Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2010

BREAKINGNEWS,MONICA MBEGA APINGA MAHAKAMANI UBUNGE WA MSIGWA

Monica Mbega
Mchungaji Peter Msigwa (MB)
Katibu wa ccm wilaya ya Iringa mjini Bw.Charles Charles
MBUNGE wa zamani wa jimbo la Iringa mjini na mkuu wa mkoa wa KIlimanjaro ambaye alikuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Monica Mbega amefungua kesi namba 3 ya mwaka 2010 katika mahakama kuu kanda ya Iringa akipinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea mbunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mchungaji Peter Msigwa.

Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Charles Charles alithibitisha mbele ya waandishi wa habari leo ofisini kwake kuhusiana na Mbega kwenda mahakamani kupinga ushindi wa mchungaji Msigwa wa Chadema kwamadai ya kuwepo kwa kasoro zaidi ya 10 zilizopata kujitokeza siku ya uchagua mkuu octoba 31 ikiwemo ya vituo vya kupigia kura kuhamishwa dakika za mwisho na kufanya baadhi ya wapiga kura kutopiga kura.

Kasoro nyingine ni ile ya tofauti ya matoke yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini ambayo kwa mujibu wa Mbega kuwa yalionyesha kutofautiana kwa kura kama 800 na sehemu ila matokeo ya pili yaliyotangzwa bila kuwepo kwa wakala wala mgombea wa CCM yanaonyesha mgombea huyo wa CCM alipitwa kwa kura zaidi ya 2000 na mgombea wa Chadema.

Hivyo alisema kuwa kutokana na kasoro hizo na nyingine nyingi mgombea huyo wa CCM Mbega amelazimika kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo ya uchaguzi mkuu .

Charles alisema kuwa matokeo ya kwanza ya ubunge yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi yalionyesha mgombea wa NCCR-mageuzi Mariam Mwakingwe alikuwa amepata kura 950 na Monica Mbega (CCM) alikuwa amepata kura 16,916 huku mchungaji Msigwa akipata kura 17742 na kuwa matokeo hayo yalitangazwa huku mawakala wa CCM wakiwepo na kupokea hivyo.

Japo baadaye msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo mapya ambayo mgombea wa CCM wala wakala wake hakuwepo ambapo matokeo hayo Msigwa yalimpa ushindi mkubwa Msigwa kwa kupata kura 17,352 wakati Mgombea waNCCR Mageuzi Mwakingwe akipata kura 1292 .

Hivyo alisema kuwa ukitazama matokeo hayo unapata picha halisi ni jinsi gani ambavyo msimamizi wa uchaguzi alivyoshindwa kutoa matokeo sahihi ya jimbo hilo na kuwa hadi sasa mgombea wa CCM hajapata nakala ya matokeo hayo mapya ambayo ndiyo yamempeleka Msigwa bungeni.

Pia alisema kuwa kasoro nyingine ni ile ya idadi ya wapiga kura katika baadhi ya vituo kuonekana kubwa zaidi ya wale waliojiandikisha na sehemu nyingi idadi ya waliopiga kura na wasio piga kura ukijumlisha unakuta kuna tofauti kubwa ya kura kuzidi.

Hata hivyo alishindwa kutaja wakili anayesimamia kesi hiyo kwa madai kuwa atajulikana pindi kesi hiyo itakapoanzwa kusikilizwa pamoja na kujua idadi ya halisi ya kasoro zilizotolewa na Mbega ambaye hakuweza kupatikana kuelezea suala hilo.

Kwa upande wake Mchungaji Msigwa alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya Mbega kwenda Mahakamani kupinga ushindi wake alisema kuwa hata yeye amekuwa akisikia kuwepo kwa suala hilo japo hadi jana alikuwa hajapatakufikishiwa taarifa yoyote rasmi toka mahakamani juu ya kuwepo kwa kesi hiyo.

"Mimi mwenyewe nimekuwa nikisikia kama Mbega amekwenda mahakamani kupinga ushindi wangu ila mimi sijapata taarifa rasmi za kuitwa mahakamani japo ni haki yake ya msingi kwenda mahakamani"alisema Mbunge Msigwa alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi.

November 29, 2010

GWIJI WA BLOG ISSA MICHUZI AWAPA DARASA WASANII

Ankal Michuzi akitoa elimu kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa kuhusu umuhimu wa blogs katika kukuza sekta ya sanaa nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti,habari na Mafunzi wa BASATA,Godfrey Lebejo na Katibu wa CAJAtz,Vicky Kimaro.

Ankal Michuzi akiwaonyesha wadau wa Jukwaa la Sanaa jinsi ya kuweka video kwenye U-Tube.


Mdau wa Sanaa akimuuliza Ankal Michuzi swali.

Ankal Michuzi (Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.

