Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

September 30, 2010

SITAZIBWA MDOMO KWA VITISHO ,NIPO TAYARI KUFA KWA KUSEMA KWELI DAIMA........

Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin

UPO usemi kuwa ukitaka kazi ya jeshi usiogope kufa na siku zote mkweli hutengwa wa waongo kama hivyo ndivyo basi kwa mara ya kwanza leo kwanza ninapenda kuanza kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amepata kunileta duniani na kuniongoza kwa kila jambo na kunilinda na maadui wangu kwa kuwapa roho ya upendo na huruma mwingi.

Pia napenda kuwapongeza wanahabari wenzangu wote wa Tanzania ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kuipasha habari jamii ya kitanzania kulingana na uwezo wetu kweli nawapongeza wote bila kuwasahau wakurungezi wenzangu ambao tunamiliki vyombo vyetu yaani Blog na Website .

mimi Francis Godwin kama mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima napenda kutumia uwanja wangu huu wa kujidai kueleza masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari hii chini ya japo sijapokea simu ya wahusika wenyewe ila wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika .

Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitoogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache .


Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la leo na katika mtandao huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni Chadema japo si dhambi kuwa chadema wala chama chochote cha siasa kwa mtanzania ila ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na hapa nilipo ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa vijijini japo taaluma yangu haina chama ,dini wala kabila.

HII NI CHANZO
MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete jana ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.

Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.

Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.

Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano mkubwa ndani ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo
Amani Mkeremi kati ya viongozi wa UVCCM mkoa walioongozwa na katibu wao mkoa Rhoda George na wale wa vyama vya upinzani walioongozwa na katibu kata ya Kitwiru Baraka Kimata (Chadema) wakivutana juu ya CCM kuzuia wanafunzi kuendelea na masomo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.

Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 7 mchana lilipelekea mkuu wa shule kupata wakati mgumu kulitolea ufafanuzi huku walimu wake wakijifungia ofisini kukwepa vurugu iwapo vingejitokeza kati ya wafuasi hao.

Akielezea juu ya tukio hilo kiongozi wa vijana hao wa upinzani Kimata alisema kuwa walilazimika kuweka mtego katika shule hiyo baada ya kuona heka heka za makada wa CCM hazipungui shuleni hapo na wanafunzi wakirudishwa nyumbani kwa madai kuwa shuleni kuna ugeni wa kitaifa yaani mtoto wa Rais anatembelea shule hiyo.

"Kweli sheria ya tume ya uchaguzi inakataza taasisi za umma kuingia katika kampeni ....sasa tulipatwa na wakati mgumu kuona CCM inatumia shule ya msingi kufanya kampeni ndio sababu ya kuweka ulinzi ili kuhakikisha sheria haivunjwe ....tunashukuru tumefanikiwa baada ya viongozi hao wa CCM kumkimbiza mgeni wao mtoto wa Rais Kikwete" alisema kada huyo wa upinzani.

Hata hivyo alisema kuwa kabla ya msafara wa Ridhiwan kukimbizwa shuleni hapo kulikuwa kumetokea mvutano ndani ya ofisi ya mkuu wa shule huku akitaka watu wa CCM wabaki ndani na wale wa upinzani watoke nje kwanza ila baada ya kuonekana kuwa wale wa upinzani ndio walifika mapema CCM waliamua kutoka na kutoonekana kabisa eneo hilo.

Hata hivyo alisema kuwa wao wameelekeza tuhuma zao kwa mkuu wa shule hiyo ambaye amekuwa akionyesha ukada wake wazi wazi dhidi ya CCM hata kuruhusu shule hiyo kugeuzwa jukwaa la siasa kwa CCM.

Kwa upande wake mkuu huyo wa shule alikiri kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na kuwa taarifa ambazo CCM walikuwa wamefikisha shuleni hapo ni kuomba eneo la kufanya kikao na mgeni wao sio kufanya kampeni na kukusanya vijana kama ilivyokuwa.

Hata hivyo alisema kuwa hana barua yeyote ya CCM kuomba darasa na eneo hilo la shule kwa ajili ya kufanya kampeni
wala juu ya ugeni huo.

Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Rhoda ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa Kikwete katika shule hiyo alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi hakuweza kupokea zaidi ya kukata .

