Sakata la mauwaji ya kinyama yanayonyika usiku kwa watu kupigwa nodo jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa 45.

Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Mbeya Esther Macha anaripoti kuwa Kamanda mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alisema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu 45 wanaohusika na mtandao huo na kwamba doria bado inaendelea usiku na mchana ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo vya usalama na kushirikisha wananchi katika polisi jamii Ulinzi shirikishi katika kata na vijiji vya jiji la Mbeya hususan taarifa za siri.Hata hivyo kufuatia kuibuka kwa wimbi la upiganaji Nondo Mkoani Mbeya waharifu wamebuni mbinu mpya ya kuwatuma watoto wadogo kuwalaghai wananchi kuwa wamepotelewa na familia zao pindi wanapowarejesha huvamiwa na kupigwa nondo na makundi ya waharifu yaliyoibuka kwa kasi Mkoani hapa.

Akizungumza wakati mamia ya watu walipofika katika katika eneo la FFU polisi kumuaga Askari polisi kitengo cha karakana PC Meshack Urasa (28) mwenye namba za kijeshi STG 2795 aliyeuwawa kwa kupigwa nondo September 26 mwaka huu katiukia eneo la Mbalizi road kitongoji cha Mabatini na mwili wake kusafirishwa kupelekwa Mkoani Kilimanjaro ,Mwenyekiti wa kata ya Mbalizi Road sehemu alipokuwa akiiishi marehemu Meshack, Bi.Rejina Mdendemi alisema kuwa tukio hilo lilitokea septemba 26 majira ya saa 4 za usiku wakati marehemu alipokuwa akirejea nyumbani kwake .


Alisema kuwa kabla ya mauti kumkuta marehemu akiwa njiani alikutana na kundi la watu watatu waliojitambulisha kuwa ni Askari polisi huku pembeni yao kukiwa na watu watatu walikuwa wamepigwa nondo wakiwa wamelala chini na alipowataka kuonyesha vitambulisho ndipo walipomshambulia kwa nondo na kupoteza maisha.


“Mimi mwenyekiti nilipigiwa simu majira ya saa nne na nilipofika eneo la tukio nilikuta marehemu akiwa amefariki dunia na huku pembeni yake kukiwa na vijana wengine watatu wakiwa wamepoteza fahamu na kukimbizwa hosptali kupatiwa matibabu’Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Rwanda Mkoani Mbeya Bw. Michael Kandoro alisema kuwa kitendo cha askari polisi kukaa uraiani ni kuhatarisha maisha yake kwani jeshi la polisi linapaswa kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kila askari anayehitimu mafunzo lihakikishe anapatiwa nyumba katika makambi ya jeshi ili kuwahakikishia usalama wa maisha yao mahala pa kazi.

Alisema kuwa kitendo cjha askari polisi kukaa uraini ni kuhatarisha maisha yake hasa ukingatia mazingira ya kazi yake , hivyo jeshi la polisi linatakiwa kuzingatia hilo ili kuhakikishas kuwa hali hiyo inarekebishika.

Aidha alisema kuwa pia jeshi la polisi linatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha na jamii hususan vyombo vya usalama katika kuhakikisha wahusika wa matuki haya wanatiwa mikononi mwa sheria kwani hii ni aibu kwa mkoa na ukicheka na nyani utavuna mabua kwani hilo ni kundi la watu ambalo limepanga kuuchafua mkoa na kwamba endapo ushirikiano ukawepo tutaweza kulitokomeza.

Bw. Kandoro alisema kuwa kuwa isifikie wakati jehi la polisi kuto fanya masiala katika matukio haya kwani yamekuwa ni ya mfululizo na kuchangia hofu kwa wananchi kushindwa kuendelea na shughuli mbalimbali za maendeo na badalaya yake kujikuta wakiyumba kiuchumi.