha siku mbili kwa ajili ya kupokea taarifa na kutoa maoni juu ya mradi wa usimamizi wa pamoja wa rasilimali ya maji katika bonde la Rufiji imewafanya wanahabari mkoa wa Iringa kuanza kuhoji mahusiano kati ya ofisi hiyo na wanahabari Iringa.


Hadi sasa zipo taarifa za ndani ya ofisi hiyo kuwa suala la urafiki zaidi ndilo linalotawala katika ofisi hiyo ,huku baadhi wakitaka uendeshaji wa ofisi hiyo kuweza kumulikwa zaidi .

Pia wamehoji kikao kama hicho kuvibagua vyombo vya utangazaji vya mkoa wa Iringa kama Radio Ebony ,Country Fm ,Nuru Fm, Overcomers Fm na nyingine ambazo zimekuwa ni adau wakuu wa mazingira na wananchi wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakitegemea radio hiyo kupata habari na matukio ya ndani ya mkoa.


Pamoja na suala hilo la ofisi hiyo kutuhumiwa kuendeshaji shughuli zake kindugu zaidi pia baadhi ya wapambaji kumbi na wale wafanyabiashara wa chakula katika sherehe wamedai kubaguliwa katika tenda huku idadi ya washiriki wa kikao hicho na ufinyu wa ukumbi wa Siasa ni kilimo ambao utatumika kwa kikao hicho vinatajwa kuwa yawezekana idadi ya washiriki kuchakachuliwa kwa ajili ya kulipa idadi hewa ya washiriki.


Kikao hicho kwa mujibu wa barua ya mwaliko iliyosambazwa na familia ya mmoja kati ya wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa baadhi ya wanahabari barua yenye kumbukumbu namba RBWO/D.3/19/51 inasema kuwa kikao hicho kitafanyika ukumbi wa siasa ni kilimo kati ya tarehe 3 na ya mwezi wa 11. japo wafanyakazi wa ofisi hiyo kuonyesha kutofautiana na kaimu ofisa wa maji bonde la Rufiji Iringa Grece Chitanda ambaye baada ya kuhojiwa na katibu mtenaji wa IPC Frank Leonard juu ya kikao hicho alidai kuwa wamealika , ITV, TBC, Star TV na magazeti bila kutaja radio .


Japo wafanyakazi wenzake wakidai kuwa kikao hicho hakishirikishi wanahabari ni kikao cha ndani cha kikazi kwa wadau na wafanyakazi wa ofisi hiyo.


Taarifa ya kina itakujia hivi punde ndani ya mtandao huu

VIONGOZI WA KIJIJI CHA MALEUSI MAKETE KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUTAKA KUMUUA MWANDISHI WA HABARI


VIONGOZI wawili wa serikali ya kijiji cha Maleusi wilaya ya Makete mkoani Iringa wanaotuhumiwa kutaka kumuua mwandishi wa habari wa Radio Free Afrika na Star Tv mkoa wa Iringa Frederick Siwale(49) (pichani) wanataraji kufikishwa mahakamani kesho jumatatu .

Viongozi hao wanatuhumiwa kutaka kumuua mwanahabari huyo ambaye alifika kijiji hapo kufuatilia sakata la mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha familia moja .

Tayari jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia viongozi wawili wa serikali ya kijiji cha Maleusi katika Wilaya ya Makete mkoani Iringa kwa tuhuma za kutaka kumfanyia unyama huo mwanahabari huyo .Siwale alikutwa na mkasa huo juzi majira ya saa tano asubuhi wakati baada ya kufika kijijni hapo kwa ajili ya kufuatilia na kuripoti sakata ya mgogoro wa ardhi uliozuka kati ya pande mbili kati ya kijiji na familia .Kiini cha tukio hilo kimefahamika kuwa ni viongozi hao kuhusishwakatika tuhuma za ubadhilifu wa ardhi iliyotumika kwa maziko yawananchi kuibinafsisha kwa mwekezaji.Eneo lilitumika kwa maziko ambalo limefahamika kuwa nila ukoo waMbilinyi ambao kwa mujibu wa wasemaji wa ukoo huo Nazarena Mbilinyi naPaulo Mbilinyi eneo hilo lilianza kutumika kwa maziko tangu mwaka1945.Akizungumzia tukio hilo Siwale alisema baada ya kupata taarifa yakuuzwa kwa eneo la makaburi kama ilivyo ada ya kazi yake alifungasafari kwenda Makete ili kupata undani wa tukio hilo.“Nilifika Makete na siku iliyofuata nilianza safari ya kwenda kijijinihuko Maleusi kwa ajili ya kukamilisha kazi yangu ya kihabari, nilipataushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi ikiwa pamoja na wahusika wa ukoowa Mbilinyi wa,iokuwa wakiwalalamikia viongozi hao, lakini nilipotakakukamilisha habari yangu kwa walalamikiwa mwenyekiti wa serikali yakijiji aliwaita wajumbe na kuamuru ngoma ya lamgambo na mtendajialipiga simu ambayo alisikika akisema njiani yawekwe magogo ilikunizuia kupita, na niliposikia hivyo nilikimbia kwa kubadili njiandiyo ilikuwa salama yangu,” Alisema Siwale.Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa Evarist Mangala alikirikukamatwa kwa viongozi hao ambao aliwataja majina watuhumiwa wa tukiohilo kuwa ni Rubern Mbilinyi mwenyekiti wa serikali ya kijiji chaMaleusi na Michael Sanga ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji chamaleusi na kuwa watafikishwa mahakani baada ya uchunguzi kukamilika.

