Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

July 31, 2011

MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UMEONEKANA NCHINI KENYA USIKU HUU ,MFUNGO KUANZA KESHO

mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanza kesho baada ya mwezi kuonekana leo huko Mombasa Kenya taarifa hii kwa mujibu wa Mufti wa Tanzania Shaaban Bin Simba ambaye amewataka waslam nchini kote kunuia usiku huu na kuanza mfungo hapa kesho .Mtandao huu unawatakia kila mfungo mwema waislamu wote

TAIFA STARs KUMINYANA NA CHAD KOMBE LA DUNIA 2014


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 31, 2011
STARS v, CHAD KOMBE LA DUNIA 2014
Upangaji makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.
Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil.
Stars ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba 10, 2013.
Kwa mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo haikuthibitisha ushiriki wake.
Timu 10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA MJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma, leo Julai 31, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo Julai 31, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu kilichoanza leo Julai 31, 2011 katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

'LIVE" HAFLA YA KUWAPONGEZA WANAMICHEZO MASHULENI MCHANA HUU IRINGA

katibu tawala wa mkoa wa Iringa Getrude Mpaka akipiga mpira kuzindua mchezo wa kirafiki kati ya timu ya shule ya viziwi Iringa na lugalo sekondari mchezo uliomalizika bila kufungana
Wanafunzi wenye matatizo ya kusikia (viziwi) wakipongezanaHawa ndio walioufanya mkoa wa Iringa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUTA
Mgeni rasmi katiwa tawala wa mkoa wa Iringa Bi.Getrude MPaka akiwapongeza wachezaji wa timu ya Viziwi mkoa wa Iringa kwa kuwa mabingwa wa Taifa
Ras Iringa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Lugalo Sec kabla ya mchezo wao wa kirafiki na shule ya viziwi Iringa

KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA YAPATA VIONGOZI WAPYA,MMILIKI WA MTANDAO HUU AULA UKATIBU MSAIDIZI

Uchaguzi ni uchaguzi nimeshindwa kwa kura moja ila naunga mkono matokeo ni Sima Bingileki na Daud Mwangosi ambaye ni mwenyekiti mpya wa IPC
Sulemani Boki amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uweka hazina ndani ya IPC kwa kupata kura 16 kati ya 7 alizopata mpinzani wake Mawazo Marembeka(RFA) Iringa
Mwanachama wa TGNP mkoa wa Iringa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoa wa Iringa Tumain Msowoya akiomba kura kwa wanachama katika nafasi ya umakamu mwenyekiti japo hakuweza kupita baada ya kupata kura 6 kati ya 23 zilizopigwa
Mwandishi wa Radio Free mkoa wa Iringa Bw.Mawazo Marembeka akiomba kura kwa wanachama wa IPC katika nafasi ya uweka hazina japo hakuweza kupita baada ya kupata kura 7 kati ya 23 zilizopigwa
Mwandishi wa Chanel Ten Iringa Bw.Daud Mwangosi ameshinda nafasi ya uenyekiti IPC kwa kupata kura 12 kwa 11 alizopata mpinzani wake Sima
Afisa habari wa IMTV Iringa Bi.Sima Bingileki aliyekuwa mpinzani mkali wa Mwangosi katika kiti alishindwa kwa kura moja
Mwandishi wa The.Citizen na Radio Country fm Iringa Bw.Clement Sanga aliyekuwa mgombea wa nafasi ya ukatibu na kupata kura 6 kati ya 23 zilizopigwa hivyo kushindwa nafasi hiyo
Mwandishi wa magazeti ya serikali mkoa wa Iringa Bw.Frank Leonard amefanikiwa kutetea nafasi yake ya ukatibu kwa kpindi cha tatu mfululizo kwa kupata kura 17
Zulfa Shomari akijibu maswali ya wanachama ndani ya ukumbi wa Maktaba wakati wa uchaguzi mkuu wa IPC ,alikuwa akigombea nafasi ya umakamu mwenyekiti na kushinda nafasi hiyo kwa kishindo kwa kura 17 kati ya 6 alizopata mpinzani wake

