Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2011

SOLOMON MUKUBWA,NEEMA MWAIPOPO ,MARTHA RAMADHAN NA JENIFA MGENDI KUWASHA MOTO JUMAMOSI IRINGA


Martha Ramadhani akiwa na wacheza show wake
Jenifa Mgendi

TAMASHA kubwa la nyimbo za injili ambalo kwa mara ya kwanza kufanyika mkoa wa Iringa linataraji kufanyika jumamosi ya Julai 2 mwaka huu katika ukumbi wa Highland na kupambwa na waimbaji maarufu wanne akiwemo Solomoni Mkubwa kutoka Kenya.

Mratibu wa tamasha hilo Edwin Bashir aliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa tamasha hilo ambalo linategemewa kuwa ni la kihistoria ndani ya mji wa Iringa na mkoa kwa ujumla litapambwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za injili Mkubwa , Neema Mwaipopo, Martha Ramadhani na Jenifa Mgendi.

Alisema kuwa lengo la tamasha hilo ndani ya Manispaa ya Iringa ni kutaka kutoa burudani ya nyimbo kwa wakazi wa mji wa Iringa hasa kupitia nyimbo hizo za injili ambapo ni kwa mara ya kwanza wakazi wa mji wa Iringa wanashuhudia wasanii wanne mmarufu katika jukwaa moja .

Bashir alisema kuwa tamasha hilo la nyimbo za injili limeandaliwa na kituo cha Radio Ebony Fm ambapo katika kuhakikisha wadau wote wa muziki huo wa injili wanapata kushuhudia tamasha hilo kiingilio kilichowekwa ni cha hali ya chini ambapo kila mmoja atapata kuona tamasha hilo kwa kiingilio cha shilingi 10,000 na 15000 kwa V.I.P

Alisema kuwa tamasha hilo linataraji kuanza majira ya saa 1 za usiku na kuwataka wadau wa nyimbo za injili kufika mapema katika ukumbi huo ambapo kwa hali inavyoonyesha ukumbi huo utakuwa mdogo na kuna uwezekano wa wale watakaochelewa kukosa nafasi.

BREAKING NEWS....TAKUKURU IRINGA YAMNG'ANG'ANIA MWENYEKITI WA CCM KWA RUSHWA

Mkurugenzi wa TAKUKURU,Bw.Edward Hosea

TAASISI ya kupambana na kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imemfikisha mahakamani mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mtaa wa Kihodombi katika Manispaa ya Iringa Aldo Kaduma (50)kwa tuhuma za kujifanya afisa wa taasisi hiyo na kuomba rushwa ya shilingi 400,000 kutoka kwa paroko wa Ihemi Iringa vijijini asifukuzwe nchini ndani ya masaa 24 kwa kosa la kumtetea mfanyakazi wake aliyemweka kinyumba mwanafunzi.

Mwanasheria wa Takukuru, Nitume Mizizi alisema leo mahakamani hapo kuwa Kaduma alikamatwa Septemba 28, 2009 baada ya taasisi hiyo kupokea taarifa kutoka kwa Padri Pio Callegari (72) kuhusu mtuhumiwa huyo kuomba rushwa hiyo ili kusaidia kuendelea kuwepo nchini kabla ya taasisi hiyo kuwekea mtego wa rushwa uliozaa matunda.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliomba kuongezwa fedha kiasi cha shilingi 100,000 ili kufikia shilingi 400,000 ambazo aliomba awali na baadhi hya fedha hizo kupewa kabla .

"Kaduma alimtisha Padri huyo kwamba ofisi ya Takukuru mjini Iringa ambako yeye anafanya kazi imepokea taarifa ikumuhusu Padri huyo kutoa rushwa kwa askari wa kituo cha Polisi Ifunda ili kuzima kashfa ya mfanyakazi wake kumtorosha mwanafunzi huyo na kuishi naye"

Hata hivyo kabla hajapewa fedha hizo, Padri huyo na wasaidizi wake walibaini kwamba Kaduma si afisa wa taasisi hiyo na nyingine yoyote ya usalama kwani walipokwenda katika ofisi ya Takukuru mjini Iringa ili kuomba msaada wake ilibainika kwamba hakuna mfanyakazi mwenye jina kama hilo katika ofisi hiyo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu aliwaomba wakutane katika maeneo ya hotel ya Staff Inn Annex iliyopo mjini Iringa ili wamalize suala hilo ambalo bila kujua tayari suala hilo liliripotiwa Takukuru .

Kaduma aliingia mikononi mwa Takukuru kirahisi baada ya Padri huyo na Takukuru kutengeneza mtego uliowezesha kukamatwa kwake baada ya kukubali kupokea Sh 150,000 kati ya Sh 400,000 alizoomba.

