Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 30, 2011

KILA SIKU SAA 4 USIKU NDANI YA BLOGU HII UTASOMA GAZETI LA JAMBO LEOMpendwa mdau ya blogu hii ninapenda kukuarifu kuwa wakati wowote kuanzia kesho utaanza kusoma habari kubwa ndani ya gazeti la Jambo leo kupitia mtandao huu kuanzia majira ya saa 4 usiku utapata dondoo hizo usikose kutembelea,pia kumbuka wakati wote na kila siku jipatie gazeti la Jambo leo kwa habari za kina na za uhakika kwa bei nafuu sana

HATARI ,SHIMO LA AJALI LA DK MWAKYEMBE IRINGA LAIBUKA UPYA ,SERIKALI YASUBIRI VIFO NDIPO IZIBE?


Hili ni shimo lililosababisha ajali ya naibu waziri wa sasa wa ujenzi Dkt Mwakyembe lililopo eneo la mliwa wa Ihemi Iringa ambalo limepewa jina la DKt Mwakyembe ,shimo hili kwa sasa limekuwa tishio baada ya kuzibwa haraka haraka kipindi cha ajali ya Dkt Mwakyembe mwaka jana ila sasa limefumka upya
Abiria wakijaribu kuvuta daladala lililotumbukia katika shimo hilo la Dkt Mwakyembe na kuhama njia leo mchana,hakuna aliyepoteza maisha

Shimo lililosababisha ajali ya mbunge wa Kyela mkoa Mbeya Dkt Mwakyembe limeibuka upya na sasa kuwa ni shimo kubwa kuliko awali.


Tayari shimo hilo ambalo ambalo lilizibwa haraka haraka na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) ili kupoteza ushahidi wakati wa ajali ya Dkt Herrison Mwakyembe ambaye kwa sasa ni naibu waziri wa ujenzi , hivi sasa limechimbika mara tatu zaidi na barabara kuu ya Iringa -Mbeya katika eneo hilo la Mlima wa Ihemi imekatika nusu kwa nusu na tayari ajali kadhaa zimeanza kutokea aneo hilo mtandao huu umefanya ziara eneo hilo na kuhuhudia ajali na ukubwa wa shimo hilo


Rai yangu kwa serikali mkoa wa Iringa inasubiri vifo vitokee katika eneo hilo ndipo wazibe shimo hilo ama watenge bajeti?

Kwa upande wa leo pekee magari zaidi ya matatu kwa muda mfupi wa nusu saa niliyopiga kambi mimi katika eneo hilo yameonekana kuhama njia na kutaka kupinduka huku daladala moja akinusurika kusababisha vifo vya abiria wake.

T.F.A IRINGA NI MKOMBOZI WA KWELI WA MKULIMA

Tupo Iringa mjini jirani kabisa na lango bank ya NMB ama RETCO barabara ya kuelekea Ikulu ndogo ya mkoa wa Iringa ,fika uhudumiwa pembejeo bora kwa bei poa

MOROGORO SI KWEMA AJALI TENA MCHANA HUU

Habari za uhakika kutoka mkoani Morogoro zilizotua katika mtandao huu hivi sasa zinadai kuwa abiria zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Upendo ambalo walikuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Njombe mkoani Iringa kupinduka eneo la Mikumi mkoani Morogoro

Hii ni ajali ya nne kutoka mkoani kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja baada ya ajali ya wasanii wa 5 star leo bado mzimu wa ajali umeendelea kuuandama mkoa wa Morogoro.

Taarifa hizo za uhakika ambazo zimepata kuthibitishwa na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro zinadai kuwa hakuna aliyepoteza ,maisha katika ajali hiyo japo undani zaidi waajali hiyo utaupata hivi punde.

LUDEWA WATUMIA MAPOROMOKO YA MAJI KUZALISHA UMEME WAO BILI KWA MWEZI 1,500

Maporomoko ya maji katika kijiji cha Mawengi ambayo yanatumika kuzalisha umeme wa gharama nafuu
Mitambo ya kuzalisha umeme wa maji Ludewa

Baadhi ya vijiji katika Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa vimeanza kuzalisha umeme wake kwa kutumia maporomoko ya maji yaliyopo sasa wateja wanaotumia umeme huo wanalipa bili kwa mwezi shilingi 1,500,utaisoma makala hii katika gazeti la Tanzania Daima

March 29, 2011

MAPYA MENGINE YAIBUKA SASA NI KIKOMBE CHA DADA CHAIBUKA TABORA


umati wa wagonjwa wakisubiri kikombe cha Dada
Baada ya Babu Loliondo, Mangi Tarakea na Dogo wa Mbeya, mtu mwingine ameibuka safari hii toka mkoani Tabora, akito kikombe anachodai kinatibu maradhi sugu, na kuvutia umati mkubwa wa watu wa mji huo mkongwe.

Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini, amejitokeza na kudai alioteshwa kutibu watu na Bikira Maria, mpaka sasa OCD yupo hapo kwa dada na amemwambia mdau wa libeneke la kerongingi, Mkala Fundikira, kuwa yeye alishapata kikombe toka kwa dada na amejitapa hatoondoka pahala hapo mpaka askari zaidi watakapowasili kuongeza ulinzi.

Watu kadhaa wameonesha imani na dawa ya dada na kusema wana nafuu tangu wanywe dawa yake ambayo bado haijafahamika chanzo ama mchanganyiko wake.


Kamati ya ulinzi na usalama itakaa muda mfupi kujipanga na mfumuko wa watu watakaokuja kufuta huduma ya dada Magreth Mutalemwa pata picha zaidi hapa

FILIKUNJOMBE CUP KUANZA LUDEWA

Diwani wa kata ya Lugarawa Fromena Haule wilaya ya Ludewa mkoani Iringa akipokea kombe litakaloshindaniwa katika kata yake katika mashindano ya mbunge Deo Filikunjombe wa jimbo hilo ambapo mshindi atapata kombe hilo la dhahabu na Ng'ombe mashindano kama hayo ni kwa kata zote za jimbo hilo
Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Mhe.Deo Filikunjombe akiwa na wachezaji wa timu ya shule ya sekondari Lugarawa baada ya kuwakabidhi kikombe cha Dhahabu na mipira kwa ajili ya kuanza mashindano ya darasa kwa darasa

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Filikunjombe amemwaga vifaa vya michezo katika wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya kuwania kombe la dhahabu ya mbunge huyo pamoja na ng’ombe.

Fiikunjombe amekabidhi vifaa hivyo vya michezo ikiwemo mipira na makombe hayo ya dhahabu kwa uongozi wa ngazi ya kata na shule za sekondari na kuwataka vijana kujipanga vema ili kupata timu nzuri zitakazowezesha wilaya ya Ludewa kuwa vinara wa ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa Iringa na pia kupata timu itakayopata kucheza ligi kuu Tanzania bara.

Shule za sekondari ambazo zimekwishapatiwa vifaa vya michezo kama vile mipira, jezi na vikombe hivyo dhahabu kwa ajili ya kuanza mashindano hayo kuwa pamoja na shule ya sekondari Ikovo, Mavala, Mt.Masusa, Madilu, Lupanga, Madunda na Lugarawa sekondari.

Filikunjombe amesisitza kuwa anataka kuunda timu a mpira wa miguu kutoka katika vijiji vyote 76 wilayani Ludewa na kwamba mpaka sasa amekwishatoa vifaa vya michezo katika kata za Ludende, Milo,Lupanga, Mlangali, Madope, Madilu, na Lugarawa.

Alisema kuwa mashindano hayo ya kuwania kombe la FILIKUNJOMBE katika Jimbo hilo la Ludewa yanalenga katika kuhamasisha kasi ya michezo kwa vijana ili kupunguza maabukizo ya ukimwi, pamoja na kuvunja makundi ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuhamasisha kampeni kabambe ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa .

Filikunjombe aliasema kuwa moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakikwamisha vijana kusonga mbele kimichezo ni kutokana na kutokuwepo kwa umahamasishaji wa kutosha kutoka kwa viongozi hawa yeye kama Mbunge wa Ludewa atahakikisha kuwa anatoa kipaumbele kwa michezo ya vijana.

Filikunjombe amewataka Madiwani wa Kata husika kuyasimamia vema mashindano hayo akiamini kuwa mashindano hayo yatachangia sana katika kuinua ari ya michezo wilayani Ludewa.

Aidha alisema kwa ajili ya kuongeza ushindani zaidi katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza katika Kata atazawadiwa ngombe pamoja na Kombe la dhahabu

MBUNGE AKABIDHI TRECTA KUSAIDIA CHAKULA MASHULENI


Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Fiolikunjombe akizindua Trecta alilolokabidhi wa uongozi wa elimu kanda ya Lugarawa kwa ajili ya kusaidia kulima mashamba ya shule ili kutoa chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi
Mbunge wa jimbo la Deo Filikunjombe (kushoto) akimkabidhi maratibu elimu kanda ya Lugarawa Vitaris Haule kadi ya Trecta kwa ajili ya kuwezesha kulima mashamba ya shule ili kutoa chakula mashuleni

Mbunge wa Jimbo la Ludewa, mkoani Iringa, Deo Filikunjombe (CCM) ameunga mkono juhudi za wahisani, kutoka Italia, ambao wametoa trekta lenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya kusaidia kuzalisha chakula cha shule za msingi katika wilaya ya Ludewa ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula cha mchana mashuleni katika jitihada za kukuza kiwango cha ufaulu wilayani humo.

Filikunjombe, ambaye amechangia shilingi milioni 5 kama sehemu ya kuunga mkono jitihada hizo za wadau hao wa elimu, alisema lengo la Trekta hilo ni kuziwezesha shule za msingi wilayani Ludewa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi.

