Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 31, 2010

VIONGOZI CHAMA KIJIJI CHA NUNDWE MUFINDI WACHONGEWA KWA UFISADI

Undani wa sakata hili soma katika mtandao huu. www.matukiodaima.blospot.com

TRAFIC MAKAMBAKO WAWAKWAMISHA ABIRIA WA BASI LA SABCO TOKA RUVUMA KWENDA DAR ES SALAAM KUONDOKABasi la Sabco likiwa limetolewa namba zake na askari wa usalama barabarani Makamko kama njia ya kuzuiwa kuendelea na safari

Abiria akionyesha tiketi yake baada ya kukwama kuendelea na safari leo
Abiria wa basi la Sabco lenye namba za usajili T 418 ATH Scania waliokuwa wakitoka Ruvuma kwenda Dar es Salaam wakitazama basi hilo ambalo limetolewa namba zake kutokana na uchakavu wa taili kama zinavyoonekana hapo chini ,zoezi hilo la askari kutoa namba limefanyika asubuhi hii stendi ya Makambako Njombe ,SOMA HAPA

March 30, 2010

CCJ YAMTEKA MBUNGE WA CCM KISHAPU

CHAMA cha jamii (CCJ) kimeanza kukivuruga chama cha mapinduzi (CCM) baada ya kufanikiwa kumteka mbunge wa jimbo la Kishapu ambae ametangaza kujivua CCM na kujiunga na CCJ. Habari kamili kuhusu mbunge huyo wa kishapu soma gazeti la Tanzania Daima kesho jumatano

MGANGA WA JADI MWANDULAMI AMKOMBOA ALBINO KUUWAWA AELEZA KUSIKITISHWA NA WANAOUA MAALBINO


Festo kaduma ni mlemavu wa ngozi (Albino) ambaye amelazimika kuishi kwa mganga wa kienyeji Dr Antony Mwandulami ili kuyanusuru maisha yake kwa zaidi ya miezi mitatu .


Tanzania ilitoa tamko kali na kwa uwazi kabisa ikisema, “ Dhambi ya ubaguzi bado inaitafuna Afrika kusini.” Nikaanza kuangalia mambo mengine ninayoyashuhudia kila kukicha huku Marekani. Mtu akifanyiwa kitendo fulani, kwa mfano, ikiwa ni mweupe kakifanya, hukimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi.

Sasa mimi najiuliza. Je endapo Mtanzania mweusi mmoja ataenda nchi yoyote ya Magharibi kama vile kusoma au kufanya kazi halafu akauliwa na kunyofolewa viungo kama wanavyofanyiwa Albino, Tanzania itasemaje? Haina ubishi , kila mtu atasema “amebaguliwa na kuuwawa kutokana na rangi yake.” Swali langu la msingi ni hili:

Kitendo cha Albino kunyofolewa viungo vyake kinyama na hatimaye kuuawa na mtu mwenye rangi nyeusi kisa rangi yake ni tofauti na cha mtanzania mweusi aliyebaguliwa na kuuawa ugenini hususani katika nchi za magharibi? Kwa nini mauwaji ya Albino yasitajwe kama ubaguzi wa rangi? Maana Albino naye hutambuliwa kwa rangi yake! Kama tumefikia hatua ya kuuana kutokana na rangi zetu; moja nyeusi, nyingine ya rangirangi ( coloured ) na wote ni binadamu tena watanzania, tunaelekea wapi ndungu zangu?Serikali ya Tanzaia inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupambana na janga hili la mauaji ya albino.

Uamuzi wa kugawa simu kwa albino wote, pengine waweza kusaidia kwa kuwawezesha kupiga simu polisi wanapovamiwa.

Lakini Serikali inawasaidiaje albino waishio kijijini ambako hakuna umeme? Simu hiyo inachajiwa kwa teknolojia gani? Je simu hizo hizitakuwa kivutio kingine na hivyo kuwafanya wavamiwe zaidi?Kama imefikia hatua albino hawezi kutembea peke yake au kutembea baadhi ya masaa hususani jioni, kama imefikia hatua Mbunge maalum ambaye ni albino lazima apewe ulinzi maalum ili asinyofolewe viungo vyake, falsafa ya Tanzania kama kisiwa cha amani iko wapi?Ndugu zetu wa Marekani wanaelekea kuishinda dhambi ya ubaguzi wa rangi, kwani hatimaye wamefikia hatua ya kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao kwa kuangalia uwezo wake, hoja zake na si tena kigezo cha rangi kama Dr. Martin Luther King Jr aliposisitiza katika ndoto yake ( I HAVE A DREAM). Mwaka 2010 kama mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa albino, tutakuwa tayari kumpigia kura endapo atakuwa na sifa za kutuongoza? Tafakari, Chukua hatua.

Kwa upande wake Bw Kaduma anasema kuwa ameona ili kujiokoa na wauwaji hao kuishi kwa mganga huyo ambaye ndiye aliyemuokoa kuuwawa baada ya kuwekewa mtengo na mkazi mmoja wa Mbarali ambaye alitaka kumuua na kuuza viungo vyake kwa zaidi ya shilingi milioni 2.

Kaduma anasema kuwa yeye alikuwa hajua chochote juu ya mpango huu ila alishangaa kuona polisi ,magnga huyo na mtuhumiwa wakifika kijijini kwao na kudai kuwa wamekuja kumwokoa baada ya mtuhumiwa huyo kukili kutaka kufanya mauwaji.

Bw Kaduma ambaye kwa sasa amekuwa akiishi nyumbani kwa mganga huyo na kufanya kazi ndogo ndogo huku akitembea na kisu kama ngao ya kujilinda na wauwaji hao ameomba serikali kuwawajibisha waganga wanaochochea mauwaji hayo ya maalbino na kuwabakiza waganga kama Dr Mwandulami ambaye ameonyesha kuchukizwa na mauwaji hayo na kujikita katika kutetea uhai wa maalbino.

Mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ na kipindi cha Morning Talk Ebony Fm kesho jumatano asubuhi kinapiga kambi na kufanya mahojiano yatakayorushwa moja kwa moja hewani kutoka eneo la Mtwango kwa mganga Mwandulami ambaye alimwokoa albino Festo Kaduma ili kujua sababu za yeye kujitolea kumtunza albino huyo.

March 29, 2010

MBARALI BADO WALIA NA KERO YA MASHAMBA YA MPUNGA KUBINAFSISHWA ,SAKATA LA WANAFUNZI KUANGUKA LAZIDISHA HOFU


Pamoja na serikali kupiga marufuku mifuko kuwepo katika bonde la Ihefu wilayani Mbarali mkoani Mbeya bado baadhi ya wafugaji wameendelea kupiga kambi katika baadhi ya maeneo uchunguzi wa mtandao huu umebaini . Pia suala la serikali kubinafsisha mashamba ya zao la mpunga Kapunga na mengine ktk wilaya hiyo inatajwa kuwa ni moja kati ya kero kubwa kwa wananchi kugeuka vibarua katika mashamba hayo ambapo mwanzo wakulima walikuwa wakiyalima. Wakati bado wananchi hao wakikuna vichwa kwa kero hiyo ya kiuchumi bado tatizo la wanafunzi wa shule kuanguka limezidi kuwaumiza vichwa wazazi hao pamoja na kuwatia hofu zaidi mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com na kipindi cha Morning Talk leo kupokea kero za wananchi mjini Rujewa katika uwanja wa mpira

PIKI PIKI NI MALI YANGU HATA WATANO NAPAKIA!