Padri Callegari ambaye anafanyashughuli zake katika Kanisa la Romani Katoliki, Parokia ya Ihemi Iringa Vijijini ambaye mmoja wa wafanyakazi wake alikuwa akituhumiwa kumweka kinyumba mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Ihemi kabla ya paroko huyo kumsaidia .

Hata hivyo wengine wanaodaiwa kutishwa na mtuhumiwa huyo kuwa ni pamoja na Velenci Nhyengelo (44) ambaye ni mzazi wa mwanafunzi huyo ,Antony Maginga(37) ambaye ni mtumishi wa shamba la Paroko huyo na mkuu wa shule ya Ihemi Edga Mkwama ambao walitishwa kuwa kama hawatamshawishi paroko huyo kutoa fedha hizo baada ya paroko huyo kuondoldewa nchini ndani ya masaa 24 kurudi kwao Italia wao watafungwa jela miaka 30 kila mmoja.

Zaidi soma gazeti la Tanzania daima kesho

WADAU WA RUCO WAKIJINAFASI MCHANA HUU

Wadau wa mtandao huu kutoka chuo cha RUCO mjini Iringa wakijipendelea kwa vinywaji baada ya kuhitimu katika chuo hicho na leo kukutana pamoja kutoka kushoto ni Frank ,Benny na Mjuni

"Siku moja moja kwa afya si mbaya"

HALI YA MAMA WA MBUNGE ABWAO NI MBAYA

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao akimuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye amerejeshwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa mgonjwa huyo anasumbuliwa na matatizo ya mshtuko wa moyo na kupelekea kupooza mguu wa kushoto na mkono hali iliyomlazimu mbunge Abwao kusitisha kuhudhuria kikao cha bunge Dodoma na kurudi kuuuguza mzazi wake huyoMBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) Chiku Abwao amelazimika kuomba ruhusa bungeni na kurudi nyumbani Iringa kumuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye hali yake kiafya ni mbaya zaidi.

Akizungumza na mtandao huu leo nyumbani kwa mbunge huyo eneo la Gangilonga ambako kwa sasa mama yake yupo baada ya kutolewa Hospital ,Abwao alisema hali ya mgonjwa wake si nzuri sana hali ilkiyomlazimu kurudi kutoka bungeni na kuja kumuuguza .

Alisema kuwa mama yake ambaye wiki moja kabla alikuwa amezidiwa kupitia kiasi anasumbuliwa na tatizo la mshtuko wa moyo ambalo limepelekea kwa sasa baadhi ya viungo kupooza .

Abwao alisema kuwa kabla ya kulazwa katika Hospital hali yake ilikuwa ni mbaya zaidi na kuwa kwa sasa hali yake japo imeendelea kuwa nzuri ila tayari amepooza mkono wa kushoto na mguu na kuwa amekuwa ni mtu wa kushinda amelala na akijitahidi sana amekuwa akiishia kukaa juu ya kitanda chake.

Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa daktari wake amekuwa akifika kumtibu nyumbani japo bado kupona kwake tatizo hilo anamtegemea zaidi mwenyezi Mungu.

WAZAZI WA WATOTO VIZIWI WADAIWA KUWATELEKEZA SHULEWAZAZI wa watoto wenye matatizo ya kusikia (Viziwi) wanadai kutelekeza watoto wao katika shule ya msingi ya viziwi Mtwivila katika Manispaa ya Iringa.

kaimu afisa elimu Manispaa ya Iringa Vincent kalinga aliyasema hayo wakati akifungua warsha ya siku moja ya wazazi wa watoto viziwi ,watendaji wa serikali za mitaa na viongozi wa chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa mbali ya kuwepo kwa tatizo sugu la baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wao wenye ulemavu kupata elimu ila bado hata wale wachache wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo wamekuwa wakiwatelekeza watoto wao shule bila kuwahudumia wala kuwafuata mara baada ya likizo.


Afisa elimu huyo aliwataka wazazi wa wenye watoto wenye ulemavu kutoendelea kuwwatelekeza watoto wao katika shule hiyo ama kuwaficha majumbani kwao na badala yake kuwapa elimu kama ilivyo kwa watoto wengine.

Alisema katika shule hiyo ya Mtwivila kuwa watoto 199 viziwi wanaosoma hnapo na kati yao watoto 56 ni wasichana na wavulana 63 ambayo ni idadi ndogo sana ukilinganisha na ile ya watoto wote wenye matatizo hayo ambao wapo majumbani wamefichwa.