Akikabidhi Trecta hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika Kata ya Lugarawa, na kuhudhuliwa na Mkuu wa Wilaya Bi. Georgina Bundala na Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Hilda Lauwo, Filikunjombe alisema anaamini kuwa Trecta hilo litasaidia kukuza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula kwa shule za tarafa hiyo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kamati za shule katika utunzaji wa chombo hicho.

“Utaratibu wa kuwawezesha wanafunzi kula chakula cha pamoja mchana na kupata uji asubuhi utasaidia kukuza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi,” alisema mbunge Filikunjombe aiongeza kwamba “pia kutapunguza kasi ya utoro mashuleni iliyokuwa ikichangiwa na njaa kwa wanafunzi hao.”

Filikunjombe alisema Trecta hilo limenunuliwa kwa mchango wa wadau wa maendeleo ya elimu wilaya ya ya Ludewa na kuwa kuanzishwa na utaratibu wa chakula mashuleni ni agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda kwa Halmashauri zote nchini na Ludewa imeanza kwa vitendo.

“Muda wa kampeni sasa umekwisha na hima tufanye kazi. Tumkatae mtu yeyote anayetaka kuturudisha nyuma,” alisema Filikunjombe.

Filikunjombe aliwataka wazazi kuwasimamia watoto wao ili katika masomo na kuwa jitihada hizo za serikali katika kuboresha kiwango cha elimu ziende sambamba na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaofaulu mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne katika wilaya ya Ludewa .

Mratibu wa Elimu Lugarawa Bw. Vitalis Haule alisema kuwa msaada huo wa Trecta umepatikana kutokana na jitihada za mbunge wao Filikunjombe na akawataka wana Ludewa wengine kufuata nyayo.

Aliwataja wengine waliochangia upatikanaji wa Trecta hilo kuwa, Dkt Enlo Allegr na Michelangelo Chiurchiu wote wakazi wa nchini Italy, huku Kamishina wa Polisi (Utawala na Fedha) Clodwig Mtweve ambaye ni makazi wa kata hiyo ya Lugarawa akijitolea usafiri wa kulisafirisha Trecta hilo toka Dar es Salaam hadi Ludewa.

Bw. Vitalis alisema tractor hilo litazinufaisha kata tano za Madilu, Mundindi, Mavanga, Mkongobaki na Lugarawa zote zikiwa na shule 24 na wanafunzi 8,225 na kuwa Trecta hilo litawezesha kulima heka 5 kwa kila shule na baada ya hapo litasaidia kulima hekari 50 za pamoja katika kijiji cha Amani ili kuongeza akiba ya chakula mashuleni.

March 28, 2011

BREAKINGNEWS ....HAKIMU WA MWAKALEBELA AJITOA


Hakimu aliyeitupilia mbali hukumu ya kwanza ya Frederick Mwakalebela leo amejitoa kuendelea na kesi hiyo ,hata hivyo kesi hiyo sasa haitasikilizwa tena katika mahakama ya wazi kama ilivyo kuwa awali.

Habari kamili juu ya mambo yalivyokwenda leo katika kesi hiyo ya rushwa inayomkabili Mwakalebela utaipata hivi punde

MBUNGE FILIKUNJOMBE KUTUMIA TSH MILIONI 70 KTIKA MSHAHARA WAKE KUSOMESHA YATIMA..


MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Filikunjombe (CCM) ameahidi kutumia kiasi cha shilingi milioni 70 kwa miaka mitano kutoka katika mshahara wake wa ubunge kwa ajili ya kusomesha elimu ya sekondari watoto yatima na wasio na uwezo 711 katika wilaya nzima ya Ludewa .


Filikunjombe alisema kuwa gharama ya karo kwa mwanafumnzi mmoja ni Tshs. 20,000/= na kwamba kwa wanafunzi 711 itamgharimu Tshs zaidi ya Tshs. Milioni 14 kwa mwaka.

Aliwataja wanafunzi wataonufaika na msaada huo kuwa ni wanafaunzi ambao yatima na wale wanaotoka katika mazingira magunu.


Pamoja na kuahidi kujitolea mshahara wake kusomesha watoto hao pia ameahidi kujitolea kujenga bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Lugarawa wilaya ya Ludewa kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake alizopata kutoa wakati wa kampeni juu ya kuboresha kiwango cha elimu wilayani humo.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Lugarawa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho ,Filikunjombe alisema kuwa amelazimika kuanza kusaidia elimu kwa kusomesha watoto na ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule hiyo kama njia ya kuwaepusha wanafunzi hao kutembea umbali mrefu kufika katika shule hiyo ya kata kupata elimu.


Filikunjombe aliwataka wananchi wa kata hiyo kusaidia kusogeza mawe na kujitolea nguvu zao katika ujenzi wa bweni hilo huku kwa upande wake atachangia vifaa vyote vya viwandani vikiwemo bati na saruji .


Alisema kuwa kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo alikuwa akisaidia kusomesha watoto 10 kwa kila kata na kuwa sasa ameongeza kutoka watoto 10 katika kata hiyo hadi wanafunzi 30 huku baadhi ya kata wamefika watoto 25 hivyo kufika watoto 711 kwa wilaya nzima.


