Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 28, 2011

BREAKINGNEWS....SINEMA YA MWAKALEBELA NA TAKUKURU YAPOTEZA MVUTO , WANANCHI WAHOJI TAKUKURU IRINGA HAINA KAZI NYINGINE ?Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Iringa mjini na katibu mkuu wa TFF mstaafu Bw Frederick Mwakalebela akiingia katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa kwa ajili ya kuendelea na kesi yake na mkewe ya rushwa ,kabla ya maofisi wa Takukuru kumpandisha tena kizimbani kwa kesi ile ile ya mwanzo ambayoalipata kuachiwa huru na Mahakama wiki iliyopita ,hatua ambayo imeamusha jazba za wananchi wa Manispaa ya Iringa waliofurika mahakamani hapo leo huku wakimvaa boss wa Takukuru Bw.Mkono wakitaka kuachana na kesi hiyo na kuhoji Joseph Mungai kutoendelea kung'ang'aniwa kama Mwakalebela

Wakili wa Mwakalebela (kulia) akiteta jambo na Mwakalebela baada ya kuwekewa dhamana na wananchi waliofika mahakamani hapo japo dalili za Takukuru kumvunjia heshima Mwakalebela zilianza kuonekana baada ya magari zaidi ya matatu ya Takukukuru kufika mahakamani hapo na maofisa zaidi ya watano kwa ajili ya kumtia nguvuni iwapo angeshindwa dhamana ya ghafla ,kuendelea ama kutoendelea kwa kesi hiyo mpya sasa itafahamika Machi 28 mwaka huu ambapo mahakamaitasikiliza rufaa ya Takukuru dhidi ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2010 ambayo juzi mahakamani hiyo ilimwachia huru Mwakalebela


Mke wa Mwakalebela .Bi,Celina (kushoto) akitoka mahakamani hapo baada ya kesi yake kuahirishwa hadi machi 10 mwaka huu
Wananchi wakiwa nje ya mahakama hiyo wakati kesi ya Mwakalebela ikiendelea ,chini na Video ya wananchi kulalamikia usumbufu wa Takukuru Iringa

Habari zaidi ya mahakamani inakuja hivi punde endelea kutembelea mtandao huu

February 27, 2011

CHADEMA KUINGIA IKULU MWAKA 2015 YASEMA FAMILIA YA BABA NYERERE

Rais mtarajiwa na mrithi wa CCM mwaka 2015 Dr.Slaa (chadema)

Damu ya ukombozi inapomwagika
Umati wa wafuasi wa Chadema

FAMILIA ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, imekitabiria Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa kishindo wa kuongoza nchi mwaka 2015.
Familia hiyo ya mwasisi wa taifa imesema ukomo wa serikali ya CCM umefika ambapo inaamini Uchaguzi Mkuu wa urais ujao, CHADEMA itaibuka kidedea.

Kauli hiyo ya familia ya Mwalimu Nyerere, ilitolewa leo na mtoto wa tatu wa Baba wa Taifa, Magige Nyerere, akiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati viongozi wa CHADEMA Taifa walipozuru nyumbani kwa mwasisi huyo Butiama, Musoma, mkoani Mara, ambapo waliweka mashada katika kaburi hilo na Mama Maria kuongoza sala.
Alisema anaamini wapigakura mwaka 2015 watakuwa milioni 12 na kati ya hao, CHADEMA itapata kura milioni sita na CCM itaambulia kura milioni nne.
Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo wa Baba wa Taifa kwa sasa nchi iko katika joto kubwa la kisiasa.

“Lazima tuseme ule ukweli uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA haikuweza kuongoza dola, lakini mwaka 2015 wapigakura watakuwa milioni 12 na milioni sita zitaenda CHADEMA na milioni nne CCM.

“Hali ilivyo sasa, joto la kisiasa hapa nchini liko juu na wananchi wameonekana kufanya mageuzi ya kiuongozi,” alisema Magige Nyerere mbele ya mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere.
Huku akimfananisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mdogo wake, Makongoro Nyerere, ambaye naye alikuwapo alisema, “Nakiri kuwa mimi ni CCM, lakini nafurahia kazi na siasa yenu…naomba uendelee hivyo na hata ukiwa bungeni kama kiongozi wa upinzani.”

Viongozi hao wa CHADEMA na msafara wao walizuru nyumbani kwa Nyerere majira ya saa 5:55 asubuhi kwa lengo la kumsalimia mjane wa Baba wa Taifa.
Kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alimuomba Mama Maria kukiunga mkono chama hicho na kukiombea mema.
“Mama tumekuja kukusalimia na familia yako…CHADEMA tunaomba mtuombee na mtuunge mkono,” alisema Mbowe kisha Mama Maria kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo hayo.