Awali katibu wa CHAVITA mkoa wa Iringa Shaibu Juma alisema kuwa warsha hiyo imeandalkiwa na Chavita mkoa wa Iringa kwa ufadhili wa The foundation for civil society kwa lengo la kuifanya jamii kutambua wajibu wao kwa watoto wenye ulemavu.


Hata hivyo alisema kuwa walemavu wameendelea kutengwa na huduma na sheria mbali mbali zilizopo hapa chini na kufanya wajikute kama ni yatima katika Taifa .

Alisema kuwa huduma zinazotolewa kwao hazikidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu na wamekuwa wakiachwa nyuma katika mchakato mzima wa maendeleo ya Taifa, Ingawa zipo jitihada mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma muhimu mfano Elimu,Afya na usalama wa raia.

"Aidha bado inaelekezwa dhana kuwa mtu mwenye ulemavu anastahili kuishi maisha tegemezi dhana ambayo inakwenda kinyume na tamko la umoja wa mataifa kuhusu Haki za binadamu na Azimio la umoja wa mataifa kuhusu fursa sawa na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu la mwaka 1983(Un standard rule on equalization of opportunity with disabilities)"


June 29, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA BALOZI WA VIETNAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Duy Thien, wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Picha na Muhidin Sufiani-OMR

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AKUTANA NA BALOZI WA VIETNAM NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumatano Juni 29, 2011 ametembelewa na Balozi Nguyen Duy Thien wa Vietnam nchini Tanzania ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Thien pamoja na kufikisha salamu za watu wa Vietnam kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia alimueleza Makamu wa Rais kuwa anayo furaha kuwapo hapa Tanzania ambapo sasa ametimiza miaka miwili kufuatia Tanzania kuwa nchi yenye amani na utulivu. Pia alifafanua kuwa uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Vietnam ni wa kihistoria tangu wakati wa kupigania uhuru na nchi yake imekuwa ikiithamini Tanzania kama nchi rafiki ambayo wanaitazama sana katika uhusiano zaidi hasa katika sekta za uchumi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimueleza Balozi Thien kuwa Vietnam kama ilivyo Tanzania imepitia mapambano kadhaa ya kihistoria lakini akaishukuru serikali ya Vietnam kwa kupiga hatua hasa katika kilimo. “Natambua katika eneo la kilimo tunaweza kushirikiana kwa ukaribu, najua kwa upande wenu mmefanya vema hadi kuitoa nchi yenu katika nchi za chini kwa umaskini jambo ambalo na sisi tunapigana nalo kwa nguvu zetu zote,” alisema Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

Balozi Thien alimuomba Makamu wa Rais kutazama namna Tanzania na Vietnam zinavyoweza kutanua ushirikiano hasa katika kuagiza na kuuza mchele ili kuwafanya wafanyabiashara wa Vietnam kuleta nafaka nchini bila kupitia kwa madalali, jambo ambalo Makamu wa Rais alilipokea na kumuahidi Balozi Thien kuwa atalifikisha kwa wahusika serikalini ili watazame namna njema ya kulifanyia kazi. Kwa mwaka huu wafanyabiashara wa Vietnam wanashiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Sabasaba wakiwa na banda lao. Vietnam imefanikiwa kutanua uchumi wake kwa kasi licha ya kuwa sasa inakabiliwa na kushuka thamani kwa fedha yake na kwa mujibu wa Balozi wa nchi hiyo, hali hii inatokana na kutokuwa na nishati ya kutosha sambamba na hali mbaya katika soko la dunia. Kwa upande wa Tanzania eneo ambalo linabakia kuwa funzo na linaloweza kuchangia kukuza uhusiano kati ya Tanzania na Vietnam ni sekta ya kilimo na pia nchi hizi mbili zina historia ya uhusiano tangu wakati wa ukoloni.

Imetolewa na: Boniphace Makene

Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

Juni 29, 2011'LIVE' STUDIO ZA RADIO COUNTRY FM IRINGA ASUBUHI HII

Mtangazaji wa kipindi cha asubuhi Tulivu radio Country Fm Zamoyon Ngede akiwa katika kipindi asubuhi hii
Mmiliki wa mtandao huu Bw Godwin (kulia)akiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na watangazaji wa Radio Country Fm kuhusu mkatati wao kuendeleza michezo kupitia kituo chao,Godwin pia ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA ) mkoa wa Iringa
watangazaji wa Radio hiyo Temmy Mahondo na Zamoyon Ngede wakiwa katika mahojiano na mtandao huu.

KITUO hicho cha radio country Fm mkoani Iringa kimesema kwa kushirikiana na gazeti la Sayari kitaendelea kusaidia kukuza vipaji vya wasanii ndani ya mkoa wa Iringa na kuibuka vipaji vya wachezaji kupitia kipindi cha asubuhi tulivu kinachorushwa na kituo hicho kila majira ya asubuhi.

