Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 29, 2010

WANANCHI KAPUNGA WADAI KUNYANYASWA NA MWEKEZAJI .....


WANANCHI wanaozunguka shamba la kapunga wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamedai kutishwa na kunyanyaswa na msimamizi wa mashamba hayo ya kapunga Bw. Badri Dart.

Pamoja na kutishwa pia wamedai msimamizi huyo mwenye asili ya kiasia amekuwa akiwatuhumu wananchi hao kwa madai ya kuiba mpunga shambani mwake huku wafanyakazi wake akiwatuhumu kuwa ni wezi wa vifaa vya kampuni na kuwatishia kuwaua endapo wataendelea kufanya hivyo.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya wananchi ambao hawakupenda majina yao yakuandikwa gazetini kwa usalama wao walisema kuwa toka mhindi huyo ajiunge na kampuni hiyo mwaka 2007 akijitambulisha kuwa yeye ni Afisa mipaka wa shirika hiloyao ikiwa chanzo ni yeye.

Wananchi hao walidai kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwatishia kuwa atauwa mtu kama wataendelea kupita kwenye mashamba ya shirika hilo wakati ndiyo njia pekee yakupita kwenda kwenye mashamba yao .

Waliongeza kuwa Bw.Badri amekuwa akiwatuhumu nakuwakashfu wananchi hao kuwa ni wezi na kudai kuwa yeye hawezi kutishiwa na mtu yeyote kwa kuwa yuko pamoja na viongozi wanchi ikiwa ni pamoja na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel.

“Huyu kijana amekuwa akitukashfu sana kwa kusema sisi wakazi wa Kapunga ni wezi, inasikitisha sana maana tupo hapa kapunga mdakama hayo” alisema mzee mmoja jina linahifadhiwa.

“ Kwanza amelifanya shirika lichukiwe na wanachi wa eneo hili kwa sababu ya kashifa zake na kauli ya kusema yuko pamoja na viongozi wetu kitu labda kwa kuwa baadhi ya viongozi wanalima kwenye mashamba hayo na akajenga urafiki na viongozi hao ndiyo maana anakiburi” aliongeza mzee mwingine jina linahifadhiwa.

Kapunga bila Badri Dart inawezekana tena kutakuwa na amani nje na hata ndani ya shirika maana hata wafanyakazi wanaendeshwa kama

Aidha wafanyakazi hao walisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo walisema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwanyanyasa vilivyo na kuwashutumu mara kwa mara kuwa ni wezi huku wengine wakifikishwa mahakamani.

Wafanya kazi hao walisema kuwa waamekuwa wakiwafanyisha kazi kama watumwa akidai asiyetaka aishie zake milango iko iko wazi na kudai kutokana na shida za vibarua ndiyo maana wamekuwa wakivumilia unyanyasaji huo.

“Amekuwa akitutukana matusi na kuwafikisha polisi baadhi ya wafanya kazi akidai ni wezi bila kosa lolote na kwamba anajidai kuwa yeye yu pamoja na viongozi wakubwa hivyo hakuna watakachokifanya juu yake” alisema mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo .

“Tunaomba mtufikishie malalamiko yetu kwa viongozi wa juu ili watambue kwamba sisi watanzania bado ni watumwa licha ya kuwa kuwa kwenye nchi yetu na mtu mmoja tu Bw.Badri Dart” alisema mfanyakazi mwingine.

“Ikiwa huyu kiongozi ataondoka ni ukweli kwamba hili shirika litatengamaa ndani na nje ya shirika hili maana hata wanachi wanamlalamikia yeye tu.aliongeza mfanya kazi mwingine.

Hata hivyo Bw.Badri Darft alipotakiwa kujibu shutuma hizo alikana kuhusiana na shutuma hizo kwa kudai kuwa ni za uongo.

Alisema kuwa yeye amekuwa akifuata sheria za shirika na kwamba yeye ni mfuatiliaji sana wa mambo ya kampuni na kudai kuwa hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchukiwa na wafanyakazi na hata wananchi wa nje.

Hata hivyo Bw.Badri alikili kuwafikisha baadhi ya wafanya kazi katika vyombo vya sheria kwa madai ya wizi ingawa alisema kuna wengine kesi zao walishinda na wengine shirika lilishinda huku akisema wengine zinaishia juju tu.

“Asili ya watu wa kapunga ni wezi ingawa wengine wanatushinda kesi na wengine tumeshinda kesi mahakamani ila wengine kesi zao zinaishia juju tu” alisema Bw.. Ba.Badri

Akizungumzia kutumia uhusiano wake na viongozi wakubwa kuwanyanyasa wananchi pamoja na wafanyakazi wake alisema hiyo si kweli isipokuwa viongozi wameomba mashamba katika shirika lao na kudai wapo pale kama watu wakawaida na si kama mtumishi wa serikali hiyo hizo shutuma ni za uzushi.

Hata hivyo alikili kuwepo viongozi wakubwa katika mashamba hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Jaji Mkuu wa Mkoa maAfisa wa TRA pamoja na Askali 6 ambao wamepewa mashamba katika shirika hilo .

Awali alikana kuwepo na uhusiano wa karibu na kiongozi aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel lakini baada ya kubanwa na maswali alikili kuwepo na uhusiano na mtu huyo na kudai kuwa ni rafiki yake na baadaye kuwa ni Bwana shamba.

Amekuwa akizua mitafaruku mbali mbali ikiwemo ya wakazi wa Mapogoro hasa jamii ya wasukuma ambao walidai walipokonywa mashamba mlefu hatujawahi kuambiwa na mtu yeyote maneno watumwa kwa kweli haiwezekani mtu mmoja akaivuruga kampuni kwa mitafaruku na wananchi, kwanini viongozi wengine wasishutumiwe? Alisema kijana wa kimasai.

WANANCHI KAPUNGA WADAI KUNYANYASWA NA MWEKEZAJI .....


WANANCHI wanaozunguka shamba la kapunga wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamedai kutishwa na kunyanyaswa na msimamizi wa mashamba hayo ya kapunga Bw. Badri Dart.

Pamoja na kutishwa pia wamedai msimamizi huyo mwenye asili ya kiasia amekuwa akiwatuhumu wananchi hao kwa madai ya kuiba mpunga shambani mwake huku wafanyakazi wake akiwatuhumu kuwa ni wezi wa vifaa vya kampuni na kuwatishia kuwaua endapo wataendelea kufanya hivyo.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya wananchi ambao hawakupenda majina yao yakuandikwa gazetini kwa usalama wao walisema kuwa toka mhindi huyo ajiunge na kampuni hiyo mwaka 2007 akijitambulisha kuwa yeye ni Afisa mipaka wa shirika hiloyao ikiwa chanzo ni yeye.

