Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 31, 2010

MAUWAJI WA KINYAMA IRINGA,MWANAMKE AUWAWA ATOLEWA NYETI ZAKE ,MWINGINE ANYONGWA KAMA KUKU...WATU wawili wauwawa kinyama Mkoani iringa akiwemo mwanamke mmoja makazi wa kijiji cha Idunda wilaya ya Njombe Christina Mayala (50) aliyeuwawa na kunyofolewa sehemu zake za siri .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla ameueleza mtandao huu kuwa matukio hayo yametokea juzi majira 1 asubuhi na tukio la pili lilitokea katika kijiji cha Tanangozi majira ya saa 12 jioni.

Akielezea tukio la mwanamke huyo mkazi wa Idunda Mangalla alisema kuwa watu wasiofahamika walimuua mwanamke huyo kinyama kwa kumpiga na kitu kinachosadikika ni butu kichwani na baadaye kutoa sehemu zake za siri na mwili wake kuutupa kandokando ya barabara ya kijiji hicho.

Hata hivyo alisema kuwa watu hao ambao idadi yao haijafahamika kabla ya kumnyofoa sehemu za siri mwanamke huyo walimpiga katika maeneo mbali mbali ya mwili wake kwa kutumia kitu hicho kinachosadikika kuwa ni butu .

Akielezea tukio la pili kamanda huyo alisema kuwa alisema kuwa mkazi wa kijiji cha Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini Kasim Dinga (58) aliuwawa kwa kunyongwa shingo yake mithiri ya kuku na watu watatu wakazi kijiji hicho ambao wanasadikika kuwa ni ndugu na kisha mwili wake kuutumbukiza katika dimbwi la maji .


Pasipo kutaja chanzo cha watu hao kuchukua uamuzi huo wa kufanya mauwaji ya kinyama kamanda Mangalla aliwataja watu hao kuwa ni Magnus Kikula (47) , Shaibu Kikula(42) George Msemwa (53) ambao tayari wamekamatwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kuhusika na mauwaji hayo .

Kamanda Mangalla alisema kuwa jeshi la polisi mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha watuhumiwa hao katika vyombo vya sheria ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwasaka watu wanatuhumiwa kufanya mauwaji ya kinyama katika kijiji cha Idunda wilaya ya Njombe.

MAMA WA KAMBO AFANYA UNYAMA WA KUTISHA AMCHOMA VISU MTOTO WA MWENZAKE


Habari iliyotua hivi punde katika mtandao huu kutoka Makorongoni Iringa inaeleza unyama wa kutisha uliofanywa na mwanamke mmoja kwa mwanaye wa kambo ,kisa na jina kamili na picha zaidi utazipata hivi punde

KAMA MJINI JENEZA LINABEBWA KATIKA PIKIPIKI ,VIJIJINI ITAKUWAJE?


Mapanda pikipiki ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akikatisha mitaa ya mji wa Iringa huku akiwa amebeba jeneza katika pikipiki yake kwa ajili ya kwenda kulitumia katika shughuli za mazishi baada ya kutoka kununua japo haikufahamika mara moja kama ndani ya jeneza hilo kulikuwa na nini ,ila swali tu hapa iwapo mjini jeneza linabebwa hivi vijijini kwenye shida ya usafiri itakuwaje?

August 30, 2010

BREAKINGNEWzzzz CHADEMA WAMWEKEA KIZUIZI MGOMBEA URAIS WA CCM DR.JAKAYAKIKWETE


Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha rasmi pingamizi dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete kwa madai ya kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi (iliyosainiwa na Kikwete kama Rais).
Kwa mujibu wa habari zilizotua katika mtandao huu hivi punde zinadai kuwa Kikwete ameongeza mishahara ya watumishi wa umma kinyume cha taratibu, na inatafsiriwa kuwa ni rushwa,habari hii na pingamizi hili litakujia wakati wowote katika mtandao wa www.shwari.com

CHADEMA IRINGA KUMTUMIA MWAKALEBELA KUENDELEZA SOKA


MGOMBEA ubunge kutipia chama cha Demokrasia (chadema) jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ametuliza hasira wana CCM wa jimbo hilo na kuwaomba wawe watulivu na kujitokeza kuchagua Chadema huku akiwahakikishia kuwa iwapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anamrudishia heshima yake na kumtumia vizuri aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela (pichani)kuendeleza michezo jimboni.

Huku akidai kuwa iwapo chadema itashinda ubunge jimbo hilo kazi ya kwanza na kuurudisha uwanja wa michezo wa Samora uliopo chini ya CCM kwa wananchi na maghala yaliyojengwa katika uwanja huo kwa kumtumia mtaalam wa michezo Mwakalebela yanavunjwa ndani ya siku tatu.