Mratibu wa mpango huo Zamoyon Ngede alisema kuwa wamelazimika kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na gazeti hili kama njia ya kutangaza kazi za wasanii ndani ya mkoa wa Iringa pamoja na michezo mbali mbali ambayo kimsingi imekuwa haipewi uzito wa juu katika vyombo vya ndani ya mkoa wa Iringa katika kuitangaza.

Ngede alisema kuwa kuanzia sasa kila siku ya Alhamis kituo hicho kitakuwa kikitoa nafasi ya kupromoti kazi za sanaa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali ambazo zitakuwa zikichapishwa pia katika gazeti hili huku jumatatu kipindi hicho kitakuwa kikichambua kwa kina habari mbali mbali za soka ndani ya Sayari kutoka mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa kusudi la kuanzisha mpango huo ni kutaka wadau wa burudani ndani ya mkoa wa Iringa kuhakikisha wanapata burudani kupitia vyombo hivyo ambavyo vimekuwa vikitegemewa zaidi na wadau wa mkoa wa Iringa na watanzania katika kupata burudani mbalimbali.

Zaidi soma gazeti la Sayari Alhamisi (Kesho)

CCM YAIVURUGA CUF MTWARA

Aliyekuwa mwanachama wa CUF na mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita, Mohamed Chiungulumana akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipotangaza kurejea CCM kwenye mkutano uliofanyika 28/6/2011 mjini Mtwara. Jumla ya wanachama 154 wa CUF walijiunga na CCM katika mkutano huo.Kuhsoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.
NA BASHIR NKOROMO, MTWARA

CHAMA cha CUF kimepata pigo mkoani Mtwara, baada ya wananchama wake 154 kutangaza kukihama chama hicho na kukabidhi kadi zao kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini hapa.

Baada ya kutangaza kuhama CUF wanachama hao walikabidhiwa kadi za CCM na kusema wameamua kuhamia CCM baada ya kubaini kwamba viongozi wa CUF wanapigania maslahi yao binafsi na si ya wananchi kama ambavyo wamekuwa wakijinadi.

"Nisingependa kusema mengi siku ya leo, kwa kuwa nina furaha sana kurudi nyumbani, nimerudi na wenzangu baada ya kubaini kwamba wale viongozi wa CUF hawapiganii maslahi yetu wananchi bali yao binafsi", alisema, Mohammed Chiungulumana baada ya kukabidhi kadi yake ya CUF kwa Nape na kupewa ya CCM.

Chiungulumana ambaye alikuwa mgobea udiwani Mtwara mjini, aliwataka Watanzania kuacha kuhadaika na vyama vya upinzani kwa sababu hawataambulia chochote kama ilivyomtokea.

Mapema akihutubia mkutano huo uliofurika mamia ya watu, Nape alisema, alisema vyama vya upinzania ni sawa na baba wa kambo ambaye huonyesha mapenzi kwa mtoto kwa sababu ya kumfurahisha mama wa mtoto huyo hivyo viongozi wa upinzani wanapopiga kelele kwamba wanatetea haki za wanannchi huwa si kweli bali wanatengeneza mazingira ya kuboresha maisha yao binafsi.

Alisema, ni kutokana na tabia hiyo ndiyo sababu serikali inapopanga mipango mizuri yenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi wapinzania huibuka kupinga kwa kuwa kufanikiwa kwa mipango hiyo huwakosesha njia ya kuwalaghai wananchi.

Nape alisema moja ya mfano wa tabia hiyo ya wapinzani kuwa ni ule uliotokea katika bunge wakatika kupitisha bajeti ya mwaka 2011/2012, katika kikao kinachoendelea mjini Dodoma.

Alisema, baada ya CCM kuituma serikali iondoe ushuru kwenye mafuta ili kupunguza ukali wa maisha uliosababishwa na kupa kwa bei ya nishati hiyo, katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa upinzania walipinga isipitishwe lakini ikafanikiwa kupita kwa kuwa idadi yao ni ndogo kuliko ya wale wa CCM.

Nape alitumia fursa hiyo kufafanua kwa kina sababu na hatima iliyopo sasa baada ya maamuzi yaliyofanywa na CCM Aprili mwaka huu, katika kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma.

Alisema baada ya mabadiliko hayo hanayiotwa kujivua gamba, CCM imeongeza uwezo zaidi katika utendaji wake ikiwemo kusimamia serikali ili iweze kutekeleza vilivyo ilani ya uchaguzi ya Chama na pia kusogea zaidi kwa wananchi ili kukifanya Chama kuwa chao kuliko ilivyoanza kuonekana miaka ya karibuni.