Wananchi hao walidai kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwatishia kuwa atauwa mtu kama wataendelea kupita kwenye mashamba ya shirika hilo wakati ndiyo njia pekee yakupita kwenda kwenye mashamba yao .

Waliongeza kuwa Bw.Badri amekuwa akiwatuhumu nakuwakashfu wananchi hao kuwa ni wezi na kudai kuwa yeye hawezi kutishiwa na mtu yeyote kwa kuwa yuko pamoja na viongozi wanchi ikiwa ni pamoja na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel.

“Huyu kijana amekuwa akitukashfu sana kwa kusema sisi wakazi wa Kapunga ni wezi, inasikitisha sana maana tupo hapa kapunga mdakama hayo” alisema mzee mmoja jina linahifadhiwa.

“ Kwanza amelifanya shirika lichukiwe na wanachi wa eneo hili kwa sababu ya kashifa zake na kauli ya kusema yuko pamoja na viongozi wetu kitu labda kwa kuwa baadhi ya viongozi wanalima kwenye mashamba hayo na akajenga urafiki na viongozi hao ndiyo maana anakiburi” aliongeza mzee mwingine jina linahifadhiwa.

Kapunga bila Badri Dart inawezekana tena kutakuwa na amani nje na hata ndani ya shirika maana hata wafanyakazi wanaendeshwa kama

Aidha wafanyakazi hao walisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo walisema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwanyanyasa vilivyo na kuwashutumu mara kwa mara kuwa ni wezi huku wengine wakifikishwa mahakamani.

Wafanya kazi hao walisema kuwa waamekuwa wakiwafanyisha kazi kama watumwa akidai asiyetaka aishie zake milango iko iko wazi na kudai kutokana na shida za vibarua ndiyo maana wamekuwa wakivumilia unyanyasaji huo.

“Amekuwa akitutukana matusi na kuwafikisha polisi baadhi ya wafanya kazi akidai ni wezi bila kosa lolote na kwamba anajidai kuwa yeye yu pamoja na viongozi wakubwa hivyo hakuna watakachokifanya juu yake” alisema mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo .

“Tunaomba mtufikishie malalamiko yetu kwa viongozi wa juu ili watambue kwamba sisi watanzania bado ni watumwa licha ya kuwa kuwa kwenye nchi yetu na mtu mmoja tu Bw.Badri Dart” alisema mfanyakazi mwingine.

“Ikiwa huyu kiongozi ataondoka ni ukweli kwamba hili shirika litatengamaa ndani na nje ya shirika hili maana hata wanachi wanamlalamikia yeye tu.aliongeza mfanya kazi mwingine.

Hata hivyo Bw.Badri Darft alipotakiwa kujibu shutuma hizo alikana kuhusiana na shutuma hizo kwa kudai kuwa ni za uongo.

Alisema kuwa yeye amekuwa akifuata sheria za shirika na kwamba yeye ni mfuatiliaji sana wa mambo ya kampuni na kudai kuwa hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchukiwa na wafanyakazi na hata wananchi wa nje.

Hata hivyo Bw.Badri alikili kuwafikisha baadhi ya wafanya kazi katika vyombo vya sheria kwa madai ya wizi ingawa alisema kuna wengine kesi zao walishinda na wengine shirika lilishinda huku akisema wengine zinaishia juju tu.

“Asili ya watu wa kapunga ni wezi ingawa wengine wanatushinda kesi na wengine tumeshinda kesi mahakamani ila wengine kesi zao zinaishia juju tu” alisema Bw.. Ba.Badri

Akizungumzia kutumia uhusiano wake na viongozi wakubwa kuwanyanyasa wananchi pamoja na wafanyakazi wake alisema hiyo si kweli isipokuwa viongozi wameomba mashamba katika shirika lao na kudai wapo pale kama watu wakawaida na si kama mtumishi wa serikali hiyo hizo shutuma ni za uzushi.

Hata hivyo alikili kuwepo viongozi wakubwa katika mashamba hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Jaji Mkuu wa Mkoa maAfisa wa TRA pamoja na Askali 6 ambao wamepewa mashamba katika shirika hilo .

Awali alikana kuwepo na uhusiano wa karibu na kiongozi aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel lakini baada ya kubanwa na maswali alikili kuwepo na uhusiano na mtu huyo na kudai kuwa ni rafiki yake na baadaye kuwa ni Bwana shamba.

Mwisho.
amekuwa akizua mitafaruku mbali mbali ikiwemo ya wakazi wa Mapogoro hasa jamii ya wasukuma ambao walidai walipokonywa mashamba mlefu hatujawahi kuambiwa na mtu yeyote maneno watumwa kwa kweli haiwezekani mtu mmoja akaivuruga kampuni kwa mitafaruku na wananchi, kwanini viongozi wengine wasishutumiwe? Alisema kijana wa kimasai.

April 28, 2010

MTANDAO IRINGA NI TABU TUPU!!!!?

Hali ya huduma ya mawasiliano ya Internet katika mikoa ya nyanda za juu kusini ukiwemo mkoa wa Iringa kwa zaidi ya siku nne sasa huduma hiyo imeendelea kusumbua huku watumiaji wa huduma ya Internet wakiendelea kupata shida kubwa.

Bado hakuna taarifa zozote za huduma hiyo kusumbua na jitihada za mtandao huu kumtafuta waziri mwenye dhamana ya mawasiliano zinafanyika ili kupata jibu sahihi.

April 26, 2010

KIJANA AUWAWA KINYAMA IRANGA NA KUTOLEWA NYETI ZAKE

WATU wasiofahamika wamemuua kinyama kijana mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana mara moja na kumnyofoa sehemu zake za siri .

Tukio hilo ambalo ni la kwanza na la aina yake kutokea mjini Iringa limetokea katika eneo la darajani jirani na chuo kikuu cha Tumaini mjini Iringa leo majira ya asubuhi .

Wakizungumza na mtandao huu eneo la tukio wakazi wa eneo hilo Jackson Sanga,Sara John na Juma Saimon walisema kuwa mwili wa kijana huyo anayekadiriwa kuwa ni miaka kati ya 35 na 40 ulikutwa jirani na daraja la korongo la kuvuka kwenda chuo kikuu cha Tumaini na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Alisema Sanga kuwa mwili wa kijana huyo ulikutwa ukiwa na majeraha katika maeneo mbali mbali hali ambayo inaonyesha kuwa kabla ya kuuwawa kwake alikuwa amekatwa na kitu chenye ncha kali kama mapanga hivi.