Pamoja na kuahidi kuendelea kutumia mshahara wake kusomesha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu bado alisema kuwa fedha hizo hatazitoa kwa maofisa watendaji wa kata ambao kipindi cha mwanzo waligeuza fedha hizo za ada za wanafunzi ni mradi kwao na kutumia wao badala ya kuwalipia ada walengwa.


Awali mkuu wa shule ya Lugarawa Hashim Masoli alimweleza mbunge huyo baada ya kutembelea shule hiyo ,kuwa pamoja na mafanikio mbali mbali yaliyopatikana bado shule hiyo inakabiliwa na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa 4, Mabweni 3 nyumba za walimu 4 pamoja na uchakavu wa vyumba za walimu 7.


Hata hivyo alisema kuwa kipaumbele cha shule hiyo ni kuanza ujenzi wa mabweni 2 ya wanafunzi likiwemo la wasichana na wavulana.


Alisema kuwa shule hiyo inawanafunzi 712 wakiwemo wasichana 395 na wavulana 317 huku walimu wa kudumu 14 na wa muda 2 kati yao walimu wa masomo ya sayansi wapo 5 na sayansi ya jamii 12.

March 26, 2011

BREAKINGNEWSzzzzz TAIFA KTK MSIBA MKUBWA TENA 17 WACHINJWA AJALINI PWANI

IGP MWEMA

HUKU bado Taifa likiwa katika kumbukumbu ya vifo vya wasanii wa kundi la 5 star 13 na watu wengine watatu waliokufa katika ajali mfululizo huko mkoani Morogoro ajali nyingine Coaster imeua watu 17 na kujeruhi 18 mkoani Pwani.

Watu hao wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zimetokea leo kwa kuhusisha magari matano, ikiwamo Coaster iliyokuwa ikitokea Morogoro kwenda Dar es Salaam.

Ajali ya Coaster yenye namba za usajili T. 566 AZP ilitokea eneo la Mbala wilayani Bagamoyo, ambapo basi hilo lililigonga kwa nyuma lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 353 AAG lililokuwa limeegeshwa pembeni.

Kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 3:45 usiku wamedai kuwa basi hilo lilikuwa likitaka kulipita lori ambalo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara lakini dereva wa basi hilo aliliona gari jingine likitokea mbele.

Walisema gari lililokuwa likija mbele lilikuwa ni lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 398 ATB, hivyo kumfanya dereva wa Coaster kuamua kurudi nyuma na kugonga tela la Scania pamoja na kukwaruzana na Fuso hiyo na baadaye kupinduka.

Mashuhuda hao walisema kuwa baada ya ajali hiyo watu 14 walifariki dunia papo hapo huku wengine 12 walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali Teule ya Tumbi.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema waliofariki dunia katika ajali hiyo ni wanaume 12, mwanamke mmoja pamoja na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11.

Mwakyoma, aliwataja maiti waliotambuliwa kuwa ni Salehe Rashidi (21) mkazi wa Chaalinze, Rajabu Mnyalikwa (35) mkazi wa Ubena, Ediluck Mluge (28) mkazi wa Mbala Chalinze na Amina Saidi (35) mkazi wa Mbala.

Wengine ni Charles Mhando (35) mkazi wa Mbala Chalinze, Gift Charles ambaye hajajulikana alikokuwa akiishi, huku maiti wanane bado hawajatambuliwa na wamehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Tumbi.

Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo waliolazwa katika hospitali hiyo ni Mkunduge Mganga (29) mkazi wa Dumila, Godwin Sakarani (55), Haruni Mgangaruma (24) mkazi wa Mbarali (Mbeya) na Khalid Hamza (29) mkazi wa Mawenzi, Morogoro.

Wengine ni Edwin Mbele (49) Ofisa ununuzi Kilombero, Madaraka Rashidi (42) mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, Leornad Mkoba (45) mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, Ester Shija (38) mkazi wa Dar es Salaam, Juma Omari (29) mkazi wa Morogoro na Justine Mathew (31) mkazi wa Dar es Salaam.

Alibainisha kuwa majeruhi wawili ambao hawajatambuliwa hali zao si nzuri, wamekimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika tukio jingine, ajali nyingine iliyotokea eneo la Ubena Zomozi, barabara kuu ya Dar es Salaam - Morogoro, imesababisha vifo vya watu watatu baada ya magari matatu kugongana.

Katika tukio hilo gari lenye namba za usajili T 817 AZU /T 951 AMZ Scania lori likiwa limebeba mbao likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam lililigonga kwa nyuma lori lenye namba za usajili T 890 aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likitokea Kiteto kwenda Dar es Salaam.

Baada ya kugongwa gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Anthony Matende (56) mkazi wa Dodoma nalo lilikwenda kugonga gari lenye namba za usajili T 317 ATN Mitsubishi Fuso lililokuwa limeharibika.

