Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 29, 2010

HAYA NI MAAJABU YA DUNIA.....Wanyama hawa pichani ni vigumu sana kuwakuta wakiwa pamoja kama hivi, ila hapa ni Iringa na hii ni historia ya mwaka naweza kusema kwetu Iringa wanyama wote ni ndugu wanaishi kwa upendo mwingi na waweza sema haya ni maajabu ya dunia pia

MGOMBEA PEKEE WA URAIS CCM RAIS DKT.JAKAYA KIKWETE KUREJESHA FOMU


Mgombea pekee wa nafasi ya urais kupitia chama tawala CCM ,rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) Julai Mosi mwaka huu anataraji kurejesha fomu hiyo mjini Dodoma ,katika sherehe hiyo fupi mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com,www.matukiodaima.blogspot.com na www.shwari.com utaweza kupata matukio yote "LIVE' kumbuka matukio yote hayo kutoka Dodoma yatakujia kwa udhamini wa kituo cha mafuta cha TOTAL Mafinga na Iringa chini na mkurugenzi wake Bw Ibrahim Hamis

June 28, 2010

WAGENI KARIBUNI IRINGA, KARIBUNI SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA
Tofauti ya bei isikutishe kuna maelewano pia ....
Chakula chetu cha leo....
SETY MOTO ACHANGIA SH.MILIONI MOJA UZINDUZI WA ALBAMU SASA TUJIANDAE MUHIMIDINI KWAYA

Msaidizi wa askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa mchungaji B.gavile (kushoto) akisaidiana na mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo na mkurugenzi wa kampuni ya udalali ya Majembe Bw Sety Moto kuzindua albamu ya Muhimidini kwaya ambapo kwa upande wake Moto alichangia shilingi milioni 1

Muhimidini Kwaya
Kwaya ya Muhimidini
Msaidizi wa askofu ,mchungaji Gavile (kulia) akiwa na Upendo Nkone na mapenzi wengine wa Muhimidini
Dr.Oscra Gabone ambaye ni mlezi wa kwaya hiyo akichukua kumbukumbu zake


Mama Mwasongwe ambaye ni mlezi wa kwaya hiyo akinunua CD kutoka kwa mgeni rasmi Sety Moto ambaye alichangia shilingi m.1
Mgeni rasmi ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Bw Sety Mwamoto akimkabidhi mmiliki wa mtandao huu CD ya Muhimidini ambayo aliinunua kwa sh.120,000 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya kwaya hiyoMlezi wa Muhimidini ,Mama Mfugale akinunua CD kwa shilingi 50,000
Kwaya ya Vijana KKKT Mlandege
Waimbaji wa Muhimidini wakiingia katika uwanja wa Samora leo wakati wa uzinduzi wa albamu yao

Waimbaji wa Paradise (KKKT-IRINGA)
,habari zaidi na picha soma gazeti la Msemakweli jumapili

MISHEMISHE ZA USIKU NDANI YA IRINGA

Mkazi huyu wa mjini Iringa akiwa amepoteza mawasiliano baada ya kunywa pombe kupita kiasi katika eneo la New Luxury bar mjini hapa leo usiku ,kweli pombe sio chai

P.Henry mchoma mishekaka maarufu Iringa akiwajibika leo usiku

Wadau wa mtandao huu ,Banzi na Brown

June 27, 2010


Wasamaria wema wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiongozwa na Jescar Msambatavangu (wa pili kushoto) kumsaidia binti ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja binti huyu alipandisha mashetani jana katika kati ya barabara na kueleza jinsi nyumba yao ilivyoteketea kwa moto na yeye kuishia kuungua sikio pekee

BEI ZA MAFUTA MJINI IRINGA LEOHiki ni kituo pekee katika manispaa ya Iringa ambacho kimekuwa kikisifika kwa kuendesha biashara hiyo kwa uaminifu mkubwa bila kuchanganya mafuta kipo jirani na ofisi za posta mjini Iringa

WANA CCM IRINGA WATAKA ZOEZI LA KUMDHAMINI KIKWETE LIRUDIWE UPYA


Baadhi ya majina 1105 ya wana CCM mkoa wa Iringa waliojitokeza juzi kumdhamini mgombea urais wa CCM ,Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete hata hivyo baadhi ya wana CCM mkoani hapa wanadai kuwa muda wa siku moja uliotumika kumdhamini mgombea huyo ni mfupi sana na hivyo wengi wao walishindwa kufika kumdhamini na hivyo wanaomba siku ziongezwe na zoezi hilo lirudiwe upya ili waweze kuongeza idadi ya udhamini ndani ya mkoa wa Iringa kutoka wanachama 1105 hadi 200,000 ,wadai idadi ya 1105 waliojitokeza bado ni ndogo sana kutokana na jinsi ambavyo wanavyo muunga mkono Kikwete

June 26, 2010

EXTRA BONGO YAITAKE IRINGAmashabiki wa Extara Bongo Iringa wakionyesha ujuzi wao katika kucheza
Wanenguaji wakiingia ukumbini
Husein Machozi akiwajibika sna EXTRA Bongo jana katika ukumbi wa Club V.I.PWapenzi wa EXTRA BONGO

DJ Kwassa akiwa na Ally Choki mzee wa farasi (kulia mwenye suti)


KIJANA AKUTWA AMEKUFA MFEREJINI


Picha namba 1

picha namba 2picha namba 3

Picha namba 2 ;Askari polisi mjini Iringa wakiuokota mwili wa kijana mwenyhe miaka 30 na 35 ambaye alikutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha na mwili wake kutupwa katika mfereji wa mchamba wima eneo la Don bosco mjini Iringa leo asubuhi ,kijana huyo hakuweza kufahamika jina wala eneo analoishi

Picha namba 1-3;Wakazi wa eneo la Don Bosco mjini Iringa wakiutazama mwili wa kijana ambaye hakuweza kufahamika jina wala eneo analoishi,mwili huo ulikutwa leo asubuhi katika mfereji wa mchambawima mjini hapa huku ukiwa umetolewa nguo zote

June 25, 2010

WANA CCM IRINGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMINI RAIS JAKAYA KIKWETE KUGOMBEA
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abed Kiponza (kulia)akimkabidhi majina 1105 ya wana CCM walijitokeza kumdhanini Daud Yassin ambaye ni kiongozi wa timu ya vijana wa CCM kutoka nyuo vikuu mbali mbali waliomaliza kuzunguka kanda ya nyanda za kuu kusini kumtafutia udhamini mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete ,zoezi hilo lilifanyika katika ofisi ya CCM mkoa wa IringaMratibu wa zoezi la kuzungusha fomu za udhamini wa mgombea urais wa CCM ,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Bw Daud Yasin akielezea jinsi ambavyo mkoa wa Iringa ulivyovunja rekodi katika udhamini wa mgombea huyu wa urais ukilinganisha na mikoa mingine ambayo wamepata kuzungusha fomu hizo .Wana CCM waliojitokeza kumdhamini Rais Kikwete leo ofisi ya CCM mkoa wa Iringa soma hapa

June 24, 2010

MWANAMKE ASIMULIA ALIVYOISHI KUZIMUMwanamke huyu mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaaam amedai kuwa amepata kuishi kuzimu kwa zaidi ya miaka miwili na sasa hivi ametengwa na familia yake kutokana na kupingana na uamuzi wa mama yake ambaye anamtaka asikanyage kanisani wala msikitini


Mtoto wa mwanamke huyo ambaye anadaiwa kupotea katika mazingira tata hadi leo akiendelea kumtafuta bila mafanikio ,mtoto huyu anadaiwa kupotea baada ya mama yake kutoa kuzimu na kusimulia maisha ya huko, vuta subiri ndani ya gazeti la Msemakweli jumapili ya Julai 4 utausoma mkasa huu katika ukrasa wa 14

SERIKALI NA JAMII YATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA....


Mkazi wa Dar es Salaam Bw Dany akijipumzisha katika gari lake eneo la ofisi za Majembe jijini hapa DSM.

RAI imetolewa kwa serikali na jamii hapa nchini kutoa ushirikiano kwa vituo vinavyo toa huduma za kulea watoto yatima na wale wa naoishi katika mazigira hatarishi na yatima badala ya kuviachia vituo vilivyo pekee.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tushikamane care trust fund bwana Grathomes Mbele alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo .

Bw. Mbele amebaiinisha kuwa kituo hicho kilianzishwa 2001 kikiwa na watoto 233 ambapo walikuwa wakiwapatia huduma wa kiwa majumbani kwao na walezi wao wanawapatia chakula mavazi,nguo,pamoja na kuwalipia ada za shule kwa wale ambao walikuwa wakisoma .

Amewataka watu wanao toa huduma za kuwatunza watoto ya tima kubadilika pale wanapopata wafadhili kuhakikisha wana jengewa shule ili watoto wanao wahudumia waweze kupata elimu ya uhakikika kuliko kutegemea ada zitoke kwa wafadhili kwani wafadhili wanatuma pesa za ada na wakati mwingine huchelewesha zaidi.

Bw. Mbele amewataka wazazi waache malumbano na mitafaruko jambo ambalo linasasababisha kuongezeka kwa watoto wanaoishi katika mazingila magumu na hatarishi iwapo wazazi wataingia katika mitafaruku isiyo kwisha badala ya kuonyesha mahusiano mazuri kwa watoto wao .

Pia alisema serikali kupitia ustawi wa jamii inapaswa kuhakikisha inafuatilia kwa karibu watoto wanaoishi mazingira hatarishi kwani baadhi yao ni wale wanaotokana na malezi ambayo siyo sahihi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao
(Habari hii na mwandishi wa blog hii jijini Dar es Salaam Bw. ERICK SOLOMON GERVAS)

WANAWAKE NI WAWAJIBIKAJI WAZURI KAZINI....
Mhariri wa habari za kimataifa katika gazeti la Tanzania Daima Bi.Ratifa Baranyikwa akiwazungumza na mwandishi wa mtandao huu baada ya kufanya ziara katika ofisi za gazeti hilo la Tanzania Daima jijini Dar es Salaam leo ,hakika kutokana na umakini niliopata kushuhudia kutoka

kwa mwanamke huyu bila shaka ni ushahidi tosha kuwa mwanamke akipewa nafasi anawajibika ipasavyo

BREAKINGNEWzzzzzzz MOTO WAWAKA OFISI YA WIZARA YA NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZIGari la zimamoto jiji Dar es Salaam ikiwa kazini kuokoa jengo la wizara ya nyumba ,ardhi na maendeleo ya makazi kuwaka moto
Hili ndilo jengo lililopona kuwaka moto
Wafanyakazi wa ofisi hizo na wateja wao wakiwa nje baada ya moto huo kuwaka


Orodha ya ofisi zilizonusurika kuteketea kwa moto leo


Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw Wiliam LukuviZikiwa zimepita siku chache toka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw Wiliam Lukuvi kuzisambaratisha ofisi za ardhi katika wilaya zote za mkoa huo kwa kufanya utapeli wa viwanja, moto wazuka makao makuu ya wizara ya ardhio,nyumba na maendeleo ya makazi na kuharibi baadhi ya nyaraka ,moto huo umezuka leo majira ya saa 3 asubuhi ,habari zaidi soma gazeti la Tanzania daima kesho