May 24, 2011

BREAKINGNEWS........WANANCHI IRINGA WAANDAMANA KUMPINGA MREMBO ALIYETEMBEA NUSU UCHI...Eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ambako dimbwili lilianzia
Umati wa wananchi wa mji wa Iringa wakiandamana kutaka vitendo vya wanawake kutembea nusu uchi vikomeshwe
Hapa wananchi wakiwa wamevamia studio na duka la spea ya PhotoNex wakitaka atolewe wamwadhibu
Hapa akiwa amehifadhiwa kituo cha polisi stendi kuu
Abiria waliokuwa wakisubiri usafiri katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa wameungana na wapiga debe katika stendi hiyo na baadhi ya wananchi wa mji wa Iringa kumfanyia vurugu kubwa mrembo mmoja ambaye alikuwa akikatisha maeneo ya stendi hiyo huku akiwa amevaa nguo za ndani nje.


Mavazi hayo ya nusu uchi yameonyesha kuwakasirisha wananchi hao pamoja na abiria wa stendi hiyo na kuamua kuanza kumfukuza huku wakitaka kuichana nguo hiyo ili atembee uchi kabisa.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya wanawake waliokuwepo katika tukio hilo walidai kuwa pamoja na kuwa hawaungi mkono hatua ya vijana hao kutaka kumchania nguo mrembo huyo ila bado wao kama wanawake wamesikitishwa na mavazi ya mrembo huyo nakuwa mavazi hayo yalipaswa kuvaliwa clab usiku sio mchana.

Hata hivyo walisema kuwa mkoa wa Iringa unaongoza kwa UKIMWI hivyo haipendezi kwa wanawake ama wanaume kutembea nusu uchi kwani kufanya hivyo na kuendelea kuhamasisha ngono badala ya kukemea ngono.

Wanawake hao walishauri serikali ya mkoa wa Iringa kuweka sheria ndogo inayokataza mazavi ya nusu uchi kama hayo kama njia ya kupambana na virusi ya UKIMWI.

Tukio la kumfukuza mwanamke huyo mrembo lilianza majira ya saa 11;45 hadi saa 12.05 jioni baada ya polisi kuingilia kati kunusuru usalama wa mrembo huyo ambaye alikimbilia studio za Photo Nex eneo la Miyombini kuomba kuhifadhiwa ili kukwepa kichapo baada ya wananchi hao kuchukizwa na mavazi yake na tabia yake ya kuwaonyesha kidole cha katikati wakati wakimzomea.

Hata hivyo polisi walifika kumwokoa mwanamke huyo ambaye alipewa kanga na mwanamke mwenzake kabla ya wenyeji wake kutimua mbio kukwepa kichapo kwa madai kuwa mrembo huyo ni mtanzania ambaye ameishi sana UK na Iringa anakuja kufanya kazi katika benki moja .

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unalaani kitendo cha kutaka kumchania nguo mwanamke huyo na kukemea tabia ya dada zetu kutembea nusu uchi kwani kufanya hivyo ni kuwavunjia heshima mama zetu pia.

10 comments:

Anonymous said...

WALIVYOMFANYIA HIVYO NI VIZURI KABISA ILI AKOME. NA HILO LIWE NDIYO FUNDISHO KWA WANAWAKE WENGINE WOTE WANAOTEMBEA NUSU UCHI. NYINYI DADA ZETU WENYETABIA KAMA HIYO EMBU ELEWENI KWAMBA WEWE KAMA NI MZURI UTAONEKANA MZURI TU HATA KAMA UKIVAA GUNIA. UKIVAA NGUO NDEFU YA KUSITIRI MWILI WAKO VIZURI HAINA MAANA KWAMBA UZURI ULIONAO UTAJIFICHA. HAPANA. TENA HUWA NDIYO VIZURI ZAIDI KWA SABABU WATU WOTE WATAKUFURAHIA NA HIVYO KUJIONGEZEA NAFASI YA KUPATA MCHUMBA WA KUKUOA MAANA WANAUME WALIYO WENGI KAMA SI WOTE HUCHAGUA KUMUOA MWANAMKE MWENYE HESHIMA, MWENYE ADABU NA MWENYE KUJISITIRI VIZURI KIMAVAZI. EMBU WALE WENYE TABIA KAMA HIYO YA HUYO DADA MLIELEWE HILO KWA MASLAHI YANU NA MUACHE KUTUCHEFUA MABARABARANIA.