Askari wa usalama barabarani kituo cha Migori Mtera katika wilaya ya Iringa vijijini aliyefahamika kwa jina moja ya Peter akiwa amekamata piki piki ambayo ilikuwa imevunja sheria za usalama barabarani kwa kupakizana zaidi ya abiria wawili huku wakiwa hawajavaa kofi ya kuzuia michubuko iwapo wapata ajali , madereva wengi wa piki piki katika eneo hilo wamekuwa wakiendesha bila leseni wala kuvaa kofia kwa madai kuwa chombo hicho ni mali yao haina haja na kuwa na leseni na kuwa wanaweza kupakizana idadi yoyote

UMAARUFU HUU WA WATANGAZAJI WA RADIO EBONY FM UNAWEZA KUCHANGIA KUHIFADHI MAZINGIRA?

Mti huu umeendelea kutunzwa vilivyo na kuheshimika na wakazi wa eneo la Nyan'goro katika wilaya ya Iringa vijijini kutokana na heshima kubwa uliopewa na hata kuandikwa majina ya watangazaji na DJ maarufu kituo cha Radio Ebony Fm Bw Edo Bashir ambaye ni mtangazaji na Mubaambaye ni DJ maarufu katika vituo vya radio hapa nchini


Huyu ni mmoja kati ya wakazi wa Iringa ambaye amevutiwa na majina ya watangazaji hao na hata kuamua kujipumzisha katika mti huo ambao umeendelea kutunza na wananchi bila kukatwa tofauti na ilivyo miti mingine

March 28, 2010

MREMBO AGEUKA KICHAA BAADA YA KUMWIBIA SIMU MTEJA BAR

Katika hali isiyokuwa ya kawaida binti mmoja (mrembo) aliyekuwa akiuza bar moja maarufu ktk eneo la Mugeluka Kibao wilaya ya Mufindi amegeuka kichao ghafla na kuanza kutembeza kichapo kwa wateja wake huku akiokota makopo baada ya kumwibia simu ya mkononi mteja wake. Tukio hilo limetokea juzi ijumaa na kupelekea wafanyakazi wenzake katika bar hiyo iliyo kijijini hapo kumkimbia binti huyo kutokana na hatua yake ya kuwapiga. Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa binti huyo kabla ya kuja kufanya kazi katika bar hiyo Kibao alikuwa ametokea Mbeya ambako anadaiwa ndiko aliko pora simu ya mteja wake bar na kukimbilia katika kijiji hicho kujificha japo mwenye simu alipata kumfuata na kumwomba simu yake bila mafanikio zaidi ya kuambulia matusi toka kwa mrembo huyo. Alisema shuhuda huyo kuwa baada ya kutukanwa mzee huyo anayedaiwa ndie mwenye simu ya bei ya juu ambayo ili kuwa ikimilikiwa na mrembo huyo alisikika akitamba kuwa hazipiti siku mbili bila kurudi simu yake jambo ambalo limetokea kweli kwa mrembo huyo kuanza kuweweseka huku akieleza jinsi alivyo pora simu kwa mteja wake. Kutokana na hali ya mrembo huyo kuzidi kuwa mbaya wasamalia wema wamelazimika kumsafirisha hadi mkoani Mbeya ili kwenda kumwomba msamaha mmiliki wa simu hiyo ambayo imekuwa ikiita tumboni mwake mara kwa mara. Tukio hili japo linahuzunisha ila ni fundisho kwa wahudumu wengine wa bar , Hoteli na wale wa kwenye vyombo vya usafiri wenye tabia ya udokozi kuna haja ya kuanza kurejesha mali zisizo za jasho kama njia ya kuepuka mkasa wa binti huyu wa Mbeya aliyepora simu huko na kuja kujificha kibao Mufindi

KERO YA GETI LA NYANG'ORO ,MAJI NA UVUVI HARAMU WAWALIZA WANANCHI MTERA IRINGA VIJIJINI .........


Wakati serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa soko la kimataifa la Samaki katika eneo la Migori Mtera jimbo la Ismani katika wilaya ya Iringa vijijini ujenzi unaotaraji kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 1 ,wavuvi katika bwara wa mtera na wananchi wa tarafa ya Ismani walalamikia geti halmashauri kuendelea kuweka geti katika eneo la Nyang'oro pamoja na vitendo vya watu wanaoendeleza uvuvi haramu katika bwawa la mtera .

Pia wakazi hao wameendelea kuomba serikali na mbunge wa jimbo hilo Mh.Wiliam Lukuvi kusaidia huduma ya maji safi katika eneo hilo ambalo kimsingi ni eneo linalokabiliwa na ukame afisa mtendaji wa kijiji cha migori Bw. Ayub Ngeng'ena amethibitisha kuwepo kwa kero hizo kwa wananchi.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa kushirikiana na kipindi cha morning Talk kinachorushwa na Radio Ebony Fm ,kesho jumatatu kufanya mazungumza ya moja kwa moja na wananchi wa eneo la uwanja wa mpira Mtera Migori na eneo la wavuvi wadogo bwawa la mtera ili kupata undani wa kero hizo na sababu ya kutofanikiwa kwa mapambano ya uvuvi haramu katika bwawa la Mtera .

March 27, 2010

IGOWOLE NA DON BOSCO NJE MASHINDANO YA VODA COM MUFINDI MUUNGANO CUP 2010


Mratibu wa Voda Com Mufindi Muungano Cup 2010 Daud Yassin (kulia) akiwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi (SMZ) Hamza Hassan Juma ,Soma habari kamili hapa

March 26, 2010

MBUNGE MALANGALILA APIGA MARUFUKU WANANCHI KUCHANGIA MRADI WA MAJI

Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini mkoani Iringa Mh. BenitoMalangalila amezua mtafaruku mkubwa jimboni kwake baada ya kupiga marufuku wananchi wa vijiji sita vya kata ya Mtwango kikiwemo kijiji cha kibao kuchangia mradi wa maji unaofadhiliwa na benki ya dunia kwa asilimia 95. Habari zaidi soma gazeti la Tanzania Daima kesho.