WENGI WAJITOKEZA KUWALILIA MAAFISA ARDHI WALIOKUFA KWA AJALI .....

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Abdu Sinde tayari kwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Siginda Marehemu Abdu Sinde enzi wa uhai wake
Marehemu Ally Lugenge enzi za uhai wake
Waombolezaji ambao ni watumishi wa Manispaa ya Iringa wakipata kitu nazi

Na Francis Godwin,Iringa
MAMIA ya wakazi wa mji wa Iringa leo wamejitokeza kwa wingi nyumbani kwa aliyekuwa mtumishi wa Idara ya ardhi Abdu Sinde kwa ajili ya kuaga mwili wake kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwako Singida .

Sinde na mwenzake Alli Lugenge ambao wote walikuwa watumishi wa ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa walipoteza maisha yao juzi katika ajali ya gari ndogo yenye namba za usajili T 130 Ays Toyotaambayo ilikuwa ikiendeshwa na Sinde baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso la Lori .

Ajali hiyo ilitokea juzi usiku katika eneo la Rungemba wilaya ya Mufindi wakati maofisa ardhi hao wa Manispaa ya Iringa Ally Lugenge na Abdu Sinde wakitokea mjini Mafinga kurejea nyumbani kwao mjini Iringa.

Mmoja kati ya mashuhuda wa ajali hiyo John kalinga alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo iliyokuwa na maofisa hao wa Manispaa ya Iringa kuhama upande wake na kulifuata lori hiyo ambalo lilikuwa katika mwendo mkali.

Alisema kuwa kutokana na mwendo mkali ambao dereva wa gari ndogo alikuwa akiendanao na ule wa lori ilikuwa ni vigumu kwa abiria waliokuwemo katika gari hilo ndogo kutoka wakiwa hai baada ya gari hiyo kugongwa vibaya .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kutaja lori hilo kuwa lina namba za usajili T 124 BCZ likiwa na tela lenye namba T888BDC ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mahamundu Kitenge (60) mkazi wa jijini Dar es Salaam .

Kamanda Mangalla alisema katika ajali hiyo abiria wa gari ndogo Ashiri Yusuph (22) amejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Mafinga wilayani Mufindi huku dereva wa lori hilo akishikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Akielezea juu ya kifo cha watumishi hao mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo mbali ya kutoa pole kwa familia ya marehemu hao bado alisema kuwa vifo vya watumishi hao ni pigo kubwa jingine katika Halmashauri hiyo ambayo wiki iliyopita imempoteza aliyekuwa afya wake Mareheme Emanuel Ngerera aliyefariki ghafla akiwa nyumbani kwake Frelimo.
MWISHO

November 28, 2010

'LIVE' HARUSI YA MLALAHOI USIKU HUU UKUMBI WA IDYDC

Misanjo Livigha akimvisha pete mkewe Zainab Chamwazi

Bibi harusi Zainab Chamwazi akimvisha pete Mlalahoi

MC,Maarufu mkoa wa Iringa Thobias Kikula a.k.a Kikulacho akiwamiminia mvinyo maharusi
Mpigapicha maarufu mkoani Iringa Misanjo Livingha a.k.a Mlalahoi Alwatan akiingia katika ukumbi wa IDYDC na mkewe wa ndoa Zainab Chamwazi kwa mbwembwe

Hapa wakiselebuka sebene
Ukumbi wa walipuka kwa shangwe

'LIVE' KIPAIMARA CHA ANOLD NYATO MAMBO YAZIDI KUNOGA

Zawadi kubwa kuliko zote kwa mtoto Anold ni amri kumi za Mungu ambayo imetolewa na mama mzazi pamoja na Biblia
RAs Mpaka akitoa zawadi

Babu wa Anold mzee Nyato akidua sanjari na ndugu wengine kama sehemu ya michezo mbali mbali ukumbini
RAS wa mkoa wa Iringa mama Getrude Mpaka (kulia) akijichanganya na wananchi katika Kipaimara ni viongozi wachache sana wanaweza kufika maeneo kama haya,hakina Mpaka ni mfano wa kuigwa
Mtoto Anold akicheza na watoto wenzake
Wageni waalikwa akitazama michezo mbali mbali ukumbini


Mama Mfugale na mwenzake mama Zacho (kulia) wakionyesha sanaa yao ya kupiga kigelegele