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma ambaye ameambatana na Nape katika ziara ya mkoani hapa, alisema, baada ya mabadiliko hayo Chama kitahakikisha, kinaendesha taratibu zake kisayansi zaidi ikiwemo kuweka uratibu wa kuwajua kwa undani wanachama wake.

Alisema kufanya hivyo kutasaidia kuondoa wanachama mamluki ambao hawana manufaa kwa Chama kwa kuwa wengi wao hukisaliti Chama wakati wa uchaguzi.

Mwisho.

June 28, 2011

MAMBO YA UREMBO ,KUCHA ZINAUZWA....

Zinapatikana mjini Iringa

MASHINDANO YA PLANET 2000 YASHIKA KASI IRINGA VETERAN YAZIDI KUVUTA MASHABIKI

Kikosi cha timu ya Veteran mjini Iringa
Mchezaji wa Veteran akimtoka mchezaji wa Kitanzini wakati wa mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Samora
Mwamuzi wa mchezo kati ya Veteran na Kitanzini Abuu Changawa akiwasiliana na simu na jamaa zake ndani ya uwanja huku mchezo ukiendelea

MWIMBAJI EPHRAIMU MWANSASU AMFUNIKA FROLA MBASHA IRINGA

mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Ritta Moto kabati (kulia) akimzawadia pesa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili zenye jumbe kali ,Ephrahimu Mwansasu huku MC maarufu katika mikoa ya kusini na Tanzania wa matamasha ya nyimbo za injili mwanahabari Charlesy Mwakipesile akimweka mikono kichwani siku ambayo Mwansasu alipouteka mji wa Iringa wakati wa tamasha la uzinduzi wa kituo cha radio Furaha mjini Iringa,

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo akimpongeza Mwansasu kwa nyimbo zenye ujumbe wa kumtoa nyoka pangoni ,hakuna ambaye hakuguswa na nyimbo zake kiasi cha mwimbaji Frola Mbasha kujikuta hawajaimba chochote katika tamasha hilo
MWANSASU AKIWA NA MCHUNGAJI MPELI MWAISUMBE NA MKEWE NEEMA NA FAMILIA YA MCHUNGAJI HUYO NA WACHZA SHOW WA MWANSASU ,UTAISOMA MAKALA YA MWIMBAJI HUYO NDANI YA GAZETI LA SAYARI ALMAMISI HII

MUUNGANO SACCOS YAZIDI KUWAKOMBOA WANANCHI

MUUNGANO wa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo (MVUAMITA) umesema kuanzishwa kwa SACCOS bado hakujaleta tija ya kuwaondoa wajasiriamali katika uteja wa kunyonywqa na taasisi kubwa za kifedha.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Mbeya Bw.Joachim Nyambo anaripoti kuwa hali hiyo imebainishwa katika kongamano la ushirikiano wa vya ma ushirika wa akiba na mikopo lililofanyika mkoani Mbeya likiwakutanisha wadau mbalimbali kutoka Saccos zilizopo mkoani hapa huku watoa mada wakiwa ni pamoja na viongozi wa MVUAMITA taifa.

Mwenyekiti wa MVUAMITA(SCULT) taifa Amro Shayo amesema lengo la kuanzishwa kwa Saccos ilikuwa kuwawezesha wajasiriamali kuondokana na unyoonyjai uliotokana na riba kubwa inayotozwa katika mikopo kutoka taasisi kubwa za kifedha.

Hata hivyo Shayo amesema malengo hayo bado hayajafikiwa kwakuwa Saccosi zote nchini zimebaki tegemezi kwa taasisi kubwa za kifedha kwa kuchukua mikopo ya fedha ambazo huwakopesha wanachama wake hivyo unyonyaji kuendelea kuwepo.

Hata hivyo amesema ni wakati kwa Saccos kurejea katika malengo yake iwapo kweli zimedhamiria kuwakomboa wajasiriamali ambapo alisema moja ya mbinu mahususi itakayoziwezesha kuzipa nguvu ni umoja utakaotokana na Saccos zote kujiunga katika muungano wa Mvuamita ili ziwe na sauti ya pamoja.

Kwa mujibu wa Afisa ushirika mkoa wa Mbeya Frederick Kifaru mkoa wa Mbeya una jumla ya vyama vya ushirika vilivyosajiriwa 572,kati ya hivyo Saccos ni 318 sawa na asilimia 55 ya vyama vyote vya ushirika huku wanachama wakiwa 56,842 sawa na asilimia 63 ya wanachama 90,473 wa ushirika idadi anayosema bado ni ndogo.