Anonymous said...

ushamba ndio unawasumbua ukiwemo wewe francis godwin kwa habari hii ya kipuuzi kuanzia leo sisi tulikuwa tuna fuatilia habari zako huku europe tunaacha kabisa kuangalia mtandao wako na kusoma habari zako huna kazi na kuandika hab ari za udahalilishaji

Anonymous said...

kweli hakuna watu wasenge kama anonymous namba 2. eti sisi huku europe, unamjumlisha na nani. kama kuna washamba dunia hii basi ni watu kama anonym namba 2, mtumwa wa akili. kafie mbele huko.

Anonymous said...

kwani mikoa mingine hayo hayatendeki jamani? mi nahisi huo waweza kuwa mfano mzr wa kuigwa hata kwa mikoa mingine<kwamsisitizo narudia tena tumechoka hence we need changes.said elibariki mwana wa shukia

tolaman said...

HIYO SAWA KABISA HAWA WAYU WAMEZIDI HUKU DAR ES SALAAM WANAWANGALIA TU SIKU HIZI SIJUI WALE DUNGA DUNGA WAKO WAPI WAMEANZA MPAKA HUKO NYUMBANI KWELI HALI NI MBAYA SANA BORA WAKOMESHWE MAANA MAANA SIKU HIZI WANAVAA SKIN TIGHT MWISHO WA YOTE WATATEMBEA UCHI KABISA

KATATANAMA said...

Anonymous Na.2 yaelekea akili zako niza kushikiwa, huwezi ukawa na akili zako timamu ukaandika comment za kijinga kama hizo. Usifikili kwenda nchi za watu ndiyo inayokufanya u-copy na ku-paste kila ukionacho huko uliko. Huo ni utumwa wa akili.Pia dada zetu mjirekebishe, Wengine mnasema hamna bahati ya kuolewa kumbe ni jinsi gani mlivyojiweka mbele ya jamii. Hivi kama unavaa nusu uchi ni mwanaume yupi atakaye kuwa na hata shauku yakutaka kujua habari zako kama siyo kukuona kama kahaba yeyote yule. Mbadilike.

Tanzania Today said...

Mie sioni tatizo la hawa wadada kuvaa hivi... Mnaposema si utamaduni wetu kuvaa hivyo ni kutokujua vizuri historia ya nchi yenu... Hatukuwa na hizi nguo za sasa sisi... Nawasihi watanzania wenzangu tuwaache waendelee kuvaa hivi na hii itapelekea kupungua kwa vitendo vya ubakaji baada ya watu kuwazoea...
Samahanini kama nitakuwa nimewakwaza ila huo ni wangu mtazamo

Anonymous said...

Wengi wa hao vijana wanaojifanya hawataki hao mabinti watembee nusu uchi ndio hao hao mate yanawatoka wanajifanya kumzomea kumbe wanatoa udenda, hamna lolote ukweli hao vijana hawana kazi za kufanya, halafu nguo wanazijua wapi nguo zimekuja afrika karne ya 18 mwishoni watu walikuwa wanatembea uchi, uzuri wa mwanamke ni miguu na mapaja yake, msitake kuleta utamaduni wa kiarabu mkafikiri ndio heshima upuuzi mtupu, mnajifanya mnachukia mmh ndo wabakaji wa kwanza acheni hizo kuna siku tutawataja kwa majina nyie vijana wa stand mbona mnapoibia watu hamuoni mnavunja maadiri, tena ni kikundi cha watu wanne watano hivi ndo zao dawa yenu inachemshwa kaa chonjo

Anonymous said...

Wengi wa hao vijana wanaojifanya hawataki hao mabinti watembee nusu uchi ndio hao hao mate yanawatoka wanajifanya kumzomea kumbe wanatoa udenda, hamna lolote ukweli hao vijana hawana kazi za kufanya, halafu nguo wanazijua wapi nguo zimekuja afrika karne ya 18 mwishoni watu walikuwa wanatembea uchi, uzuri wa mwanamke ni miguu na mapaja yake, msitake kuleta utamaduni wa kiarabu mkafikiri ndio heshima upuuzi mtupu, mnajifanya mnachukia mmh ndo wabakaji wa kwanza acheni hizo kuna siku tutawataja kwa majina nyie vijana wa stand mbona mnapoibia watu hamuoni mnavunja maadiri, tena ni kikundi cha watu wanne watano hivi ndo zao dawa yenu inachemshwa kaa chonjo

Anonymous said...

VITENDO WANAVYOFINYA DADA ZETU VINATUDHALILISHA SANA, WATANZANIA HATUNA UTAMADUNI KAMA HUO. WALICHOKIFANYA NI SAHIHI KABISA KWAMAANA TUSIPOAMUA KUCHUKUA JUHUDI BINAFSI SISI KAMA WANANCHI WA MKOA WA IRINGA TUTAZIDI KUWA VINARA WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI. DADA ZETU JIREKEBISHENI JAMANI.

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE