Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

July 31, 2010

'LIVE' MKESHA WA MWENGE KIJIJI CHA IGWACHANYA WILAYA YA NJOMBE


Mpendwa mdau wa mtandao huu kumbuka unapata matukio ya moja kwa moja kutoka kijiji cha Igwachana wilaya ya Njombe mkoani Iringa ambapo hivi sasa umati kubwa wa wananchi wa wilaya ya Njombe wanaendelea na burudani mbali mbali kwa ajili ya kukesha na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2010,pichani ni chikupizi wakionyesha ufundi wao wa kuunda herufi za mbio za Mwenge , wanannchi wa wilaya ya Njombe wameweza kuchangia zaidi ya sh. milioni 18 kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo iliyopitiwa na mbio za mwenge

MBIO ZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA NJOMBE LEO

Mratibu wa mbio za mwenge kimkoa Bw Samwel Nyagawa (kushoto) akitambulisha viongozi INGIA HAPA

MWAKALEBELA AWAKANA TAKUKURU


ALIYEKUWA katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Frederick Mwakalebela ambaye anatuhumiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa ameziruka tuhuma hizo dhidi yake na kuwa hazina ukweli wowote za zinalenga kumchafua kisiasa kwa wapiga kura wake wa jimbo la Iringa mjini ambako anatafuta ridhaa ya wana CCM kutaka kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge .

Pamoja na Mwakalebela pia Mbunge wa Mufindi Kaskazini Joseph Mungai na Dr Norman Sigalla ambao pia wamekanusha tuhuma hizo na kuwa si kweli kama tuhuma hizo zinaukweli wowote na kuwataka wana CCM kuzipuuza na kutoa maamuzi yao katika kura za maoni kwa kuwapigia kura.

Wagombea hao walikanusha tuhuma hizo kwa nyakati tofauti jana wakati wakizungumza na mwanadishi wa habari hizi ambapo kwa upade wake Mwakalebela aliweza kuitisha kikao cha wanahabari na kutolea kukanusha tuhuma hizo, Mwakalebela alisema hajawahi kukamatwa kwa madai hayo, lakini akakiri kuhojiwa na Takukuru ili atoe ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa dhidi yake kwa taasisi hiyo.

Akinukuu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Donasian Kessy kwamba Julai 20 katika kijiji cha Mgongo aliitisha kikao nyumbani kwa Gwido Sanga ambacho kilihudhuriwa na wana CCM 22, Mwakalebela alisema alikutana na wana CCM hao na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, na kwamba katika kikao hicho hakutoa rushwa ya aina yoyote kama ilivyodaiwa.

"Nilikutana kweli na wanachama hao nikawaleza historia yangu, na nikatangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hili la Iringa Mjini na baadaye nikawaleleza malengo yangu endapo azma yangu hiyo itafanikiwa,baada ya hapo nikaondoka" alisema.

Hata hivyo alisema katika mkutano huo, mkewe Selina Mwakalebela anatuhumiwa na Takukuru kwa kutoa sh 100,000 kwa wanachama hao.

"Sifahamu chochote kuhusiana na madai ya mke wangu kutoa kiasi hicho cha fedha kwa wanachama hao, na malengo ya kufanya hivyo," alisema.

Alisema anashangaa kwanini Takukuru wamemuhusisha katika madai hayo ya mkewe kutoa kiasi hicho cha fedha, hususani katika kipindi hiki ambacho wanaCCM wanaenda kufanya maamuzi magumu ya kumpata mgombea wao.

"Mke wangu ni mke wangu, lakini kama kuna ushahidi wa yeye kufanya kosa, hilo lisichukuliwe kosa la familia," alisema.

Kwa upande wake Dr Sigalla na Mungai walisema kuwa wao wanapingana na taarifa hiyo ya Takukuru na kuwa imelenga kuwaharibia kiasiasa kwani kama kweli wangekuwa wamekamatwa mapema .


Hata hivyo wamewataka wana CCM kutodanganyika na taarifa hiyo ya Takukuru na badala yake kujitokeza kuwapigia kura.