Amefafanua kuwa kati ya Saccos 318 zilizosajiriwa,ni 114 pekee sawa na asilimia 36 zilizojiunga na Mvuamita hivyo kuendelewa kuwepo na changamoto ya kuhakikisha kunakuwepo na muungano wa vyama hivyo ili kuweza kuwa na kauli moja katika masualaa ya mikopo.

Awali akifungua kongamano hilo la siku moja,katibu tawala msaidizi Moses Chitama amesema hivi sasa umejitokeza urafiki mkubwa kati ya Saccos na wakopeshaji wanaolenga kupata faida kubwa kwa kivuli cha kuzisaidia kimitaji na uwezo wa kujiendesha jambo linaloleta hofu kwakuwa hakuna uhakika kuwa urafiki huo una nia njema.

Mwisho.

WAKULIMA 20,000 katika wilaya za Mbeya,Kyela na Mbozi mkoani Mbeya wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uhifadhi wa mazao gharani wa Storage and Proper Post Harvest Improvement for Resource Efficiency (SAPPHIRE).

Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoa wa Mbeya Joachim Nyambo anaripoti kuwa Mradi huo utakaowanufaisha wakulima wa mahindi na mpunga katika wilaya hizo utaendeshwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo na shirika linalojihusisha na masuala ya kilimo la Techno Serve kwa kushirikiana na shirika la mapinduzi ya kijani barani afrika AGRA.

Mkurugenzi wa mradi huo kupitia Technoserve nchini Hillery Miller alisema katika mkutano na wadau mbalimbali wa kilimo uliofanyika jijini Mbeya kuwa takwimu zinaonesha asilimia 40 ya mazao ya mkulima nchini hupotea kutokana na uhifadhi mbovu ambao huanzia wakati wa kuvuna.

Miller amesema kutokana na ufinyu wa maeneo ya kuhifadhi mazao yao,wakulima wamekuwa wakilazimika kuuza mazao yao kwa bei ya hasara mara tu baada ya kuyavuna na hivyo kutonifaika ipasavyo na matunda ya kazi yao.

Amefafanua kuwa hata wachache wanaoonekana kuhifadhi,wanafanya hivyo kwa kungoja bei pekee pasipo kuangalia uweezekano wa kuyaongezea ubora mazao yao.

Ameelezea mikakati iliyowekwa kukamilisha mpango huo kuwa ni pamoja na kuhakikisha unapunguza upotevu wa mazao mashambani na maghalani kwa kuanzisha na kufanya kazi na maghala 20 yaliyopo mkoani Mbeya.

Amesema mkakati wa pili ni kuhakikisha mghala hayo yanajiendesha kibiashara ili yaweze kuwaletea tija wateja watakaojiunga na mradi huo ili waweze kubadili maisha yao na kuonesha mfano bora kwa wenzao.

Mkakati mwingine ni kuwaunganisha wakulima na vyombo vya kifedha ikiwemo mabenki ili waweze kupata mikopo kwa urahisi na kwa riba nafuu ili waweze kuendesha shughuli zao kwa urahisi pasipo kulazimika kuuza mazao yao hata kwa bei ya hasara ili watatue matatizo yao.

Kuzijengea uwezo taatisi kubwa za kuwasaidia wakulima utakuwa ni mkakati pia ambao utalenga kuzipa uwezo bodi ya maghara nchini pamoja na baraza la mazao Afrika mashariki.

Hata hivyo Miller amesema kufanikiwa kwa mradi huo kutategemea mchango wa wadau aliowataja kuwa ni pamoja na idara mbalimbali za serikali za wilaya na mkoa,vikundi vya wakulima,Saccos,wasafirishaji pamoja na mtu mmojammoja.

Mwisho

"LIVE" MKUTANO WA INJILI UMOJA WA MAKANISA MWEMBETOGWA IRINGA MAPACHA WAWILI WAITEKA IRINGA

Mhubiri kutoka Uganda akiingiza kundini waumini wapya
Wakristo wapya wakiombewa na mhubiri toka Uganda jioni hii
mamia ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiwa katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa katika mkutano wa injili uliandaliwa na umoja wa makanisa mjini Iringa kuendeshwa na wahubiri kutoka nchini Uganda maarufu kwa mapacha wawili
Viongozi wa huduma ya kiroho mjini Iringa wakizama katika maombi
mmoja kati ya wahubiri Mapacha wawili kutoka Uganda akihubiri katika uwanja wa Mwembetogwa ,mkutano huu umeonyesha kuuteka mji wa Iringa
maombezi yakiendelea katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa ,mkutano huu unataraji kuhitimkishwa jumapili ijayo katika uwanja huu.