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) imeeleza kusikitishwa na hatua ya viongozi hao wa vijiji kutaka kwenda kinyume na katiba ya nchi ambayo inatoa nafasi kwa kila mtanzani kupata habari na ile ya uhuru wa vyombo vya habari inayowataka wanahabari kufanya kazi yao bila kunyanyaswa.

Katibu mtendaji wa IPC Frank Leonrad alisema kuwa mbali ya kulipongezwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kamanda wake Mangalla kwa kuwakamata wahusika hao bado alitaka viongozi wa serikali kutowaona wanahabari wanaofika katika maeneo yao kuwa ni maadui .


Huku muungano wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kupitia mjumbe wake Juma Nyomayo umeeleza kusikitishwa na waandishi kuelekea kunyanyaswa wanapokuwa kazini.

CHUO KIKUU CHA TUMAINI IRINGA CHAZIDI KUONGEZA KOZI ZAIDI

Mkuu wa chuo vyuo vya Tumaini Tanzania ,Askofu Dkt Alex Malasusa

CHUO kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira Iringa kimepanua wigo wa utoaji wa kozi mbali mbali ili kama njia ya kuwavutia wengi zaidi kuendelea kupata elimu ya juu hapa nchini.

Mkuu wa wa chuo cha Tumaini Makumira Iringa Profesa Nicholaus Bangu aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na kwa niaba yake na makamu mkuu wa chuo cha Tumaini Makumira Prof.Joseph Parsalaw wakati wa sherehe za mahafali ya 14 ya chuo hicho .

Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa kimepanua wigo wa utoaji wa kozi mpya zaidi ya tano ikiwemo ya Shahada ya uzamili katika sheria , Shahada ya uzamili katika maendeleo ya jamii na usimamizi wa miradi, Shahada ya uzamili wa Misioni na maendeleo ya jamii na shahada ya uzamili katika Saikolojia ya ushauri Nasaha.

Kozi nyingine ni Shahada ya kwanza ya elimu yenye michepua ya masomo ya Historia,Kiswahili,Jiografia na kiingereza pamoja na kuanzisha masomo ya jioni ya shahada ,stashahada na astashahada kwa vituo vya Iringa na Mbeya.


Akielezea idadi ya wahitimu 1062 waliohitimu chuoni hapo katika Mahafali ya 14 alisema na idadi yao katika mabano alisema kuwa kati ya wahitimu hao ni pamoja na wahitimu (74 )waliotunukiwa shahada ya uzamili katika utawala wa biashara,( 7 )Stashahada ya Uzamili ya Uongozi,( 3 )stashahada ya uzamili ya elimu (Ufundishaji) na 18 ni wa stashahada ya uzamili ya elimu (utawala).Aliwataja wahitimu wengine na idadi yao kwenye mabano kuwa ni wa shahada ya uandishi habari (35), shahada ya theolojia-Divinity (9), Shahada ya Sheria (172), shahada ya utawala wa biashara (110), shahada ya elimu katika hisabati (82), shahada ya ushauri nasihi (58), Shahada ya Maendeleo ya Jamii (205), shahada ya sayansi ya Technolojia ya habari-IT (30) na Shahada ya Athropolojia ya Utamaduni na Utalii (139).Wahitimu wengine waliotunukiwa ni pamoja na wale wa stashahada ya theolojia (14), cheti cha utawala wa biashara (88), cheti cha theolojia (12) na cheti cha sheria (6).
Alisema kuwa jumla ya wahitimu 1062 ndio ambao wamepata kuhitimu katika mahafali hayo ya 14 jana kwa kutunukiwa Shahada , stashahada na astashahada katika kozi mbali mbali.