"Kati ya viongozi ambao nawakubali katika Taifa hili kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania katika sekta ya michezo ni pamoja na Mwakalebela ...kwani amefanya mambo mengi sana katika Taifa hili na kuja kwake kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini ni uzalendo tu wa kutaka kuwasaidia wananchi wake kuleta maendeleo na sio vinginevyo ....lakini kazi zote na mambo aliyoyafanya Mwakalebela kwa CCM ni sawa na shukrani ya punda wameishia kumdhalilisha yeye na mkewe kwa kumchomekea kwa Takukuru .....sasa Chadema tunasema wana Iringa msiendelee kulia sana na ukatili aliyofanyiwa Mwakalebela jipangeni vizuri ili kuhakikisha octoba 31 Chadema inashinda ili Mwakalebela aweze kurudishiwa heshima yake ndani ya Manispaa ya Iringa kwa kuendeleza michezo"alisema Msigwa huku wananchi wakipasa sauti kuwa CCM Iringa imefika mwisho wake.

BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz,OFISI YA UMMA DODOMA YATEKETEA KWA MOTO


Habari ziliziufikia mtandao huu hivi punde kutoka mjini Dodoma zinadai kuwa ofisi ya serikali katika jengo la mkuu wa mkoa wa Dodoma zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.habari kamili na picha za tukio hilo utapata hivi punde ,endelea kufaidika na mtandao huu

CHADEMA ILIVYOUNGANA NA WAKAZI WA JIMBO LA IRINGA MJINI KUMLILIA MSHINDI WA KURA ZA MAONI CCM FREDERICK MWAKALEBELA,WENGI WAREJESHA KADI

Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akionyesha kadi ambavyo vilirudishwa katika mkutano huo na wana CCM waliopinga kuenguliwa kwa Frederick Mwakalebela ,Picha zaidi ingia hapa

August 29, 2010

RUVUMA WAKUTANA KUTAZAMA MIIKO YA VYOMBO VYA HABARI DHIDI YA KURIPOTI UCHAGUZI MKUU

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt Christine Ishengoma (Kushoto) akimshika mkono Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma, Juma Nyumayo ikiwa ishara ya kuwashukuru waandishi wa habari wa mkoa huo jana kwa kazi nzuri ya kuhabarisha umma na kuutangaza mkoa licha yakuwa pemebezoni mwa nchi.,Picha juu kabisa ni waandishi wa habari na inayofuata ni RC Ruvuma na mwenyekiti wa Ruvuma Press akipongezwa
,picha chini ni Mwenyekiti wa kamati ya Maadili na Mafunzo wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Mikoani (UTPC), Juma Nyumayo (Kulia) akitoa mada kwa wadau wa habari vyama vya siasa, taasisi za serikali na waandishi wa habari mkoani Ruvuma katika kikao cha siku moja juu ya maadili ya vyombo vya habari katika kuripoti uchaguzi mkuu Oktoba 31, mwaka huu, (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo Dkt Christine Ishengoma.(picha kwa hisani ya Ruvuma Press Club)

'LIVE' OCD IRINGA AOMBWA RADHI MBELE YA WANANCHI


mgombea udiwani wa kata ya Makorogoni David Kombo akijinadi baada ya kutambulishwa na mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa.Chadema pia waomba radhi jeshi la polisi kwa yaliyoyotokea wakati wa ziara ya Dr Slaa Iringa kuwa aliyechanganya mambo ni Beny Kapwani.

MGOMBE URAIS WA CCM DR. JK AITEKA SUMBAWANGA LEO
Mgombea urais wa CCM Dr Jakaya Kikwete alivyotikisa Sumbawanga leo wakati wa mkutano wa kampeni za Urais .picha zaidi zinakuja pia waweza kuingia hapa

'LIVE' NYAGAWA AMTAKA MGOMBEA UBUNGE CCM AKASOME MEMKWA,MGUNGAJI MSIGWA AMLILIA MWAKALEBELA AWAPONDA CCM KUWAITA ORIJINO KOMEDY IRINGA

Mchugaji Peter Msigwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjiniAlatanga Nyagawa
UZINDUZI wa kampeni za uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mkoa wa Iringa waiweka pabaya CCM baada ya chadema kutumia mkutano huo kumlilia aliyekuwa mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela huku wananchi wakipaza sauti kuwa hawadanganyiki na orijino komedy na ujio wa John Malecela Iringa.

Asema kuwa Mchungaji Peter Msigwa ( jimbo la Iringa mjini),Thomas Nyimbo(Njombe Magharibi) na yeye Alatanga Nyagawa ( Njombe Kaskazin) wao tayari ni wabunge wa chadema mkoa wa Iringa ambao hawana upinzani na kuwa wana Iringa wasikubali kushiriki mikutano ya kampeni ya CCM ambayo wanahonga rushwa ili kulazimisha ushindi usio wao katika jimbo hilo la Iringa mjini na majimbo mengine ambayo wamebanwa na chadema.