Wanachama wa IPC wakipitia taarifa mbali mbali za chama kabla ya uchaguzi kutoka kushoto mbeli ni Frederick Siwale,Getrudde Madembwe na Anita Boma
Rais wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Simbaya ndiye alikuwa mwenyekiti wa IPC kabla ya kuamua kustaafu nafasi hiyo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard na kulia ni weka hazina wa IPC Sulemani Boki
Baadhi ya wanachama wa IPC wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliochaguliwa kuongoza IPC ,mwenye pama katikati ni mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin ambaye alipita bila kupingwa katika nafasi ya ukatibu msaidizi wa IPC

Katika uchaguzi huu viongozi walioanguka katika uchaguzi huo ambao walikuwemo katika safu ya uongozi katika uongozi uliopita ni pamoja na Sima Bingileki ambaye alikuwa makamu mwenyekiti,huku Eliasa Ally ambaye alikuwa mjumbe kipindi kilichopita akijitoa kugombea tena nafasi hiyo na Kenneth Simbaya akiamua kustaafu nafasi ya kiti pamoja na Hakimu Mwafongo ambaye hakugombea tena nafasi ya ukatibu msaidizi .

Katiba nafasi ya uweka hazina msaidizi Vicky Macha wa Nipashe Iringa alipita bila kupingwa huku nafasi ya katibu msaidizi pia Francis Godwin mwandishi wa gazeti la Tanzania daima Irina ,kurugenzi wa kampuni ya Free Community Media's na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za jinsia Tanzania (TGNP) mikoa ya kusini akipita bila kupingwa pamoja na wajumbe 13 7 wa kamati ya utendaji ndani ya IPC pia wakipita bila kupingwa kufuatia Eliasa Ally kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Wajumbe 13 wanaounda kamati ya utendaji ndani ya IPC ni pamoja na Daud Mwangosi, Frank Leonard ,Zulfa Shomary, Francis Godwin, Suleman Boki,Vicky Macha, Getrude Madembwe, Shabani Lupimo, Frederick Siwale,Conard Mpila,Fulgence Malangalila,Janeth Matondo na Jackson Manga .

SENGO NI MABINGWA KOMBE LA PLANET 2000 IRINGA YAIADHIBU POLISI

Wachezaji wa timu ya Sengo FC wakishangilia ubingwa dhidi ya polisi Iringa
Mratibu wa mashindano hayo Abuu Changawa Majeki(kulia) akiwashukuru TASWA Iringa kupitia mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na wadau wengine kwa kudhamini mashindano hayo
viongozi mbali mbali wakiongowa na katibu wa chama cha soka mkoa wa Iringa Elud Mvella (wa pili kulia) Jesca Msambatavangu na dhamini mkuu wa mashindano hayo MR.Mbata ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Planet 2000 wa kwanza kushoto ni katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Alex
Mkurugenzi wa shule ya Star na kada maarufu wa CCM mkoa wa Iringa Jescar Msambatavangu akikabidhi zawadi kwa mfungaji bora katika mashindano ya Planet 2000

Timu ya Sengo ya Kihesa imeibuka bingwa katika fainali ya mashindano ya Planet 2000 baada ya kuiadhibu timu ya polisi Iringa kwa jumla ya magoli 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Katika mashindano hayo chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) mkoa wa Iringa kupitia mtandao huu kilipata kutoa zawadi kwa waamuzi na mashindano hayo na timu yenye Nidhamu kwa kuizawadia mpira pamoja na kununua magoli mawili ya Sengo kwa jumla ya shilingi 35000.

Huku mkuu wa shule ya Star Jesca Msambatavangu akitoa zawadi kwa mfungaji bora mashindano hayo yameendeshwa kwa muda wa mwezi mmoja kwa timu zaidi ya 10 kushirikishwa

MAONYESHO YA WIZARA YA MADINI BANDA LA TANZANITE LAVUTIA

Watanzania wakipata maelezo ya mgunduzi wa Tanzanite
Moja ya kivutio kilichokuwepo katika maonesho ya Wizara ya Nishati na Madini ni ushiriki wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite kama anavyonekana.( Picha na Samwel Mtuwa - GST-Dodoma)


Wanafunzi wa Shule ya msingi Mtendeni , wakiwa katika banda la Wakala wa Jiolojia (GST) wakiangalia Darubini ya upimaji madini ya enzi za Mkoloni iliyopo katika makumbusho ya GST , DODOMA , hii ilikuwa katika maonesho ya Wizara ya Nishati na Madini ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru

BREANKING NEWzzzzzzzzzzzz MEYA WA SONGEA AFARIKI DUNIA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Ali Saidi Manya, Diwani wa kata ya Lizaboni(Mwenye suti Nyeupe) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Misheni Peramiho.