Akitoa nasaha zake mbele ya kaburi la Nyerere, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mchakato wa Nyerere kuwa Mtakatifu mwenye kheri bado haujakamilika, hivyo raia wawe na uvumilivu.
Alisema nchi ya Uganda imepiga hatua juu ya mchakato huo, hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
Kuhusu maandamano ya CHADEMA nchi nzima, Magige Nyerere alisema,” Awali nilipatwa na wasiwasi mkubwa, lakini nimebaini kumbe ni maandamano mazuri; yaendelee.”

Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa alisema maandamano hayo ni vema yakaendelea kwa amani, ili kufikisha ujumbe husika katika mamlaka husika.

Wakiwa wilayani Tarime jana Mbowe alimtaka Rais Kikwete kuacha mara moja kuwajaza hofu Watanzania juu ya kuwepo mipasuko ya kidini. Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa kabla ya mkutano, alihoji sababu ya Rais Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwasweka ndani wanaoleta chokochoko za kidini.

undani wa habari hii soma gazeti la Tanzania daima la kesho jumatatu

BREAKINGNES ...UGUMU WA MAISHA KUONGEZEKA ,BEI YA PETROL DUNIANI YAPANDA

Moja kati ya vituo vya mafuta mjini Iringa

Bei ya mafuta ghafi ya Brent imeongezeka mno
Kiwango cha bei ya mafuta ya petroli kimepanda kufikia viwango ambavyo haviwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka miwili kutokana na hofu iliyosababishwa na ghasia nchini Libya zinazotishia kuathiri mtiririko wa mafuta yanayotoka mashariki ya kati.


Bei ya mafuta ghafi ya Brent maarufu kama North Sea Brent crude yanauzwa kwa dola 117 kwa pipa moja.

Bei ya petroli kimataifa imepanda kwa asilimia 5 tangu machafuko ya Libya yaanze.
Libya ni ya 12 kati ya nchi zinazozalisha mafuta duniani, na hivyo haipo miongoni mwa nchi zinazouza mafuta kwa wingi, ingawa mafuta ghafi ya Libya yanapendwa mno kwa sababu inaaminika kuwa kiwango chake ni cha juu na mepesi kusafisha.Hofu iliyopo katika masoko siyo kupoteza mafuta ya Libya bali ni machafuko hayo kuenea kote katika nchi za Mashariki ya kati, hususan Saudi Arabia.

Kupanda kwa bei kwa sasa hivi kumetokana na ripoti iliyochapishwa na benki ya kuwekeza ya Goldman Sachs ikionya juu ya kupungua kwa mafuta yanayoagizwa.

Bei ya mafuta ghafi ilipanda kwa dola saba katika muda wa dakika 90 katika masoko ya hisa ya Ulaya mapema leo, ishara ya hofu iliyoyakumba masoko ya mafuta.

UN SASA YAMWEKEA VIKWAZA RAIS GADDAFI...Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi(pichani) kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.


Rais Jakaya Kikwete na Mkewe wakisalimiana na Rais Gaddafi katika moja kati ya mikutano ya Marais
Wajumbe wa UN wakipiga kura ya vikwazo kwa Gaddafi
Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.
Serikali ya mpito
Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.
Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.
Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.Waandamanaji Benghazi
Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.
Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.
Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.

BREAKINGNES ..JARIBIO LA KUMPINDUA RAIS KABILA CONGO LAKWAMA

RAIS KABILA
Habari kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa watu saba wameuawa baada ya kufanya jaribio la kumpindua Rais Joseph Kabila katika makazi yake.
Watu hao waliuawa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.
Mwandishi Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa amethibitisha kumetokea taarifa hizo. Hata hivyo watu waliohusika bado hawajajulikana.
Taarifa zaidi tutawaletea kadri zitakavyokuwa zikipatikana.