Katika taarifa yake aliyoitoa juzi kwa waandishi wa habari Kessy alisema pamoja na Mwakalebela, aliyekuwa waziri katika serikali za awamu karibu zote Joseph Mungai anayewania ubunge Mufindi Kaskazini na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk Norman Sigalla anayetafuta ridhaa hiyo jimbo la Makete na Fadhili Ngajilo jimbo la Iringa Mjini,walihojiwa kwa madai ya kuhusishwa na vitendo vya rushwa katika majimbo wanayogombea.
SOMA TAARIFA YA TAKUKURU KWA VYOMBO VYA HABARI HAPA

MWENGE KUPITIA MIRADI 71 YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 8 IRINGA

JUMALA ya miradi 71 ye nyenye thamani ya shilingi 8,369,893,729 kufikiwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2010 mkoani Iringa.

Katika taarifa ya mkoa iliyosomwa na Katibu tawala mkoa wa Iringa Bibi. Gertrude Mpaka juzi wakati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupokea mwenge wa uhuru mwaka 2010 katika kijiji cha Kipingu, kata ya Manda wilayani Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma.

Bibi. Mpaka amesema “mwenge wa uhuru mwaka 2010 katika mkoa wa Iringa utakagua, utazindua, utafungua na kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi (71) yenye thamani ya shilingi 8,369,893,729. Aidha miongoni mwa fedha hizo, shilingi 2,890,484,593 ni fedha toka Serikali kuu, shilingi 951,705,586 ni michango ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa, thamani ya nguvu kazi ya wananchi ni shilingi 1,557,402,245, shilingi 1,413,904,000 ni michango ya watu binafsi na shilingi 1,556,397,305 ni michango ya wahisani na taasisi mbalimbali za maendeleo .

Mwenge wa uhuru mwaka huu unaongozwa na ujumbe usemao “Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na Malaria”

Katibu Tawala Mkoa ameeleza mapambano dhidi ya Ukimwi yanaendelea kwa kasi mkoani Iringa, na mkoa kwa kushirikiana na asasi za kitaifa na kimataifa na tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) umetekeleza mpango maalumu wa miaka minne wa kupambana na tatizo la Ukimwi ambapo utekelezaji wake ulianza Oktoba, 2008 na utamalizika Septemba 2012 .
Ameyataja maeneo makuu kuwa ni; kuhakikisha upatikanaji wa kutosha na kuendelea kutoa elimu ya juu ya matumizi sahihi ya kondomu, kupeleka karibu na kuboresha huduma za afya kwa jamii ambapo katika kipindi cha 2008/ 2009 jumla ya vituo 35 vya kupima virisi vya Ukimwi na kuto ushauri nasaha (CTC) vimeboreshwa kwa kufanyiwa ukarabati na samani.

Aidha wataalam 227 wamepatiwa mafunzo rejea kuhusu virusi vya Ukimwi na ushauri nasaha na jumla ya wagonjwa 51,137 walifikiwa na huduma za kupima virusi vya Ukimwi na kupata ushauri nasaha (CTC).

Eneo jingine amelitaja kuwa ni kuzijengea uwezo jamii wa kupambana na mila na desturi hatarishi zinazochangia ongezeko la maambukizi mapya ya VVU.


Pia kuboresha huduma za magonjwa ya zinaa ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/ 2009 kulikuwa na jumla ya vituo 293 vinavyotoa huduma ya magonjwa ya zinaa, wataalamu 288 walipatiwa mafunzo rejea ya huduma za matibabu ya magonjwa ya zinaa na watu 7,569 walifikiwa matibabu ya magonjwa ya zinaa.

Bibi. Mpaka ameongeza eneo lingine kuwa ni kuongeza elimu na uhamasishaji juu ya masuala ya ngono salama kwa makundi yaliyo katika mazingira atarishi ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/2009 jumla ya mikutano 395 ya uhamasishaji katika ngazi mbalimbali za jamii ilifanyika, aidha vikundi 181 vya kijamii vilishiriki na jumla ya vipeperushi na mabango 23,000 vya kuelimisha jamii.
Wakati huohuo katika mbio zake zilizoanza wilayani Ludewa jana Mwenge wa uhuru umekagua umekagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