Kamanda Mwakyoma alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa usiku na kuwataja waliofariki dunia katika ajali hiyo ni pamoja na utingo wa gari lenye namba T 317 ATN Rober Luwena (30) mkazi wa Mtoni Dar es Salaam na Miraji Mwinyi (22) mkazi wa Ngusero, Kiteto.

Mwingine aliyefariki dunia alijulikana kwa jina moja la Joseph, ambaye ni fundi aliyekuwa anatengeneza gari namba T 317 ATN lililokuwa limeegeshwa pembeni baada ya kuharibika.

Kamanda Mwakyoma aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Anthony Matende dereva wa gari lenye namba za usajili T 890 AUR, Aman Hamis (28) mkazi wa Matui, Kiteto na Myemo Hamis (19) mkazi wa Matui, Kiteto.

Wengine ni Leokadia Leonard (24) mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Ibrahimu Zakayo (42) mkazi wa Matui Kiteto, Charles Mhina (42) mkazi wa Matui, Kiteto wote walikuwa abiria wa gari lenye namba za usajili T 890, ambao wamelazwa katika kituo cha afya Chalinze.

Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Tumbi. Chanzo cha ajali kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa gari lenye namba za usajili T 817 AZU/T 951 AMZ Scania.

Zaidi soma gazeti la Tanzania Daima

HAYA NDIO YALIYOSEMWA NA SUMAYE...

SOMA TAMKO LA SUMAYE DHIDI YA UV CCM NA CCM HAPA

NAONDOKA LEO DAR ,NIMECHOSHWA NA TABIA YA BLOGU YA KASHAVUDODO...

Wavuvi wakiwa kazini katika bahari ya Hindi,

NB.Nategemea kuondoka jijini Dar es Salaam asubuhi hii kurejea mkoani kwangu Iringa ,Rai yangu kwa wamiliki wa Blogu wote kuheshimu kazi za wengine hata kama kuna tukio umelipenda kutoka katika blogu nyingine ni vema kutaja chanzo cha habari husika ama Blogu iliyochapisha tukio/habari husika binafsi sijapendezwa hata kidogo na Blogu ya kashavudodo kwani mmiliki wa blogu hii kazi yake ni kukopi kila kitu na kuweka katika blogu yake kama kazi hiyo ameifanya yeye nasema huo ni wizi na nina uwezo wa kuchukua hatua kwa kazi zangu.

Naomba Kashavudodo na wengine wenye tabia kama hii kuiga mfano kwa wakongwe wa Blogu duniani kama Issa Michuzi na wengine ambao wakipenda tukio kutoka blogu nyingine lazima chini wataje chanzo cha habari husika.

Napenda kuwaomba radhi wadau wa blogu yangu ya www.francisgodwin.blogspot.com kwa usumbufu uliojitokeza hadi baadhi yenu kuniuliza kama blogu ya kashavudodo inamilikiwa na nani na ina mahusiano na blogu yangu,nasema hivi blogu hiyo haina mahusinano hata chembe moja na blogu yangu ila imekuwa ikifanya ufisadi wa kazi za blogu yangu.

March 25, 2011

FORMER PRESIDET MKAPA MOURNS JAPAN'S TSUNAMI DISASTER


Former President Benjamin Mkapa offers his condolences to the Ambassador of Japan to Tanzania His Excellency Hiroshi Nakagawa this morning at the Embassy of Japan in Dar es salaam this morning.Bofya hapa

'LIVE" SUMAYE ATOA ONYO KWA TAIFA ASEMA UV CCM IMEFIKIA PABAYAWAZIRI mkuu mstaafu wa serikali ya jamhuri ya muungano Frederick Sumaye amejitokeza mbele ya vyombo vya habari kwa mara ya kwanza leo kujibu tuhuma mbali mbali zilizoelekezwa kwake na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM ) mkoa wa Pwani na baraza kuu la UVCCM Taifa kuwa ni kauli za uchochezi dhidi yake.

Sumaye amesema kuwa pamoja na kuwa UVCCM katika kauli zake imedai kuwa yeye ni mmoja kati ya wana CCM wanaotaka kugombea Urais Mwaka 2015 bado kauli hizo ni za kichochezi zinazolenga kumvuruga yeye na CCM pamoja na serikali iliyopo madarakani.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Hotel ya Protea,na kuwa hategemei kuendelea kusikia kauli za uchochezi kama hizo zikiendelea kutolewa dhidi yake.

Kwani amesema kuwa kauli ya UV CCM mkoa wa Pwani kuwa Rais Jakaya Kikwete anatambua ni nani anafaa kuwa Rais baada yake ni kauli ya kukiharibu chama cha CCM ambacho ni chama cha kidemokrasi na kuwa ni vema viongozi kutonyamaza kimya kwa kauli kama hizo za UV CCM.

Sumaye amesema kuwa yeye ni mwanachama safi ndani ya CCM na kuwa anapingana na kauli ya UVCCM na katibu mkuu wa CCM Taifa Yusuph Makamba kuwa yeye na wenzake wamepanga kuivuruga CCM.Kada wa CCM na waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye akizungunza na waandishi wa habari sasa katika ukumbi wa Hotel ya Protea kuhusu kauli mbali mbali zinaoelekezwa kwake na UVCCM.


Habari zaidi inakuja..............

BENDI YA BWAGAMOYO SOUND YAZIDI KUSAMBARATISHWA....


WAKALI wa dansi hapa nchini, Manchester Musica wamezidi kuibomoa bendi ya Bwagamoyo Sound kwa kumnyakua mwimbaji wao mahiri, Joseph Venas ‘Wera Baba’.

Kiongozi wa Manchester Musica Musica, Adam Hassan alimweleza mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salam kuwa, wamemchukua Wera Baba ili kuimarisha safu yao ya uimbaji.

Aidha, Adam alisema kuwa, anaamini kwa kumnasa mwimbaji huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, bendi yake itakuwa imejiweka katika mazingira mazuri kiburudani.

“Tayari tumeshaanza kushiriki na Wera katika maonyesho yetu mbalimbali kwenye kumbi tunazotumbuiza, ambako pia tunaandaa naye vibao vipya kwa ajili ya albamu yetu ijayo,” alisema Hassan.
habari na picha na mwandishi wa Blogu hii Bw Abdallah Menssah,Dar es salaam

MIAKA ZAIDI YA 15 ANATESEKA KWA KUFUNGWA KAMBA,USIKOSE GAZETI LA TANZANIA DAIMA KESHO

Huyu ni mkazi wa Sadani mkoani Tanga anayeishi kwa kufungwa kamba kama mfungo ,sababu za kufungwa kamba na kuishi kama mnyama utazipata kesho katika gazeti la Tanzania Daima,hakikisha hukosi nakala yako

NATO YATUMA MAJESHI YAKE LIBYA KULINDA ANGA


Shirika la kujihami la NATO sasa limekbali kuchukua jukumu la kuthibiti anga ya Libya ili kuhakikisha marufuku ya ndege kutopaa inatekelezwa.


Hatua hii imeafikiwa kwenye kikao cha waakilishi wa nchi wanachama wa shirika hilo mjini Brussels Ubeljiji.


Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema wanachama wote wa shirika hilo wameunga mkono uamuzi huo.


Marekani ndio imekuwa ikisimamia utekelezaji huo lakini inataka kukabidhi wadhifa huo haraka iwezekanavyo.


Nchi wanachama wa NATO walikubaliana alhamisi usiku kuwa wachukue jukumu hilo na huenda wakakabidhiwa rasmi na Marekani katika siku mbili zijazo.


Kwa sasa shirika hilo linaongoza juhudi za kuzuia silaha kuingia Libya. Lakini bado haijaamuliwa ni nani atakae ongoza harakati za mashambulizi zinazoendelea katika lengo la kulinda raia wa Libya.


Katibu mkuu Rasmussen amesema kuwa wanajadiliana kuhusu uwezekano wa wao kuchukua wadhifa huo.


Kuna baadhi ya wahusika ambao hawapendezwi na kuwa wanajeshi kutoka nchi za magharibi wanaendesha operesheni za kijeshi katika nchi ya Kiislamu.


Kufuatia tashwishi hizo, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Uturuki inasemekani wamekubaliana kimsingi kuwa usimamizi wa harakati zote za kijeshi nchini Libya zinakabidhwa shirika la Nato.
Ikiwa hivyo, baraza la mawaziri kutoka nchi wanachama wa NATO wakiwemo viongozi wa nchi za kiarabu zinazounga mkono hatua zinazochukuliwa dhidi ya Libya, watahusika kikamilifu katika maamuzi ya operesheni hiyo.

WABUNGE KENYA WAMINYANA NA KLABU ARUSHA


Washambuliaji wa timu ya wabunge wa Kenya wakilishambulia lango la timu ya wazee klabu Arusha huku golikipa wa timu hiyo akiwa amelala chini,wakati wa mchezo wa kirafiki zaidi bofya hapa

March 24, 2011

LEO NI SIKU YA KIKUA KIKUU DUNIA,

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Hadji Mponda(katikati)

Leo ikiwa ni siku ya maradhi ya kifua kikuu duniani,Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Koffi Annan amesema juhudi zinapasa kufanywa kupambana na maradhi ya hayo.


Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Afya ulimwenguni WHO,iliyotolewa leo kiwango cha maradhi hayo kimepungua kwa kiasi katika mataifa kadha ya ulimwengu lakini hata hivyo, maradhi hayo yameongezeka kwa kiwango cha kutisha katika bara la Afrika ambapo ongezeko la kifua kikuu na vifo vingi inahusishwa na maradhi ya Ukimwi.


Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kifua kikuu kimepungua kwa asilimia 20 katika maeneo mengi duniani tangu mwaka 1990 na kuongezeka mara tatu katika bara la Afrika.


WHO imeonya kwamba ugonjwa huo pia umeongezeka katika ulaya ya mashariki kufuatia matibabu ya chini.