Pia alitaja baadhi ya shughuli ambazo zimekuwa zikiendelea kufanyika chuoni hapo kuwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa jingo la mafunzo ya sayansi katika fani ya fizikia ,kemina ,Biolojia na kilimo .

Aidha alisema kuwa chuo hicho kimeendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora katika vituo 43 katika maeneo ya vijijini kwenye wilya ya Kilolo,Iringa na Njombe kupitia taasisi ya maendeleo ya kilimo.

'LIVE" IBADA YA KUMKUMBUKA YA KIFO CHA WAKILI NELSON THOMAS MWAKINGWE YAFANA IRINGA

Mpendwa wetu wakili na mtetezi wa wanyonge katika tasnia ya sheria nchini Marehemu Nelson Thomas Mwakingwe tutakukumbuka daima
Mke wa waziri mstaafu wa serikali zote nne Joseph Mungai ,Bi.Mary Mungai (kushoto) akimfariji mke wa wakili Mwakingwe ambaye ni mweke hazina wa taifa wa NCCR- Mageuzi Bi,Mariam Mwakingwe
Mjane Mariam Mwakingwe ambaye ni mzee wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) ushari wa Iringa mjini akitoka kanisa hapo baada ya ibada maalum ya kumkumbuka ubavu wakefamilia ya Mwakingwe ikitoka ibadani
Mary Mungai akiwa na mama Mariam Mwakingwe (kulia)
Mama Mwasongwe akitoa sadaka ya shukrani
Wakili maarufu mkoani Iringa Basil Mkwata akiungana na familia ya wakili Mwakingwe kumshukuru mwenyezi Mungu kwa sadaka leo
Wakili maarufu Mr. Kigwe (katikati)ambaye ni mmoja kati ya familia ya marehemu Nelson Thomas Mwakingwe akiwa katika ibada ya kumbukumbu
Kulingana na siku zinavyozidi kusogea ndivyo yunavyozidi kukukumbuka na kuona pengo lako ndani ya familia na jamii nzima ya mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla .

Hakika tutaendelea kukumbuka daima siku zote baba yetu na mpendwa wetu wakili wetu Nelson Thomas Mwakingwe

Mwenyezi Mungu azidi kuilaza roho yako mahali pema Daima
AMINA

MASHABIKI MECHI YA YANGA NA SIMBA WAINGIZA ZAIDI YA TSH. MILIONI 337

Mechi namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 337,537,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 53,366 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 51,488,694 na gharama za awali za mchezo sh. 27,405,250 kila timu ilipata sh. 77,592,916.

Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 25,864,305), TFF (sh. 25,864,305), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 12,932,152), gharama za mchezo (sh. 25,864,305), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 10,345,722) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 2,586,430).

STARS YAPANGIWA MSUMBIJI CAN 2013
Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kucheza na Msumbiji katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

Upangaji ratiba wa mechi hizo za mchujo ulifanywa juzi (Oktoba 28 mwaka huu) na kamati ndogo ya michuano hiyo mjini Malabo, Equatorial Guinea.

Jumla ya nchi 47 ikiwemo mwenyeji Afrika Kusini ndizo zilizothibitisha kucheza michuano hiyo. Nchi 16 zilizofuzu kucheza fainali za mwakani nchini Gabon na Equatorial Guinea zenyewe zimepitishwa moja kwa moja hadi raundi ya mwisho ya mchujo itakayoanza baada ya fainali za 2012.

Raundi ya kwanza ya awali itahusisha nchi nne ambazo kwenye ubora wa viwango ndizo ziko chini ili kupata mbili zitakazoingia raundi ya pili ya awali itakayokuwa na nchi 28. Nchi hizo ni Swaziland, Sao Tome, Lesotho na Shelisheli.

Stars imepangiwa kucheza na Msumbiji katika raundi hiyo ya pili ya awali. Tarehe za mechi hizo ambazo zitachezwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2012 zitatangazwa baadaye.

Mechi nyingine za raundi hiyo zitakuwa kati ya Ethiopia na Benin, Rwanda na Nigeria, Congo na Uganda, Burundi na Zimbabwe, Algeria na Gambia, Kenya na Togo, Sierra Leone na mshindi kati ya Sao Tome na Lesotho.

Nyingine ni Guinea Bissau na Cameroon, Chad na Malawi, mshindi kati ya Shelisheli na Swaziland dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Misri, Madagascar na Cape Verde na Liberia na Namibia.