July 30, 2010

DUA ZA WANA CCM LUDEWA KWA DEO FILIKUNJOMBE KUJULIKANA JUMAPILI

Wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kote nchini kesho jumapili wanataraji kushiriki katika zoezi la kura za maoni za kuwateua wabunge na madiwani watakao simama kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu utakao shirikisha vyama vingi ,wakati katika jimbo la Ludewa mwana Tasnia mwenzangu Deo Haule Filikunjombe amejitosa kujitolea kumpokea mbunge wa sasa wa jimbo hilo Profesa Raphael Mwalyosi hivyo naamini kushinda kwake Mwanahabari huyo ni ushindi wa wanahabari wote Tanzania na Duniani kama ilivyo kwa dada yetu Mpendwa Kasilida Mgeni alivyoshinda ubunge viti maalum mkoani Njombe basi sina budi kuchukua nafasi hii kumwombea Mpambanaji Filikunjombe ushindi wa kishindo kesho ili aweze kwenda kuongeza nguvu ya kutusemea bungeni kama wana habari ,Mungu libariki Jimbo la Ludewa ,Mungu ibariki Tanzania ,Mungu bariki wsanahabari waliopo katika mchakato huu washinde na umpe moyo wa ujasiri Deo Filikunjombe ili aweze kuuvaa katika siku ya leo na mara atakapotangawa mshindi japo katika hili dua wa wana CCM Ludewa naungana nazo


MCHUANO MKALI JIMBO LA KALENGA NI ABASI KANDORO NA DR.WILIAM MGIMWADr Wiliam Mgimwa(kulia)
Bw Abasi Kandoro
Hali ya nani zaidi katika jimbo la kalenga bado ni tete kutokana na nguvu kubwa aliyonayo mkuu wa mkoa wa Mwanza Abas kandoro na mkuu wa chuo cha Benki kuu Mwanza (BOT) Dr Wiliam Mgimwa huku wanachama wawili Mhandisi Gabriel Kalinga na Mwanamke Hafsa Mtasiwa wakionekana kuchomoza katika mchakato huo ukilinganisha na wana CCM wengine .

HII NI 'LIVE' MBIO ZA MWENGE WA UHURU LUDEWA IRINGARaia wa Marekani Bw Michael akisalimia na kiongozi wa mbio za wenge leo wilayani Ludewa.Wanafunzi zaidi ya 300 wa shule mbali mbali wilaya ya Ludewa wakiimba wimbo maalum wa mwenge wa uhuru jioni hii katika viwanja vya mkesha wa mwenge wa uhuru Mlangali LudewaNgoma ya wana Ludewa katika mbio za mwenge

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Nassoro Matuzya aizindua josho wilayani Ludewa leo

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATAKA WA CCM KUWANYIMA KURA WAGOMBEA WALIOTOA RUSHWA
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Bw Nassoro Matuzya akizungumza na wanafunzi wa sekondari ya Chifu Kidulile wilaya ya Ludewa
KIONGOZI wa mbio za mwenge Kitaifa Nassoro Matuzya amewataka wanachama wa chama cha apinduzi (CCM) kumsaidia Rais Jakaya Kikwete katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa wagombea kwa kuwanyima kura kesho wale wote waliofanya kampeni za rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Kauli hiyo aliotoa leo katika wilaya ya Ludewa wakati wa makabidhiano ya mbio za mwenge wa uhuru kati ya mkoa wa Ruvuma na Iringa .

Alisema kuwa Rais Kikwete ameendelea kuwa kiongozi wa mfano katika Taifa la Tanzania kwa kukemea vitendo vya ufisadi na rushwa ndani ya chama na serikali yake ila bado wapo baadhi ya wagombea wameendelea kutumia pesa zao kutafuta nafasi za uongozi jambo ambalo linapaswa kukemewa na kila mtanzania .

Kiongozi huyo alisema ili kumsaidia Rais kupambana na Rushwa ni vyema wana CCM ambao leo wanaingia katika mchakato wa kuwapigia kura wabunge na madiwani kutumia nafasi hiyo kuwahukumu wale wote waliotoa rushwa mbali mbali katika kampeni zao ili iwe fundisho.

“Hakuna asiyetambua jitihada za Rais wetu Kikwete katika mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi hapa nchini ….sasa ili tuweze kwenda pambano ni lazima kila mmoja wetu kuchukia vitendo hivyo”

Hata hivyo alisema sehemu ya ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ni ule unaokemea rushwa katika uchaguzi mkuu na kuwa ili nchi iweze kuwa na viongozi bora ni lazima suala la rushwa katika uchaguzi mkuu kukemewa na watanzania wote na kuwabeza wale wote watakaotaka kutumia pesa kununua uongozi.