Robo ya idadi ya watu milioni moja na laki saba wanaokufa kila mwaka kutokana na kifua kikuu inatoka Afrika.
Wakati daktari anapotoa ushauri kwa mgonjwa kumeza tembe moja mara tatu kwa siku, mara nyingi hana njia ya kuhakikisha kuwa maelekezo yake yanafuatwa.


Wengi wanaacha kutumia dawa mara wanapohisi wamepata nguvu – hususan wakati wa tiba katika miezi ya mwisho.


Wakati madawa yanatumika kwa ugonjwa unaoenea kwa kasi kama kifua kikuu, kukosea tiba kunaweza kusababisha madhara makubwa.


Daniel Ngetich na Patrick Kipngetich kwa sasa wanapoza visigino vyao katika magereza ya serikali ya Kenya; labda mahakama kama itatoa amri nyingine, wataendelea kubakia huko kwa miezi minne hadi watakapomaliza tiba ya TB.


Henry Ngetich, ambaye pia alikamatwa kutokana na kukosea tiba yake, alikuwa na bahati ya kuishia hospitalini kutokana na hali yake kuwa mbaya. Hatua ya serikali ya Kenya kukamata na kuwasweka ndani wagonjwa wa TB imekemewa na mashirika ya haki za binadamu ambayo yamesema ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


"Kila mtu ana haki ya kupata huduma sawa za tiba na hizi lazima zitolewe kwa utu na heshima," alisema Pascaline Kang’ethe mratibu wa taifa, haki ya afya na VVU/UKIMWI katika shirika la ActionAid International Kenya.


"Hii ni kesi ya ubaguzi na hatua ambayo inaweza kusababisha wengine wanaohitaji tiba kukimbia kutokana na kuhofia kukamatwa." Nelson Otwoma, afisa mtendaji mkuu wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI, alisema wanaume hao wawili wanashikiliwa gerezani katika mazingira ya kusikitisha na hawapati lishe bora ambayo inahitajika kwa wagonjwa wa TB.


Wakati tunapowatembelea, tunawakuta wakishikiliwa katika vyumba kama vya wafungwa wengine. Hawajatengwa.Katika kufanya mambo kuwa mabaya zaidi wanatibiwa kama wafungwa wa kawaida na wana pingu na chini ya ulinzi wa askari wenye silaha," Otwoma alisema. Akizungumza na IPS, mkuu wa mpango wa taifa wa Kudhibiti Ukoma na TB, Joseph Sitienei alitetea hatua ya serikali, akisema walifanya hivyo kulinda maslahi ya wengine baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wanafamilia."Afisa afya ya umma katika mkoa huo alitumia sheria chini ya sheria ya afya ya umma kifungu cha 27 – ambayo inampatia mamlaka ya kuchukua hatua inayofaa ikiwa ni pamoja na kuweka kizuizini wagonjwa wanaoeneza ugonjwa kuzuia kueneza zaidi ugonjwa huo," Sitienei alisema.


Makadirio ya mwaka 2008 ya Shirika la Afya Ulimwenguni yanasema watu 5,000 duniani kote wanakufa na TB kila siku. Mataifa mengine kadhaa pia yanaonekana kusweka watu jela kudhibiti kuenea kwa TB.


Mwaka 1994, mamlaka ya afya ya Israel ilifungua mashitaka ya kutaka kutengwa kwa lazima kwa mtu asiyekuwa na makazi ambaye ameambukizwa TB sugu kutokana na kushindwa kumaliza tiba. Nchini Afrika Kusini mwaka 2007, kugundulika kwa TB sugu zaidi kulisababisha mjadala wa kutengwa kwa lazima kwa wagonjwa.


Uamuzi ulichukuliwa kuwaweka katika kizuizi wagonjwa wa TB isiyosikia dawa kabisa katika majengo kama la hospitali ya Brooklyn Chest mjini Cape Town.


"Kuna changamoto ambazo hazina majibu," Simon Moeti, msimamiaji mkuu wa madawa katika jimbo hilo aliliambia Shirika la Habari la Afrika Kusini. "Kuna watu ambao wanachanganya tiba, watu ambao wanataka kuacha kutumia tiba.


" Otwoma alisema kufungwa jela kwa watu wawili nchini Kenya katika Jimbo la Bonde la Ufa kumepeleka ujumbe mbaya na kusababisha kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wengine wa TB ambao wameacha kutumia dawa.


"Kwa kweli tulipotembelea makazi ya Daniel… mke wake alisema kuwa mtoto wao wa mwisho pia amekuwa akikohoa, anahofia kwenda kupima kutokana na kuogopa kuwekwa kizuizini pamoja na mtoto wake kuwezesha tiba," alisema.


Chini ya sheria ya afya ya umma, kulinda usalama wa wengine kunavuka haki ya mtu kufurahia maisha.


Wagonjwa ambao wanapatikana na magonjwa ya kuambukiza wanaweza kutengwa kuzuia kueneza ugonjwa na hii inatakiwa kufanyika katika wodi maalum katika hospitali za serikali. Lakini Allan Ragi, mkurugenzi mkuu wa Umoja wa NGOs za UKIMWI Kenya, anasema hospitali za serikali hazina vifaa.