ASKOFU BOAZ SOLLO WA KITUO CHA MAOMBI CHA OVERCOMERS ATENDA MIUJIZA KWA VIPOFU IRINGA

Askofu Boaz Sollo wa kituo cha maombi cha Overcomers Iringa akimwombea mwanamke aliyekuwa akisumbuliwa macho kwa zaidi ya miaka mitatu na mwanamke huyo kufunguliwa na kuona

Mzee Garevas Sanga mkazi wa Mtwivila Iringa akiombewa na askofu Sollo nakufanikiwa kuona kwa uwezo wa Mungu ,mzee huyo anadai zaidi ya miaka miwili alikuwa akisumbuliwa na macho na kutoona kabisa sasa ameona
Nimeona nakuona na wewe askofu namshukuru Mungu ndivyo alivyokuwa akisema mwanamke huyo katika ushuhuda wake leo baada ya kuombewa katika ukumbi wa IDYDC Makosa Iringa ,ibada nyingine ya maombezi ni Alhamisi majira ya saa nane mchana

Huduma ya maombezi kwa wagonjwa wa macho Iringa

Mashuhuda wa macho Iringa ,wengi waponywa kwa damu ya Yesu

"Najisikia kuona sasa "


Askofu Sollo akimchezea Bwana kwa shangwe baada ya watu zaidi ya kumi ambao walikuwa na matatizo ya macho kufunguliwa leo
Tazama Video ya shuhuda aliyeweza kuona kwa uwezo wa YESU na sehemu ya maombi ya askofu Boaz Sollo leo jioni mjini Iringa

VIFAA VYA MASHULENI NA MAOFISINI FIKA GWIVAHA ENTERPRISES Co.STATIONARI IRINGA

Gwivaha Enterprises co ni Stationari ya kisasa yenye wahudumu wenye ujuzi wa hali ya juu ndani ya mji wa Iringa

Tonauza vifaa mbali mbali vya mashuleni na maofisini kwa gharama nafuu kuliko stationari nyingine ndani ya mji wa Iringa
Tunafanya kazi kwa mfumo wa kisasa zaidi na mfumo wa sayansi na Teknolojia ndani
Pia Gwivaha Enterprises ni mawakala wa serikali katika uandaaji wa kazi mbali mbali na tumekuwa na uhakika zaidi wa huduma zetu
Shule mbali mbali na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mji wa Iringa wamekuwa wakichagua Gwivaha Enterprises kama chaguo lao sahihi ya Photo copy na kuchapa kazi mbali mbali
Pia vifaa vya semina vinapatikana kwa bei poa


CD tupu zenye viwango zinapatikana

Karatasi pia zinauzwa kwa jumla na reja reja


Vifaa vyote zinapatikana ndani ya Gwivaha Enterprises Iringa hakuna haja ya kuuliza stationari uwapo mjini Iringa uliza Gwihava ni jibu la swali lako ,kwetu unaminifu na ubora wa huduma zetu ni sehemu ya kazi yetu


Gwivaha Enterprises co. ni stationari maarufu mkoani Iringa inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya maofisini na mashuleni ,uchapishaji wa nakala mbali mbali ,Binding,lamination,utoaji wa Photo copy zenye ubora wa kweli.n.k

Gwivaha Enterprises co. tunapatikana jirani na stendi ya daladala za zienadazo chuo kikuu cha Mkwawa ( stendi ya M.R. Hotel ) ama barabara ya kuelekea ofisi ya CCM mkoa wa Iringa .

Wasiliana nasi kwa simu 0754 624738,0755912277 Tutakusikia tuatakufikia hapo ulipo

Karibu Iringa ,karibu Gwivaha Enterpris Co Stationari bora Iringa

BREAKINGNEWS....BOSS WA MOHAMED ENTERPRISES IRINGA MATATANI KWA UCHAFU

kaimu OCD Iringa akiwa na viongozi wa Manispaa baada ya kumtia hatiani meneja wa METL,Iringa
HALMASHAURI ya manispaa ya Iringa imezindua siku ya usafi kwa kila jumamosi ya kwanza ya mwanzo wa mwezi ikiwa ni pamoja na kuweka sheria kali kwa wanaotupa taka ovyo na kujisaidia maeneo yasiyo rasmi kuwa adhabu ya papo kwa papo itakuwa ni shilingi 50,000.

Huku kaimu meneja wa kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Ltd (METL) mkoani Iringa Ivani Ole Mganga akifikishwa polisi kwa kuwashambulia kwa lugha chafu viongozi wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mstahiki meya, kaimu mkurugenzi na mkuu wa polisi wilaya ambao walikuwa katika kampeni za usafi jirani na ofisi za kampuni hiyo eneo la Mlandege.

Kaimu meneja huyo wa kampuni hiyo METL ,Mganga alikamatwa na polisi majira ya saa 4.02 asubuhi akiwa nje ya ofisi yake baada ya uongozi huo wa Manispaa ya Iringa kumhoji sababu ya kuacha mazingira ya ofisi yake katika hali ya uchafu na badala ya kuwajibu vizuri alianza kuwatolea lugha za matusi kabla ya kaimu mkuu wa polisi wilaya kuagiza askari waliokuwepo eneo hilo kumkamata na kumfikisha kituoni.