Hata hivyo kwa upade wake Flatei Masai akitoa ujumbe wa mbio za mwenge katika viwanja vya kesha katika kijiji cha Mlangali alikemea tabia ya baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari ambao wamekuwa wakitumia vibaya taalum yao kwa kufanya mapenzi na wanafunzi wao na matokeo yake kuwaachia maambukizi ya virusi vya UKIMWI na mimba za utotoni .Alisema kuwa amoja na mkoa wa Iringa kuendelea kuongoza kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado kikwazo cha mapambano hayo ni walimu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi kimapenzi jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

"Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imekuwa mbele katika mapambano dhidi ya UKIMWI hata kutumia nguvu nyingi kupambana na ugonjwa huo pamoja na kukemea vitendo vya watu wazima wanaowapa mimba wanafunzi ...ila ndugu zangu walimu katika hili naomba kuwaonya ninyi mmepewa kazi ya kuwapa elimu hawa watoto sio kuwapa mimba na UKIMWI....nawaomba walimu fundisheni watoto masomo sio kufundisha ngono "


Kwani alisema kuwa jitihada za serikali za kupambana na mimba pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI haitafanikiwa iwapo wale waliopewa jukumu la kusimamia elimu na kuelimesha jamii wakawa sehemu ya kupinga mapambano hayo.
Mwenge wa uhuru mkoani Iringa unataraji kukimbiwa katika miradi 71 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8 ambapo utakagua,kutembelea na kufungua .
MWISHO

July 29, 2010

MWANAHABARI KASILIDA MGENI ASHINDA UBUNGE VITI MAALUM NJOMBE


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi akimpongeza mwanahabari Mgeni ambaye ameshinda ubunge viti maalum mkoa wa Njombe

KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI NA KALENGA ZAINGIA DOA .....

Wakati kivumbi cha kampeni katika majimbo mbali mbali ya uchaguzi kikikaribia kufika ukomo wake jumapili baada ya wana CCM kushiriki kupiga kura za maoni kuchuja wagombea hao na kuwateuwa wale watakaopeperusha bendera ya chama hicho ,hujuma na kampeni za kupakana matope zaendelea kutikisa katika jimbo la Iringa mjini na Kalenga kwa taarifa ziliuzotoa katika mtandao huu ambazo hata hivyo bado kuthibitishwa na wahusika wenyewe na vyombo vyenye mamlaka zinadai kuwa tayari katika jimbo la Kalenga mmoja kati ya wagombea ameaandaliwa taarifa chafu zitakazopelekea kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho na fedha zaidi ya shilingi milioni 54 zimetolewa ili kuhakikisha anahujumiwa mgombea huyo ambaye ni mmoja kati ya wagombea watatu wenye nguvu jimbo la Kalenga na pia ni msomi mzuri kuzidi wenzake wote.

Huku katika jimbo la Iringa mjini inadaiwa baadhi ya wagombea wamemchongea aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Bw Frederick Lameck Mwakalebela katika taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kuna taarifa kuwa mgombea huyo tayari anahojiwa na TAKUKURU japo jitihada za kumtafuta kamanda wa Takukuru mkoa wa Iringa Bw Donasian Kessy zinafanywa na mtandao huu leo utapata taarifa sahihi.

MSOMI WA CHUO KIKUU CHA DODOM A AKUTWA AMEJINYONGAKamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarit Mangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwanafuzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Bw Deo Kipinga (24) mkazi wa Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini ambaye amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia taulo chumbani kwake ,huyu ni kijana wa pili kujinyonga ndani ya wiki mbili mkoani hapa ambapo kijana wa kwanza ni Hamad Witala mkazi wa Frelimo (chini pichani ) ambaye alijiua kwa kujinyonga kwa waya wa umeme chumbani kwake baada ya kutotautiana na mkewe SOMA HAPA