March 25, 2010

KERO YA MAJI NA BARABARA ZAKAMISHA MAENDELEO KIJIJI CHA KIBAO MUFINDI

WANANCHI WA KIJIJI CHA KIBAO WILAYA YA MUFINDI WANAENDELEA KUTUMIA MAJI YA MABONDENI YASIO SAFI NA SALAMA KWA ZAIDI YA MIAKA 10 SASA JAMBO AMBALO NI HATARI KWA AFYA ZAO. KERO YA MAJI IMEKUWA NI MTIHANI KWA VIONGOZI WA WILAYA HIYO. WAKAZI HAO KWA SASA WANAHOJI SABABU YA KUCHANGIA WAHISANI BENK KUU AMBAO WAMEJITOLEA KUSAIDI MRADI HUO WA MAJI. AIDHA KERO NYINGINE KUBWA KATIKA KIJIJI HICHO AMBACHO KILIKUWA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA MUFINDI KABLA YA KUHAMISHWA KUELEKEA MJINI MAFINGA NI PAMOJA NA BARABARA YA TANROAD AMBAYO INAFANANISHWA NA MBAVU ZA MBWA. UCHUNGUZI WA MTANDAO HUU NA RADIO EBONY FM AMBAO LEO WAMEPIGA KAMBI YA SIKU MBILI ENEO LA MUGELUKA KIJIJI CHA KIBAO UMEBAINI KUWEPO KWA IDADI KUBWA YA WAFANYABIASHARA WENGI KUKIMBIA KIJIJI HICHO KUTOKANA NA KUYUMBA KIUCHUMI

KERO YA MAJI NA BARABARA ZAKAMISHA MAENDELEO KIJIJI CHA KIBAO MUFINDI

WANANCHI WA KIJIJI CHA KIBAO WILAYA YA MUFINDI WANAENDELEA KUTUMIA MAJI YA MABONDENI YASIO SAFI NA SALAMA KWA ZAIDI YA MIAKA 10 SASA JAMBO AMBALO NI HATARI KWA AFYA ZAO. KERO YA MAJI IMEKUWA NI MTIHANI KWA VIONGOZI WA WILAYA HIYO. WAKAZI HAO KWA SASA WANAHOJI SABABU YA KUCHANGIA WAHISANI BENK KUU AMBAO WAMEJITOLEA KUSAIDI MRADI HUO WA MAJI. AIDHA KERO NYINGINE KUBWA KATIKA KIJIJI HICHO AMBACHO KILIKUWA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA MUFINDI KABLA YA KUHAMISHWA KUELEKEA MJINI MAFINGA NI PAMOJA NA BARABARA YA TANROAD AMBAYO INAFANANISHWA NA MBAVU ZA MBWA. UCHUNGUZI WA MTANDAO HUU NA RADIO EBONY FM AMBAO LEO WAMEPIGA KAMBI YA SIKU MBILI ENEO LA MUGELUKA KIJIJI CHA KIBAO UMEBAINI KUWEPO KWA IDADI KUBWA YA WAFANYABIASHARA WENGI KUKIMBIA KIJIJI HICHO KUTOKANA NA KUYUMBA KIUCHUMI

POLISI MAKAMBAKO WATEMBEZA KICHAPO KWA MGAMBO

JESHI LA POLISI MJINI MAKAMBAKO LAWAMANI KWA KUVAMIA KITUO CHA MAUZO YA SODA ZA JUMLA ENEO LA OFISI ZA RFA ZAMANI NA KUTEMBEZA KICHAPO KWA ASKARI MGAMBO WANAOLINDA ENEO HILO. TUKIO HILO LA AIBU KWA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA NA KINYUME NA MAADILI YA JESHI LA POLISI LIMETOKEA MAJIRA YA SAA 5.10 USIKU LEO NA KUDUMU KWA NUSU SAA KTK ENEO HILO . MWANDISHI WA MTANDAO HUU ALIPATA KUSHUHUDIA TUKIO HILO NA KUTOA TAARIFA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA KUTOKANA NA ASKARI HAO ZAIDI YA WANNE WAKIWA NA PINGU MIKONONI KUENDELEA KUTEMBEZA KIPIGO KWA MGAMBO HAO WASIO NA HATIA HUKU WANANCHI WALIOFIKA KUAMUA PIA WAKIAMBULIA KIPIGO. MMOJA KATI YA MGAMBO ALIYELAZIMIKA KUKIMBIA LINDO LAKE KUKWEPA KIPIGO TOKA KWA ASKARI HAO WA DORIA WALIOKUWA WAKINYWA POMBE KTK BAR MOJA JIRANI NA LINDO HILO ALISEMA ASKARI MMOJA AKIWA NA MWANAMKE ALIKUTWA AMESIMAMA NDANI YA ENEO LA LINDO AMBALO LILIKUWA LIMEZUNGUSHWA KAMBA NA BAADA YA KUTAKIWA KUTOKA ALICHUKIA NA KUCHOMOA PINGU MFUKONI NA KUANZA KUMWADHIBU MGAMBO HUYO HUKU AKIDAI KUWA YEYE NI ASKARI YUPO KAZINI NA MHUDUMU HUYO WA BAR. HATA HIVYO KUTOKANA NA MGAMBO HUYO KUJIBU MAPIGO NDIPO ASKARI WENGINE WALITOKA BAR NA KUANZISHA MASHAMBULIZI KWA KILA RAIA ANAYEONEKANA MBELE YAO. ALISEMA MBAYA ZAIDI ASKARI HAO HAWAKUWA NA SARE ZAIDI YA PINGU NA BAADA YA UMATI WA WANANCHI KUFIKA ENEO HILO WAKIWA NA MAWE NDIPO ASKARI HAO WALIPO AMUA KUKIMBIA. KTK TUKIO HILO VIJANA WAWILI AKIWEMO MLINZI MMOJA WALIUMIZWA NA ASKARI HAO AMBAO WANADAIWA WAGENI KTK KITUO CHA MAKAMBAKO.

March 24, 2010

BASI LA HEKIMA LAPATA AJALI IRINGA

HABARI ZILIZOTUA KTK MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINADAI KUWA BASI LA KAMPUNI YA HEKIMA LILILOKUWA LIKITOKA TUNDUMA MKOANI MBEYA KWENDA DAR ES SALAAM LIMEPINDUKA ENEO LA TOSAMAGANGA IRINGA. MKUU WA USALAMA MKOA WA IRINGA KEDMUND MNUBI AMEUTHIBITISHIA MTANDAO HUU JUU WA AJALI HIYO NA KUWA ABIRI 7 NDIO WALIOJERUHIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA , HABARI KAMILI INAKUJA

March 23, 2010

BINTI WA MIKA 14 ATOROKA KUTUMIKISHWA BAR NJOMBE AHUKUMIWA POLISI


Binti yatima mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa mji mwema Mafinga wilaya ya Mufindi Mariam Nyagawa (pichani ) amenusulika kubakwa usiku wa manane na kuishia kukamatwa na polisi mjini Njombe baada ya kukimbia katika eneo lake la kazi katika bar moja maarufu mjini Njombe inayofahamika kwa jina la Sovyo ambako alikuwa akitumikishwa kufanya kazi ya kuuza bar kwa ujira wa shilingi 10,000 kwa mwezi.

Binti huyo aliuleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com nje ya kituo cha polisi Njombe kuwa tukio hilo lilitokea jana machi 22 mwaka huu baada ya kufanya kazi katika bar hiyo kwa muda wa siku tatu bila kupumzika.

Anasema kuwa pamoja na kufanya kazi hiyo ya kuuza pombe bado alikuwa akipewa wanaume ambao sawa baba yake wa kwenda kulala nao hali iliyopelekea kuiona kazi hiyo chungu kwake na kuamua kutoroka usiku wa manane.