Hata hivyo mmoja kati ya makada waliopo katika msafara huo wa mtoto wa Kikwete alisema kuwa kikao hicho kilikuwa maalum kwa ajili ya kampeni za wagombea wa CCM kupitia vijana hao pia kuweza kumuunganisha Mbega na Mwakalebela kwa vijana hao ambao wameendelea kupinga CCM kumsimamisha Mbega .

Kada huyo alisema kuwa pamoja na kufukuzwa na vijana hao wa Chadema katika shule hiyo ya msingi pia uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha ulizuia majengo yake kutumiwa na CCM kwa kampeni hizo.

NINI KINAENDELEA CCM

MVUTANO wajitokeza sakata la msafara wa mtoto wa mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete kuzuiwa na vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) kufanya kampeni katika shule ya msingi Ipogolo kinyume na sheria za tume ya taifa ya Uchaguzi .

Mvutano huo umekuja siku moja baada ya mtoto huyo wa Kikwete ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Taifa Ridhiwan Kikwete na msafara wake kukwama kufanya kampeni katika shule hiyo pamoja na uongozi wa shule hiyo kupitia mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ipogolo Aman Mkeremi kueleza wazi kuwa UVCCM ngazi ya kata waliomba darasa moja katika shule hiyo kwa ajili ya kukutana na vijana kwa ajili ya mambo yao.

Ufafanuzi wa Mjumbe huyo mbele ya waandishi wa habari leo ofisi ya CCM Iringa mjini ni kuhusiana na tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wa habari hizi jana na wanahabari wengine ,unaonyesha wazi kuwa UVCCM imemgeuka mkuu huyu wa shule baada ya kudai kuwa hakuna aliyeomba kufanya kampeni katika shule hiyo zaidi ya msafara huo kusimama kwa muda shuleni hapo kwa ajili ya kuuliza eneo lilolokuwa limeandaliwa kwa ajili ya mkutano huo.

“ Ni ukweli sisi kati ya vikao vyetu tulikuwa na kikao chetu ndani ya kata ya Ruaha …tulifanya kama wenzetu walivyotuambia na kuelekea katika eneo la mkutano ila tulipofika eneo hilo ipo shule moja ya msingi na ndipo tulipokutana na wenzetu ndani ya kata ya ruaha wakiwa katika eneo hilo la shule huku wakiwa na wanafunzi wamevalia vizuri masweta ya kijana ishara ya chama chetu …na kama mnavyojua kuwa chame chetu sisi ndio wasimamizi wakubwa wa amani hivyo ingekuwa si busara kwetu sisi kama tungeshuka kwenda kufanya mkutano katika shule hiyo”alisema

Kuwa kutokana na hali hiyo yeye na viongozi wenzake walikaa ndani ya gari huku wale wa mkoa wakiongozwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa ndio walioshuka kwenda katika shule hiyo kuuliza na baada ya hapo waliondoka kwenda eneo la mkutano waliloelekeza .

Hata hivyo pamoja na mjumbe huyo kupinga kuandaliwa mkutano katika shule hiyo mkuu wa shule hiyo Mkeremi aliwaeleza viongozi wa Chadema na waandishi wa habari kuwa darasa moja ndilo ambalo liliombwa na vijana hao wa CCM kwa ajili ya kufanya kikao chao .

Wakati huo huo Ridhiwan Kikwete amesema njaa ya matumbo imeendeleza makundi yaliyotokana na kura za maoni katika jimbo la Iringa Mjini na kumpa wakati mgumu mgombea wao ubunge Monica Mbega ambaye ni mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo la Iringa mjini.


Alisema katika ziara yake hiyo jimbo hilo alichojifunza katika kampeni ni kwamba baadhi ya wanaCCM wanaendelea kulea na kushabikia makundi kwa faida ya matumbo yao.