"Huu ni unyama wa kutisha ambao umepata kutokea katika eneo hili ...kwani inaonyesha wazi wauwaji wamefanya hivi kwa imani za kishirikina na ndio maana wameweza kuondoka na sehemu zake za siri"

Hata hivyo alisema kuwa wapo baadhi ya majirani wa eneo hilo ambao walidai kusikia kelele za mtu huyo akiomba msaada kwa kupiga yowe kubwa baada ya kuvamiwa na wauwaji hao ila hakuna mtu aliyejaribu kutoka huku baadhi yao wakidhani ni wanafunzi wanatoka kutazama mpira .

Kwa upande wake Sarah alisema kuwa unyama huo unaonyesha kufanywa na vibaka ambao wamekuwa wakijificha katika maeneo hayo ya chuo kwa lengo la kuvizia wanafunzi ili kuwapora .

Kwani alisema kuwa kawaida vibaka wamekuwa na kawaida ya kuvizia wanafunzi katika daraja hilo na maeneo mengine yanyozunguka chuo hicho ambayo ya giza nene kwa lengo la kuwapora fedha wanafunzi hao hasa wale wanaoishi nje ya chuo hicho.

Hata hivyo alilipongeza jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kufika eneo la tukio mapema zaidi baada ya kupigiwa simu na wananchi kuhusiana na tukio hilo na kuomba ulinzi zaidi katika maeneo hayo ya chuo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari polisi wa kituo cha kati wakiuchukua mwili wa kijana huyo na kuupeleka katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya utambuzi zaidi.

Huku kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evalist Mangalla baada ya kupigiwa simu na mwandishi wa habari hizi alikiri kupokea taarifa za kifo hicho na japo bado uchunguzi unaendelea ili kujua sababu ya kuuwawa kwake na watu waliohusika katika mauwaji hayo.

NB. Mpenzi mdau wa mtandau huu napenda kukuomba radhi kwa kushindwa kukupatia matukio zaidi katika mtandao huu kama ulivyozoea kutoka na matatizo la mawasiliano ambayo yamepata kujitokeza ndani ya mkoa wa Iringa kwa zaidi ya wiki moja sasa ,hivyo nimekuwa nikishindwa hata kuweka picha kutokana na matatizo hayo

April 24, 2010

RADIO EBONY FM YAANDIKA HISTORIA YA SOKA IRINGA,YAICHAPA TATU BILA D.S.J

Timu ya Radio Ebony FM Iringa leo imeandika historia ya mwaka katika mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari kutoka Dar (D.S.J) baada ya kuichapa kwa jumla ya magoli 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Chuo cha ualimu Kreluu na kuvunja recodi ya kuwa na mashabiki wengi tofauti na michezo mingine iliyopatwa kufanyika ndani ya mkoa wa Iringa.


Pamoja na jitihada za D.S.J kutaka kusawazisha mabao hayo bado wachezaji wa radio Ebony FM walionekana kukazi buti na kupelekea timu hiyo ya DSJ kunyosha mikono na kukubali kichapo hicho .


Timu hiyo ya radio Ebony Fm kwa sasa inajiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa mei mosi mwaka huu kati yake ya timu ya watuma salam mchezo utakaopigwa mjini Mafinga ,mchezo ambao ushindi ni mkubwa zaidi kwa Radio Ebony japo mpira unadunda na dakika 90 jibu litapatikana.

April 23, 2010

TIMU YA EBONY FM ;TUPO KAMILI KUIVAA DSJ KESHO

Baadhi ya wachezaji wa Radio Ebony FM Iringa watakaocheza na timu ya DSJ kesho katika uwanja wa chuo cha ualimu Kreluu mchezo wa kirafiki
Tupo safi kikweli

MKUU WA WILAYA IRINGA AMFIKISHA POLISI MTENDAJI ALIYEGAWA MBOLEA KWA MAREHEMU........
Mjane wa marehemu Yohana Mtweve akionyesha kaburi la mumewe ambalo linadaiwa kupewa vocha za mbolea ya ruzuku
Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin akitoa zawadi ya kanga kwa mjane huyo baada ya kuonyeshwa kaburi
Mtangaji wa Radio Ebony Fm Julian akifanya mahojiano na mtendaji wa kijiji cha Kibena Laurent Kidava anayetuhumiwa kugawa mbolea kwa marehemuHili ni kaburi la marehemu nikionyeshwaGari la mkuu wa wilaya ya Iringa likimshusha mtendaji huyo polisi kwa tuhuma za wizi wa mbolea ya ruzukuHapa mtendaji huyo akinipa kitabu cha wageni kabla ya kuanza mahojiano

Soma gazeti la Tanzania Daima Jumapili kwa undani wa sakata hili ama gazeti la Msemakweli pia katika mtandau huu jumapili

BENKI YA NBC IRINGA CHUPU CHUPU KUTEKETEA KWA MOTO.......................


Askari wakiwa wameweka ulinzi mkali katika benki ya NBC tawi la Iringa mapema leo wakati moto ulipozuka ghafla kutoka chumba kimoja wapo cha jengo hilo eneo la Mshindo


Ulinzi mkali wawekwa barabara yafungwa kwa muda
Jitihada za zimamoto zimeweza kuokoa benki hiyo isiteketee kwa moto

Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa japo hasara zilizojitokeza dhamani yake bado kufahamika habari zaidi soma gazeti la Tanzania daima kesho au Bofya hapa

April 20, 2010

MWANAMKE SHUJAA AIBUKA IRINGA.......


Mwanamke shujaa mkazi wa mjini Iringa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amemthibiti kikamilifu kijana anayedaiwa kuwa ni kibaka baada ya kumwimbia mashine ya kusagia nyama nyumbani kwake na kukimbia ,mwanamke huyu aliweza kupambana na kibaka huyo katika eneo la uhindini mjini hapa jana na kumpeleka yeye mwenyewe kituo cha polisi kama alivyo kutwa na camera na mtandao huu.

Ni Kama sinema na kama wanaongea vile ;Mwanamke :Hata huna ujanja tutafika popote kibaka mkubwa wewe unanikimbia mimi sio?


Kibaka: samahani mama mwanajeshi naomba nifunge mkanda vizuri

Mwanamke: wewe funga ila sikuachii hapa
Mwanamke: Ukijua unavyonikwaza sijui nianza kukutandika vichwa ama kukuchapa mateke ?