Hata hivyo alisema kabla ya kuja Njombe alirubuniwa na mwanamke mmoja kuwa kuna kazi nzuri ya kufanya ambayo ingemwezesha kupata fedha za haraka za kumwezesha kulipa karo ya shule ya ufundi ili kuendelea na mafunzo ya kushona baada ya kufeli mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana.

Ila baada ya kufika Njombe anadai ilipewa nguo fupi na kupelekwa katika bar hiyo kwa ajili ya kufanya kazi ya ukahaba ambayo haiwezi .

Kutokana na polisi wa doria kumkamata usiku wa manane akiwa mbioni kurudi Mafinga kwa kutembea kwa miguu walimpeleka kituo cha polisi ambako alilazwa hadi asubuhi na kutokana na kujieleza waliweza kumwachia katika kesi ya uzembe na uzurulaji kwa kumpa hukumu ya kudeki choo kwa mikono pamoja na nyumba mbili za askari polisi.

Hata hivyo kutokana na hali hiyo ya binti huyo kutojua wapi kwa kwenda mmiliki wa mtandao huu aliweza kuwasiliana na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu pamoja na kumpa nauli ya shilingi 10,000 kwa ajili ya kurudi Mafinga ili uongozi wa wilaya kuweza kumsaidia kuendesha maisha yake hata kumtafutia shule ya kusoma japo jitihada za mtandao huu kumsomesha zinaendelea kufanywa.

Pamoja na mkasa wa binti huyo bado uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu katika bae nyingi za mji wa Njombe idadi kubwa ya wahudumu wake ni watoto wa miaka 12,14 na 20 jambo ambalo linapaswa uongozi wa wilaya kufanya msako ili kuwarejesha shule watoto hao.

TOPE ZINAPOKWAMISHA MABASI STENDI YA NJOMBE ,RC IRINGA KUTUA NJOMBE ASUBUHI KESHO KUSIKIA KILIO CHA WAKULIMA WA CHAI LUPEMBE


Mwandishi wa habari wa gazeti la majira Bw Carlos Mtoya (wa pili kuliaaliyeulamba mkanda nje ) akisaidia kusukuma basi linalofanya safari zake kati ya Ludewa Njombe baada ya basi hilo kukwama katika mashimo stendi kuu ya Njombe leo mchana .


Hali ya ubovu wa stendi hiyo ya Njombe imeendelea kutishia usalama wa mabasi ya abiria yanayoingia katika stendi hiyo hasa katika kipindi hiki cha masika na iwapo jitihada za kuziba mashimo yanayoendelea kuchimbika katika stendi hiyo hazitafanyika upo uwezekano wa stendi hiyo kukimbiwa na wamiliki wa vyombo vya usafiri.


Mdau wa mtandao huu bado nipo wilayani Njombe ambapo leo asubuhi mkuu wa mkoa wa Iringa Bw Mohamed Abdulaziz anataraji kukutana na kamati ya watu sita ya wakulima wa chai Lupembe ambao juzi waliandamana kutaka mwekezaji wa kiwanda hicho kwa asilimia 70 Nawabu Mulla kufungua kiwanda kama alivyoagizwa na mahakama ya ardhi mapema mwaka jana.

WAKULIMA WA CHAI LUPEMBE WAPONGEZA KIPINDI CHA MORNING TALK RADIO EBONY FM .....
Meneja wa Radio Ebony Fm ,BW ,Cosmas Byekwaso.

Kituo hicho cha Radio Ebony Fm kimeendelea kujizolea umaarufu mkubwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini na kupelekea baadhi ya mikoa na wilaya mfano wilaya ya Njombe na Makete ambako wakazi wake wamekuwa wakiendelea kuzihama radio zao na kupenda kusikiliza radio Ebony ambayo kwa wakazi wa mkoa wa Iringa Radio hii wamekuwa wakiifananisha na kituo cha Runinga cha Al jazira kutokana na upashaji wake habari kwa wakati na kujikita kila kona tofauti na vyombo vingine vya utangazaji ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa.


Anasema mkazi wa mji wa Njombe Bw Salum Kibasa kuwa toka Radio Ebony imeanza kusikika katika maeneo ya mji wa Njombe hasa katika radio za kwenye magari wananchi wengi wameanza kuhama kusikiliza Radio Njombe na kukimbilia Radio Ebony Fm japo wameomba jitihada za radio hiyo katika kufika kwa wananchi vijijini kuchukua kero zao ziendelee.

March 22, 2010

NIMENUSURIKA KIFO NIMEAMBULIA KUIBUA SIRI NZITO JUU YA STENDI YA NJOMBE


Hili ni eneo ambalo lilipaswa kujengwa stendi kuu ya mabasi katika mji wa Njombe ambalo kwa sasa linatumika kwa kilimo bora na viongozi wa halmashauri ya mji wa Njombe wakiongozwa na mkurugenzi wa mji huo George Lukindo

Tax ikiwa imeegeshwa kando kando ya eneo la stendi lililogeuzwa mashamba ya watumishi eneo hili lipo umbali wa km.zaidi ya 7 toka Njombe mjini kuelekea Ruvuma


Hii ni stendi ya Njombe ilivyo sasa ni tope kwenda mbele

Haya ni maua ambayo ni sehemu ya Majaribio ya kuigeuza stendi ya Njombe ambayo inaongoza kwa ubovu katika mkoa wa Iringa


Gari hili mali ya Kafyelilo ndilo ambalo limenigonga leo asubuhi wakati nikizungumza moja kwa moja ya madereva pamoja na abiria wa stendi ya Njombe kuhusu ubovu wa stendi hiyo katika Radio Ebony Fm

Kabla ya kuanza kueleza siri nzito juu ya stendi ya Njombe ambayo inalalamikiwa kwa kukusanya mapato yasiyofanya kazi ya kuboresha stendi hiyo na kuiacha katika hali mbaya mfano wa stendi iliyotelekezwa ,niweze kukushukuru wewe msikilizaji wa Radio Ebony Fm ambaye umeweza kutumia gharama zako nyingi kwa kupiga simu kwangu binafsi ana Radioni kunijulia hali kutokana na tukio la kusukumwa na gari lililonipata majira ya saa 9 asubuhi jana wakati nikiendelea kuzungumza hewani na wananchi kuhusu kero ya stendi ya Njombe.

Kwa ujumla hali yangu ni salama kwani gari hilo ambalo lilinigonga na baadae kukimbia kabla ya askari wa usalama barabara wakiongozwa na askari mmoja aliyefahamika kwa jina la Tunu kuweza kumkamata dereva huyo na kumweka chini ya ulinzi huku wakitaka kujua hali yangu ,kwa vile sijaumia kupita kiasi na kusudi langu la kwenda Njombe lililenga kuchunguza ubovu wa stendi hiyo na sio kupambana na madereva basi natamka wazi kuwa dereva husika nimemsaheme kwa yawezekana kabisa alinigonga kwa bahati mbaya kama mwenyewe alivyojieleza ila yawezekana pia ilipangwa japo sina hakika ila yote namwachia Mungu shida yangu na ubovu wa stendi na hatma ya michango ya wananchi katika stendi hiyo.