"Chini ya duru ya tano ya Mfuko wa Dunia, Kenya ilipata dola milioni 19 kujenga wodi zilizojitenga katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta. Miaka mitano tangu wakati huo, bado mradi huu haujakamilishwa," Ragi alisema. Alisema badala ya kuwekeza katika kukamata wanaokiuka masharti ya dawa, serikali inapaswa kuwekeza katika kujenga uelewa kuhusu kifua kikuu na tiba yake.


"Nchi hii iko hatarini kukumbwa na janga la TB isiyosikia dawa kwasababu hatuna uwezo wa kupima kila mtu na kufuatilia tiba. Serikali inatakiwa kuwekeza katika kujenga uelewa na kutibu wahamasishaji wa TB ambao watafanya kazi katika jamii kuelimisha wengine ukweli kuhusu TB kuwa inatibika kama mtu atazingatia tiba," alisema Ragi.


Serikali imesema kuwa watu wawili ambao wamewekwa kizuizini wana TB sugu, lakini taarifa hii imekanushwa na wanaharakati wa haki za binadamu ambao wanasema vipimo vya kuthibitisha hilo havijachukuliwa.


Mwishoni mwa mwaka 2009 Kenya ilikuwa na wagonjwa 110,065 wa TB. Makosa ya kutumia tiba ni asilimia tano na serikali inafanya kazi ya kupunguza asilimia hii hadi tatu.


Hadi ifikapo mwaka 2009 Kenya ilikuwa na matukio 500 ya TB sugu kwa madawa mengi ijulikanayo kama MDR-TB. Ni wagonjwa 117 tu wanatumia tiba.


MDR-TB ni sugu kwa madawa mengi ya mstari wa kwanza. Hata hivyo, inaweza kutibika kwa kutumia tiba ya muda mrefu yenye gharama kubwa ya madawa ya mstari wa pili, ambayo yana madhara zaidi.


Kumtibu mgonjwa mmoja kunataka madawa yenye thamani ya zaidi ya dola 16,250. Kenya ni ya 13 kwa kuwa na mzigo mkubwa wa wagonjwa wa TB katika orodha ya Shirika la Afya Ulimwenguni.

FREE MEDIA QUEENS YAIFUNDISHA SOKA UHURU QUEENS YAAMBULIA KICHAPO....


Kikosi cha Uhuru Queens kilichomtoa nyoka pangoni leo
Boss yaania ningecheza mimi hawa uhuru wasinge tufunga Tanzania daima ni kama anamweleza boss wake mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania daima Absalom KIbanda ,kulia akielezwa jambo na mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo Happnes Katabazi ambaye ni daktari wa timu ya Free media Queens ambayo leo haikuwa riziki yake dhidi ya uhuru queens
''Hapa tumekupenda sana mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania daima na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini kwa kuvipenda vyombo vyote bila ubaguzi kwani ilikuwa ni vigumu kwa kipigo tulichotoa kwa timu yake sasa sisi kuwa pamoja nawe ni kama wanamweleza Absalom KIbanda wachezaji hawa na Uhuru Qeens''michezo furaha dada zangu msikonde pamoja sana
Na wewe umecheza hongera sana ndivyo alivyokuwa akiwapongeza wachezaji wa Uhuru Queens mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda
Mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda akiwapongeza wachezaji wa Uhuru queens kwa kuiotea timu yake ya Free ,media queens katika mchezo huo ,"Duh leo mtachonga sana kwa kuwafunga mabinti wangu "Wazee wa kazi Uhuru Queens wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka washindi kutoka kulia waliochuchumaa ni Selina Wilson,Salome Mwasamale ambaye ni kepteni,Samira kiango na waliosimama kuanzia kushoto ni sheila Luksas,Liliani Timbuka,Sophia Asheri,Fatna Likwata na Jane Mibaji

Mazoezi makali yaanza kwa timu ya Free media Queens baada ya kuotewa 15-1 na Uhuru Queens leo
Mchezaji matata wa Free Media akionyesha uwezo wake mkubwa uwanjani
Mwalimu we acha tu wacha wajipendekeze tena watatukoma

Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima jumapili Sarehe Mohamed akiwapongeza wachezaji wa Free media Queens baada ya kuifunga Uruhu Queens goli 1-15
Kazi leo ilikuwepo
mabinti wa kazi walio kutana na mpira wa moto kutoka Kikosi cha CCM Uhuru Queens
Timu ya netboll ya Kampuni ya Free Media,( Free Media Queens) inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake na timu ya Uhuru Queens mchezo ambao ulikuwa mgumu kwa timu ya Free Media baada ya kuadhibiwa 15-1 katika viwanja vya TCC Chang'ombe mchezo wa kuwania kombe la NSSF,kutoka kushoto ni daktari wa timu hiyo Happynes,Katabazi,Efrasia Masawe,Samia Mussa,,Iren Mark,Marietha Kayara,Maria Kayala,Heren Ngoromera,na Kocha wa timu hiyo Mussa