Kibaka: Samahani mama sikujua kama ile mashine ni yako mbona nisinge jaribu kuiba kama kazi yenyewe ndio hii ,ila mama nini swali


Mwanamke: We Uliza ila lazima utafika


Kibaka: wewe ni mwanajeshi


Mwanamke: utajua kama ni mwanajeshi ama polisi tukifika mbele ya safariKibaka: sasa huku tunakwenda wapi

Mwanamke: utajua mbele ya safari kanyaga twende kibaka mkubwa wewe !!!.Mwanamke: kaza mwendo twende mbele ya sheria

Kibaka: Leo kazi ipo na hivi sina mazoezi ya kutosha nikitoka hapa wizi basiMwanamke: Hapa ndio sahizi yako mpenda kula bila kufanya kazi wewe.


Kibaka: Mungu mkubwa nimefika salama bila kuchomwa moto.
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unatoa pongezi nyingi kwa mwana mke huyu kwa jitihada zake za kupambana na vitendo vya uharifu na waharifu ndani ya manispaa ya Iringa na kutokana na ujasiri huu mkubwa mimi kama mmiliki wa mtandao huu najitolea zawadi ya fedha kiasi cha shilingi 10,000 kwake kwa kazi nzuri aliyoifanya hivyo anaweza kuwasiliana na mmiliki wa mtandao huu wa simu 0754 026 299 ama kufika kituo cha radio Ebony Fm

April 19, 2010

WANANCHI MAFINGA WALIPIA VIWANJA HEWA ......


hii ni Risti niliyolipia kiwanja toka mwaka 2007 bila kupewa.

WANANCHI zaidi ya 500 katika mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamedai Halmashauri yao ilitumia jina la Rais Jakaya Kikwete kutapeliwa fedha zao za viwanja walivyo lipia toka mwaka 2006 na 2007 katika halmashauri ya wilaya hiyo kitengo cha ardhi bila kuonyeshwa viwanja husika .
Katika uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa kushirikiana na kipindi cha Morning Talk cha Radio Ebony Fm ,umebaini kuwepo kwa madai hayo ambayo yamepelekea wananchi hao kumwomba Rais Kikwete kuwasaidia kupata haki yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wananchi hao akiwemo Janeth Mtagawa , Salum Kalinga na mjane Anna Sanga walisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo ulitangaza zoezi la upimaji wa viwanja kwa gharama nafuu kwa wakazi wa mji huo kwa zaidi ya miaka miwili sasa wamelipia zoezi hilo ila hakuna kiwanja wanachopimiwa.Utaisoma habari hii katika gazeti la Tanzania Daima ama sikiliza Radio Ebony Fm AU BOFYA HAPA

April 18, 2010

WAGOMBEA WA CCM JIMBO LA IRINGA MJINI WAANZA KAMPENI KUGAWA POSHO

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akiteta jambo la mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa


Wana CCM wakiwa katika maandamano hivi karibuni mjini Iringa


KIVUMBI cha kinyang'anyiro cha ubunge ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) katika jimbo la Iringa mjini mkoani hapa kimezidi kutimuka huku wagombea hao wa nafasi za ubunge wakizunguka nyumba kwa nyumba kuhonga zawadi mbali mbali kwa wajumbe ikiwemo ya fedha kiasi cha shilingi 2000 kwa kila mjumbe huku chama cha demokrasia na maendeleo (chadema ) wilaya ya Iringa mjini kikilalamikia hali hiyo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwepo kwa mbinu hiyo chafu ndani ya CCM huku wagombea hao wanaotaka kuchukua nafasi hiyo ya mbunge aliyepo madarakani Monica Mbega wakizunguka kuwarubuni wana CCM kwa kuhonga posho ya shilingi 2000 hadi 10,000 kwa wapiga kura posho inayodaiwa kuwa ni ahsante kwa kunisikiliza.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wana CCM ambao hata hivyo hawakupenda kutaja majina yao ,walidai kuwa wagombea hao wa nafasi za ubunge wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya makatibu kata wa CCM kuzunguka nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuwanadi wagombea wao huku wakiwa na zawadi hizo .
Hata hivyo walisema mbali ya kupewa fedha katika bahasha na zawadi mbali mbali kama kanga na mchele na mafuta na kula bado baadhi ya wagombea wamekuwa wakitoa ahadi ya kuwanunulia wajumbe hao simu na usafiri wa pikipiki na baiskeli iwapo watafanikiwa kushinda nafasi za ubunge .
"Hadi sasa wagombea katika jimbo hili la Iringa mjini wapo zaidi ya 5 ambao wanajulikana na kila mmoja amekuja na mbinu yake ya kushawishi wapiga kura ...lakini sisi tumekuwa tukipokea kwani kama ni rushwa mbona watu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wapo hapa hapa mjini na haya mambo wanaona" alihoji mmoja kati ya makada wa CCM mjini hapa.
Pia alisema wapo baadhi ya viongozi wa jumuiya za chama ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinadi kwa wapiga kura na hata kuwatumia viongozi wa jumuiya na chama kuzunguka mitaani kugawa posho kwa wajumbe.
Alisema kuwa kutokana na uwezo wa kiuchumi kwa wagombea hao kutofautiana wapo wanaoweza kushindwa nafasi hiyo kutokana na kutoa posho ndogo kwa wajumbe na wapo watakaopata kutokana na kugawa posho kubwa.
Pia alisema kutokana na mbinu hiyo inayotumiwa na wana CCM wanaotaka ubunge katika jimbo hilo upo uwezekano mkubwa wa wananchi wa jimbo hilo kununuliwa kwa fedha na kuishia kumpata mbunge asiyefaa.
Kwani alisema kuwa katika jimbo la Iringa mjini lenye wagombea zaidi ya watano wana CCM wenye upinzani mkubwa ni pamoja na katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela,Jescra Msambatavangu na Thomas Kimata
Japo wapo wagombea wengine ambao hawavumi lakini wamo kuwa ni pamoja na diwani wa kata ya Gangilonga Edwin Sambala, Zuberi Mwachula, Ben Mpete na mweenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Iringa Fadhil Ngajilo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akielezea kuhusiana na madai hayo ya wagombea kuanza mbinu ya kugawa posho kwa wajumbe ,alisema kuwa kwa upande wake amekuwa akisikia madai hayo japo hana uhakika nayo na kuwa iwapo itabainika kuwa yupo mgombea anayehonga wajumbe atapoteza sifa ya kuwa mgombea.
Hata hivyo aliwataka makatibu kata wa CCM kuepuka kujiingiza katika upambe kwa mgombea mmoja mmoja kwani wagombea wote ndani ya chama ni safi na wanapaswa kupewa nafasi sawa ya utambulisho kwa wajumbe muda wa kufanya hivyo utakapofika.
Kiponza alisema chama kimeruhusu wanachama wake kutangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali ila bado hakijaruhusu kampeni kwa wanachama wake na kuwa ni vyema taratibu ziheshimike.
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa wana CCM wanatumia fedha zao kutaka kuwanunua wapiga kura na kuomba Takukuru kuamka ili kupambana na wagombea watoa rushwa katika nafasi za uongozi.
Msigwa alisema kutokana na kasi iliyopo sasa ndani ya CCM inaonyesha wazi kampeni za uchaguzi mkuu ndani ya CCM zimeanza kama ya tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza rasmi kuanza kwa kampeni hizo.
Hivyo alisema iwapo NEC itanyamaza kimya na Takukuru kushindwa kuwashughulikia wana CCM wanaotumia pesa kutafuta nafasi za ubunge na udiwani upo uwezekano mkubwa wa uchaguzi mkuu kuvurugwa na wana CCM hao.
Habari hii imechapwa katika gazeti la Tanzania Daima leo Jumapili