Mdau wa mtandao huu katika tukio hilo linigongwa kiunoni na gari hilo japo sijapata majeraha yoyote wala michumbuko hivyo naendelea na mzigo kama kawaida.

Katika sakata hili la stendi ya Njombe nimepata kuelezwa mengi na wakazi wa mji wa Njombe ambapo baadhi ya wananchi wa eneo la mji mema ambako stendi tarajiwa anatakiwa kujengwa wamedai kuwa uongozi wa halmashauri hiyo uliwapokonya mashamba yao kwa maiadi kuwa eneo hilo linatakiwa kujengwa stendi mwaka huu jambo ambalo halifafanyika zaidi ya wao wenyewe kugawana na kulima katika eneo hilo na stendi.

Mmoja kati ya wakulima wa eneo hilo mzee Amos Samson alisema kuwa miaka yote wamekuwa wakilima katika eneo hilo la stendi ila mwaka jana walifukuzwa kwa madai kuwa serikali inataka kujenga stendi mpya ya kisasa ila walishangaa kuana eneo hilo linalimwa na kupandwa mahindi kama njia ya kutekeleza sera ya serikali ya kilimo kwanza.

Diwani wa kata ya Njombe mjini Augustin Mbanga alipoulizwa na mtandao huu jana mbali ya kutaka kukwepa ukweli wa jambo hilo ambalo tayari mtandao huu ulikuwa umepata ukweli wake alikiri eneo hilo kutumika kama eneo la mashamba ya watumishi wa mji wa Njombe japo alisema mpango wa kujenga stendi upo pale pale na shilingi bilioni 1 ndizo zilizotengwa kwa kazi hiyo.

Pamoja na kuuthibitishia mtandao huu kuwa wanaolima hapo ni watumishi wa halmashauri bado alikanusha madai ya wakulima kuwa walipokonywa eneo hilo bila kulipwa fidia kwani alisema wote walilipwa fidia zao

Huku kwa upande wake mkurugenzi wa mji wa Njombe George Lukindo aliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa njia ya simu kuwa kweli wanaolima hapo ni watumishi wa halmashauri japo si kweli kama wananchi walitolewa katika eneo hilo.

Alisema kuwa eneo hilo ni mali ya halmashauri na kuwa hakuna aliyelipwa fidia na kuwa hata mpango wa kujenga stendi katika eneo hilo haupo sasa kwani hakuna bajeti iliyotengwa zaidi ya kuendelea kutafuta fedha na eneo hilo kuzidi kuliweka safi kwa kulima mahindi.

"Ni kweli tunalima mahindi katika eneo la stendi kama upo Njombe hata kesho asubuhi tunaweza kuongozana na wewe kwenda kuona eneo hilo " mkurugenzi huyo alikiri kuwa na shamba katika eneo hilo kama ambavyo wananchi walivyomlalamikia.

Hii ndio siri inayoendelea kujificha katika stendi ya Njombe japo mtandao huu unaendelea kujua uhalali wa mkandarasi anayepewa kazi ya kutengeneza stendi hiyo chini ya kiwango kila mwaka .

MAANDAMANO YA WAKULIMA WA CHAI LUPEMBE NJOMBE YAISHIA MIKONONI MWA POLISI


Wakulima wa chai Lupembe wilaya ya Njombe wakiwa nje ya kituo cha Polisi Njombe baada ya kuwekwa chini ya ulinzi leo kwa masaa 6 na kuachiwa huru kwa madai ya kufanya maandamano yasiyo na kibali kwa lengo la kushinikiza kiwanda cha chai Lupembe kufunguliwa na mwekezaji wake Nawab Mulla SOMA HAPA

March 21, 2010

NAIBU SPIKA NA MADIWANI WAWILI NJOMBE KUPOTEZA NAFASI ZAO KWA UBOVU WA STENDI YA MAKAMBAKO NA NJOMBE ...

Hii ni hali halisi ya stendi kuu ya mji wa NjombeYaani ukishuka katika basi ndani ya stendi ya Njombe yahitaji kivuko ili usikumbane na tope .
UBOVU wa stendi kuu ya mabasi Makambako na Njombe umezidi kuchukua sura mpya baada ya madereva katika stendi hizo kuwataka wakurugenzi wake kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia vizuri fedha za serikali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ wilayani Njombe madereva hao wamesema kuwa wamekuwa wakilipa ushuru kila siku katika stendi hiyo huku hali ya stendi ikiendelea kugeuka mashimo kila kona.
Hata hivyo walisema kuwa mkandarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza stendi hiyo yeye ni mtaalam wa kutengeneza samani na sio kazi hiyo ya ukandarasi kama ambavyo halmashauri hiyo imekuwa ikiendelea kumpa tenda.
Madereva hao walisema kutokana na wao kuendelea kulipa ushuru na hali ya stendi hiyo kuendelea kuwa mbaya ni vyema uongozi wa mkoa wa Iringa kuweza kuingilia kati suala hilo kwa kuchunguza uhalali wa mkanadarasi huyo na kiasi cha fedha zinazotumika kulipa matengenezo hewa kila mwaka katika stendi ya Makambako na Njombe.
Kwani walisema iwapo uongozi wa halmashauri ya Njombe mji na mji wa Makambako umeshindwa kusimamia vyema fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya matengenezo ya stendi hizo ni vizuri hata ushuru katika stendi hiyo kutochukua kabisa.
Walisema kwa nyakati za masiki katika stendi hizo tope tupu na kiangazi na vumbi kwenda mbele jambo ambalo ni hatari kwa afya wa watumiaji wa stendi hizo
Hivyo walisema kutokana na hali hiyo kuwa mbaya zaidi wamewataka wakurugenzi wa mji mdogo wa Makambako na diwani wa kata hiyo Deo sanga ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa na mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini mzee Jackson Makweta kusimamia ufisadi unaofanywa katika stendi ya makambako ama kujiuzulu nafasi zao kwa kushindwa kusimamia kero za wananchi .
Pamoja na kuwataka viongozi hao mjini Makambako kuachia n gazi pia kwa upande wao madereva wa mji wa Njombe wamemtaka mbunge wa jimbo la Njombe kusini Anne Makinda ambaye ni naibu Spika wa bunge la Tanzania na diwani wa kata ya Njombe mjini Augustino Solomon Mbanga kumbana mkurugenzi wa mji huo ili kueleza makusanyo ya ushuru katika stendi hiyo yanatumika kwa kazi gani na kujua sababu ya kuendelea kumweka mkandarasi Mrando katika ujenzi wa stendi hiyo wakati akiendelea kufanya chini ya kiwango na kama watashindwa kufanya hivyo wasitegemee kupata kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kwa upande wake diwani Mbanga alisema kuwa stendi hiyo inafanyiwa matengenezo ya muda na kuwa eneo la stendi limetengwa na ujenzi wake unataraji kufikia kiasi cha shilingi bilioni 1 na kuwa eneo hilo la stendi litatumika kama bustani ya mji.

