Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

October 31, 2010

BREAKINGNEWs MATOKEO YA UCHAGUZI HALI SI NZURI KWA CCM IRINGA


Na Francis Godwin,Iringa

MATOKEO ya awali katika jimbo la Iringa mjini, Njombe Kaskazini na Njombe Magharibi yameanza kutoka jana usiku huku vituo mbali mbali wagombea wa ubunge na urais wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakionekana kung’ara zaidi .

Katika jimbo la Njombe Magharibi mgombea ubunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo zaidi ya vituo 10 vya kata ya Ilembula ,Mdandu na Saja ameonyesha kufanya vizuri ukilinganisha na mgombea wa CCM Gyerson Lwenge kama ilivyo katika jimbo la Njombe Kaskazin ambako mgombea wa Chadema Alatanga Nyagawa akionyesha kuvutaka shati mgombe wa CCM Deo Sanga katika maeneo ya Lupembe ,Wangama na baadhi ya maeneo ya Makambako ambako hata hivyo kata ya mji mwema uchaguzi wa udiwani haujapata kufanyika baada ya karatasi ya kupigia kura kukosewa kwa zile za Rukwa kuja kata hiyo na kata hiyo kwenda Rukwa.

Katika jimbo la Iringa mjini mbali ya kujitokeza kasoro kadhaa kwa baadhi ya wana CCM katika kata ya Nduli kushindwa kupiga kkura zao baada ya kukosa majina yao katika daftari la wapiga kura kama ilivyo kituo cha stendi kuu ya mabasi ya mikoani ambako idadi kubwa ya wana Chadema walizuiliwa kupiga kura kwa matatizo kama hayo ,bado Chadema imeonyesha kufanya vizuri katika uchaguzi huo.

Matokeo ya awali katika jimbo la Iringa mjini ambayo yalikuwa yamebandikwa vituoni hadi jana majira ya saa 3 usiku ni pamoja na kituo cha Stendi kuu ambako mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete alipata kura (50) mgombea wa Chadema Dk Willibrod Slaa ( 33) na Prof.Ibrahim Lipumba (1).

Ubunge mgombea wa CCM Monica Mbega (36) ,mgombea wa Chadema,Mchungaji Peter Msigwa (97) na mgombea wa NCCR-Mageuzi Mariam Mwakingwe ( 1)

Kituo cha Ngome namba moja mgombea urais wa CCM Dk Kikwete ( 58) Dk Slaa (74) APPT-Maendeleo Peter Mziray (1),wakati nafasi ya ubunge mgombea wa CCM Mbega ( 39)Msigwa wa Chadema( 90) na Mwakingwe wa NCCR-Mageuzi ( 5)

Kituo cha Umati namba moja Kikwete ( 98) Dk Slaa 108 Mziray (1) ubunge Mbega ( 82) Msigwa ( 120) Mwakingwe ( 5),Kituo namba 2 umati Kikwete (97) Dk Slaa( 98)Mziray (1) na TLP (1) huku ubunge Mbega ( 73),Msigwa (114) Mwakingwe(8) na kituo cha umati namba 3 Kikwete ( 64) Dk Slaa(57)Prof LIpumba (1) ,ubunge CCM( 58) Chadema( 64) NCCR-mageuzi(1).

Kituo cha FFU namba 1 Urais CCM(47) Chadema( 63) huku ubunge CCM(36) Chadema(68),NCCR-Mageuzi (3) na kituo cha FFU namba 2 Urais CCM( 64) Chadema( 57) na CUF( 1), ubunge CCM(58)Chadema( 64) na NCCR-Mageuzi (3).

Kituo cha IDYDC namba 1 nafasi ya Urais CCM( 62) Chadema(75) na ubunge CCM ( 46) Chadema(84) na NCCR-mageuzi (5) na kituo cha IDYDC namba 2 Urais CCM (82) Chadema(68) na NCCR Mageuzi (1) Ubunge CCM( 67) Chadema(78) na NCCR mageuzi (7).

Kituo cha THB Urais CCM (97) Chadema(138) CUF( 3) na ubunge CCM(75) Chadema(159) na NCCR-Mageuzi (2) kituo cha Gangilonga urais CCM( 88),Chadema(70) NCCR-Mageuzi (1) na kituo cha Zimamoto namba 1 Urais CCM(84)Chadema(94) na CUF(2) kituo namba 2 Urais CCM( 103) Chadema(84) CUF (1) NCCR-mageuzi (1) ubunge CCM (87) Chadema(106) NCCR-Mageuzi (8) kituo cha soko la Kitanzini namba 1 Urais CCM( 79) Chadema(49) na CUF (1) kituo namba 2 Urais CCM(84) Chadema(68) na CUF(1),ubunge CCM( 70) Chadema(82) na NCCR Mageuzi (1) kituo cha Makorongoni ofisi ya mtendaji kata CCM Urais (66) Chadema( 77) na CUF( 1) ,ubunge CCM( 49) Chadema(96) NCCR-Mageuzi (1), kituo namba mbili ofisi ya mtendaji kata ya Makorongoni Urais CCM (81) Chadema(81) ,CUF(2) UPDP(1)Ubunge CCM(78)Chadema(108) na NCCR-mageuzi (5)

Hata hivyo matokeo hayo baadhi ya vituo hadi majira ya saa 3.30 usiku yakiwa bado kubandikwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwa wamekaa nje ya vituo hivyo wakisubiri kutangazwa kwa matokeo hayo huku FFU wakizunguka zunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kulinda amani japo hakuna vurugu zozote zilizopata kutokea jimbo la Iringa mjini
..............Yataendelea hivi punde.......................