“wanaCCM hao hawana budi kufahamu kwamba CCM kama chama kinatetea maisha ya watu na wala hakitakuwa tayari kutetea matumbo ya watu na ndio maana wameendelea kuwasihi wanaCCM wa aina hiyo waache tamaa na matarajio waliyokuwa nayo kutoka kwa wagombea ambao hawakupata nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho”


“Ndio maana tangu kampeni zianze viongozi mbalimbali wa kitaifa kwa kuijua hali hiyo wamekuja mjini hapa na kufanya vikao na wanaCCM ili kuwasihi watangulize maslai ya chama kwanza na watu baadaye kama kauli mbiu yetu ya kukijenga chama inavyosema chama kwanza mtu baadaye,” alisema.


Nimelazmika kuambatanisha na habari hizo ili kutoa nafasi kwa yeyote anayelalamika kuchukua hatua za kisheria badala ya kunitishia kifo ,ambacho kimsingi hupangwa na Mungu pekee.

Napenda ifahamike hakuna hata mmoja wetu anayetambua siku zake za kuishi hapa duniani zaidi ya Mungu pekee hivyo sioni sababu ya mimi kuogopa kifo wala adhabu ya aina yeyote dhidi yangu .

Mungu ubariki uchaguzi mkuu wa Tanzania umalizike kwa amani na utulivu Amina

BALOZI PETER KALLAGHE KUNENE


Habari Godwin
Kaka naomba utuwekee hili tangangazo la Mh. Balozi kuzungumza na Watanzania wa Birmingham na vitongoji vya siku ya jumamosi 02/10/2010 kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11. address ipo kwenye hiyo flyer nimekutumia.
Naomba uwasisitize Wabongo watakuwa wanakuja kuzingatia sana muda.

Asante kwa kazi yako njema kaka.

Jackson M
Katibu TA-Birmingham / Mjumbe TA-Taifa

MGOMBEA URAIS WA CCM DR. KIKWETE AITEKA URAMBO

JK akihutubia mkutano wa kampeni Uyowa Wilayani Urambo leo
Wananchi wa Uyowa wakiwa na nyuso za furaha wakati wakifuatilia hotuba ya JK kwenye mkutano wa kampeni leo
Umati mkubwa wa watu wakimshangilia JK wakati akiingia Uyowa, Ulyankulu Wilayani Urambo leo.
umati mkubwa wa watu wa Uwoya,wilayani Urambo ukimsikiliza JK wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni leo.

TUSHIRIKIANE KUSAFIRISHA MWILI WA MPENDWWA WETU SALUKELE


Mr. Matthew Salukele (Marehemu)Date of Birth: 22/02/1941 - Died: 09/28/2010 @ 4:30 pm at St Ann’s Hospital Columbus Ohio.

Happyness na David Salukele wanasikitika kuwataarifu habari ya msiba wa mpendwa baba yao,Mzee Matthew Salukele uliotokea jumanne Sept 28,2010 saa 10 unusu(4:30pm),St Ann's Hospital,Columbus Ohio.

Tunaomba msaada wenu katika kukamilisha kusafirisha mwili wa marehemu Tanzania,Gharama za kuusafirisha mwili zinafikia $25,000.
Unaweza kusaidia kupitia Chase Bank Acc #917118267 Routing # 044000037.

Msiba upo Add:
1427 hideaway Woods Dr
Westerville OH 43081


Tunatanguliza Shukrani kwa msaada wako wa hali na mali utakaotoa hasa kwa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa Baba yetu.

Baba Tulikupenda Sana lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,kimwili hatuko pamoja,kiroho tutakua nawe siku zote mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena,
Jina lake lihimidiwe.

For more information Please contact:
David Salukele cell# 614-859-9602
Walter kalosi cell#614-537-1448
Happiness Salukele cell#614-772-5126
Adella Njau cell#614-446-9710
Dorah Njau cell#614-589-5685
Jacqueline Mjengwa Cell# 614-804-5237

Uongozi wa mtandao huu na ule wa www.shwari .com unayoheshima kubwa kukuomba wewe mdau kuungana na familia hii katika kipindi hiki kigumu kwa kusaidia kuchangia gharama za mazishi hata kusafirisha mwili wa marehemu na Mungu atakuzidishia daima

KESI YA MUNGAI YASOGEZWA MBELE

Aliyekuwa waziri wa serikali zote nne za jamhuri ya muungano wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazin (mstaafu) Bw Joseph James Mungai ( kulia) akitoka katika jengo la mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa leo baada ya kesi yake inayomkabili ya tuhuma za rushwa katika kura za maoni CCM kusogezwa mbele hadi Octoba 15 mwaka huu
Bw Moses Masasi (mbele) ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa wawili waliounganishwa na Mungai akitoka mahakamani hapo asubuhi ya leo
Bw Mungai na ndugu na jamaa zake wakitoka mahakamani hapo


KESI ya rushwa katika kura za maoni ndani ya CCM inayomkabili aliyekuwa waziri wa serikali zote nne na Mbunge wa Mufindi Kaskazini Joseph Mungai (66) na wapambe wake wawili imesogezwa mbele hadi Octoba 15 mwaka huu .