Taarifa za Msiba huo zimetangazwa na naibu Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Mariam Dizumba na kupokelewa kwa mshtuko mkubwa na wakazi wa manispaa ya Songea Mkoa wa ruvuma kwa ujumla.

Naibu Meya Dizumba amesema mazishi ya Mstahiki Meya Ali Saidi Manya yatafanywa nyumbani kwake Lizaboni Manispaa ya Songea Siku ya Jumatatu Tarehe 1 Agosti 2011. Maandalizi yanaendelea na wageni kadhaa wa vyeo mbalimbali wamethibitisha kuhudhuria.

Mtandao huu unaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAFUNIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB

Mwanamuziki Ludacriss akipewa tafu na mwanamuziki mwenzake Jazman aliyeongozana naye katika ziara yake hii ya kimuziki nchini Tanzania.
Mashabiki mbalimbali wakiangalia fataki zilizokuwa zikipigwa katika viwanja vya Leaders kama ishara ya kusherehekea miaka kumi ya Serengeti Fiesta.
Fataki zikilipuka juu baada ya kupigwa katika viwanja vya Leaders usiku huu katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Msanii wa muziki wa bongofleva Linex kutoka jijini Mwanza akipagawisha mashabiki lukuki waliojitokeza katika, tamasha la mwendelezo wa msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta .
Mashabiki wakishangilia kwelikweli katika tamasha hilo.
Msanii Lina kutoka THT akionyesha uwezo wake katika jukwaa huku akiwa amepiga kivazu cha aina yake.
Hapa mashabiki wakisherehekea miaka 10 ya Serengeti Fiesta kama unavyoona katika picha.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bw. Richard Wells na Mkurungezi wa Masoko Ephrahim Mafuru wakionyesha Golden Moments ndani ya Serengeti Fiesta.
Rais wa Masharobalo akiimba katika tamasha hilo.
Yaani ni Full majotrooo kama unavyoona mdau wa Fullshangwe.
Msanii wa muziki wa bongo fleva Juma ataluma akiwashangwesha mashabiki wa muziki
Kama unavyoona umati mkubwa katika tamasha hilo ni kweli Serengeti Fiesta ni tamasha la watu
Kulia ni Bahati Singh na Nandi Mwiyombela kutoa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL wakicheza kwa furaha.
Mwasiti aliyesimama katikati akiwa na wasanii wenzake kutoka THT.
Fid Q katikakati na Dully Sykes aliyeinama kwa nyuma wakiwa na wasanii wenzao katika onyesho hilo.
Kushoto ni Recho , Lina kutoka THT na kulia ni Chege Chigunda kutoka TMK Family. Msanii Juma Mataluma na wenzake wakifuatilia luninga iliyopo nyuma ya jukwaa ili kujua kinachoendelea katika tamasha hilo
Mashabiki wakishangilia kwa furaha kutokana na burudani murua zinazotolewa na wasanii mbalimbali katika tamasha hilo.

Mwanamuziki Ludacriss wa kimataifa kutoka nchini Marekani akifanya vitu vyake kwenye tamasha la mwendelezo wa msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta, linaloendelea usiku huu katika viwanja vya Leaders Kinondoni umati mkubwa wa watu umeingia katika tamasha hilo na watu wengine wanaendelea kuingia katika viwanja vya Leaders Mwanamuziki huyo ameonekana kuwachanganya mashabiki wake kutokana na mashabiki hao kuonyesha kufurahishwa na muziki wa msanii huyo kutoka Marekani, huku wakipiga mayowe na kunyoosha mikono yao juu juu, kama ishara ya kuunga mkono kila alichokuwa akikifanya jukwaani mwanamuziki Ludacriss.