Akizungumza katika uzinduzi siku ya usafi katika manispaa ya Iringa katika maadhimisho yaliyofanyika kwenye kata ya Kwakilosa mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema kuwa idadi kubwa ya wakazi wa Manispaa hiyo wamekuwa na jeuri kubwa pindi wanapoelezwa juu ya utunzaji wa mazingira .

Hata hivyo alisema kukamatwa kwa meneja huyo wa kampuni ya METL ni fundisho kwa wamiliki wengine wa kampuni mjini Iringa na wananchi wa mji huo ambao wamekuwa wakishindwa kuheshimu sheria ya usafi na kuchafua ovyo mazingira yao.

Mwamwindi alisema kuwa kuanzia sasa uongozi wa manispaa ya Iringa utaendelea kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuchafua mazingira kusudi ama kushindwa kuweka mazingira katika hali ya usafi .

"Ujue huyo meneja wa METL kutokana na kufanya kazi katika kampuni ya mwarabu na yeye amejiona ni Mwarabu na kuanza kuleta lugha chafu mbele ya wananchi na viongozi kwa kujiona yupo juu ya sheria....sasa tumeamua sheria hii kuanza kwake kama fundisho kwa wengine"

Alisema kuwa lengo la kuweka sheria kali za uchafu ni kutaka manispaa ya Iringa kuja kushika nafasi ya kwanza kiusafi katika Tanzania pia kuepusha magonja ya milipuko kama kipindu pindu na magonjwa mengine ya milipuko .

Alisema Meya Mwamwindi kuwa wapo baadhi ya watu wanaoendelea kuchafua mazingira ovyo katika maeneo yao kinyume na sheria ndogo za mji ambazo zinapiga marufuku uchafuzi wa Mazingira na kuwa kutokana na sheria ya sasa adhabu kali imewekwa kwa kundi ,ama mtu yeyote atakayebainika akichafua mazingira kusudi.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Mashaka Luhamba alisema kuwa tayari elimu kwa wananchi wa Manispaa hiyo imeanza kutolewa kupitia vyombo vya habari ili kila mkazi wa mji wa Iringa kuitambua vizuri sheria hiyo na pale atakapokwenda kinyume asilalamike kuadhibiwa .

Pia alisema kuanzia sasa ni marufuku mifugo kuchungiwa katikati ya mji pia marufuku mtu kutupa taka ovyo kama vocha za simu na kuwa sheria hiyo pia itawabana wamiliki wa nyumba za kuishi na zile za wageni watakaokutwa wanatiririsha maji machafu ovyo.

Nao wakazi wa kata ya Kwakilosa ambao walishiriki katika uzinduzi huo wamepongeza jitihada hizo za manispaa ya Iringa katika kumwajibisha meneja huyo wa METL Iringa kwa kuonyesha jeuri wakati wa utekelezaji wa sheria hiyo na kuwa kutokana na mkakati huo upo uwezekano wa mazingira ya mji wa Iringa kuboreshwa zaidi japo waliomba kwa upande wa Manispaa kuhakikisha gari ya taka taka inafika mapema kusomba taka zinazohifadhiwa katika vituo.

SIMU ZA MIKONONI ZISIVYO NA SIRI

Kuna uzuri na ubaya wa mawasiliano ya simu za mikononi kama vijana hawa walivyokutwa wakisikiliza simu moja jana eneo la Posta ,inasemekana kuwa aliyepiga simu amekuwa na kawaida ya kudanganya
"Hatupo pamoja wewe ongea kwa uhuru"

February 26, 2011

BREAKINGNEWS.....TAKUKURU YAZIDI KUMNG'ANG'ANIA MWAKALEBELAMwanasheria wa Takukuru (kushoto) akiwa na wakili wa Mwakalebela Basil Mkwata nyuma ni mwakalebela

SIKU moja baada ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa kumwachia huru aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Frederick Mwakalebela katika shitaka lake la rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini,taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa imekusudia kuendelea na kesi hiyo.

Akizungumza na mtandao huu wa
http://www.francisgodwin.blogspot.com/ mwanasheria wa TAKUKURU mkoani Iringa Ntime Mizizi alisema kuwa maamuzi ya mahakama hiyo chini ya hakimu Festo Lwila ameyakubali na kuwa mapungufu yaliyokuwemo awali katika kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2010 taasisi hiyo inayafanyia kazi na kufungua kesi yenye maelekezo ya mahakama.

Alisema kuwa maamuzi ya mahakama katika kesi hii ya Mwakalebela yameonekana ni mazuri na yenye maelekezo ya kina zaidi kuliko ilivyo kuwa kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Joseph Mungai ambao mahakama haikwenda kiundani zaidi kama ilivyo katika maamuzi madogo ya kesi ya Mwakalebela.

Hata hivyo alisema kuwa kesho jumatatu kutakuwa na majibu sahihi dhidi ya uamuzi wa takukuru katika kuendelea na kesi hiyo ama lah.

“Nakuomba unitafute jumatatu nitakuwa na majibu sahihi ….japo maandalizi ya shitaka jipya yatakuwa yamefanyika” alisema mwanasheria huyo wa Takukuru
Habari kamili inakuja

MANISPAA YA IRINGA YAZINDUA SIKU YA USAFI ,WANAOJISAIDIA OVYO KUKIONA

Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bw.Mashaka Luhamba (kulia) na Msitahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi wakifanya ussafi katika eneo la Samora mjini Iringa wakati wa uzinduzi wa siku ya usafi mjini Iringa ,huku sheria ndogo ikizinduliwa kwa wanaotupa taka ovyo na kujisaidia ovyo kupigwa faini ya papo kwa papo shilingi 50,000
Mwanasheria wa manispaa ya Iringa (kulia ) akiwa katika maadhimisho hayo leo la Mlandege
Habari inakuja

T.R.A IRINGA LAWAMANI...

Mfanyabiashara Thobias Kileo Mawishi akionyesha baadhi ya malipo ambayo amekuwa akilipia mapato TRA ambao wamefunga duka lake kwa deni ya Tsh.180,000 kuwa ni mdaiwa sugu katika mkoa wa Iringa


hapa akiwa nje ya duka lake baada ya kufungwa na madalali wa Majembe
Huu ndio ufungaji wenyewe wa duka hilo hali ambayo ni hatari kwa usalama wa mali

Watumishi wa kampuni ya udalali ya Majembe wakipongezana baada ya kufunga duka hilo eneo la Miyomboni Iringa ,chini Video Bw Mawishi akieleza masikitiko yake


MFANYABIASHARA Iringa mjini ailalamikia mamlaka ya mapato Tanzania (T.R.A) kwa kumnyanyasa na kuitumia kampuni ya udalali ya Majembe kufunga duka lake kwa zaidi ya siku mbili kwa madai kuwa ni mdaiwa sugu anayedaiwa shilingi 180,000.

Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mfanyabiashara huyo Thobias Kileo alisema kuwa yeye ni mmoja kati ya wafanyabiashara mwenye TIN. 101330830 na kati ya wafanyabiashara waaminifu katika Manispaa ya Iringa .

Alisema kuwa wakati madalali wa Majembe wanafika kufunga duka lake kwa nguvu Februari 24 walidai anadaiwa kiasi cha shilingi milioni moja ila kumbukumbu ambazo zimekutwa ofisi za TRA mkoa wa Iringa hadi juzi deni ambalo anadaiwa ni kiasi cha shilingi 180,000 .

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na kudaiwa fedha hizo ila bado anasikitishwa na utaratibu wa kampuni ya udalali ya Majembe kufika kufunga duka lake huku wakitupa ovyo vitu katika duka hilo la kutoufunga mamalango wa duka hilo vizuri hali ambayo inaweza kusababisha upotevu wa mali.

“Kweli huu utendaji kazi wa TRA mkoa wa Iringa unashangaza kwani kitendo cha kufunga duka la mtu bila kuandikiana sehemu yeyote ana kusaini ni kosa kwani pale mali zinapoonekana kupotea na nani wa kumlalamikia ….binafsi ninaomba uongozi wa TRA makao makuu kuchunguza utendaji kazi wa TRA Iringa”

Kileo alisema kuwa kutokana na udhalilishaji uliofanywa na vijana wa udalali wa Majembe alifika kufikika malalamikio yake kwa meneja wa TRA mkoa wa Iringa pamoja na kufikisha kilio hicho kwa uongozi wa juu wa TRA ngazi ya Taifa .


Hata hivyo alihoji kuwa iwapo yeye ni mdaiwa sugu wa mwisho katika mkoa wa Iringa anayedaiwa shilingi 180,000 basi ni wazi

Meneja wa T.R.A mkoa wa Iringa hakuweza kupatikana kuelezea suala hilo huku vijana wa kampuni ya udalali ya majembe wakidai kuwa wao si wasemaji wa juu wa suala hilo japo walikili kulifunga duka hilo na kuwa wao wakipewa majina ya wadaiwa kazi yao na kutekeleza na si vinginevyo.