Mungai ambaye jana amejaza umati mkubwa mahakamani hapo wakiwemo waliokuwa wapiga kura wake wa jimbo la mufindi kaskazini na baadhi ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini alifika mahakamani hapo kwa msafara mkubwa wa magari ambayo yalifika kumsindikiza pamoja na kusikiliza kesi hiyo ambayo ilipaswa kuwekewa pingamizi na mawakili wake wawili akiwemo Basil Mkwata na Alex Mgongolwa.

Mbali ya Mungai wapambe wake wawili akiwemo Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM wa Wilaya ya Mufindi, Fidel Cholela (39) na Moses Masasi pia wameunganishwa katika mashtaka hayo 15 ya rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupamna na rushwa ya mwaka 2007 na sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 .

Watuhumiwa hao kwa pamoja, kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Agosti 11, mwaka huu na kusomewa mashitaka hayo ambayo pia waliyakana jana walionekana ni watu wasio na wasiwasi ukilinganisha na siku za nyuma ambapo walikuwa na hofu kubwa.

Hata hivyo kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa, Marry Senapee jana hakuwepo mahakamani hapo na badala yake hakimu Gladies Bath aliweza kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana na mhusika kutokuwepo kutokana na sababu za kiafya.

Mwendesha mashtaka wa Takukuru Mitume Mizizi aliiomba mahakama hiyo kupanga siku nyingine ya kuanza kusikiliza pingamizi hilo kutokana na hakimu husika kutokuwepo ombi lililokubaliwa na hakimu huyo.Awali Mungai na wenzake hao walipandishwa kwa mara ya pili mahakamani hapo Augosti 25 mwaka huu ambapo Wakili anayewatetea washitakiwa hao, Basil Mkwatta aliomba tarehe itakayopangwa na mahakama hiyo am,bayo ni jana alete pingimizi la awali la kisheria ( PO ) kwamba kesi hiyo haistahili kuwepo mahakamani hapo.

Pande zote mbili zilikubaliana ambapo Hakimu Senapee alipanga kesi hiyo irejeshwe mahakamani hapo Septemba 30 mwaka huu ambapo Mkwatta ataleta pingamizi hilo na hivyo kumfanya mwendesha mashitaka wa Takukuru,asisome maelezo ya awali siku hiyo na badala yake atalazimika kusubiri kusikia pingamizi hilo na kutoa hoja za kujibu.

Kwa mujibu wa Takukuru Mungai na wenzake hao wanadaiwa kutoa rushwa hiyo Julai 08, mwaka huu, katika kata ya Ihalimba, Wilaya ya Mufindi, Mungai akiwa mmoja wa makada wa CCM waliokuwa wanawania kupitishwa katika kura za maoni kugombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, kwa pamoja na watuhumiwa wenzake, walitoa hongo ya Sh.10,000 kwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Vikula kama kishawishi cha kumpigia kura wakati wa zoezi la upigaji wa kura za maoni.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja, siku na katika eneo hilo walitoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Konjesta Kiyeyeu ambaye alihudhuria kikao cha kamati ya CCM Kijiji cha Vikula.

Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa, katika shtaka la tatu, nne, tano na sita, watuhumiwa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Aldo Lugusi, Ezekiel Mhewa, Tulaigwa Kisinda na Jiston Mhagama kwa lengo hilo hilo la kuwashawishi wampigie kura za maoni.

Katika shitaka la saba,watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Maria Kihongosi na shtaka la nane kutoa hongo ya Sh.5,000/- kwa Lurent Mdalingwa wakati shtaka la tisa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Victory Kalinga ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Ugessa.