KWAKHERI MPENDWA WETU DADA YETU PRIMITIVA PANKRASI TUTAKUKUMBUKA MILELE


Ni pengo kubwa katika familia ,Taifa na dunia kwa ujumla kwa kuondokewa na mpiganaji mwenzetu Primitiva na Hilda Mtenzi ndani ya wiki moja hakika wanahabari hawa walikuwa ni jeshi lenye nguvu katika tasnia hii ya habari
Binafsi namfafanisha Primitiva kama shujaa na kumchukulia Hilda Mtenzi kama komandoo katika tasnia hii lakini yote zaidi ya yote kifo cha Primitiva kwangu ni pengo kubwa hasa njisi tulivyo pata kushiriki pamoja katika ziara kadhaa za viongozi wa kitaifa ndani ya mkoa wa Iringa kwa kutembea ndani ya gari moja na kupeana ushauri na kukosoana kwa maana ya kujenga Taifa letu katika tasnia hii mengi amepata kunikumbusha na kamwe katika kumuenzi sitayaacha milele
Dada Primitiva leo unazikwa dua na sara zetu wanahabari twaomba uzipokee ,naamini kabisa kimwili haupo nasi ila katika kumbukumbu zetu tupo pamoja nasi kwani tutakukumbuka daima.

MBIO ZA MWENGE WA UHURU KUANZA KESHO MKOANI IRINGAMkuu wa mkoa wa Iringa Bw.Mohamed Abdulaziz akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr.Christina Ishengoma ,wakuu hao kesho wanataraji kukabidhiana mwenge katika wilaya ya Ludewa mkoani hapa ambapo mbio hizo zinatanza rasmi katika mkoa wa Iringa kwa muda wa siku sabaMratibu wa mbio za mwenge mkoa wa Iringa Bw Samwel Nyagawa akipokea mwenge wa uhuru mwaka jana ,

GREEN DARD WA CCM IRINGA MJINI WANATUMIWA NA WAGOMBEA KUIVURUGA CCM


Katibu mtendaji wa Club ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bw Frank Leonard jana amezingirwa na vijana wasiojua hata sheria moja ya ulinzi waliojipachika jina la Green Gard wa CCM katika wilaya ya Iringa mjini ambao wamekuwa kero kubwa katika kampeni za ubunge CCM jimbo la Iringa mjini.(pichani ni mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini MwlChelestino Mofuga akirejesha fomu ya ubunge hivi karibuni)
Green Gard hao kama wanavyojiita wao walimzuia mwanahari huyo kuchukua matukio katika mkutano wa kampeni za ubunge jimbo hilo la Iringa mjini huku wakidai kuwa wametumwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abed Kiponza na katibu wake Otyatya kuwabana waandishi wa habari wasifike katika kampeni hizo .


pamoja na kumzuia katibu huyo tayari hadi sasa vijana hao waliojipachika majina yasiyo yao ya ugreen Gard wameendelea kuwatisha hata baadhi ya wana CCM ambao wameonyesha kutofautina na wagombea wao wanaowapigia debe ambao hata hivyo hawakubaliki mbele ya wana CCM wenye utashi .


Kundi hilo la vijana hao waliogeuka oba omba katika kampeni hizo kwa kivuli cha kulinda amani katika mikutano hiyo limekuwa likitumiwa na mgombea mmoja wa nafasi hiyo kuchana abango ya wagombea wengine pamoja na kumsemea vibaya mbunge aliyeko madarakani Monica Mbenga kama huku wqakitambua wazi mbungea wao huyo pamoja na kuwa kada mzuri wa CCM bado hana nguvu ya kisiasa zaidi ya ile ya kuchana mabango ya wenzake na kuendesha siasa za ukabila kwa kuwatumia wafanyabiashara wa mjini hapa ambao ni kabila la kwake.Wachambuzi wa masuala ya siasa mjini Iringa wanasema kuwa siasa zinazofanywa na mgombea Fadhil Ngajilo kwa kuwatumia wapambe wake kuchana mabango ya wagombea wenzake zinaweza kumweka pabaya kiasiasa na anaweza kuambulia patupu katika mchakato huo baada ya wana CCM kubaini mchezo huo mchafu anaocheza mgombea huyo ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa.


Pia wadai kuwa mbali ya memyekiti wa CCM wilaya Bw.Kiponza kudaiwa kuliunga mkono na kulituma kundi hilo la Green Gard kuwafukuza waandishi kuandika habari za CCM katika kampeni hizo bado mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa ameakuwa akihusika kuwatumia vijana hao kufanya fujo na kuwasema vibaya wagombea wenzake .


Kwa kuwa lengo la vyombo vya habari ni kuhabaisha umma ni wakati umefika sasa kwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bi.Mary Tesha kusimama na kupaza sauti ya onyo kwa Green Gard hao ambao wamegeuka vibaka katika kampeni hizo hata kuwanyanya kwa vitisho wana CCM wanaotak kuhoji maswali wagombea hao pamoja na wanahabari wanaofika kuwapima wagombea na kutoa habari zao.


Kwa maelezo yanayotofautiana ya vibaka hao katika kampeni waliojipa jina la Green Gard ni kwamba wamekuwa wakilipwa fedha za ulinzi na mmoja wa wagombea wa ubunge na ndie ambao wamekuwa wakimsikiliza na wamekuwa wakimfuata mgombea huyo baada ya CCM kushindwa kuwapa posho zao na hivyo akumua kuomba wao kwa wagombea japo ni rushwa kufanya hivyo.
Tukio la waandishi wa habari kujfukuzwa ni la pili ambapo tukio kama hilo la katibu kufukuwa liliwakuta wanahabari wa kituo cha IMTV ambao pia walizuiwa kupiga picha na kutakiwa kuondoka katika mkutano huo japo katibu wa CCM mkoa na Kiponza kwa nyakati tofauti waliwaomba radhi wanahabai japo hawakuwakanya vijana wao waliojipachika jina la Green gard .

July 28, 2010

AJALI MBILI NDANI YA DAKIKA 10 IRINGA ,GARI YA MWENYEKITI WA UWT MGOMBEA UBUNGE YAGONGWA


Gari ya mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa mjini Bi,Nicolina Lulandara ikiwa imegongwa jioni hii eneo la Ruco wakati dereva wake akimfuata mwenyekiti huyo katika mkutano wa uchaguzi ,Lulandara alikuwa mmoja kati ya wagombea sita wa nafasi ya ubunge viti maalum mkoa wa Iringa na kushindwa nafasi hiyo baada ya kura kushindwa kutosha

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw.Abed Kiponza na mjumbe mmoja wa UWT wakitazama ajali ya gari la mwenyekiti wa UWT Iringa mjini ambalo lilogongwa na daladala leo jioni muda mfupi baada ya ajali nyingine ya daladala kutokea Kihesa na kujeruhi

Kiponza akiwa katika daladala iliyogonga gari ya mwenyekiti wa UWT leo


Daladala ikiwa ikivutwa na gari la vijana wa kazi majembe Auction Mark baada ya kujeruhi kwa ajali eneo la Kihesa Sokoni jioni hii


MBUNGE LEDIANA MNG'ONG'O NA PIINDI CHANA WAPITA UBUNGE TENA DADAKA MWAMOTO NAYE ASHINDA


Lediana Mafulu Mng'ong'o baada ya kutangazwa mshindi

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi huu Bw Chatanda akiwajibika vyema


Wahabari na katibu wa UV CCM mkoa wa Iringa Roda George wakifuatilia matokea


Ritha Kabati Moto (kushoto) akiwa na mgombea mwenzake japo yeye ameshinda nafasi hiyo


Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Jackson Msomi akitangza matokeo jioni hiiLediana Mng'ong'oRitha Motto KabatiEdith Matata

Rinata ApoloMsimamizi mkuu wa uchaguzi wa wabunge viti maalum mkoa wa Iringa Bw Jackson Msome ametangaza matokeo ya uchaguzi huo na kumtaja Renata Apolo ambaye ameshinda katika kundi la Vyuo vikuu baada ya kukosa mpinzani huku kundi la maalum walemavu akichaguliwa Edithi Matata kuwa mgombea pekee na kushinda nafasi hiyo.

Wakati katika kundi la wabunge viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mng'ong'o akiwashinda wapinzanio wake kwa mbali baada ya kupata kura

Khoja Ahamida (10)Nicolina Lulandara na Rukia Masasi wamegongana kwa kupata kura 23 kila mmoja . Eva Kkihwele (96),Ritha Kabati (194) na Mng'ong'o kufunika kwa kura 248 kati ya kura 298 ambapo kura moja pekee iliharibika.

Wakati katika mkoa wa Njombe kwa mujibu wa mwenyekiti wa UWT mkoa Pindi Chana ameshinda wapinzani wake sita waliojitokeza kwa kupata kura 267 na Rose Sitaki mfanyabiashara akishinda kwa kura 142 hivyo kwa mkoa wa Njombe wabunge waliochaguliwa na Chana na Sitaki Ingia hapa