VIFAA VYA MPIGAPIGA WA MAKAMU WA RAIS VYANASWA ,POLISI WAPONGEZWAMpiga picha mkuu wa makamu wa Rais (kushoto) ambaye aliporwa vifaa vyake vyote mjini IringaGari lililovunjwa na kuporwa vifaa vya mpigapicha wa makamu wa Rais likiwa limeegeshwa nje ya Hoteli ya Anex Staff Inn mjini Iringa eneo ambalo vibaka walivunja na kuiba
Wakati baadhi ya vifaa v ya mpigapicha mkuu wa makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein vimeanza kupatikana baada ya msako makali uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Iringa chini ya RCO Craus Mwasyeba wananchi mjini Iringa wamelipangeza jeshi la polisi chini ya kamanda wake Evarist Mangala kwa kazi nzuri .
Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wananchi hao wamesema kuwa kazi iliyofanywa na jeshi la polisi ni kubwa na inapaswa kupongezwa .
Kwani walisema kuwa kama si umakini wa jeshi la Polisi mkoani Iringa uwezekano wa baadhi ya vifaa na watuhumiwa kukamatwa ulikuwa ni mdogo sana .
Pamoja na pongezi hizo bado wananchi hao wameeleza wasiwasi wao na ulinzi katika nyumba za kulala wageni mkoani hapa na kulitaka jeshi la polisi kutoa elimu kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni ili ikiwezekana kuweka walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo ili kuondoa aibu kama hiyo ambayo mkoa umeipata baada ya kumwibia mkamu wa rais
Hata hivyo walisema kuwa baaadhi ya nyumba za kulala wageni mkoani Iringa vimekuwa maficho ya majambazi na kuwa ni vyema jeshi la polisi kuendesha msako wa mara kwa mara katika nyumba za kulala wageni .
Walisema sehemu kubwa polisi wamekuwa wakifanya msako katika nyumba za kulala wageni za bei ya chini na kuacha nyumba za heshima kama hizo ambazo zimekuwa zikishiriki pia kuhifadhi majambazi .

VODACOM YAZIDI KUONGEZA UDHAMINI MUUNGANO CUP MUFINDIMambo ya Voda com Tanzania katika mashindano ya kombe la Muungano MufindiMratibu wa kombe la muungano Mufindi Daud Yassin akiwa ameshika mpira akimwongoza waziri kulia kwenda kufungua mashindano hayo jana
ibu meya wa manispaa ya Iringa ambaye ni kocha wa timu yaru Ally Mbata akipokea vifaa kwa akili ya timu yakeMmoja kati ya waamuzi wa kike akipokea vitendea kazimkurugenzi wa voda com kanda ya kusini Jackson Kiswaga (kushoto) akimkabidhi waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hamza Hasann Juma vifaa vya michezo ambavyo vimetolewa na Voda com kwa ajili ya kudhamini mashindano ya kombe la Muungano Mufindi 2010 ,vodacom imedhamini mashindano hayo kwa zaidi ya shilingi milinio 70

Mh. Waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi Zanzibar Hamza Hassan Juma akipongeza udhamini wa Voda com na Chai Bora katika mashindano ya kombe la Muungano Mufindi

Mwenyekiti wa kombe la Muungano Mufindi mbunge Benito Malangalila akipokelewa na viongozi katika uwanja wa Igowole


Chai bora watoa shavu kwa Voda como Muungano Cup


Vijana wa Mucoba


Usikose kusoma habari kamili ya uzinduzi wa kombe la Muungano Mufindi katika gazeti la Tanzania Daima na Sayari kesho jumatatu au BOFYA HAPA

March 19, 2010

WAKAZI WA KIJIJI CHA IFUNDA WASUSIA KUPOKEA MRADI WA MAJI VIONGOZI WALAZIMISHA.......


Wakazi wa kijiji cha Ifunda kibaoni wakipinga hatua ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa kutaka kuukabidhi mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150 ambao wamedai kuwa bado haujakamilika ipasavyo


Kibao kinachoonyesha ufunguzi wa maradi huo badala ya uzinduzi wa mradi kama ambavyo wananchi hao walivyoelezwa


Hapa maji yanavuja kabla ya mradi hatujaupokea


Sikiliza maswali ya wananchi na majibu ya viongozi yaliyotolewa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Bw Stephen Mhapa leo

March 18, 2010

MPIGA PICHA MKUU WA MAKAMU WA RAIS DR.SHEIN AIBIWA IRINGAKamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla
Mpigapicha mkuu wa makamu wa Rais Bw Amour Nassor (kulia)akiwa na wanahabari wa mkoa wa Iringa Daud Mwangosi na Adolph Mbata
Ziara ya makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein yamalizika kwa dosari Iringa ni baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni vibaka kuvunja gari ya matangazo katika msafara wa makamu wa rais kutoka Ikulu yenye namba za usajili T 192 A aina ya Toyota na kupora vifaa vya mpiga picha mkuu wa makamu wa rais Amour Nassor.

Kwa mujibu wa Nassor mwenyewe alipozungumza na mtandao huu katika uwanja wa Ndege Nduli Iringa leo asubuhi alidai kuwa vifaa hivyo viliibiwa jana majira ya saa 4 hivi usiku muda mfupi baada ya gari hilo kuegeshwa katika hoteli hiyo ambayo yeye na mwandishi wa makamu wa rais pamoja na waandishi wengine kutoka jijini Dar es Salaam walikuwa wamefikia hao.

Alisema vifaa vilivyoporwa ni pamoja na kamera mbili ikiwemo ya picha za mgando na ile ya video pamoja na kumbukumbu zote za picha ambazo alikuwa amepiga toka mwanzo wa ziara ya makamu wa Rais ndani ya mkoa wa Iringa.

Mmoja kati ya wahudumu wa hoteli hiyo ya Staff Inn aliyepata kuzungumza na mtandao huu kwa sharti la kutotaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa juu ya Hoteli hiyo alisema kuwa tayari jeshi la polisi linawashikilia walinzi zaidi ya wawili wa eneo hilo kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla alipoulizwa na mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ kwa njia ya simu leo alikiri kuwepo kwa tukio hilo japo alisema kuwa kwa sasa ni mapema mno kulizungumzia tukio hilo ambalo linafanyiwa kazi kwa nguvu zote na jeshi la polisi

Mpenzi mdau wa mtandao huu habari kamili utaipata mara baada ya jeshi la polisi kukamilisha uchunguzi wake na kuitoa kwa vyombo vya habari

MUFINDI WADAI MAKAMU WA RAIS DR.SHEIN AMEPOTOSHWA KUHUSU MSITU WA SAO HILI...

Mzee SIKAUKA MWACHANGU kushoto na Mzee RAFAEL NGOGO Kulia ambao ni kati ya Viongozi wa Kabila la Kihehe katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wakimvalisha Vazi la Utawala wa kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN alipowasili katika uwanja wa Mashujaa Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. MOHAMED ABDULAZIZI(picha na
AMOUR NASSOR -VPO)

WAKATI makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr .Ali Mohamed Shein akiwaahidi wananchi wa Mafinga wilaya ya Mufindi kuwa serikali italishughulikia tatizo la kupanda kwa gharama za miti katika msitu wa serikali wa Sao Hili ,wananchi wamedai kuwa kiongozi huyo amepotoshwa na tofauti za bei za miti kati ya kiwanda cha karatasi Mgogolo na ile ambayo wananchi wananunua.