MENEJA WA MRADI WA MAJI AJINYONGA HADI KUFA BAADA YA KUIBIWA NG'OMBE WAKE ....


MENEJA wa mradi wa maji katika kijiji cha Usolanga kata ya Malenga makali wilaya ya Iringa vijijini Alex Mhanga amejiua kwa kujinyonga kwa kamba baada ya kuibiwa ng'ombe wake watatu wa rafiki yake.

Imeelezwa kuwa meneja huyo alifikia uamuzi huo wa kujiua kwakujinyonga ikiwa ni siku moja toka watu wanaosadikika kuwa na wezi kuvunja zizi la ng'ombe na kuiba ng'ombe zaidi ya watatu waliokuwemo katika zizi hilo wakiwemo ng'ombe watatu ambao ambao ambao si wake .

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo Yohana Kalinga alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya asubuhi .

Alisema kuwa kabla ya kujinyonga marehemu huyo alikuwa akituhumiwa kufanya njama na wezi ili kuiba ng'ombea hao hali iliyopekea kuamua kujiua kama njia ya kukwepa fedheha.
Diwani wa kata ya Malenga mangali Franziscar Kalinga amethibitisha kifo cha meneja huyo na kuwa mazishi yake yamefanyika kijijini kwake Ilula juzi jumamosi .

Diwani kalinga alisema kuwa meneja huyo alikutwa na wananchi wa kijiji hicho akiwa amejinyonga huku kukiwa hakuna hata maandishi yoyote ambayo aliacha kuelezea sababu ya kuchukua uamuzi huo mzito.

"Hata sisi tumechanganyikiwa sana na uamuzi wa meneja wetu wa kuamua kujinyonga .....ni kweli marehemu alikuwa akijishughulisha na ufungaji ikiwa ni pamoja na kumsaidia rafiki yake kuhifadhi ng'ombe wake "

Hata hivyo alisema hana hakika kama kweli marehemu huyo alikuwa ameshirikiana na wezi kuiba ng'ombe hao.
Kwani alisema suala la wizi wa ng'ombe katika tarafa hiyo ya Isimani limekuwa kubwa na kuwa wengi wamekuwa wakiibiwa mifugo yao.

Alisema tatizo kubwa la wananchi kuibiwa mifugo yao linasababishwa na tishio la njaa katika kata hiyo ya Malenga Makali na tarafa nzima ya Ismani ambapo hali ya mazao si nzuri na hivyo baadhi ya watu wameendelea kufanya vitendo vya wizi wa mifugo kama njia ya kujipatia mahitaji yao.

Jeshi la polisi mkoani Iringa limethibitisha kutokea kwa kifo hicho .

TIMU YA RADIO EBONY FM YAANZA KUITAFUTIA MAKALI DSJ

Raymond Francis
Francis Godwin
Hosten kushoto akitoa pande kwa Raymond huku George akijiandaa kupokea
Housten :"Kiukweli hapa nimejipiga chenga mwenyewe hadi nimesahau mpira nyuma"

Mwalubadu akisakata soka

Mazoezi ya uzeeni haya ,hapa naweza kusema ng'ombe hanenepi siku ya mnada
Juliani akikokota kabumbu

Mwalubadu (kulia) akimilikia mpira


KIKOSI cha timu ya Radio Ebony Fm Iringa kimeanza maandalizi makubwa ya mchezo wake wa kirafiki kati ya timu ya chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) pamoja na mashindano ya kombe la Mei Mosi mkoani hapa .
Akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu wa timu katibu msaidizi Bahati Alex alisema kuwa timu hiyo imeanza maandalizi yake mapema ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya michezo miwili ya kirafiki pamoja na mchezo mmoja wa kuwania kombe la mei mosi mkoa wa Iringa.
Alex alisema kuwa DSJ wapo mbioni kuja mkoani Iringa kwa ziara ya kimasomo na katika ziara yao katika kituo hicho cha Radio pia watapata kuchezo mchezo mmoja wa kirafiki kama njia ya kudumisha mahusiano zaidi .
Hivyo mbali ya kuwapongeza wanafunzi hao wa chuo hicho cha habari kwa kufanya ziara ndani ya mkoa wa Iringa bado alisema uamuzi wao wa kuomba mchezo wa kirafiki ni moja ya changamoto kubwa kwa wadau wa soka ndani ya mkoa katika kufufua soka la Iringa.
Hata hivyo alisema pamoja na mchezo huo kati ya Radio Ebony Fm na DSJ pia alisema mchezo mwingine kama huo wa kirafiki utachezwa mjini Mafinga na timu ya watuma salam mkoa wa Iringa.
Alisema baada ya michezo hiyo miwili kikosi chake kitaendelea na mazoezi ya kawaida kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Mei mosi mkoa wa Iringa.
Pamoja kuwataka wadau wa soka ndani ya mkoa kuendelea kuelekeza nguvu zao kwa timu changa ili kama njia ya kuibua vipaji vya wachezaji bado alisema kuwa moja kati ya mikakati ya timu hiyo ni kuendelea kuhamasisha soka zaidi ndani ya mkoa .
Alex alisema kuwa kwa upande wa kikosi chake maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya michezo hiyo miwili ya kirafiki na kuwa hivi sasa kikosi hicho kimekuwa kikijinoa katika uwanja wa chuo cha ualimu Mkwawa mjini hapa.
Habari hii itachapwa katika gazeti la Sayari na Tanzania Daima

April 16, 2010

WAZIRI WASIRA UPO? MAREHEMU IRINGA WAGAWIWA MBOLEA YA RUZUKU ...