Katika mashtaka namba kumi hadi 12 washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa walitoa hongo ya Sh.2,000/- kwa Francis Chonya, Alfred Kisinga na Issac Tewele wakati shtaka la 13 wanadaiwa walitoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Sosten Kigahe.

Aidha, Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa shitaka namba 14 watuhumiwa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Raphael Lutumo na shitaka la mwisho walitoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Andrew Mkiwa.

MIKUTANO YA JK YAZIDI KUTIKISA TABORA,MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA

Umati ukimsikiliza JK mjini Bukene wakati wa
mwanzo wa ziara yake ya kampeni mkoani TaboraJK akiingia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora


Sehemu ya umati wa mjini Tabora JK akihutubia Tabora
JK akimnadi mgombea ubunge Tabora Mjini Alhaj Ismail Aden Rage
Zaidi ingia hapa

MIKUTANO YA JK YAZIDI KUTIKISA TABORA,MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA

Umati ukimsikiliza JK mjini Bukene wakati wa
mwanzo wa ziara yake ya kampeni mkoani TaboraJK akiingia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora


Sehemu ya umati wa mjini Tabora JK akihutubia Tabora
JK akimnadi mgombea ubunge Tabora Mjini Alhaj Ismail Aden Rage

OFISI YA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA IRINGA MJINI YAHUJUMU PICHA ZA MGOMBEA URAIS WA CCM DR.JAKAYA KIKWETE

Wakati chama cha mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani kikiwemo chama cha Demokrasia na maendeleo -Chadema kuchaniwa mabango ya kampeni ya wagombea wa nafasi mbali mbali ikiwemo ile ya urais ,wananchi mjini Iringa wameilalamikia ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kwa kubandika matangazo yake juu ya picha za Kikwete kinyume na taratibu na kuwa yawezekana ofisi yake imekuwa ikihusika na zoezi la uchanaji wa picha hizo katika kuta za bustani ya Manispaa ya Iringa
Hili ni tangazo lililobandikwa juu ya picha ya Kikwete

ALIYEKUWA WAZIRI WA TANZANIA JOSEPH MUNGAI KESHO KUPANDISHWA TENA KIZIMBANI

Aliyekuwa mbunge wa Mufindi kaskazin na waziri wa serikali zote nne Bw Joseph James Mungai (kushoto)na wapambe wake wawili akiwemo Moses na Fidelis ambaye ni katibu wa UVCCM kata ya Mafinga kesho Septemba 30 wanafikishwa tena mahakamani kwa mashtaka 15 ya tuhuma za rushwa katika kura za maoni ndani ya CCM.

KADA WA CCM MZEE FRAISER EMMANUEL MSAFIRI AMEFARIKI DUNIA

Kada wa CCM ,Marehemu Fraiser Emmanuel Msafiri
Ndugu na viongozi wa dini wakiwa wamezunguka kaburi la babu yake mtangazaji wa redio Wapo FM Ritta Chiwalo ( Kulia)leo baada ya mazishi ya babu yake mzee Msafiri

Mtangazaji wa Redio wapo Fm Bi.Ritta Chiwalo (katikati) akiwa na ndugu zake katika mazishi ya babu yake mzee Msafiri

KIFO cha kada huyu mzee Fraiser Emmanuel Msafiri chaacha pengo kubwa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) hasa kwa kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu na kufanya kifo chake kuwa ni pigo kubwa kwa familia yake na Taifa kwa ujumla kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa hili

Mzee Msafiri alizaliwa mwaka 1932 katika kijiji cha Lithui Manda alisoma mpaka darasa la nane kwa wakati huo na amefanya kazi katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara.

Akisoma historia ya marehemu Msafiri makaburini hapo ofisa mtendaji wa kata ya Kwakilosa mjini Iringa Bw.Forward Mwasiposia kwa niaba ya ndugu alisema kuwa mwaka 1959 -1962 alikuwa ni katibu wa (W) Transport &General workers Union .

Mwaka 1962-1964 alikuwa katibu wa wilaya wa NUTA (Lindi),mwaka 1964-1968 katibu wa wilaya NUTA (Masasi) na mwaka 1969-1971 katibu wa NUTA wilaya ya (Mbeya).