Hivyo wamemwomba makamu wa Rais Dr.Shein kuweza kukutana upya na wavunaji wadogo wadogo ili kuweza kupewa kilio chao kabla ya kuanza kuishughulikia kero hiyo kama alivyo ahidi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini hapa juzi.

Mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com umebaini hali hiyo na baada ya kuzungumza na kuthibitishiwa ukweli zaidi na mjumbe wa kamati ya uvunaji katika msitu huo wa Sao Hili Mufindi Godfrey Mosha(pichani) ambae alisema kuwa pamoja na makamu wa Rais kuahidi kushughulikia suala hilo ila bado hajalipata vizuri.

Kwani alisema hata taarifa iliyotolewa na wabunge mbele yake imeonyesha kujichanganya na hivyo kushindwa kuyapata vyema matatizo ya wavunaji miti na mbao katika msitu huo wa Taifa.

Alisema kuwa katika msitu huo kuna mambo mawili ilipaswa Dr.Shein kueleweshwa vizuri .

Kwani alisema suala ambalo ameahidi kulishughulikia makamu wa Rais ni suala la kiwanda cha karatasi Mgogolo (MPM) ambacho kipo hatarini kufungwa kutokana na bei ya miti katika msitu huo kupanda zaidi huku wavunaji wadogo wadogo wamekuwa wakilia na bei kubwa ya miti ambayo imepandishwa zaidi ya asilimia 650 jambo ambalo kwao hawaliwezi.

Hivyo alisema pamoja na kupinga kwa nguvu zote kupanda kwa bei hiyo kwa sasa uongozi wa msitu huo umeshushwa bei kwa asilimia 40 bei ambayo hata hivyo bado kubwa .

Hivyo alisema kuwa ni vyema kabla ya makamu wa Rais Dr. Shein kuagiza suala hilo kufanyiwa kazi na kutangaza katika gazeti la serikali ni vizuri kurudi kwa wadau ili kujadiliana na kupandisha bei kwa pamoja badala ya kuiacha wizara husika kutumia mfumo dume katika kuamua mambo.

"Sisi kama walengwa hasa wa msitu huu tunasema kuwa taarifa aliyoipata makamu wa Rais na kutuahidi kuwa itafanyiwa kazi sio ambayo sisi tumekuwa tukilalamikia hivyo ni vyema kabla hata ya kuanza kulishughulikia suala letu kurudi tena kukutana na sisi kama wahusika ili kupata picha halisi"

Alisema hivi sasa kwibiki mita ya miti katika msitu huo inauzwa kwa shilingi 46000 kwa wananchi wa kawaida huku kwa kiwanda imekuwa ikiuzwa kwa shilingi 10,000.

Mosha alisema kuwa serikali inapaswa kuwa makini na suala hilo la matumizi ya msitu huo kwani wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kutaka kuichafua serikali iliyopo madarakani.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Benito Malangalila alimwomba Dr.Shein kuweza kusaidia kututua tatizo hilo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa CCM katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na wananchi kuanza kujenga chuki na serikali ya CCM kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Malangalila alisema kuwa toka wizara ya inayohusika na misitu kupandisha bei ya miti hali ya maisha ya wakazi wa wilaya ya Mufindi imezidi kuyumba huku wengi wao wakielekeza chuki zao kwa CCM.

Hivyo alisema ni vyema serikali kutumia busara zake katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo kabla ya kuleta madhara makubwa.

Hata hivyo Dr Shein aliahadi kulifanyia kazi suala hilo haraka iwezekanavyo japo alisema katika kunusuru kiwanda tayari suala hilo limeshughulikiwa toka machi 9 mwaka huu.
Katika hatua nyingine Dr.Shein alirudia kuwataka watanzania kujituma katika kazi na kuachana na tabia ya kufikiri kuwa na maisha bora bila kufanya kazi .

Alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa maisha ya wananchi yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya kazi na kutoa msaada wa pembejeo za kilimo kwa wakulima.
Dr.Shein alipongeza wilaya ya Mufindi kwa kutekeleza vyema mpango wa serikali wa kilimo kwanza kwa kuwawezesha wakulima kulima mahindi kwa kuzingatia sera ya kilimo bora.

usikose kupata ripoti kamili ya ziara nzima ya Dr.Shein katika mkoa wa Iringa katika mtandao huu wa www.francsgodwin.blogspot.com na katika gazeti la Tanzania daima jumanne wiki ijayo.

March 17, 2010

WANANCHI KILOLO WAMKATAA MENEJA WA MRADI WA MAJI,DR SHEIN AMALIZA VIBAYA ZIARA YAKE AFANYA KAZI YA KUMPIGIA DEBE MBUNGE MSOLLA JIMBONI


MAKAMU wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein atumia ziara yake Kilolo kumpigia debe mbunge wa jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla (CCM) ambaye ana hali ngumu kisiasa katika jimbo hilo kutokana na mpinzani wake mkuu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Venanci Mwamoto kupanga kurejea tena kutetea kiti chake.

Dr.Shein ambaye kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi alijikuta akiachwa na viongozi pekee jukwaani baada ya wananchi kukimbia eneo la mkutano kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya dakika 15.

Pamoja na wananchi wachache kurejea katika eneo hilo la mkutano bado Dr.Shein aliweza kutumia muda mwingi kumpamba mbunge Msolla tofauti na majimbo mengine kwa madai kuwa mbunge Msola amefanikisha mradi wa maji Ilula huku wananchi wapinga mbele yake kuwa hawadanganyiki na mradi huo ambao maji kwa yala ya kwanza yanatoka leo

Pia wamkataa meneja wa mradi wa maji Ilula (ILUWASSA) Edward Shelembi (pichani kulia akijieleza mbele ya Dr Shein)kuwa hawamtaki aotolewe katika nafasi hiyo kwa madai kuwa amekuwa akifanya usanii mwingi katika kutatua kero ya maji katika eneo hilo.


Habari kamili utaipata katika gazeti la Tanzania Daima kesho ama SOMA HAPA

MAKAMU WA RAIS DR.SHEIN AIFUNGUA RASMI HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KILOLOMakamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein ( kulia) akikabidhi mkasi mara baada ya kukamilisha uzinduzi wa hospitali teule ya wilaya ya Kilolo Ilula leo


YALIYOMO KATIKA TAARIFA YA UZINDUZI WA HOSPITALI HIYO

Upatikanaji wa dawa na vitendea kazi
Tangu Februari 2009 tumeendelea kupokea dawa na vifaa mbalimbali toka Bohari ya Madawa Iringa (MSD. Dawa na vifaa vinalipiwa na serikali moja kwa moja kupitia Bohari ya Madawa (MSD) Iringa.
Hospitali ina Jumla ya watumishi 98 wa kada mbalimbali, na kuna upungufu wa watumishi 67 ili kukidhi mahitaji ya watumishi 147 kwa kufuata mwongozo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.. Miongoni mwa watumishi hawa, Jumla ya watumishi 63 wanalipiwa mishahara na serikali kwa njia ya ruzuku.