Kulia ni WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira huku kushoto na baadhi ya waombolezaji wakielekea kuzika , soma habari kamili ya marehemu Iringa kugawiwa mbolea ya ruzuku ya serikali hapa

KIPINDI CHA MORNING TALK RADIO EBONY FM CHAZIDI KUIBUA MENGI

Bw Raymond Francis akiwa katika kipindi hicho kinachoibua kero za wananchi na kufanya radio Ebony Fm kupendwa zaidiMmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin (mwenye koti jeusi) akiwa katika moja kati ya vipindi vya morning Talk

WAZEE IRINGA WAJIUNGA KATKA CHAMA CHA OMBA OMBA"Big Up RC Iringa ingekuwa Dar tusinge jaribu kukaa hapa"


Mmoja kata ya wasamaria wema katika mji wa Iringa akitoa msaada kwa wazee ambao wamekuwa wakikusanyika katika nyumba za wahindi na waharabu pamoja na maduka ya wafanyabiashara wakibongo kwa ajili ya kuomba misaada mbali mbali zikiwemo fedha wazee hawa wameunda umoja wao usio rasmi wa kuzunguka mitaani kuomba hasa siku za ijumaa japo kwa mikoa mingine wamekuwa wakipigwa vita vikali na serikali kwa Iringa hakuna noma

WANANCHI ILULA WAFANYA HUJUMA YA MRADI WA MAJI ILI KUPATA PESA ....


Wizi wa maji yazidi Ilula hapa wanawake hawa wakiwa wamekata bomba la maji kwa ajili ya kupata huduma hiyo nyeti


Mtangazaji maarufu wa kituo cha Radio Ebony Fm Bw Raymond Francis (kulia) akiwa ameongozana na wakazi wa kijiji cha Ilula baada ya kumaliza kipindi cha Morning Talk kuhusu kero ya maji katika mji wa Ilula
Wananchi wa mji wa Ilula wilaya ya Kilolo wakiendelea kuchota maji katika bomba la maji ambalo wamelikata ili kujipatia fedha za matumizi kwa kuuza maji kwa wananchi waliombali na mradi huo kama walivyokutwa na camera ya mtandao huu hapa ni mtaa wa Nyakalomo

April 15, 2010

USIKOSE KUSOMA MKASA MZIMA WA KIFO CHA KINYAMA CHA GA-BAKAMA NDANI YA MSEMAKWELI JUMAPILI HII


MTAMBUE mwalimu maarufu wa kwaya katika kanisa la Sabato na mkuu wa shule ya sekondari Mwembetoga mjini Iringa na kada wa CCM marehemu Zacharia Ga-Bakama anayedaiwa kuuwawa kikatili akiwa amelala na mkewe Oliver Chengulla .

Upo usemi unatumika na wengi japo si rasimi ila umepewa nafasi kubwa zaidi usemi huo ni ule wa ndoa ndoano usemi huu umekuwa ukitumiwa zaidi katika mitafaruku ya ndoa lakini umekuwa haupewi nguvu za kutosha katika kuutetea ama kuupinga japo ukisoma kisa hiki waweza kubani kuwa kweli ndoa ni ndoano.

Amini usiamini watu waliopo katika ndoa baadhi yao wamekuwa wakitaka kutoka katika ndoa na wale ambao hawapo katika ndoa wamekuwa wakipigania kuingia katika ndoa tena kwa gharama kubwa,undani zaidi ni katika gazeti la Msemakweli jumapili na katika mtandao ya mtandao wa
www.matukiodaima.blogspot.com

April 13, 2010

NASHUKURU KWA KUMZIKA BABA YANGU ,NIMEMALIZA MSIBA SALAMA

Mwonekano wa mji wa Iringa ukiwa katika jiwe la NgangilongaMpendwa mdau wa mtandao huu kwa niaba yangu mwenye mimi Francis Godwin na familia nzima ya mzee Godwin Sibonike Malila wa Soweto jijini Mbeya ,ninapenda kuwashukuru wote walioshiriki nasi kwa namna moja ama nyingine katika mazishi ya baba yangu mpendwa.
Binafsi naamini kabisa pamoja na kuwa msiba huu ulikuwa ukinihusu mimi ila nyuma yangu kulikuwa na wadau wengi ambao kufiwa kwangu kuliweza kupelekea wadau kukosa haki yao ya msingi ya kupata matukio mapya.
Pia naamini kabisa wengi walipenda kushiriki nami katika mazishi na hata maombolezo ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao ikiwemo ya kuishi mbali ya mkoa wa Mbeya ama Iringa wengi walishindwa kufika hata baadhi yao kuishia kutuma salam zao za pole kwa njia ya mtandao na sms katika simu yangu kwa umoja wenu nasema ahsante sana naamini wote tuliungana katika kipindi kifupi cha maombolezo na Mungu awabariki zaidi.

April 10, 2010

SAFARI YA MWISHO YA BABA YANGU MZEE GODWIN SIBONIKE MALILA

Taarifa kwa wadau .
Mimi Francis Godwin kwa niaba ya familia ya mzee Godwin Sibonike Malila wa Soweto Mbeya ninasikitika kutangaza kifo cha baba yangu mdogo mzee Godwin Sibonike Malila (Pichani) kilichotokea tarehe 8 mwezi huu wa nne katika jijini Mbeya.

Habari ziwafikie kaka wa marehemu Bw Kenani Kazimoto Ngao wa Makete Iringa na Ally Kikombe wa Sumbawanga Rukwa
Mdogo wa marehemu LUvoneko Siwonike wa Sumbawanga Rukwa na Enock Malila wa Chunya Mbeya.

Shemeji wa marehemu Mh.Wiliam Lukuvi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na mbunge wa jimbo la Ismani Iringa ,Wadau wenzangu wote katika tasnia hii ya habari pamoja na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.

Mazishi yanataraji kufanyika leo tarehe 10.4.2010 majira ya saa saba mchana katika makaburi ya sabasaba jijini Mbeya.

Kwa pamoja tunaamini kabisa Mungu ni muweza wa mambo yate pamoja na sisi kumpenda zaidi baba yetu mpendwa Mungu yeye kampenda zaidi yetu hivyo hatuna budi kusema jina la Bwana na libariiwe daima.
AMINA.

NB. Mpendwa mdau wa mtandao huu kutokana msiba huu napenda kukuomba uvumilivu wako kwa muda wa siku nne kuanzia leo mtandao huu na ule wa http://www.matukiodaima.blogspot.com/ hakuta kuwa na tukio lolote jipya kwani nitakuwepo katika maombolezo .nashukuru kwa ushirikiano wako.Bofya hapa

April 8, 2010

MBOLE YA RUZUKU YADAIWA KUHUJUMIWA

Pamoja na serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete kupania kwa nguvu zote kuboresha kilimo kwanza kwa kugawa pembejeo za ruzuku kwa wakulima mpango huo wadaiwa kuhujumiwa katika kijiji cha Kibena Iringa vijijini. Baadhi ya wakulima waliokuwepo katika mpango huo wa kupewa pembejeo na kukosa baada ya pembejeo zao kutolewa kwa watu walio kufa wamefichua siri ktk mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa wahusika wa hujuma hiyo ni viongozi wa serikali ya kijiji. Katika hali ya kusaka ukweli wa kero hiyo mtandao huu na radio ebony Fm kupitia kipindi cha Morning Talk leo asubuhi kuwakutanisha viongozi wa serikali ya kijiji na wananchi ktk mkutano wa hadhara utakao rushwa Live na Radio Ebony Fm

STAR COM -KITONGA YAJITOKEZA KUONGEZA NGUVU MISS VODA COM IRINGA


MAANDALIZI ya kumsaka Miss Voda com 2010 mkoani Iringa yamvutia mkurugenzi wa hoteli ya Star Com kitonga kujitokeza kuongeza nguvu ya udhamini katika mashindano hayo mwaka huu.

Mratibu mkuu wa mashindano hayo kutoka Radio Ebony Fm Edo Bashir alisema kuwa kasi ya udhamini kwa mwaka huu inaonekana kuwa kubwa zaidi kuliko mwaka jana na kuwa hadi sasa wadau mbali mbali wa urembo ndani na nje ya mkoa wa Iringa wamejitokeza kuomba kudhamini shindano hilo .

Bashir alisema kwa mara ya kwanza uongozi wa Hoteli Star Com Kitonga mkoani Iringa wamekuwa wadhamini wa kwanza kutoka mkoa wa Iringa kujitokeza kudhamini mashindano hayo mwaka huu jambo ambalo ni mafanikio makubwa katika tasnia ya urembo mkoani hapa.

Mratibu huyo alisema kuwa mbali ya Voda com ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo ,wadhamini wengine ni BTL kupitia kinywaji cha Reds na hoteli hiyo ya Star Com Kitonga na kuwa majina ya wadhamini wengine wanaendelea kuyafanyia kazi .

Hata hivyo alisema zoezi la utoaji fomu kwa washiriki wa taji la urembo ndani ya mkoa wa Iringa limeanza na kuwa hadi sasa jumla ya warembo 7 wamejitokeza kuchukua fomu.

Bashir alisema kuwa katika kuhakikisha idadi ya washiriki wa taji la urembo ndani ya mkoa wa Iringa inaongezeka zaidi fomu zimekuwa zikitolewa bure kwa washiriki wote ambao wataingia kambini hivi karibuni .

Mratibu huyo alisema kuwa wamelazimika kutoa bure fomu hizo kwa washiriki ili kuwawezesha warembo wote kushiriki bila kuwepo pingamizi lolote la kiuchumi katika ushiriki wao.

Alisema kuwa shindano ya kumsaka Miss Voda Com Iringa 2010 litafanyika mei 21 mwaka huu katika ukumbi wa St.Dominic mjini Iringa.

BASI LA VITU LAINI LAPATA AJALI LAUA IRINGA


Basi la kampuni ya vitu laini (pichani )lililokuwa likitoka Lulanzi wilaya ya Kilolo kuja mjini Iringa limepinduka katika eneo la Tagamenda mpakani mwa wilaya ya Kilolo na Manispaa ya Iringa na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 10
Ajali hii imetokea majira ya saa mbili asubuhi undani halisi wa tukio hili utaupata hivi punde ama katika gazeti la Tanzania daima kesho Ijumaa

April 7, 2010

BARABARA ZA MITAA NA STENDI YA MJI WA MAFINGA NI KITUKO

Wananchi wa mji wa Mafinga katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wanahoji sababu ya uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo na uongozi wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa (Tanroads) kuchelewa kutekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuweka lami baadhi ya barabara katika mji wa Mafinga .

Wakazi hao wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa Rais Kikwete alipata kuwaahidi kutatua kero ya ubovu wa barabara za mji huo ila katika hali ya kustaajabisha ahadi hiyo ilielekezwa katika barabara ya kwenda Ikulu ndogo ya mkuu wa wilaya na ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo jambo ambalo wamemwomba mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz kuingilia kati suala hilo .

Pia wameeleza kusikitishwa na ubovu wa barabara za mitaa yote ya mji wa Mafinga ambao upo chini ya mbunge mkongwe kuliko wote katika bunge la Tanzania Mh.Joseph James Mungai na kuwa mbaya zaidi hadi barabara za kwenda nyumbani kwa mbunge huyo ni mbovu kuliko na zinafananishwa na mbavu za mbwa .

Mkazi wa mji wa Mafinga John Kalinga alisema mbali ya kero hiyo kero nyingine ubovu wa stendi ambao umepelekea mabasi makubwa kususia kuingia katika stendi hiyo kwa hofu ya kuvunja springi za mabasi hayo kutokana na stendi kuwa na mashimo.

Kutokana na kero hizo kwa wakazi wa mji wa Mafinga mtandao huu kwa kushirikiana na kipindi cha Morning Talk cha Radio Ebony Fm kesho (alhamisi ) kukutana na wananchi wa mji wa Mafinga katika stendi hiyo na eneo la soko kuu na maeneo mengine ambayo yanakabiliwa na kero ili kupokea kero za wananchi na kupata majibu ya viongozi

April 6, 2010

KIFO CHA MKUU WA SEKONDARI YA MWEMBETOGWA (1)Marehemu Zachalia Gabakama

Afisa utamaduni manispaa ya Iringa Sophia Sarehe akiwa ameshika tama wakati wa kuaga mwili wa mkuu huyo wa shule

Afisa elimu mkoa wa Iringa Bw Salmu Maduhu akitoa heshima za mwishoKADA maarufu wa CCM na mkuu wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa ambaye inamilikiwa na jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Zacharia Gabakama amekutwa ameuwawa katika mazingira yenye utata mkubwa akiwa chumbani kwake na mkewe Oliver Chengula.


Imedaiwa kuwa marehemu wakati akiuwawa na watu hao wawili wasiojulikana kwa kupigwa na kitu kizito kichwani alikuwa amelala kitanda kimoja na mkewe chumbani kwake huku mwanamke huyo akiwa salama bila kupata misukosuko yeyote.

Ndugu wa karibu wakiwemo watoto wa marehemu huyo ambao walizungumza na mtandao huu walisema kuwa hata wao wanashindwa kujua mazingira halisi ya kifo hicho ambacho kinazua utata mwingi.

Kwani walisema wao walikuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo iliyopo eneo la Ilala mtaa wa Embakasy Inn ila jambo la kushangaza katika chumba alichokuwa amelala mlango ulikutwa umefungwa kwa ndani na geti la nyumba hiyo likiwa limefungwa kama lilivyofungwa wakati wa kwenda kulala juzi usiku.

Mtoto huyo wa marehemu Pisi Gabakama alisema kuwa kimsingi nyumba hiyo ina ulinzi wa kutosha na madirisha yote na milango imezungushiwa nondo na mlango ukifungwa hakuna mtu kutoka nje ambaye anaweza kuingia ndani ya nyumba hiyo.

"Kweli inashangaza sana kama mwandishi unavyoona hii milango hakuna hata moja uliovunjwa wala kuwepo alama yeyote inayoonyesha kuna mtu mgeni na nyumba hii ameingia...mbaya zaidi mama yetu mdogo ambaye alikuwa amelala na baba alikuwa chumbani na yeye ndie aliyetujulisha sisi kwa kupiga kelelea kuwa baba yetu ameuwawa na majambazi na yeye alikuwa amefungwa kamba ambayo kimsingi kama ilikuwa imeshikizwa tu"


Alisema mtoto huyo huku akibubujika machozi kuwa mtu wa kwanza kuingia chumbani kwa baba yao alikuwa ni mdogo wake na mama yao mdogo anayeitwa Aida Chengula ambaye kwa siku hiyo alikuwa amefika kuwasalimia na kulala hapo na yeye ndie anayedai kuwa alimfungua kamba dada yake huyo ambaye kwao ni mama yao mdogo.

Hata hivyo alisema mazingira ya kufungwa kamba hiyo na jinsi majambazi walivyoingia ndani ya nyumba hiyo ni utata mtupu na hivyo wao wanahisi kuwa mama yao mdogo na mdogo wake huyo wanaweza kulisaidia vizuri jeshi la polisi kujua mhusika halisi wa tukio hilo.

Kijana huyo alisema kutokana na uchunguzi wao na ule wa jeshi la polisi ambao walifika katika eneo la tukio wakiongozwa na mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa (RCO) Crausy Mwasyeba hakuna dalili zozote zilizoonyesha kuwepo kwa mtu kutoka nje ya nyumba hiyo kufanya mauwaji hayo.

Hata hivyo alisema mama yao mdogo ya saa 5 hivi usiku alitoka chumbani na kumfukuza mmoja kati ya wapangaji ambaye alikuwa akiendelea kukaanga samaki jirani na dirisha la chumba chao huku akimfokea kuwa atoke dirishani hapo wao wanataka kupumzika.


"Mama yetu mdogo alitoka akiwa mkali na kumfukuza mpangaji ambaye alikuwa akiandaa samaki kuwa anawachelewesha wao kulala ...ila baada ya kupita kama masaa kama matatu hivi tulishangaa tunaamushwa na dada yetu kuwa baba ameuwawa na majambazi "

Alisema kuwa baada ya wao kuingia chumbani kwa baba yao walimkuta akiendelea kukoroma kwa tabu huku akiwa amelala kitandani na mama yao akiwa amekaa pembeni baada ya kufunguliwa kamba na mdogo wake .

Kutokana na hali mbaya ambayo walimkuta naye baba yao walilazimika kukimbia hadi mjini eneo la stendi ya M.R. umbali wa kilomita zaidi ya 2 kutoka nyumbani kwao Ilala na kwenda kukodi Tax kwa ajili ya kumkimbiza hospitali ya mkoa kwa matibabu na baada ya kufika hospitali majira ya saa 8.45 hivi alikuwa tayari amekufa.

Pia alisema kabla ya kuuwawa baba yao alikuwa akimlalamikia mama yao mdogo kuhusu upotevu wa kadi ya benki (ATM) pamoja na bengi lake (Blockface) ambalo lilikuwa na nyaraka nyeti.

Alisema kuwa kimsingi baba yao ambaye ana watoto zaidi ya wanne kwa mwanamke huyo hakuna na mtoto hata mmoja kwani wameoana hivi karibuni baada ya kuishi bila mke kwa kitambo kirefu.

Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo John Sanga alisema kuwa kwa upande wake akikutana na mwalimu huyo majira ya saa 3 hivi usiku akipandisha mjini huku akiwa katika hali isiyo ya kawaida kama mtu mwenye mawazo mengi tofauti na siku siku zote.

"Tumekuwa na kawaida ya kutaniani sana na ile usiku nilijaribu kumtania kwa kumuita jina lake la utani la serikali ambalo alikuwa akipenda kujiita bado alionekana mwenye mawazo na kwa mbali sana baada ya kuulizwa wapi anakwenda usiku alisema anakwenda mjini na kuwa nyumbani kwake si kwake mjini ni kuzuri zaidi"

Diwani wa kata ya Ilala Grevas Ndaki akielezea juu ya kifo cha mkuu huyo na kada wa CCM alisema kuwa kifo chake kimeacha pengo kubwa katika shule hiyo pamoja na CCM kutokana na mchango wake mkubwa aliopata kuonyesha wakati wa uhai wake.

Ndaki alisema kuwa Gabakama alikuwa mkuu wa shule mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza shule hiyo ambayo kwa kipindi kifupi alichopata kuwepo kama mkuu wa shule shule hiyo imeweza kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kushika nafasi ya juu kitaifa ukilinganisha na shule za wazazi katika maeneo mengine.

Hata hivyo alisema kwa sasa wanaviachia vyombo vya dora kufanya kazi yake ili kujua mazingira na wahusika katika mauwaji hayo ambayo hata wao bado yanawachanganya zaidi.Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa mbali ya shule hiyo na familia kumpoteza mkuu huyo ila pengo lake ni kubwa ndani ya CCM kutokana na mchango wake mkubwa ambao amepata kuonyesha ndani ya chama.

Wadau wengine wa CCM walioonyesha kugushwa na mauwaji ya mkuu huyo wa shule ni pamoja na kamanda wa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Salim Asas,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Deo Sanga pamoja na mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa Zainabu Mwamwindi ambao walieleza kuwa kifo hicho kimewachanganya na kuwaacha katika maswali magumu yasiyo na majibu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla amethibitisha kuuwawa kwa mkuu huyo wa shule usikose kupata kisa hiki katika safu ya mikasa ya maisha gazeti la Msemakweli jumapili ijayo