NIMETUMIA VIZURI HAKI YANGU YA KITATIBA YA KUCHAGUA KIONGOZI WANGU .....

Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin akitumbukiza karatasi ya kupigia kura ya Rais katika box maalum mara baada ya kukamilisha mchakato wa kuweka alama ya Vema na chama lengwa ,hapa ni kituo cha Ilala Sokoni mjini Iringa
Hapa nikipokea karatasi tatu za kupigia kura ya Rais,Diwani na mbunge mara baada ya kuhakikisha jina langu nje ya chumba cha kupigia kura

Napiga kura ya siri kumchagua kiongozi na chama nikipendacho kitakachoniongoza kwa kipindi cha miaka mitano ,kweli taratibu zote za mchakato huu zimezingatiwa hakuna zengwe
Kura ya diwani hapa box la mfuniko mweupe
Box lenye mfuniko mweusi ni diwani
Hapa ni rangi ya bluu sahihi kwa Rais

Kazi imemalizika na nimeweza kutumia vizuri haki yangu ya kidemokrasia ya kuchagua kiongozi nawekwa alama maalum ili nisirudie tena

UCHAGUZI MKUU TZ BIKIZEE WA MIAKA 120 ATINGA KUCHAGUA VIONGOZI IRINGA

Mpiga kura mwenye miaka 120 Adelphina kayombo akisubiri kusaidiwa kupiga kura katika kituo cha Kihesa chekechea mjini Iringa leo
Hapa akisaidiwa na mtoto wake wa mwisho (kushoto) Ade mgohamwende mtoto na mjukuu wake Esta Mahagama
Mtangazaji wa Redio Country Fm (88.5) Iringa ambayo inarushwa live mchakato huo Bw Zamoyon Ngede akipiga picha ya pamoja na bibikizee huyo
hapa akisaidiwa kuingia katika gari

'LIVE' ZOEZI LA UCHAGUZI MKUU TANZANIA,MUNGU TUNAOMBA UWE KATIKATI YETU ........

Wananchi wa kata ya Gangilonga katika Manispaa ya Iringa wakiwa wamejipanga katika vituo vya kupigia kura tayari kwa kuchagua viongozi wao kwa maana ya Rais,mbunge na diwani
Wananchi wakiwa wamejipanga katika kituo cha Radio Nuru Fm mjini Iringa wakisubiri kupiga kura leo
Mgambo akilinda kituo cha kupigia kura

Hapa ni soko kuu la Manispaa ya Iringa
Hapa ni kituo cha zima moto mjini Iringa

Mkurugenzi wa blog hii ya www.francisgodwin.blogspot.com na www.shwari.com tunapenda kuungana na wasomaji wetu kuutakia uchaguzi mwema wa Rais,wabunge na madiwani leo pia kila mmoja wetu atambue kuwa amani na sifa ya Taifa letu ipo mikononi mwake hivyo ni vema kuendelea kudumisha amani hii zaidi na tuepuke vurugu zisizo na heshima kwa taifa letu,
Mungu ubariki uchaguzi wa Tanzani,Mungu wabariki watanzania ,Mungu bariki amani yetu

KURA YAKO LEO KWA NANI KATI YA HAWA JIMBO LA IRINGA MJINI?

Mariam Mwakingwe (NCCR-Mageuzi) umoja ni nguvu nitashirikiana na wakazi wa Manispaa ya Iringa kuleta maendeleo zaidi
Monica Mbega (CCM) tuliahidi tumetekeleza tunaomba kura yako tena tuweze kufanya mengi zaidi
Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) ,Chadema imepania kutoa elimu bure tunaomba kura yako

MGOMBEA URAIS WA CUF AFUNGA KAMPENI KWA KISHINDO

Mgombea wa Urais kupitia chana cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwenye mkutano wake wa kampeni za lala salama mchana wa leo kabla ya kurejea Dar es Saalam kufanya mkutano wa mwisho wa kufunga kampeni za chama
hicho.

Staili ya kumaliza mkutano kwa mgombea wa urais kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba , kama alivyoonesha leo mjini Morogoro kwa kusema ' kwishaaa'..
Manjonjo ya mashabiki wa CUF Wilaya ya Morogoro Mjini , wakati wa ujio wao wa Mgombea Urais, Prof Ibrahim Lipumba

Viongozi wa wanawake wa CUF ngazi ya Wilaya ya Morogoro na Taifa wakimsikiliza mgombea urais, Profesa Ibrahimu Lipumba leo
Wanachama wa CUF Wilaya ya Morogoro mjini, wakiuza skafu za chama hicho kwa wanachama na wapenzi wa CUF Mjini Morogoro leo

KAMPENI ZA LALA SALAMA CHADEMA IRINGA MJNINI NA DK SLAA MBEYA...

wafuasi wa CHADEMA katika mkutano wa mwisho wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho Dk. Wilbroad Slaa huko Mbeya leo
Nyomi ya CHADEMA katika mkutano huo
Dk. Slaa akihutubia umati wa wafuasi wa CHADEMA
Dr. Slaa akiondoka eneo la mkutano baada ya kuhutubia huko mbeya leo

Hakuna kulala tuchape mwendo

FFU wakielekeza njia ya maandamano leo

Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (kulia) akiwapungia mikono wananchi

October 30, 2010

KAMPENI ZA FUNGA DIMBA..........

JK akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
JK akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
JK akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.

KAMPENI ZA FUNGA DIMBA..........

JK akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
JK akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
JK akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.