"LIVE" ZIARA YA KUBAINI VIVUTIO JIWE GANGILONGA MJINI IRINGA

mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin akiwa juu ya jiwe Gangilonga huku akiendeleza libeneke kama kawa ,ni katika ziara ya kutembelea vivutio vya ndani ya Manispaa ya Iringa ambavyo vipo ila havipo katika orodha ya vivutio vya mkoa
Wadau wa mtandao hjuu akiwa amejipumzisha juu ya jiwe Gangilonga mjini Iringa ,Gangilonga kwa wenyeji wahehe ni jiwe linaloongea
Mwanafunzi wa sekondari ya Mwembetogwa mjini Iringa Alex Kibasa (kushoto) akiwa na mwanalibeneke Godwin katika jiwe hilo akitazama jinsi matukio yanavyowekwa katika mtandao
wadau Alex Kibasa ,Mengi Myovela na Chely wakiwa juu ya jiwe gangilonga mjini Iringa jioni hii ni katika kuhamasisha utalii wa ndani
kazi inaendelea juu ya jiwe Gangilonga hapa mtandao unapatikana vizuri zaidi ya mjini
Changamoto kwa serikali ya mkoa wa Iringa kuangalkia jinsi ya kulitangaza jiwe hilo ambalo ni asili ya eneo la gangilonga ambako ndiko kuna Ikulu ndogo ya mkoa wa Iringa

MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI MATATANI KWA KUINGIA BENKI YA CRDB NA SILAHA

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia Manispaa ya Iringa wakiwa wamemkamata mlinzi wa kampuni mmoja ya ulinzi jina (limehifadhiwa) baada ya kuingia banki ya CRBD mchana huu na silaha kinyume na taratibu za taasisi za fedha na kudhaniwa kuwa ni jambazi
Hapa akipelekwa kituo cha polisi pamoja na mteja wake ambaye alikuwa amemkodi mlinzi huyo kwa ajili ya kumsindikiza kuchukua fedha
wananchi wakishuhudia tukio la kukamatwa kwa mlinzi huyo na kupokea kipigo toka kwa FFU

OFA MAALUM NDANI YA BC STATIONARY&SECRETARIAL SERVICES

Ni stationary mpya kabisa katika Manispaa ya Iringa tupo kihuduma zaidi kwa gharama nafuu kuliko kote ndani ya mkoa wa Iringa
Kumbuka tunatoa kwa ofa maalum huduma kama Photocopy kwa Sh 25/=,Lamination kwa Sh 500/,lim paper kwa Sh 7500/, kuchapa page 1 kwa Sh 500/n.kWasiliana nasi kwa simu 0757051666 na 0756212902 tutakusikiliza tutakufikia kumbuka tunatoa huduma kwa ubora na uhakika zaidi tupo jirani na ofisi ya CCM mkoa wa Iringa ,tunatazamana na jengo hilo la CCM barabara ya MR- MKWAWA IRINGA ana uliza Luxury Bar

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA, SUDAN NA ZAMBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mavis Lengalenga, baada ya mazungumzo wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, John Mutinda Mutiso, wakati alipofika kumtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Juni 28, 2011. Kushoto ni Msaidizi wa Balozi, Muthomi Muithiga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania, Abdelbagi Hamdan Kabeir, wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Juni 28, 2011 na kufanya mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR .

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI ZA SUDAN, KENYA NA ZAMBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumanne Juni 28, 2011 ametembelewa na Mabalozi wa nchi tajwa hapo juu ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. Ziara ya kwanza ilikuwa ya Balozi wa Sudan Abdelbagi Hamdan Kabeir ambaye alifika kwa lengo la kumsalimia Makamu wa Rais huku pia akitumia fursa hiyo kumuaga kufuatia muda wake wa kushika wadhifa huo hapa nchini kufikia mwisho. Balozi Kabeir alifafanua kuwa maisha yake nchini Tanzania yamemfanya kuifahamu nchi yetu na anashukuru kwa ushirikiano wa wananchi wa Tanzania hali inayompa fursa sasa kuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini kwao.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimshukuru Balozi Kabeir kwa kazi nzuri na hasa katika sekta ya elimu ambapo Watanzania kadhaa wamepata nafasi za kusoma nchini Sudan, huku pia nchi hiyo ikisaidia katika sekta ya elimu na kubadilishana wataalam wa sekta hiyo nchini. Pia Makamu wa Rais alifafanua kuwa, binafsi angependa kuona kura ya maoni iliyopigwa na kufanikisha kuundwa kwa nchi mpya Sudan Kusini inaheshimika na hivyo Sudan kuwa eneo la amani tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Balozi Kabeir alimshukuru Makamu wa Rais na kisha kumuelezea kuwa wao kama Sudan wana mengi ya kujifunza katika kudumisha amani na akatumia mfano wa Zanzibar kama eneo ambalo Tanzania imeonyesha uwezo wake wa kumaliza kero za ndani kwa kutumia watu wa ndani kujadiliana na kukubaliana.

