Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

May 31, 2010

BREAKINGNEWzzzzz WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MKWAWA WAGOMAWANAFUNZI wa chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) wamegoma kuingia madarasani kwa siku nzima ya leo wakishinikiza serikali kupewa fedha za malazi na chakula kiasi cha shilingi 300,000.(pichani ni wahitimu wa chuo hicho)

Wanafunzi hao wameeleza kusikitishwa kwao na hatua ya serikali kuileta timy ta Brazil kuja kucheza na timu ya taifa (Taifa Stars ) kwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3 huku wanafunzi wa vyuo vikuu wakiendelea kulia njaa kwa kushindwa kupewa fedha zao hizo kama walivyo ahidiwa .

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wanafunzi hao walisema kuwa mgomo wao ni mgomo wa amani na hata maandamano yao waliyoyafanya yalikuwa ni ya amani ila wanashangazwa na hatua ya uongozi wa chuo hicho kuwaita askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kuja kuyayawanya waandamanaji chuoni hapo.

wageni wa mwaka wa kwanza ilipaswa kupewa fedha ya kujikimu kiasi cha shilingi 350,000 pamoja na shilingi 300,000 ambazo wanafunzi wote walipaswa kupewa.

Wakielezea juu ya tukio hilo kwa sharti la kutotaja majina yao wanafunzi hao walisema kuwa mgomo huo ulianza majira ya saa tatu asubuhi kabla ya FFU kufika chuoni hapo majira ya saa 5 asubuhi.

Walisema kuwa kutokana na mgomo huo kutokuwa na vurugu zozote askari hao hawakuweza kufyatua risasi kama ilivyo siku nyingine japo bado waliendelea kupiga kambi katika eneo hilo la chuo ili kupambana na wanafunzi hao iwapo wangefanya vurugu.

Pia wanafunzi hao walihoji sababu ya uongozi wa chuo hicho pamoja na bodi ya mikopo kuendelea kuchelewesha malipo yao pamoja na yale ya mwaka wa kwanza wakati vyuo vingine vya umma wamepewa malipo hayo .

Hivyo waliahidi kuendelea na mgomo huo hadi pale watakapotimiziwa madai yao .

Wanafunzi hao pia walieleza kusikitishwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo kwa kujitenga kwao na mgomo huo na kuwa iwapo watatimiziwa madai yao hawapo tayari kuendelea kuongozwa na viongozi hao ambao wapo kwa maslahi ya viongozi wa chuo.

Mkuu wa chuo hicho Profesa Philimon Mushi akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuhusiana na mgomo huo alikiri kucheleweshwa kwa wanafunzi hao madai yao na kuahidi kuwa wataanza kulipwa madai yao kuanzia alhamisi wiki hii .

Alisema kuwa checki kwa ajili ya malipo hayo imekwisha tolewa na ipo benki kuu kwa ajili ya kumalizia taratibu za mwisho ili wanafunzi hao waweze kuingiziwa fedha zao.

Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuingia madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida wakati mchakato huo ukiendelea.

Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuwa hakuna mwanafunzi aliyekamatwa wala hakuna uharibifu wowote uliofanywa na wanafunzi hao.
MWISHO

PIGA NIKUPIGE!?

Askari wa kikosi cha Mafinga wilaya ya Mufindi akiigiza upaparazi kwa kunitanii kunipiga picha mimi kabla ya kumpiga kweli yeye

Mwandishi wa gazeti la majira Carlos Mtoya akipunga upepe katika moja kati ya ghorofa jijini Dar leo kama alivyonaswa na kamera yangu

Mpendwa mdau wa mtandao huu nimewasilia Dar kwa mapumziko ya siku kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya kumleta mwimbaji Solomon Mkubwa kutoka Kenya katika mji wa Makambako Njombe jumamosi hii

TIMU YA RADIO EBONY FM YAAMBULIA AIBU KWA WATUMA SALAMU WA CHIMALASiku ya kufa nyani .......?
kikosi cha watuma salamu wa Chimala (kilichokaa chini ) kilichoibebesha zigo la aibu timu ya Radio Ebony Fm


Kikosi cha Radio Ebony Fm
Hapa tunaona vizuri mchezo huu hatuatapenda kusimuliwa

Benchi la timu ya Radio Ebony Fm likiwa limepoteza matumaini baada ya kuchapwa bao la piliMtangazaji maarufu wa kipindi cha michezo Radio Ebony Fm Maregesy Gilison (kulia) akifuatilia kwa makini mpambano huo ,kati ya watangazaji maarufu hapa nchini wa michezo Mafregesi ni kaka yao amepata kuwepo radio Free Afrika na baada kuondoka kwake kipindi kimeendelea kupooza kupitia kiasi

SOMA HABARI CHINI

PAMOJA na kutamba kwa kuzifunga timu mbali mbalia ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa huo ,timu ya Radio Ebony Fm imeonyesha kushindwa kutamba mbele ya watuma salamu wa Chimala wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya baada ya kukubali kichapo cha goli 2-1 .
Kutokana na kichapo hicho chama cha waanadishi wahabari za michezo Taanzania (TASWA) mkoa wa Iringa kimetoa zawadi ya fedha kwa timu ya watuma salama wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya kama pongezi kwa kuichapa timu ya wanahabari wa kituo cha Radio Ebony FM katika mchezo wake wa kirafiki .

TASWA imeweza kuipongeza timu hiyo ya watuma salamu wilaya ya Mbarali baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa kirafiki kati yao na wanahabari wa kituo cha Radio Ebony Fm ambapo katika mchezo huo ,watuma salamu waliweza kuiadhibu Radio Ebony Fm kwa jumla ya magoli 2-1.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Chimala juzi jumamosi wilaya ya Mbarali na kushuhudia na umati mkubwa wa mashabiki kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya ya Iringa wakiongozwa na mgeni rasmi katika mchezo huo msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa mitego ambaye pia aliweza kupagawisha mashabiki .

Timu ya Radio Ebony Fm ndio ilianza kujipatia goli lake la pekee mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza goli lililopatikana kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Chimala kushika mpira langoni akijaribu kuokoa.


Hata hivyo goli hilo la Ebony Fm lilionyesha kuwaongezea hasira zaidi wachezaji wa Chimala ambao waliweza kucheza soka safi na kupelekea kujipatia magoli mawili ya haraka haraka ndani ya kipindi cha kwanza .

Hadi timu zote mbili zinakwenda mapumziko tayari Radio Ebony Fm ilikuwa nyuma kwa goli moja hali iliyopelekea kipindi cha pili wanahabari hao kujaribu kucheza soka kwa uwezo mkubwa japo ilionekana sio riziki katika mchezo huo baada ya mwamuzi kuhitimisha mchezo huo kwa filipi ya mwisho huku Chimala wenyewe wakiwa mbele kwa goli 2 dhidi ya 1 la wanahabari hao.

Wakati huo huo TASWA mkoa wa Iringa kupitia mwenyekiti wake mimi Francis Godwin wameipongeza timu hiyo ya watuma salamu kwa kuweza kuifunga timu hiyo ya Ebony Fm ambayo imekuwa ikitoa upinzani mkubwa na kujigamba zaidi kupitia vipindi vyake kana kwamba hakuna timu ambayo ingeweza kuifunga timu hiyo.


TASWA katika pongezi zake imeweza kununua magoli yote matatu yaliyofungwa kwa timu ya Chimala ya ili ya Ebony Fm kwa kiasi cha shilingi 10,000 kwa kila goli kama njia ya kuhamasisha michezo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneo mengine ambayo timu za mkoa wa Iringa zinapata kwenda kucheza.

MWISHO

May 28, 2010

BREAKINGNEWzzzzzzzz WANA CCM WANNE LUDEWA MATATANI KWA KUMPINGA MBUNGE WAO


WACHAMA wanne wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Ludewa mkoani Iringa wamekamatwa na afisa mtendaji wa kijiji cha Ilinindi kata Madilu humo Dennis Luoga kwa kosa la kumzuia mbunge wao wa jimbo la Ludewa Profesa Raphael Mwalyosi(pichani ) kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji chao cha Ilinindi kwa kudai kuwa ameshindwa kutimiza ahadi zake

Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya wananchi wa kijiji hicho kumfukuza mbunge wao Prof. Mwalyosi (CCM) ili asihutubie mkutano wa hadhara kijijini hapo kama njia ya kushinikiza kutekelezewa ahadi yao kwanza kama alivyo kuwa amepata kuwaahidi .

Mmmoja kati ya viongozi wa madhehebu ya dini ambaye alikuwepo katika mkutano huo alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa kitendo kilichofanywa na vijana hao si cha kiungwana kutokana na hatua yao ya kumkatia umeme mbunge huyo

Alisema kuwa kabla ya mbunge huyo kufika eneo la mkutano kiliandaliwa kikundi cha kwaya kwa ajili ya kumwimbia mbunge huyo na kusifia utekelezaji wa Ilani ya CCM jambo ambalo wananchi wa eneo hilo walishindwa kuunga mkono hali iliyopelekea kufanya vurugu kwa kukata umeme ili kumzuia mbunge huyo kuwahutubia kabisa .

“Sisi kama viongozi wa dini tumesikitishwa na hatua ya vijana hao ila bado tunawakumbusha wana siasa kujenga utamaduni wa kusema kweli ili kuepusha migogoro miongoni mwa jamii wanayoiongoza”

Mmoja kati ya vijana hao wa CCM waliokamatwa kwa kumzuia mbunge huyo kufanya mkutano Evaristo Mhagama alisema kuwa Prof. Mwalyosi aliahidi kuwapelekea maji kijijini hapo (Ilininda), jambo ambalo hajalitekeleza hadi sasa.

Aidha alisema hatua ya wao kumzuia ni kutokana na kushindwa kuwaongeza wahudumu wa afya katika dispensari ya Kijiji hicho, ahadi ambayo bado hajaitekeleza mpaka sasa japo kwaya hiyo ilionyesha kumpamba kwa kufanya kazi vizuri .

“Tumechoka kupewa ahadi hewa,” alisema kwa hasira Luciana Nziku(63)mkazi wa Ilininda huku akiwa amefunga kanga kiunoni “toka tumekuchagua ulikuwa wapi mpaka unakuja leo?”

Mbunge Mwalyosi alikwenda kijiijini hapo akiwa ameambatana na Mhe. Benard Libato - Diwani wa Madilu - ambaye naye licha ya kuwasihi wananchi hao wamsikilize mbunge wao walimkatalia kata kata.

Wana CCM hao wa Ilininda, walioonekana dhahiri kuchoshwa na ahadi zisizo na utekelezaji, na ndipo walipoamua kuzima umeme na kumwamuru aondoe vipaza sauti vyake.

Hata hivyo kutona na vurugu hizo kikundi cha Kwaya cha UVIKANJO kilichokuwa kitumbuize nacho kiligoma kuendelea kumwimbia mbunge huyo kwa kuhofia kichapo kutoka kwa wananchi hao wenye hasira kali .

“Tutamwimbiaje mtu asiyetekeleza ahadi zake …kwa sasa hatupo tayari kuendelea kuimba tena”alisikika akisema mmoja wa wana UVIKANJO

Wana CCM hao waliokamatwa na afisa mtendaji huyo Luoga na kuwekwa mahabusu ya kijiji kwa kutuhumiwa kumfanyia fujo mbunge wao ni pamoja na Deo Mgaya, Joseph Mlowe, na Evaristo Mhagama.

Hata hivyo afisa mtendaji huyo wa kijiji Luoga alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa kukamatwa kwa wananchi hao ni utekelezaji wa agizo la mbunge wao kutokana na wananchi hao kuonyesha nidhamu mbaya mbele yake .

Mbunge wa jimbo hilo Prof. Mwalyosi amekanusha madai hayo na kuwa kama mtendaji aliwakamata aliwakamata kwa nafasi yake na sio kutumwa na yeye kama mbunge.

Prof. Mwalyosi ambaye amekuwa akizunguka katika vijiji vya jimbo lake kwa lengo la kuhamasisha maendeleo na kuwaomba wananchi wamchague tena kipindi kijacho amekuwa akipambana na misuko suko mingi ikiwemo ya kuhojiwa juu ya ahadi zake .

Alisema kuwa mradi huo wa maji ni mradi wa benki ya dunia ambao unatekelezwa katika vijiji 10 vya kila wilaya na kuwa kijiji hicho ni kimoja wapo na kuwataka wananchi hao kuwa na subira juu ya mradi huo

May 25, 2010

UGONJWA GANI HUU JAMANI NISAIDIENI...
MTAMBUE mwanamke mjane Bitia Msigwa (40) mkazi wa kijiji cha Mlevela kata ya Igima wilaya ya Njombe mkoani Iringa anayesubiri kifo kwa kukosa fedha kiasi cha shilingi milioni 10 za kutibu ugonjwa wa uvimbe katika shavu lake,iwapo umeguswa na matatizo ya mwanamke huyu unaweza kuwasiliana nami kwa ajili ya kumsaidia piga simu 0754 026 299 kwa pamoja tunaweza kuokoa maisha ya mwenzetu huyu .

HIVI NDIVYO WAKAZI WA IRINGA WALIVYOSHIRIKI KUMPATA MISS IRINGA
Mdau Mwangosi

Wadau wakifuatilia kwa karibu kinyang'anyiro cha Voda Com Miss IringaKazi na dawa hapa bila kupata moja moto na moja baridi hatutaweza kuona vizuri na kujua mrembo ni yupo hapa


May 24, 2010

NYUMBANITU NI MSITU WENYE MAAJABU TELE


Msitu wa nyumbanitu uliopo wilaya ya Njombe ni msitu mdogo wenye maajabu tele ,katika msibu huo wenye kuku weusi wasiozeeka milele yote iwapo utaingia kienyeji unaweza kukesha ukizunguka ndani ya msitu huo wenye ukubwa wa ekari mbili pekee.

YONO KEVELLA ACHANGIWA FEDHA ZA FOMU ,NYIMBO AAMBIWA ATAFUTE KAZI NYINGINE...

WANANCHI wa jimbo la Njombe Magharibi wamemchagia kiasi cha shilingi 20,000 mbunge wa jimbo hilo Yono Kevella (pichani)ili muda ukifika achuku fomu ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo na kumtaka aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo kutafuta shughuli nyingine ya kufanya na sio kurudia kugombea ubunge kwani kufanya hivyo ni sawa na kula matapishi yao.

Wananchi hao wa kijiji cha Mlevela kata ya Igima walitoa msimamo wao huo jana katika harambee iliyoendeshwa na mbunge Kevella ambapo pia mbali ya kuanchagi fedha hizo za kuchukua fomu pia walimuunga mkono katika harambee hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 1 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo.


Akizungumza baada ya kumalizika kwa harambee hiyo kwa niaba ya wakazi wa kijiji mwenyekiti wa chama cha TLP jimbo la Njombe Magharibi Yohana Mgowelo alisema kuwa toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kijiji hicho hakijapata kuwa na kituo cha afya hali iliyokuwa ikiwalazimu wagonjwa kutembea masaa zaidi ya mawili kwenda kupata huduma ya afya katika kijiji cha jirani ama katika hospitali ya wilaya ya Njombe.

“Mimi hapa ni mwenyekiti wa jimbo hili la Njombe Magharibi kupitia chama cha TLP ….ila ukweli lengo letu wapinzani sio kubeza kila jambo ….jimbo hilo huyu ni mbunge wa pili kuongoza ambapo mtangulizi wake alikuwa Thomas Nyimbo …lakini maendeleo yaliyopatikana sasa huwezi linganisha nay ale ya Nyimbo ….sasa kwanini tusimpongeze hata kwa kutuwezesha kupata huduma hii ya afya hapa…nasema tupo pamoja”alisema kiongozi huyo

Pia alihoji sababu za wabunge wa CCM ambao wamepata kuongoza majimbo na kung’olewa katika nafasi zao kurudi kutaka kugombea tena ubunge na kuwa ni vema wananachi kuwa makini na njama chafu zinazofanywa na chama cha mapinduzi kwa kuendelea kuwapitisha wabunge wale wale miaka yote.

Hata hivyo kwa upande wake mbunge Kevella akiwapongeza wananchi hao kuwa michango yao kwa ajili ya shuguli za kimaendeleo alisema kuwa jimbo hilo ni moja kati ya majimbo yanayo piga hatua kubwa katika maendeleo na kuwa mbali ya Manispaa ya Iringa kuwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu ila bado wilaya ya Njombe katika jimbo la Njombe Magharibi ni miongoni mwa wilaya na majimbo yenye maendeleo makubwa kwa kuanzisha chuo kikuu kishiriki cha Tumaini .


Kevella alisema kuwa pamoja na kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo ameweza kuponda jitihada za kimaendeleo katika jimbo hilo ila bado wananchi wana kila sababu ya kuwabeza wale wote hasa wana CCM wanaotaka kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ambao wanajitokeza kupinga kazi zilizofanywa na chama hicho .


Kwani alisema ni vizuri kazi ya kupinga ifanywe na wapinzani ila sio wana CCM na kuwa mwana CCM mwenye tabia kama ya Nyimbo ya kupinga kazi zilizofanywa na chama tawala chini ya Rais Jakaya kikwete atakuwa amepoteza mwelekeo wa kuja kuomba kuwatumikia wananchi .

Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na kituo hicho cha afya kukamilika bila kuwa na kitanda hata kimoja kwa upande wake kama mbunge atajitolea vitanda vyote katika kituo hicho pamoja na kununua madawati katika shule ya awali ya kijiji cha Idunda ambayo wanafunzi wake zaidi ya 60 pamoja na walimu wamekuwa wakikaa chini.

Wakati huo huo wana CCM katika kata hiyo wamekitaka chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe kukemea tabia ya uongo kwa wanachama wanaotaka kuwania ubunge katika jimbo hilo ambao wamekuwa wakiwasema uongo wabunge na madiwani wa CCM huku wakisahau kuwa kauli zao na uongo zinakiweka pabaya chama hicho na kuonekana vibaya kwa wapinzani kuwa hakuna jipya ambalo limefanywa kwa kipindi chote cha miaka mitano alisema katibu wa CCM kitongoji cha Idunda Ayubu Mwipela
MWISHO

May 22, 2010

BREAKINGNEWzzz MSANII DIAMOND ACHAPWA IRINGA

DJ Muba ni DJ maarufu anayetikisa mkoa wa Iringa na Tanzania ila ni DJ mpole aliyetaka kuzichapa na msanii chipukizi Diamond


Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro 2010 Diamond (jukwani )akiwajibika katika jukwaa la Voda com Miss Iringa kabla ya kupokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu .

Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipinga muziki katika ukumbi huo .

Hatua ya msanii huyu kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo hali iliyopelekea mashabi hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.

Mwalubadu

MSHIRIKI NAMBA 5 RAHMA GEGE ATWAA TAJI LA MISS VODA COM IRINGA 2010
Mshiriki huyu Rahma Gege amefanikiwa kutawazwa kuwa malkia wa urembo wa Voda com Miss Iringa 2010 katika kinyang'anyiro kilichofanyika usiku huu katika ukumbi wa St.dominic mjini Iringa ,huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Grace Simon na nafasi ya tatu ikitwaliwa na Mary Kigari (picha za ukumbini zitawekwa wakati wowote kuanzia sasa.

May 21, 2010

UV-CCM YATOLEA UFAFANUZI KUJIUZULU KWA MASAUNI YATAKA MCHAWI ASITAFUTWE.....

katibu wa iadara ya uhamasishaji na chipukizi Taifa Estar Bulaya akimtazama Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Martine Shigella wakati akifafanua mbele ya wanahabari leo ofisi za CCM mkoa kuhusiana na kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Hamad Yusuph Masaun na kusisitiza kuwa asitafutwe mchawi katika sakata hilo mchawi ni Masauni mwenyewe kudanganya CV zake awataka viongozi wengine wa vijana wenye CV feki kujisalimisha kwa kujiondoa katika nafasi zao

Shigella na timu yake baada ya kujitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya wanahabari mkoani Iringa kuelezea sakata la Masauni ,Shigella pia ametumia nafasi hiyo kuvipongeza vyombo vya habari ndani ya mkoa wa Iringa kwa kuwa vivumilivu kusubiri kauli ya kweli toka UVCCM badala ya kuripoti vile vinavyojua vyenyewe na kuwa wanahabari Iringa wamelinda maadili ya uandishi
Mkutano kati ya Shigella na wanahabari mjini Iringa leo ,Msimamo wa UVCCM Taifa ni kutaka CCM kubariki ombi lao la kumpitisha Rais Jakaya Kikwete kuwa mgombea pekee katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu ,ili kujua sakata la Shigella na Moyo usikose kusoma gazeti la Tanzania Daima kesho

MATOKEO YA KURA ZA NANI KUWA MISS VODA COM IRINGA ,MSHIRIKI NAMBA MOJA TISHIO

Matokeo ya utabiri wa mshindi wa Voda com Miss Iringa hadi saa 4 .1 asubuhi hii mshiriki namba 1 anaendelea kupewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya kupigiwa kura 2 za kwenye mtandao huu na kura 14 kwa njia ya SMS katika simu ya kiganjani.
Huku washiriki wengine hawajapata kura hata moja kupitia mtandao japo katika kupitia SMS mshiriki namba 4 amepewa nafasi ya pili kwa kupata kura 13,mshiriki namba 9 amepata kura 11 mshiriki namba 2 amepata kura 10, mshiriki namba 3 kura 9 ,mshiriki namba 5 kura 6, huku mshiriki namba 6 hadi 7 wote wamepata kura 4 kila moja na mshiriki namba 8 akiambulia kura moja pekee
Kura hizi zitaendelea kupigwa hadi saa 1 usiku wa leo na namna na kumpata mshindi wetu wa utabiri huu namba zote za simu sitachanganywa na washindi wa urembo na mshindi wa kwanza atachagua jina moja la shabiki wake atakayepata zawadi hiyo pia mshindi pili na watatu watafanya hivyo hivyo kupata mashabiki wao watakaoondoka na zawadi hiyo leo .
Kumbuka lengo la shindano hili ni kuhamasisha masuala ya urembo ndani na nje ya mkoa wa Iringa

May 20, 2010

NANI KUTWAA TAJI LA VODA COM MISS IRINGA KESHO ? TABIRI USHINDE MUDA WA MAONGEZI(1)

Mary Kigali


(2)

Prisca Mlekwa(3)
Mahadiya Rabii


(4)

Faraja Kivenule
(5)
Rahma Gege


(6)

Catherine Kisinde
(7)Grace Simon


(8)

Diana Beny


(9)

Ziada Mbega


Mpenzi mdau wa matandao huu unaweza kujishindia muda wa maongezi wa shilingi 10,000 iwapo utatabiri mshindi wa kwanza kati ya hao ,na shilingi 5000 kwa mshindi wa pili wakati mshindi wa tatu utapata shilingi 3000.

Jinsi ya kushiriki tuma ujumbe mfupi katika namba 0754 026 299 ama kwa njia ya maoni katika eneo la maoni kwenye mtandao huu huku ukitaja jina lako kamili na kuweka namba yako ya simu ya kiganjani .katika onyesho hili bingwa wa tuzo za Kilimanjaro mwaka 2010 Diamond Belle 9 na Awilo wa Mbeya watapamba onyesho kwa burudani huku mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na ndie atakayekabidhi zawadi ya cash shilingi laki 6 kwa mshindi wa kwanza ,laki 4 mshindi wa pili na laki 3 mshindi wa tatu na kifuta jasho cha shilingi 50,000 kwa washiriki wote onyesho litafanyika ukumbi wa St.Dominic kuanzia saa 1 usiku na wote wataingia ukumbini kwa kiingilio cha shilingi 10,000

MAANDALIZI YA MWISHO KAMBI YA VODA COM MISS IRINGA 2010 LEO ,KESHO KUPANDA JUKWAANI

Washiriki wa taji la Miss Iringa wakakao panda jukwaani kesho


Wadhamini na waandaaji wa taji hilo

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini ,SOma habari hapa

AKUDO WAACHA SIMULIZI IRINGA

Wanenguaji wa Akudo wakiwajibika jana usiku katika ukumbi wa club V.I.P


Mambo juu ya mambo
Hakuna aliyetulia bila kucheza ama kutikisa kichwa Iringa


Shauri akiselebuka dansi la akudo
'Sisi ni watu maarufu sana ila hatujijui "aliyekuwa mshiriki wa maisha Plus kutoka Iringa Shauri Myinga akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji maarufu wa Radio Ebony Fm Edo Bashir

Mwandishi wa Chanel Ten Iringa Daud Mwangosi na mwandishi wa Radio Country Fm Iringa Sophia Mpunga wakiselebuka hapa kazi na dawa

Makada wa UVCCM wakiongozwa na dada Esta Bulaya (kulia) ambaye ni katibu wa idara ya uhamasishaji chipukizi Taifa wakisakata dansi

Esta Bulaya (kulia) ambaye ni katibu wa idara ya uhamasishaji chipukizi Taifa
Picha zaidi za akudo Iringa hapa