Timu 14 zitakazopita hatua hiyo zitaungana na 16 zilizofuzu kwa ajili ya fainali za Gabon/Equatorial Guinea kucheza raundi ya mwisho kupata 15 zitakazoungana na wenyeji Afrika Kusini kwa ajili ya fainali za 2013. Raundi hiyo itachezwa kati ya Septemba na Oktoba mwakani.rights reserved

LIGI KUU YA VODACOM
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatavyo;

Oktoba 30- Kagera Sugar vs Azam (Uwanja wa Kaitaba)
Oktoba 30- Villa Squad vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 30- Mtibwa Sugar vs Moro United (Uwanja wa Manungu)
Novemba 2- Oljoro JKT vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid)
Novemba 2- Moro United vs Simba (Uwanja wa Taifa)
Novemba 2- Polisi Dodoma vs Yanga (Uwanja wa Jamhuri)
Novemba 2- Toto Africans vs Azam (Uwanja wa CCM Kirumba)
Novemba 2- Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu)
Novemba 2- Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi)
Novemba 3- Kagera Sugar vs Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba)

LIGI DARAJA LA KWANZA
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatazo;

Kundi A
Oktoba 30- Morani vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Kiteto)
Oktoba 30- Transit Camp vs Burkina Faso (Uwanja wa Mkwakwani)
Oktoba 31- Temeke United vs Mgambo Shooting (Uwanja wa Mlandizi)

Kundi B
Oktoba 30- Mbeya City vs Small Kids (Uwanja wa Sokoine)
Oktoba 30- Majimaji vs Tanzania Prisons (Uwanja wa Majimaji)
Oktoba 31- Polisi Iringa vs Mlale JKT (Uwanja wa Samora)
Novemba 3- Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Samora)

Kundi C
Oktoba 31- 94KJ vs Manyoni (Uwanja wa Mlandizi)

POULSEN vs WAANDISHI WA HABARI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen atakutana na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya mechi dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu ikiwemo kutaja kikosi chake.

Tarehe: Oktoba 31, 2011
Muda: Saa 5 asubuhi
Mahali: TFF

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

NAPE NNAUYE AROPOKA,MAHAKAMA YAMTAMANIJAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aloyce Mujulizi, ameamuru Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, afikishwe mahakamani kwa madai kwamba anatoa matamshi yaliyoingilia uhuru wa mahakama.

Mwandishi Grace Macha kutoka Arusha anaripoti kuwa ,Jaji Mujulizi alitoa uamuzi huo jana mara baada ya kusikiliza hoja iliyowasilishwa mahakamani hapo na Wakili Method Kimomogoro anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye alidai kuwa Nape amesema kwamba ana uhakika CCM itashinda katika kesi hiyo.

Wakili Kimomogoro alisema kuwa kauli hiyo, ambayo Nnauye hajawahi kuikanusha, inatoa picha kuwa pengine jaji ndiye aliyewahakikishia ushindi, au ni kujaribu kumtisha ili atoe maamuzi ya kupendelea upande mmoja.

“Nape alisema kwa sasa (CCM) wako katika mchakato wa kwenda kupiga kambi katika Mkoa wa Arusha ili waweze kulichukua jimbo hilo, na alisema wana uhakika wa kushinda kesi yao dhidi ya mbunge wa jimbo hilo (Godbless Lema) na kulichukua uchaguzi utakapofanyika,” wakili Kimomogoro alinukuu sehemu ya habari iliyochapishwa katika gazeti la Nipashe.

Wakili huyo aliieleza mahakama kuwa wakati wakiendelea kutafakari kauli ya Nape, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Chiligati, alinukuliwa na vyombo vya habari, ikiwamo gazeti la Mwananchi la Oktoba 17 mwaka huu akisema kuwa CCM ina msemaji mmoja tu, naye ni Nnauye, hivyo wakabaini kuwa kauli hiyo imetolewa na mtu mzito ndani ya chama hicho tawala hivyo haikupaswa kupuuzwa.

Kimomogoro alishauri Nape apewe onyo, huku akiomba jaji mkuu ateue majaji watatu mpaka watano kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo ili kuondoa hofu kwa mteja wake, chama chake, mashabiki na wapenzi wa chama hicho.