Pia marehemu Msafiri enzi wa uhai wake amepata kufanya kazi ya ukatibu wa NUTA mkoa wa Tabora mwaka 1971-1972 katibu wa JUWATA mkoa wa Iringa na mwaka 1985-1990 katibu wa OUT mkoa wa Lindi na kuwa katika mikoa yote hiyo amepata kufanya kazi kama katibu wa mkoa wa vyama vya wafanyakazi .

Aidha amepata kupata kozi kwa maana ya kuongeza kiwango cha elimu yake kwa ngazi ya uongozi katika nchi za ujerumani na Urusi na baada ya kustaafu kulitumikia Taifa katika nafasi zake hizo bado aliendelea kuwa na shauku ya kuwatumikia wananchi wa mkoa wake wa Iringa kwa kupitia CCM katika nafasi mbali mbali ndani ya kata yake ya kwakilosa.

Kicho chake kimetokana na ugonjwa wa miguu uliokuwa ukimsumbua tangu mwaka 2006 na hadi kufikia septemba mwaka huu ndipo alipozidiwa na kuishiwa nguvu na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kabla ya kufariki kwake septemba 28 majira ya saa 12 asubuhi .

soma makala hii katika gazeti la Msemakweli jumapili ijayo ya tarehe mosi mwezi wa 10

September 29, 2010

DUA ZETU WATANZANIA KWAKO MISS TANZANIAMkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi kinyago Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu,Mlimbwende huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China ambako mashindano hayo yatafanyika.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimvisha skafu yenye bendera ya Taifa Miss Tanzania 2010,Geneviev Emmanuel katika hafla fupi iliyofanyika leo katika viwanja vya kituo cha uwekezaji nchini (TIC).mrembo huyu anataraji kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China kwenye mashindano ya Dunia.
Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel akiwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa Sekta Binafsi nchini,Ester Mkwizu (pili kushoto) na baba yake mzazi, Emmanuel Mpangala pamoja na Mama wakiwa katika picha ya pamoja katika halfa hiyo ya kumuaga mrembo huyo iliyofanyika leo jijini Dar.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkabidhi bendera Miss Tanzania 2010 kwenye viwanja vya TIC mapema leo asubuhi jijini DarMwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkabidhi bendera Miss Tanzania 2010 kwenye viwanja vya TIC leo jijini Dar
mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania,Martina Nkurlu (katikati) akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo fupi ya kukabidhiwa bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel.
Baadhi ya wanahabari na wadau wengine wakifuatilia kwa makini shughuli hiyo ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel iliyofanyika leo katika viwanja vya kituo cha uwekezaji nchini (TIC).

BREAKINGNEW, RIDHIWAN KIKWETE AVAMIWA NA VIJANA WA CHADEMA ASHINDWA KUFANYA KAMPENI ....

Msafara wa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete Bw Ridhiwan Kikwete ukiondoka katika shule ya msingi Ipogolo baada ya kikao chao cha vijana shule hapo kushindikana leo

Mkuu wa shule ya msingi Ipogolo Aman Mkeremi akiomba msamaha kwa wafuasi wa Chadema kwa hatua yake ya kuruhusu CCM kufanya kampeni shuleni Darasalililoandaliwa kwa ajili ya kampeni za CCM hili hapa
Mwanafunzi wa shule ya msingi Ipogolo akiwa nje ya ofisi baada ya walimu kujifungia ndani
Na Francis Godwin,I

MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete leo ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.

Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.

Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.

Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.

Habari kamili utaipata hivi punde

IRINGA YETU YAZIDI KUPENDEZA

Kazi hii ya kukokota mikokoteni haina umri
Huu ni mji waIringa unavyoonekana ukiwa juu ya majengo ya ghorofa
Kijana mkazi wa mji wa Iringa akiwa amebeba baiskeli cxhakavu kwa ajili ya kwenda kuziuzatena

NONINI & MATONYA ' LIVE' IN LONDON•★•★•★BONGOUK PRESENT EAST AFRICAN SHOW DOWN 2010•★•★★•
@ TEREZA JOANNE BOAT
KING GEORGE V DOCK E16 2QY
London, United Kingdom

•★•★•★•BONGOUK ENTERTAINMENT ARE TAKING ENTERTAINMENT TO NEW HEIGHTS WITH THE VERY BEST ENTERTAINERS, THE GODFATHER OF GENGE NONINI AND THE BONGO FLAVA KING MATONYA★•★•★•★

★•★•★•★ PERFORMING LIVE ON THE SAME STAGE FOR THE FIRST TIME EVER IN THE UK "THE EAST AFRICAN SHOW DOWN"★•★•★•★

***********************************************

•★•★•NONINI WILL PUT THIS PARTY ON FIRE BY PERFORMING HIS HITS LIKE NEVER B4...........