Kwa upande wa Balozi wa Kenya nchini; John Mutinda Mutiso yeye naye alitoa salamu za watu wa Kenya nchini kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye tangu achaguliwe katika wadhifa huo. Balozi Mutiso alimueleza Makamu wa Rais kuwa; Kenya inajifunza mengi kutoka Tanzania na akasifia namna Tanzania ilivyoendesha uchaguzi mkuu uliopita, huku akisema wao Kenya kila inapokaribia uchaguzi vidonda vyao vinaibuka na wananchi wanakuwa na hofu ya usalama wao wakati wa uchaguzi. Pia Balozi Mutiso alisifia kitendo cha Tanzania kutumia vyombo vya dola katika kuchunguza rushwa katika uchaguzi kwa kuanzia na kura za maoni katika vyama akasema jambo hili halifanyiki Kenya na wao wameona ni jema ambalo wangependa kuliiga.

Balozi Mutiso alimuomba Makamu wa Rais kukuza mashirikiano hasa katika eneo la Mazingira huku na akiielezea Tanzania kuwa iko juu katika utunzaji wa mazingira kulinganisha na Kenya na akamuomba Makamu wa Rais kama ataweza kuwa muda katika ratiba zake kuitembelea Kenya na kuhamasisha upandaji miti.

“Eneo kubwa ambalo Tanzania inaweza kutusaidia ni katika kupata miche ya miti. Tunahitaji kupanda miti kama milioni 100 na uwezo wetu wa kupata mbegu na miche ni mdogo kwa kuwa miti yetu mingi tumeitumia na sasa tunaumia,” alisema Balozi Mutiso.

Balozi huyo pia aliwataka Watanzania kuwa na subira na kuondoa jazba katika suala la kuandika Katiba mpya kwa kuwa wao Kenya iliwachukua miaka 20 hadi kupata katiba waliyonayo leo. “Zoezi hili ni gumu na linahitaji umakini. Hakuna watu kulitumia kwa sababu zao za kutafuta madaraka. Katiba ya nchi inapaswa kuwawakilisha watu wote na hasa walioko vijijini hivyo haiwezi kuandikwa kwa kukimbizana,” alisema Balozi Mutiso.

Makamu wa Rais alimshukuru Balozi wa Kenya na kumuahidi kufanya naye mazungumzo zaidi ya mashirikiano katika sekta ya mazingira hasa baada ya kikao hiki cha Bunge la Bajeti kumalizika.

Kwa upande wake Balozi wa Zambia nchini; Mavis Lengalenga Muyunda yeye alimshukuru Makamu wa Rais na wananchi wa Tanzania kwa ushirikiano wao katika kipindi hiki cha msiba wa kitaifa nchini Zambia, msiba wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Frederick Chiluba aliyezikwa jana. Balozi Muyunda alimuelezea Makamu wa Rais kuwa Zambia inathamini uhusiano wake na Tanzania na kwamba inaheshimu nafasi ya Tanzania katika utunzaji na uhifadhiji amani katika ukanda huu wa nchi za Kusini wa Afrika. Tena alifafanua kuwa kwa namna alivyofika Tanzania amebaini kuwa ni nchi yenye mikakati na akafafanua kuwa mfano wa kwanza ni bajeti ya mwaka huu ambayo inalenga kutoa majibu katika vipaumbele vinavyowagusa wananchi.

Kuhusu vyombo vya kiuchumi vinavyounganisha Tanzania na Zambia kama TAZARA, TAZAMA NA MOFET, Balozi Muyunda alisema nchi yake inaendelea na jitihada za kuiboresha TAZARA ambapo huko wameshapata mkopo toka China wenye lengo la kuboresha chombo hicho muhimu kwa usafirishaji wa ukanda wa Kusini.

Kwa upande wa Makamu wa Rais alimtakia kila la heri Balozi Muyunda hasa sasa ambapo Zambia inaingia katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba ama mwanzoni mwa Oktoba. Pia alimsisitizia kuhusu umuhimu wa nchi hizi kuheshimu mambo mazuri waliyoyaanzisha waasisi wa nchi zetu mbili na kuhakikisha kuwa wanayafunza kwa vizazi vijavyo vya nchi hizi ili kuzidisha moyo wa kuthaminiana na kupendana kwa nchi zote mbili.

Imetolewa na: Boniphace Makene

Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

Juni 28, 2011