Hata hivyo Nyagawa alisema kuwa iwapo ataapishwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo la Njombe kaskazin atahakikisha afisa elimu wa wilaya ya Njombe anamsimamia mgombea ubunge wa CCM jimbo Njombe kaskazin mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Deo Sanga anaendelea na elimu ya MEMKWA baada ya kuwa na elimu ya darasa la saba ambayo amedai kuwa si elimu ya kuwatumikia wananchi katika ulimwengu wa sasa.

Kwa upande wake Msigwa alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amemkubali sana Mwakalebela kutokana na kuwa kijana msomi na muelewa mzuri ndani ya Taifa.

"Mimi kweli natoa pole kwa familia ya Mwakalebela kwa kudhalilishwa vibaya na serikali ya CCM kwa kupelekwa hamakamani yeye na mkewe kwa tuhuma za rushwa ya shilingi 100,000 wakati wagombea wengine akiwemo mgombea ubunge wa jimbo hilo na wengine wamtoa rushwa kubwa zaidi ya hiyo..kweli CCM inarudisha nyuma demokrasia kwa kuwalazimisha watanzania na wana Iringa kumchagua Mbega asiyekubalika mbele ya wana Iringa"alisema Mchungaji Msigwa huku umati wote uwanjani hapo ukipasa sauti ya kuafiki kauli hiyo.

Huku mjumbe wa halmashauri kuu ya Chadema taifa Chiku Abwao akimwomba radhi mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kutokana na kumjibu vibaya wakati wa ziara ya mgombea urais wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa na kuwa aliyesababisha amjibu vibaya kiongozi huyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Iringa Beny kapwani ambaye amesimamishwa kwa kukihujumu chama hicho .

Wakati mgombea udiwani kata ya Makorogoni David Kombo akijitangazia kuwa tayari ni diwani wa kata hiyo na kuwa atahakikisha anafanya kampeni chumba kwa chumba,kitanda kwa kitanda ili kuhakikisha kuwa CCM haiibi kura kwa wananchi wa kata ya Makorongoni ambao wanahitaji mabadiliko.

Zaidi habari hii utaisoma katika gazeti la Tanzania Daima kesho

"LIVE' UWANJA WA MKUTANO WA CHADEMA WAFURIKA MAELFU YA WAKAZI WA MJI WA IRINGAUwanja wa mwembetogwa katika uzinduzi wa kampeni za Chadema mkoa

hautoshi,aliyejiengua CCM Alatanga Nyagawa naye atua mkutanoni sasa ndani ya dakika chache atapanda Nyagawa kumnadi Msigwa

KADA WA CCM AIBOMOA CCM JUKWAANI'LIVE"Aliyekuwa kada wa CCM na diwani wa CCM kata ya Miyomboni Grevas Kalolo na mgombea ubunge kata ya KwakilosaAbuu Changawa wakipasua chama cha Mapinduzi (CCM) wasema CCM mbila Orijino Comedy haiweze kusonga mbele.

Pia wamtuhumu vibaya mgombea ubunge wa CCM jimbo la Iringa mjini kuwa amekuwa akihonga wenyeviti wa mitaa usiku ,

Huku mjumbe wa halmashauri kuu cha Chadema Taifa Chiku Abwao akiwataka wakazi wa jimbo la Iringa kuendelea kuhukua rushwa kutoka CCM ila kura zote zitue hadema.

Abwao amewataka watanzania kutokubali kudanganyika na porojo za CCM na badala yake kujitokeza kuleta mabadiliko ya kweli kwa kuhagua Chadema na sio chama kingine nje ya chadema.

Pia aeleza sababu ya Chadema kutojiunga na muungano ulianzishwa Manispaa ya Iringa kuwa umelenga kukibomoa chadema na kukipigia debe chama cha mapinduzi (CCM) asema kamwe hawatajiunga na muungano huo wa kinafiki.mkutano unaendelea katika viwanja vya Mwembetogwa sasa Nyimbo la Alatanga bado kuingia.

'LIVE'MAANDAMANO YA CHADEMA IRINGA YATETEMESHA MJI


Mgombea ubunge wa Chadema Iringa mjini Mchungaji Peter Msingwa akiingia uwanja wa Mwembetogwa kwa mbwembwe
Maandamano ya Chadema katika Manispaa ya Iringa yameonyesha kuutikisa mji wa Iringa .


Hivi sasa mkutano wa uzinduzi wa mkutano unaendelea huku umati mkutwa wa wannachi ukiwa umefurika katika uwanja wa mwembetogwa tofauti na jana ambapo CCM ilitumia kundi la Orijino Komedy kuvuta wananchi kuja katika mkutano huu.


NIPO "LIVE' SHEREHE ZA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CHADEMA MKOA WA IRINGA


Mpendwa mdau wa mtandao huu na mitandao mingine inayomilikiwa na mtandao huu ninapenda kukukaribisha tena leo kufuatilia sherehe za uzinduzi wa kampeni za chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Iringa ambao leo wanazindua rasmi kampeni zao katika uwanja wa Mwembetogwa ,

Kumbuka maandamano yataanza katika ofisi za Chadema eneo la Mshindo mjini Iringa majira ya saa 6 mchana na kuzunguka katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kuingia katika viwanja vya mwembetogwa kwa kuwahutubia wananchi majira ya saa 8 mchana ,mtandao huu utakuwezesha kupata matukio yote Live pia kumbuka kutembelea www.shwari.com

HIVI NDIVYO UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM IRINGA ULIVYOFANA.....(1)Mwanzo wa maandamano ya CCM mkoa wa Iringa ndani ya uwanja wa Samora

(2)Kada wa CCM Daud Yassin akiwa katika gari yake viwanja vya samoro

(3)mteule wa nafasi ya ubunge jimbo la Mufindi kusini Mhe. Medrady Kigola akiwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Macelina Mkini

(4)Wanafunzi wa shule wa shule ya Sekondari Mwembetogwa wakiwa wamevalia kofia cha mgombea urais wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maandamano ya uzinduzi wa kampeni za CCM mkoa wa Iringa,PICHA ZAIDI HAPA

August 28, 2010

'LIVE" ORIJINO KOMEDI WASHAMBULIA JUKWAA LA CCM IRINGA,PIA WAMNADI MBEGA WADAI WAO WOTE NI CCM DAMU
wachekeshaji wa Orijino Komedy wakiwajibika katika jukwaa la uzinduzi wa CCM mkoa wa Iringa ,kwenye viwanja vya mwembetogwa ,mtambulishaji wa kundi hilo Masanja amesema kuwa kundi hilo limeamua kuja kuanza kampeni Iringa baada ya kuwa robo tatu ya kundi hilo kutoka ndani ya mkoa wa IringaWakazi wa mji wa Iringa wakiwashangaa Orijino Komedy ambao wapo jukwaani wakiwasha moto katika uzinduzi wa kampeni za CCM kimkoa katika jimbo la Iringa mjini viwanja vya mwembetogwa sasa,kumbuka uzinduzi huu unaletwa kwako la Maziwa ya Asas,Famari Transport, Sumry na Hoteli ya Staff Inn,matukio hayo pia waweza kuyapata katika mtandao wa www.shwari.com

'LIVE' MZEE MALECELA AWASHUKIA WAPINZANI
Mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa mzee John Malecela asema kuwa wanaopinga CCM si wazima wanapaswa kubezwa kwa nguvu zote


Mzee Malecela ambaye alikuwa ni mbunge wa jimbo la Mtera na kushindwa katika kura za maoni ,sasa yupo jukwaani amewaomba wana CCM na wananchi wa jimbo la Iringa kutoa kura zote CCM wasidanganyike na vyama vya upinzani.
Kuwa CCM ndicho chama pekee ambacho kinaweza kuongoza nchini na kuwa si kweli kama CCM imemaliza matatizo yote katika Taifa hili na kuwa bado yapo matatizo ambayo yanapaswa kutatuliwa na kuwa ambaye hana matatizo ni maiti pekee hivyo si kweli kama CCM imemaliza matatizo yote na kuwa CCM haiji kuwaeleza watanzania kuwa imemaliza matatizo katika Taifa ila bado kuna matatizo mengi ambayo bado yanahitaji kutatuliwa na kuwa iwapo watanzania watatoa nafasi tena ya kuongoza watahakikisha wanasaidiana na wananchi kutatua matatizo hao.

'LIVE" WABUNGE WAPANDA JUKWAAANI KUMNADI MONICA MBEGA


Umati wa wakazi wa mji wa Iringa waliofika uwanjani Mwembetogwa ktk sherehe za uzinduzi wa kampeni za CCM mkoa wa IringaMgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Ngezi Mbega akiomba kura jukwaani mbele ya mamia ya wakazi wa mji wa Iringa ambao wapo uwanjani hapa wakimsikilizaMbunge mteule wa jimbo la Njombe kusini na Naibu spika mstaafu Anne Makinda akimwombea kura Monica Mbega jukwaani ,asema Monica Mbega atakufa naye hadi kielewekeMbunge mteule wa jimbo la Ludewa mwanahabari Deo Filikunjombe akimpigia debe Mbega jukwaani sasa


mkuu wa mkoa wa Dar Bw.Wiliama Lukuvi na mbunge wa jimbo la Ismani ambaye ampita bila kupingwa akimnadi mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Monica Mbega( wa tatu kushoto)