Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 30, 2011

MWANAMFALME WILIAM APATA MKE

Mwana mfalme wa Uingereza, Prince William na Kate Middleton wamefunga ndoa katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.

Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.

Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.

Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.

Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".

Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge

MAELEZO WAMUAGA Clement MSHANA....

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana akiongea na wafanyakazi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na wafanyakazi hao.
Wafanyakazi wa Idara ya Habari(MAELEZO) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana(katikati) mara baada ya hafla fupi ya kumuaga rasmi jijini Dar es salaam jana.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

IRINGA MJINI NI KERO TUPU ,MAJI HAKUNA UMEME MGAO ,TAKATAKA KILA KONA...

Mmoja kati ya watu wanaofanya usafi katika eneo la stendi ya Mkwawa eneo la M.R akifanya usafi wa kuchoma moto takataka zilizosambaa eneo hilo ,huku gari likiwa jirani na taka taka hizo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa gari hilo .

NB.mpendwa mdau wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.shwari.com leo hautapata matukio mapya hadi majira ya saa 2 usiku kutokana na tatizo la umeme ambalo litaukumba mji wa Iringa kuanzia majira ya saa 4 leo asubuhi hivi sasa katika baadhi ya maeneo ya mji wa Iringa hata huduma ya maji safi hakuna kwa zaidi ya wiki tatu sasa

April 29, 2011

BAVICHA WAMVAA NAPE WAMTAKA AANZE NA RIDHIWANI KIKWETE...

wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya baraza la vijana wa chama cha Chadema(BAVICHA) Taifa Aidan Pugili (30) (kulia) anayegombea nafasi ya uenyekiti Taifa na Dennis Tesha anayegombea ujumbe wa baraza kuu ya vijana Taifa wakizungumza na mtandao huu leo kupinga tambo za katibu wa itikadi na uenyezi wa CCM Nape Nnauye dhidi ya kuwabana mafisadi ndani ya CCM

VIJANA wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoani Iringa wameibuka na kumvaa katibu wa itikadi ya uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape Nnauye kuwa hana uwezo wa kuzima moto wa viongozi wakuu wa Chadema dhidi ya ufisadi na kuwa CCM imemtumia Nnauye kucheza ngoma ya Chadema bila kujijua.

Wamtaka Nnauye kuanza kumwandikia barua ya kujivua gamba naibu katibu mkuu wa CCM bara kepteni (mstaafu )John Chiligati na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete ,Ridhiwani ambaye amekuwa ni mmoja kati ya mamilionea wakubwa nchini baada ya baba yake kuwa Rais .

“Ujue sehemu kubwa ya wanaovuliwa magamba ndani ya CCM ni wale ambao viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Dr.Slaa na Mbowe wamekuwa wakiwataja mara kwa mara kuwa ni mafisadi na wale ambao kila mtanzania anawajua hivyo hata Nnauye na CCM yake watakapowaandikia barua hakuna mtanzania wa kushangaa juu ya uamuzi huo kwani hawa ndio waliogeuzwa kondoo wa kafara ndani ya CCM ila wapo wenyewe kama Ridhiwani na kundi lake hawaguswi kabisa”

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wakati wakitangaza azma yao ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya baraza kuu la vijana wa Chadema (BAVICHA) Taifa vijana hao Aidan Pugili ambaye anagombea nafasi ya uenyekiti Taifa na ujumbe wa baraza kuu Taifa na Dennis Tesha (19) ambaye anagombea ujumbe wa baraza kuu la vijana Taifa ,walimtaka Nnauye kuacha kuwafanya watanzania ni wajinga na hawajui lolote dhidi ya ufisadi wa CCM katika Taifa hili.

Walisema kuwa watanzania wa sasa si wale wa miaka ya 1990 na 1980 wakati wa chama kimoja na kuwa iwapo CCM itaendelea kumtumia Nnauye kama sehemu yake ya kutaka kujijenga itakuwa inajimaliza yenyewe na kuwa yawezekano kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 CCM isifike baada ya kuwa imepasuka mapande mapande.

Pugili alisema kuwa pamoja na ziara za viongozi wapya wa CCM ambao wamekuwa wakizunguka mikoani na kufika ndani ya mkoa wa Iringa kwa lengo la kujiosha bado imani ya watanzania dhidi ya CCM imekwisha na hivyo ziara hizo ni sawa na kuendelea kujichafua na kutoa umaarufu kwa Chadema ambao ndio waanzilishi wa vita dhidi ya upinzani.

Hata hivyo alisema kuwa lengo la kuwania nafasi hiyo ni kutaka kuwaunganisha zaidi vijana ndani ya Chadema na wale waliopo CCM ili kujiunga na Chadema kwa lengo la kuongeza nguvu zaidi ya katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 ili kuona Chadema kinakuwa cham tawala na CCM inaingia katika orodha ya vyama vya upinzani nchini.

Huku kwa upande wake Tesha ambaye ni msomi wa chuo kikuu kishiriki cha Ruaha Iringa alisema kuwa nafasi ambayo anagombea ya ujumbe wa baraza la vijana Taifa ni moja ya nafasi ambayo ameipania ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanabadilika na kuachana na fikra mgando kuendelea kuishabikia CCM ambayo kimsingi tayari imeondoka katika mawazo ya watanzania.

Wakati huo huo wabunge wa Chadema na madiwani mkoani Iringa wamesema kuwa hivi sasa Chadema inaandaa maandamano makubwa ndani ya mkoa wa Iringa ili kutoa ufafanuzi baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakipotoshwa na CCM na serikali yake.

Wabunge hao Mchungaji Peter Msigwa wa jimbo la Iringa mjini,Chiku Abwao ambaye ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa walitoa kauli hiyo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari .

WABUNGE NA MADIWANI WA CHADEMA WAMPINGA MEYA

Mbunge Chiku Abwao ,Peter Msigwa na madiwani Suzana Mgonakulima na Frank Nyalusi

WABUNGE na madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) jimbo la Iringa mjini wapinga tamko la mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi la kulaani hatua ya wananchi wa kata ya Ruaha kufunga ofisi ya mtendaji wa kata kwa kupinga vitendo vya ufisadi wa fedha za maendeleo na kupekea mtendaji wa kata hiyo Nuhu Ferezi kujiua kwa sumu .

Wakati mstahiki meya wa Manispaa hiyo leo akitoa tamko hilo mbele ya kikao cha baraza la madiwani kama sehemu ya kulaani kitendo cha wananchi wa kata hiyo ya Ruaha kuifunga ofisi ya mtendaji wa kata katika maandamano yao ya kupinga matumizi mabaya ya fedha za miradi .

Kwa madai kuwa wananchi hao walikiuka taratibu za kufanya maandamano hayo na kufunga ofisi ya mtendaji na kupelekea mtendaji huyo kujiua na kuonya wananchi kuacha tabia hiyo na kuwa ni msimamo wa baraza la madiwani , wabunge hao na madiwani wa Chadema walipinga tamko hilo kuwa si msimamo wa baraza la madiwani bali ni msimao wa mstahiki meya huyo ambao hakupaswa kuutoa mbele ya baraza.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa jana ,mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao pamoja na madiwani Suzana Mgonokulima wa viti maalum na Frank Nyalusi (kata ya Mvinjeni) walisema kuwa kwa kauli moja hawaungi mkono tamko hilo la meya na kuwa tamko hilo linakwenda kinyume na taratibu za baraza la madiwani ambalo linapaswa kuendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia na ushirikishwaji wa madiwani wote.

Walisema kuwa toka wananchi hao wa kata ya Ruaha wafunge ofisi hiyo na mtendaji wake kujiua hakuna kikao cha baraza la madiwani kilichokutana na kumwagiza meya wa Manispaa ya Iringa kutoa tamko la kulaani wa wananchi hao kwa uamuzi wao.

Mbunge Msigwa alisema wao kama Chadema wanawapongeza wananchi hao kwa hatua yao ya kubaini ufisadi katika fedha zao za maendeleo na kuwa uongozi wa Mnaispaa ya Iringa ulipaswa kujibu hoja za wananchi hao na kutolea ufafanuzi juu ya ufisadi huo badala ya meya kutoa vitisho .

Hata hivyo alisema wananchi wa Ruaha walitumia nguvu ya umma katika kufichua ufisadi na kuwa nguvu hiyo ndio silaa ya Chadema katika kupambana na ufisadi nchini.

Mbunge Msigwa alimtaka mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kujibu tuhuma za wananchi hao na sio meya kutoa kauli za kulaani wananchi.

Kwa upande wake Abwao alisema kuwa chama cha Chadema kitaendelea kufanya kazi na wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao na kuwataka madiwani wa CCM kuacha tabia ya kujitenga na kuzuia watendaji wa mitaa na kata kushiriki katika ziara za bunge na kuwa huu si wakati wa kampeni.

Mtendaji huyo wa kata ya Ruaha Feruzi alijiua wiki mbili zilizopita baada ya kutuhumiwa kufanya ufisadi wa fedha za maendeleo na kodi za minala ya simu zaidi ya shilingi milioni 24 .6 na siku moja baada ya kutakiwa kufika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ili kujibia tuhuma hizo aliamua kujiua nyumbani kwake Mlandege Iringa

WADHAMINI WA TUZO YA TASWA WAONGEZEKA....


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatangaza kuwa kampuni ya utalii iitwayo Zara Tours Limited ya mkoani Arusha imejitosa kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2010.

Zara Tours itadhamini tuzo hizo kwa kumpa ziara ya siku tano atakayeibuka Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2010 kutembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti kwa nia ya kutangaza utalii hapa nchini.

TASWA inamshukuru Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Zainab Ansell kwa udhamini huo, ambapo mshindi huyo akiwa huko yeye pamoja na mtu mwingine atakayeamua kuambatana naye watapata huduma zote za watu mashuhuri.

Pia mshindi ataambatana na mwandishi wa habari mmoja.

Udhamini huo sasa umeongeza zawadi atakazopata mshindi, ambaye pia atapewa gari aina ya Toyota Cresta GX 100 kutoka kwa wadhamini Kampuni ya Bia ya Serengeti na Dekoda kutoka MultiChoice Tanzania.

Pia
atalala kwa siku moja hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam.

Pia naomba kutoa ufafanuzi kuwa TASWA inatafuta wanamichezo bora wa mwaka 2010 na si wa mwaka 2011 kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Tayari orodha ya vyama ambavyo wanamichezo wake watapewa tuzo tumeshaitangaza na wengi wa wanamichezo hao wanatokana na mapendekezo ya vyama vyao ukiacha michezo michache ikiwemo soka.

Soka kama tulivyotangaza juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari, kwamba kulikuwa na Kamati Maalum iliyoteuliwa ikiongozwa na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na baadhi ya wajumbe wa TASWA kulingana na vigezo ambavyo vipo kwa tuzo hiyo.

Pia ieleweke mshindi upande wa soka si kwamba ndiye moja kwa moja atazawadiwa gari, maana tuzo yetu si ya Mwanasoka Bora wa Mwaka, ila kinachofanyika mshindi wa kila mchezo atashindanishwa na wenzake wa michezo mingine ili kumpata Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2010, ambaye atapewa hilo gari.

Lakini kwa vile kila mchezo una majina matatu, washindi wa kila mchezo nao watapewa zawadi ya fedha taslimu, ambayo tayari imeshatangazwa na watahesabika ni washindi wa mchezo husika mwaka 2010.

Ahsanteni.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/04/2011

MARAM LODGE NI NYUMBA BORA YA KULALA WAGENI IRINGA MJINI

Karibu Iringa mjini karibu Maram Lodge usisumbuke kuuliza Lodge uwapo mjini Iringa uliza Maram iliyopo eneo la mjimwema jirani na soko la Mashine tatu katikati ya mji wa Iringa mita kama 100 kufika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani
Mwonekano wa Maram Lodge kwa nje na ilivyozungushiwa uzio kwa usalama wa wageni
Maram ni sehemu tulivu yenye kiwango bora kwa afya yako
Sehemu ya mapokezi ndani ya Maram Lodge Iringa
kitanda safi cha kulala na kuufanya usiku wako uonekane mfupi zaidi ndani ya Maram Lodge
Usalama wa mali zake ndani ya chumba upo wa kutosha kwani kuna kabati la kisasa la kuhifadhia mali zako japo ulinzi kwa nje ya Lodge ni wa kutosha
Feni kwa kila chumba ndani ya Maram Lodge
Huduma ya maji ya moto masaa 24,huduma ya dawa la meno , mswaki mafuta na sabuni ni bure .
Ukiwa ndani yaMaram Lodge utaweza kutazama chanel mbali mbali
Maram Lodge ina eneo nzuri na tulivu la kupumzika wakati na wageni wako

Hapa ni eneo la National mjini Iringa barabara ya kuu ya Uhuru na kulia ni njia ya kuelekea Maram Lodge mita kama 20 hivi kutoka barabara kuu
Kumbuka bei zetu ni za kawaida kuliko Lodge nyingine zote ndani ya mji wa Iringa na ni Logde pekee nyenye huduma nyingi kama chai ya bure asubuhi kwa wateja, huduma ya maji ya moto masaa 24 ,ulizi wa mali zako bure.n.k wasiliana nasi sasa kwa simu 026 270 2415 au 0684185430

April 27, 2011

'LIVE'KABURI LIKIFUKULIWA IRINGA KISA KIFO CHA MASHAKA

Wananchi wa Mtwivila katika manispaa ya Iringa pamoja na jopo la madaktari na askari polisi wakifukua kaburi na mtoto wa miaka 6 anayedaiwa kufa kifo cha mashaka huku mvutano ukizuka pande mbili upande mmoja wakidai amekufa ghafla na mwingine ukidai amenyweshwa sumu
Jeneza likiwa limefukuliwa kwa uchunguzi zaidi
Habari kamili inakuja hivi punde

DIWANI ALIYEMWITA CHILIGATI FISADI SASA AMGEUKIA MBUNGE WAKE

Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Dr.Wiliam Mgimwa

Diwani kata ya Mgama Denis Lupala

SAKATA la Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mgama, Wilaya ya Iringa Vijijini, Denis Lupala, ambaye alimwita Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Kapteni John Chiligati kuwa ni fisadi limeendelea kuchukua sura mpya ndani ya CCM baada ya diwani huyo sasa kumvaa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. William Mgimwa, kwa madai kuwa amekuwa na tabia ya kuendekeza makundi na kukitaka chama hicho kumvua gamba.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Lupala alisema kuwa upo uwezekano wa serikali ya CCM iliyopo madarakani kuendelea kuchafuliwa na viongozi wake na kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendelea kupata umaarufu kutokana na wale waliochaguliwa kuendeleza chuki za kura za maoni ndani ya CCM.

“Ujue wapo wabunge ambao hawaamini kama wamekuwa wabunge na hawaamini kama uchaguzi mkuu umemalizika ...wabunge hawa ndio ambao bado wanaendekeza makundi hadi sasa kwa kuwachukia wale waliokuwa upande wa wagombea wengine wakati wa mchakato…mfano mbunge wetu wa Jimbo la Kalenga, Dk. Mgimwa, yeye bado anaendelea kuwatumia wapambe wake kwa kila jambo na kuwatenga wale ambao hawakuwa upande wake,” alisema.

Diwani huyo ambaye wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM alikuwa akimuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema kuwa hivi sasa Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Mgimwa amekuwa akimtenga katika shughuli nyingi ambazo amekuwa akizifanya katika kata yake ya Mgama.

Akitolea mfano alisema kuwa hivi karibuni mbunge huyo alifika katika kata hiyo kwa ajili ya kukabidhi madawati katika Shule ya Sekondari ya Mgama ila yeye kama diwani hakushirikishwa katika zoezi hilo, jambo ambalo linaonyesha wazi mbunge huyo bado anaendekeza chuki kwa wana CCM ambao hawakumuunga mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo diwani huyo alikitaka Chama Cha Mapinduzi kutowavumilia wabunge wanaoendekeza makundi kwa kipindi hiki na kuwa ni vema nao kuvuliwa magamba ndani ya chama ama kupewa onyo.

Akielezea kuhusu madai ambayo alitaka kufikisha kwa Chiligati wakati wa ziara yake kabla kumwita fisadi kuwa ni pamoja na kero ya umeme, uhaba wa walimu na vitabu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. Mgimwa akizungumzia madai ya diwani huyo kwa njia ya simu alisema kuwa madai hayo si ya kweli na kuwa siku ya kwenda kukabidhi madawati alipewa taarifa ila hakufika.

“Mimi nilimpa taarifa ila hakufika katika zoezi hilo la kukabidhi madawati japo hata mimi mwenyewe sikwenda nilituma wasaidizi wangu,” alisema Dk. Mgimwa.

HAWA NDIO WANAMICHEZO WANAOWANIA TUZO YA TASWA 2011

Amir Mhando katibu wa TASWA (kulia)
 1. Riadha

Wanaume:

1. Samson Ramadhan

2. Marco Joseph

3.John Bazil

Wanawake:

1. Zakia Mrisho

2. Mary Naali

3. Magdalena Mushi

2. Wavu

Wanaume:

1. Kevin Peter (Magereza Wanaume)

2. –Mbwana Ally Mzinga Morogoro

3. Ibrahim Cristopher( Nyuki Zanzibar).

Wanawake:
1. Hellen Richard Mwegoha (Magereza Wanawake).

2. Yasinta Remmy (Jeshi Stars)

3. Zainabu Thabit (Jeshi Stars)

3. Netiboli

1. Lilian Sylidion-Filbert Bayi

2. Mwanaid Hassan-JKT Mbweni

3. Sekela Dominick-JKT Mbweni

4. Karate

Wanaume:

1. Sempai Steven Bella

2. Semapai Ayub seleman

Wanawake: Kuna jina moja haliwezi kutangazwa.

5.Kikapu

Wanaume:

 1. George Otto Tarimo- Savio-Dsm
 2. Lusajo Samwel Mwakipunda- Oilers-Dsm
 3. Gilbert Batungi

Wanawake:

1. Faraja Malaki- Jeshi Stars-DSM

2. Zakhia Kondo- Lady Lioness-Dsm

3. Doritha Mbunda- JKT Stars

6. Soka

Wanaume

1: Khamis Mcha-Zanzibar Ocean View

2.Mrisho Ngasa-Azam FC

3.Shadrack Nsajigwa-Yanga

4. Juma Kaseja-Simba

Wanawake:

1.Asha Rashid

2.Mwanahamisi Omary

3.Fatuma Omary

7. Ngumi za Kulipwa

1. Karama Nyilawila

2.Mbwana Matumla

3. Francis Cheka

8. Ngumi za ridhaa

 1. Revocatus Shomari-Bantam
 2. Selemani Kidunda-Middle Weight

3.Said Dume-Fly Weight

9. Gofu

Wanawake:

 1. Hawa Wanyeche
 2. Madina Iddi
 3. Vailet Peter

Wanaume:

  1. Frank Roman-
  2. Adam Abbas
  3. Isaac Anania

10: BAISKELI

10. Baiskeli

Wanaume:

1:Hamis Clement

2: Richard Laizer

3:Said Jumanne

Wanawake

1:Sophia Anderson

2:Martha Anthony

3:Ndashimba Kulia

11. Kriketi

Wanaume:

(1) Kassim Nassor

(2) Seif Khalifa

(3)Benson Mwita

Wanaawake:

(1) Hawa Salum

(2) Mariam Said

(3) Sophia Hemed

12. Mpira wa mikono

Wanaume:

1.Kazadi Monga-Magereza

2Hemed Saleh-JKT

3Abineri Kusena-JKT

Wanawake:

 1. Happiness Mahinya-JKT
 2. Teresia Kifukwe-Magereza
 3. Zena Mohammed-JKT

13. Watanzania wanaocheza nje

 1. Hasheem Thabeet-soka
 2. Henry Joseph-Soka
 3. Rogers Mtagwa-ngumi
 4. Nizar Khalfan-soka

14. Wachezaji wa nje wanaocheza Tanzania

1. Emmanuel Okwi-soka (Simba)

2. Yaw Berko-soka (Yanga)

3. Kanda Kabongo-kickboxing

15. Wanamichezo Chipukizi

1: John Bazil-riadha

2.Magdalena Cristian-riadha

3. Lilian Sylidion-netiboli

4. Vailet Peter-Gofu

16. Judo

Wanaume:

Khamis Azan Hussein-Zanzibar
Abeid Omar Dola-Zanzibar

Masoud Amour Kombo-Zanzibar

17: TUZO YA HESHIMA:Itatangazwa siku ya siku.

Katibu Kamati ya Tuzo

27/04/2011

April 26, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA MUUNGANO LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, akipunga mkono kwa wananchi wakati alipokuwa akiingia kwenye Uwanja wa Amani katika sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano mjini Zanzibara
Sehemu ya washereheshaji wa sherehe hizo wakiwa jukwaani wakichora mfano wa Bendera ya Tanzania.

Kutoka (kuli) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa`Zanzibar,Dkt Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, wakiwa jukwaani wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Zakia Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Zanziba, baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano mjini Zanznibar leo . Picha na Muhidin Sufiani-VPO Sehemu ya washereheshaji wa sherehe hizo wakiwa jukwaani wakichora mfano wa Bendera ya Tanzania. Sehemu ya washereheshaji wa sherehe hizo wakiwa jukwaani wakichora mfano wa Bendera ya Tanzania. Askari Magereza wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa mgeni rasmi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati) Rais wa Zanzibar, Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, wakiwa jukwaani wakati wa sherehe hizo. Picha na Muhidin Sufiani-VPO
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea heshima na kupigiwa mizinda 21 mara tu alipowasili katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini unguja kuongoza hsrehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na amiri jeshi mkuu akiukagua gwaride lilioandaliwa namajeshi ya ulinzi katika uwanja wa michezo wa Amaan wakati wa shrehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Picha zote na Muhidin Sufiani-VPO

WANANCHI TANGASISI WAIBANA SERIKALI

Na Said Tanga

SERIKALI imeombwa kuwaeleza wakazi wa Tangasisi Jiji la Tanga, ukubwa wa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji (EPZA) badala ya sasa baadhi ya wananchi kushindwa kuendeleza na kufanya shughuli nyingine za kijamii kwa tishio la eneo lao kutajwa kuwemo katika mpango huo.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo Mbugani lililopo kata ya Tangasisi linalotajwa pia kutengwa kwa ajili ya EPZA, Bw. Winston Mosha wa Kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake (WLAC),

amesema serikali inaweza kuwa na nia nzuri kwa ajili ya kuchukua eneo la uwekezaji lakini namna lilivyokosa uwazi wananchi wanatilia mashaka suala hilo.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya ufuatliaji wa haki za wenye mashamba na nyumba wa mtaa wa Mbugani Bw. Joseph Jeremia amesema baada ya kukosa ufumbuzi juu ya suala lao na malipo ya fidia katika eneo lao ambalo nyumba zao zimewekwa alama X na maandishi ya EPZA kwa viongozi wa Jiji na Mkuu wa wilaya, wamemwandikia barua Waziri wa Ardhi, Makazi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kumuomba aingilie kati.

Amesema wamemomba Waziri awasaidie kupata ukweli kuhusu eneo lao wanaloishi kwani wamebaini viongozi wa Jiji wanataka kulichukua eneo lao kwa kisingizio cha kutengwa eneo la uwekezaji ili waligawe viwanja vya kuishi watu wengine hatua ambayo hawawezi kukubali hali hiyo.

HATARI !HATARI ! MANISPAA YA IRINGA TAKA KILA KONA

Mfanyakazi wa usafi katika Manispaa ya Iringa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa ameuchapa usingizi nje ya jengo la NSSF mjini Iringa leo kama alivyonaswa na kamera ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com
Vitendea kazi vya mfanyakazi wa usafi manispaa ya Iringa vikiwa vimeegeshwa huku mwenyewe akiuchapa usingizi eneo la jengo la NSSF
Eneo la Frelimo
Eneo la Kihesa
eneo la Mungano shule katika Manispaa ya Iringa barabara ikiwa imefungwa kwa taka taka


Hali ya usafi katika Manispaa ya Iringa kwa siku tatu mfululizo imeendelea kuwa mbaya zaidi kama ambavyo kamera ya blogu hii ilivyotembelea katika maeneo ya Frelimo ,Muungano ,Ilala na Kihesa ,Mwangata na Makanyagio.

Kwa upande wa eneo la shule ya msingi Muungano wananchi wamelazimika kufunga barabara ya kuelekea Don Bosco na barabara hiyo kutumika kuhifadhi takataka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa .

GAMBA JIPYA LA CCM LAWEKWA DOA DIWANI AJITOSA KULICHAFUA

GAMBA jipya la chama cha mapinduzi (CCM) laanza kutobolewa baada ya diwani Denis Lupala (Pichani) wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mgama wilaya ya Iringa vijijini ambaye alimwita naibu katibu mkuu wa CCM Bara Kapten John Chiligati kuwa ni fisadi ambaye anatakiwa kuvuliwa gamba ndani ya CCM kuibuka upya huku na kutaka waliovuliwa gamba Dodoma kufilisiwa mali zao.

Ataka waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa , Andwer Chenge na Rostam Azizi na wengine waliovuliwa magamba Dodoma kufilisiwa mali zao na kunyang’anywa kadi za uanachama kwa faida ya wanachama wote na Taifa.

Diwani hayu ambaye tayari ameitwa na sekretarieti ya wilaya / usalama na maadili ili kujadiliwa kwa utovu wa nidhamu kwa kumvaa hadharani Chiligati wakati wa ziara yake kwenye kata yake ya Mgama na kumhoji sababu za kuendelea kupewa nafasi hiyo ya juu CCM wakati ni mmoja wa wana CCM ambao walipaswa kuvuliwa gamba Dodoma.

Habari kamili inakuja