Hospitali tangu imesajiliwa mwaka 2007 imeendelea kupata fedha toka Mfuko wa pamoja yaani Common Basket Fund toka Serikalini kupitia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri. Fedha hizi imeendelea kusaidia kuboresha huduma za wagonjwa kwa ujumla.vilevile Hospitali inapokea Fedha za Matumizi mengine yaani OC toka Serikalini , hii imekuwa msaada mkubwa sana kwa Hospitali yetu.

Majengo na vitengo mbalimbali
Katika utoaji huduma hospitali imegawanyika katika vitengo mbalimbali Majengo yaliyo mengi yamejengwa kwa msaada wa watu wa Swideni na Wamarekani. Majengo yaliyojengwa na waswideni ni general ward, maternity ward, private ward,Labour ward, Reproductive and Child Health (RCH), jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la Utawala. Pamoja na majengo hayo waliweza kujenga nyumba za watumishi 6, zenye uwezo wa kuhudumia watumishi 17. Kwa msaada wa wamarekani wameongeza jengo la CTC, Upasuaji, Rest house pamoja na Maabara.
USAFIRI
Hospitali ina magari matatu, mawili ni ya mradi wa CHAI na moja ni la hospitali, kati ya haya matatu gari lenye uwezo wa kufanya kazi ni moja. Magari mawili ni mabovu ambayo yanahitaji kufanyiwa matengenezo makubwa. Kutokana na ubovu wa magari imekuwa ni vigumu kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharura wanaotoka mbali na mazingira ya hospitali.
NYUMBA ZA WATUMISHI
Hospitali ina nyumba za watumishi 6 ambazo zinahudumia watumishi wafuatao: madaktari 5, Tabibu 4, wauguzi 6, fundi sanifu 1, na mtoa dawa za usingizi 1. lengo la kuwapa nyumba watumishi ni kutoa motisha kwa watumishi, na kuhudumia watumishi wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza.

MAFANIKIO
Kuendeleza watumishi kielimu
Hospitali inasomesha wafanyakazi 12 katika vyuo na ngazi mbali mbali kama Diploma hadi Uzamili
Ujenzi wa chuo ambacho kitatumika kama education centre na chuo cha uuguzi kwa msaada wa wafadhili (King Family Foundation chini ya Peter king)
Ujenzi wa jengo la X ray na casualty pamoja na Rest house
Kuanzishwa kituo cha CTC chini ya Clinton Foundation – CHAI (Clinton HIV/AIDS Initiatives)
Ujenzi wa kisima kwa ajili ya kuvuna maji wakati wa mvua chenye uwezo zaidi ya lita 100,000 za ujazo.
CHANGAMOTO
· Kukosekana gari ya kubebea wagonjwa kutoka vijijini na kutoka hospitalini kupeleka hospitali ya mkoa.
· Upungufu wa watumishi wa kada ya Afya wenye sifa stahili.
· Kukosekana nyumba ya kisasa ya kutunzia maiti (Mortuary)
· Kukosekana kwa baadhi ya dawa MSD imekuwa ni tatizo linalopelekea kununua dawa nje ya MSD ambako ni bei kubwa, na pia wagonjwa kununua dawa maduka ya watu binafsi mara zinapokosekana hospitalini

March 16, 2010

VIONGOZI LUDEWA WAWEKWA MSALABANI MBELE YA MAKAMU WA RAIS DK.SHEIN ..

Makamu wa Rais wa Tanzania Dr.Ali Mohamed Shein akiawhutubia wakazi wa mji wa Mafinga leo
Mamia ya wanafunzi walioziba pengo la wananchi wa mji wa Mafinga leo bila wao huenda Dr.Shein angekosa idadi kubwa ya watu


HUKU serikali ikijivuna kufanikiwa katika mpango wa usambazaji wa pembejeo kwa njia ya vocha , wakazi wa Ludewa wadai mbele ya makamu wa Rais Dr. Ali Shein kuwa udanganyifu mkubwa umefanyika katika wilaya hiyo.

Wadai vocha nyingi zimetolewa kwa matajiri, viongozi na watoto wachanga.

Wakazi hao walimweleza Dr. Shein wakati wakiuliza maswali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa juzi.

Mmoja kati ya wakazi wa wilaya hiyo hiyo Yunisi Mwagama alisema kuwa pamoja na serikali kutoa mbolea hiyo kwa ajili ya wananchi masikini ila katika wilaya hiyo udanganyifu mkubwa umefanyika na kumwomba makamu wa rais kulifanyia kazi suala hilo.

Alisema wananchi walikuwa wakisubiri mgao huo wa mbolea kwa hamu kubwa ila pamoja na kusubiri bado walishindwa kupata vocha hizo baada ya vocha zilizo nyingi kutolewa kwa watoto wachanga na matajiri.

" kweli inauma sana kuona jina la mtoto mchanga limepewa
mifuko 10 ya mbolea pamoja na matajiri na wao viongozi"

Alisema mpango huo umekwamishwa katika wilaya hiyo na usimamizi mbovu hivyo kumwomba makamu kulifanyia kazi suala hilo.


Hata hivyo madai ya wakulima hao yameonyesha kupingana na maelezo ya mbunge wa jimbo Ludewa Prof. Raphael Mwalyosi na mkuu wa wilaya hiyo Geogena Bundala ambao walimweleza makamu kuwa vocha hizo zimenufaisha wengi.


Kwa upande wake Dr.Shein aliwaagiza viongozi kusimamia vema mpango huo wa mbolea ya ruzuku ili kufanikisha azma ya serikali ya kilimo kwanza.

Alisema ni vyema viongozi kusimamia vema pembejeo ili wakulima wengi wapate kunufaika na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.


Wakati huo huo makamu wa Rais ambaye jana amefanya ziara yake wilaya ya Mufindi huku akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya mashujaa ,mkutano ambao sehemu kubwa wanafunzi walizidi kuliko wakazi wa mji wa Mafinga.

Baadhi ya wananchi waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot .com kuwa wameshindwa kufika na kuamua kuendelea na shughuli zao baada ya kuona wanafunzi wakitolewa madarasani kwa ajili ya kwenda kumpokea kiongozi huyo.


katika hatua nyingine uongozi wa Halmashauri ya Mufindi umelalamikiwa na wananchi wa mji wa Mafinga kutokana na kufanya matengenezo makubwa ya barabara ya kuelekea Ikulu na ile ya uwanja wa Mashujaa ambayo siku zote ilikuwa imetawaliwa na mashimo bila matengenezo pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuagiza iwekwe lami.
Hivyo walisema hatua ya kuwatoa wanafunzi madarasani wao wameona ni vema kuendelea na shughuli zao. Mkutano huo wa makamu wa Rais ambao sehemu kubwa ulizibwa mapengo na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ulimalizika saa 1.kasoro usiku. Kesho jumatano makamo atakuwa ziarani kilolo