“Katika kesi 44 za uchaguzi, 14 zimefunguliwa na CCM na hakuna hata moja wamejihakikishia ushindi isipokuwa hii tu. Tafsiri aliyoipata mteja wangu na chama chake ni kuwa ama umewahakikishia ushindi au kauli hii wameitoa kutaka kukulazimisha utoe uamuzi wa kuwapendelea ama wao kama chama tawala wanakutisha ili utoe maamuzi kwa masilahi yao,” alisema Kimomogoro.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Angela Chacha, anayemtetea mdaiwa wa pili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuunga mkono hoja hizo, na kabla hajasimama kuongea, jaji alimuuliza Wakili Kimomogoro endapo hoja hizo ni za wadaiwa wote. Wakili alikataa akidai mwenzake ni mwajiriwa wa serikali pengine zinaweza kumsababisha kukosa ajira endapo ataziunga mkono.

Akijibu hoja hizo wakili wa wadai, Alute Mungway, alielezea kushangazwa na hatua ya wakili huyo wa wadaiwa kuwasilisha hoja hizo ghafla na kudai zina lengo baya la kuchelewesha usikilizaji wa shauri hilo.

“Hawa ni wanasiasa siku zote wanaropoka; tukianza kuuliza Slaa (Dk. Willibrod Slaa) kasema nini, Lipumba (Prof. Ibrahim) kasema nini, kesi zitaendelea mahakamani kweli? Wakili angeweza kwenda kumuuliza Nape kwanini aliyasema hayo…. Tunaomba mahakama yako isipoteze muda kumjadili Nape na Chiligati,” alisema Mungway.

Aidha, hati kama hiyo imetolewa kwa mhariri wa gazeti la Nipashe ambalo liliandika kauli ya Nape inayodaiwa kutolewa na Nape kwenye toleo namba 057162 la Oktoba 9 mwaka huu.

Jaji alikubaliana na ombi la Wakili wa wadaiwa na kuamuru Nape afike mahakamani hapo Novemba 16 mwaka huu, kujibu tuhuma hizo na aeleze kwa nini asipewe adhabu kwa kudharau mahakama.

Awali, palitokea mvutano kati ya wasikilizaji, polisi na mbunge (Lema) baada ya polisi kuamua kuzuia watu kuingia kwenye chumba cha mahakama baada ya kufurika watu.

Wananchi walilalamika kuwa walifika mahakamani hapo kuanzia saa 1:45 asubuhi lakini walizuiwa kuingia wala kusimama madirishani kama ilivyoamriwa na jaji.

Kufuatia msimamo huo wa polisi, Lema aliyekuwa ndani ya chumba cha mahakama, alitoka nje na kuzungumza na Kamanda wa Polisi wilayani hapa, Zuberio Mwombeki, akimtaka kuwaacha wananchi wasikilize shauri hilo.

Katika hatua isiyotarajiwa, polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya, Zuberio Mwombeki, waliwapiga na kuwakamata watu kadhaa waliofuatana na Mbunge Lema ofisini kwake katika jengo la mkuu wa wilaya bila sababu za msingi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema hana taarifa ya zoezi hilo na kuahidi kuwa atalifuatilia na kutoa taarifa baadaye.

October 29, 2011

'LIVE' SHEREHE YA KUMPONGEZA ATHINA ADVOCATE NYOMBI USIKU HUU IRINGA


Athina akiwa katika pozi la kisomi baada ya kutunukiwa leo
Mama mzazi wa Athina Nyombi akimkumbatia mwanae kwa furaha kubwa
Wazazi wa Athina wakiwa katika picha ya pamoja ,kulia ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Nyombi
Wadau wakiendeleza libeneneke nyumbani kwa Nyombi mjini Iringa

Mchungaji Mpeli Mwaisumbe na mkewe wakiwa na mama mzazi wa Athina kulia pamoja na Athina mwenyewe
Athina akiwa na wachungaji Mpeli Mwaisumbe na Neema Mwaisumbe
Athina akiwa na wazazi wake
Wazazi na familia ya Athina Advocate Nyombi wakifurahia kwa kugonganisha grasi na mtoto waoBaba mzazi wa Athina kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi (kulia) akigonganisha grasi na mchungaji Mpeli Mwaisumbe
Baadhi ya wageni waalikwa katika sherehe hiyoMhitimu Athina Nyombi wa pili kushoto akiwa na wazazi wake
Mama mzazi wa Athina akifungua shambeni
Wadau wakiendelea kupata taratibu huku wasishuhudia tukio

Sherehe ya kumpongeza Athina Advocet Nyombi kwa kuwa mmoja Kati ya wahitimu ktk chuo cha Tumaini Iringa (MBA-HUMAN RESOURCE MANAGEMENT)Sikiliza VIDEO yake hapa