'LIVE' KIPAIMARA CHA ANOLD NYATO NA ERICK NYATO SASA

Mambo ya msosi kwa wote

'LIVE' KIPAIMARA CHA ANOLD NYATO NA ERICK NYATO SASA

Mama mzazi wa Anold Bi.Rose Sitaki

Babu wa Anold akichukua msosi
Anold Enzi wa utoto wake

'LIVE' KIPAIMARA CHA ANOLD NYATO NA ERICK NYATO SASA

Mwanasiasa maarufu Rose Sitaki ambaye alipata kushinda katika kura za maoni ndani ya CCM ubunge viti maalum mkoa wa Njombe akitoa hosia kwa mtoto wake Anold sasa na kumtaka kufuata misingi ya dini katika maisha yake
Shangwe za ndugu na jamaa ukumbini
Mtoto Anold akimlisha keki mjombake Enock Sitaki
Keki ya Anold kwa ajili ya pongezi ya kufanya vema mafundisho ya kipaimara
Mama mzazi wa Anold Nyato ,Rose Sitaki ( kulia) akiwa na viongozi wa dini kanisani usharika wa Iringa mjini mchana leo
Msaidizi wa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa mchungaji Blaston Gavile (wa pili kulia) akigonganisha glasi za mvinyo
Sherehe inaendelea
Ndugu na mafariki wakiwa ndani ya ukumbi akishuhudia tukio la kulishana keki kwa watoto hao
Mtoto Anold Nyato aimlisha keki kaka yake Erick Nyato hivi sasa katika sherehe za kipaimara zinazoendelea katika ukumbi wa Upendo sabasaba mjini Iringa,Anold amezaliwa mwaka 1999

November 27, 2010

BREANGNEWS AJALI YAUA MAAFISA ARDHI WAWILI WA MANISPAA YA IRINGA

Ajali mbaya imetokea usiku huu katika eneo la Rungemba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na kusababisha vifo vya watu wawili. Taarifa zilizotua hivi punde toka Mafinga zinadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori kugongana na gari ndogo waliopoteza maisha wote ni watumishi idara ya ardhi ktk Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Abdu Sinda na Ally Lugenge huku mtu mmoja ndugu na marehem hao amejeruhiwa vibaya na kulazwa ktk hospitali ya wilaya ya Mufindi.

MTOTO ALIYEZALIWA UBONGO NJE .....


Hivi ndivyo kichwa cha mtoto kinavyoonekana


Matroni wa wodi ya kina mama bi. Haule akimhudumia mtoto na aliyembeba ni Bi Sabina Lyombo mama wa mtoto


Na Sekela Mwasubila, Ulanga

Mtoto mmoja katika hospitali ya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amezaliwa ubongo ukiwa nje baada ya kukosa ngozi ya kichwa huku akiwa mwenye afya njema.

Akiongea na mwandishi Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt Amani Kombe amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumatatu majira ya saa tatu usiku baada ya mama wa mtoto kujifungua mtoto huyo wa kiume hospitali hapo.

Aliongeza kuwa hali ya mtoto kuzaliwa na kukosa ngozi ya kichwa hutokea wakati wa uumbaji wa viungo mbalimbali vya mwili wa mtoto na hali hiyo huweza kusababishwa na ukosefu wa madini mbalimbali kwa mama wakati wa ujauzito aidha ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya wilaya.

Naye mama wa mtoto bi. Silvia Lyombo (20) ambaye ni ujauzito wake wa kwanza alisema kuwa hakupata matatizo yoyote ya kiafya wakati wa ujauzito na alijifungua katika hali ya kawaida mtoto mwenye uzito wa kilo 2.9 na kuwa ananyonya kama kawaida na hana tatizo lolote zaidi ya kukosekana kwa ngozi ya kichwa aidha hakuna dawa zozote ambazo alizitumia katika kipindi chote cha ujauzito wake.

Hata hivyo wataalamu wa hospitali ya wilaya walisema kuwa watampeleka mtoto huyo katika hospitali kubwa mkoani Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo la mtoto huyo ambaye hadi sasa yupo hai na afya njema.

November 26, 2010

KIPINDUPINDU KINAKARIBISHWA MANISPAA YA IRINGA.....

Huu ni mlima wa taka uliotengenezwa katika mtaa wa Kwamwogongo Manispaa ya Iringa ,kwa mujibu wa viongozi wa serikali ya mtaa huo taka hizi hazijazolewa kwa zaidi ya miaka 7 sasa na kila siku viongozi wamekuwa wakitoa ahadi bila kutekelezwa hivyo wameomba uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa kusaidia kutatua kero hiyo ambayo imepata kufichuliwa na mtandao huu kwa kushirikiana na Redio Country Fm (88.5) Iringa
Hapa watoto wakiwa wamepanda juu ya mlima wa taka kutafua mabaki ya uchafu kwa ajili ya matumizi yao
Wananchi wakitazama mlima huo wa taka ambao kwa sasa umeonekana kuzidi na kufukia baadhi ya makaburi eneo hilo .

November 24, 2010

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Mbunge wa jimbo la Ismani na waziri mteule wa serikali ya JK Mh Wiliam Lukuvi akikatiza mitaaa ya Iringa

BARAZA JIPYA LA MAWZIRI

1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe

Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira

2.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia

3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano) Samia Suluhu

2. Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa

4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi

soma hapa zaid