★•★•★•★GENGE LOVE, KADHAA, MANZI WA NAIROBI, FURAHIDAY ETC..

***********************************************

★•★•MATONYA WILL BE PERFORMING HIS HITS LIKE

★•★•★•★ANITA, VAILET, TAXI BUBU, SPAIR TIRE, SIAMINI ETC

EARLY BIRD TICKET AVAILABLE FOR ONLY £10

£15@THE DOOR B4 MIDNITE / MORE AFT

▀▀▀▀▀

►FROM 9PM TILL 4AM

MTOTO WA JK AWAUNGANISHA MBEGA NA MWAKALEBELA ,WAANDISHI WAFUKUZWA KUSHUHUDIA


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete (katikati), akiwatambulisha Monica Mbega (kulia) na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela
alienguliwa kuwania nafasi hiyo. Picha na Richard Mwaikenda.

Hata hivyo katika kikao hicho cha mjumbe huyo wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa sekondari ya Mwembetogwa ,katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Rhoda George alitimuwa waandishi wahabari wa vyombo visivyoegemea na kusifia kila jambo na kuachwa chombo kimoja pekee cha utangazaji ndani ya mkoa wa Iringa ambacho kimekuwa mbele kufagilia CCM kwa nguvu zote .

Katibu huyo ambaye kabla ya kumtumia mwanahabari huyo huku wengine wakiwa nje alimfuata katibu wa CCM mkoa Bi Mary Tesha na kumng'ata sikio na baada ya hapo alimfuata mwandishi huyo nakumweleza kuwa sahamani shughuli zetu hazihitaji wapiga picha wala waandishi wahabari tunaomba utoke nje huku mwandishi huyo wa kituo cha radio na mwingine ambaye ni mpiga picha akiachwa ndani ya ukumbi huo.


September 28, 2010

BREAKING NEWS VYAMA 14 IRINGA VYAUNGANISHA NGUVU KUIBANA CCM NA CHADEMA

Mgombea wa umoja wa vyama 14 za upinzani jimbo la Iringa mjini Mariam Mwakingwe
Hizi ni baadhi ya Bendera za vyama hivyo vilivyoungana jimbo la Iringa mjini isipo kuwa Chadema
Mgombea urais wa APPT-Maendeleo Bw.Peter Mziray (kulia) akimnadi mgombea wa muungano wa vyama 14 jimbo la Iringa mjini Bi.Mariam Mwakingwe

Barua ya umoja wa vyama vya upinzani vilivyoungana jimbo la Iringa mjini
Monica Mbega (CCM)
Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
Aliyekuwa mgombea ubunge wa chama cha wananchi (CUF) Zaitun Mwaibula amejiunga na umoja wa vyama 13 za upinzani jimbo la Iringa mjini na kuongeza nguvu ya upinzani katika jimbo hilo hivyo kufanya jimbo hilo hadi sasa kubaki wa wagombea watatu wa nafasi za ubunge .

Wagombea wanaogombea katika jimbo hilo ni Monica Mbega (CCM) ,Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na yule wa muungano wa vyama vya upinzani Mariam Mwakingwe (NCCR- Maguzi)

Vyama vinavyo muunga mkono Mwakingwe ni NCCR- MAGEUZI ,TLP, TADEA, SAU, CHAUSTA, APPT-MAENDELEO, JAHAZI ASILIA , CUF, NLD, UDP, MAKINI,DP, AFP NA UPDP.

Awali mgombea huyo wa CUF pamoja na kujaza fomu ya kuwania ubunge aliwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa Chadema mchungaji Msigwa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya udhamini katika fomu yake.