

Kikosi cha Mucoba Fc kinachofanya vyema katika ligi ya Taifa ngazi ya mkoa

Katibu wa IRFA Eliud Mvella akimkabidhi mchezaji wa Mucoba zawadi ya Taswa kwa wafungaji wa magoli mawili ya Kwanza kama njia ya kuhamasisha soka mkoa wa Iringa

Kikosi cha Lipuli ambacho kinaweza kuaga ligi hiyo kutokana na kuzidi kubanwa mbavu na timu kutoka wilaya ya Mufindi ikiwemo Mucoba na Kurugenzi

Meneja wa Benki ya Mucoba na kurugenzi wa timu ya Mucoba Bw Dany Mpogole ambaye amepania timu hiyo kufanya vyema katika ligi inayoendelea

Benki ya Mucoba
BENKI ya Wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA) iliyopo katika mji wa Mafinga mkoni Iringa ni taasisi ya kifedha iliyopania kuendeleza jitihada za serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika michezo kupitia timu yake ya MUCOBA FC ambayo imeendelea kufanya vizuri katika ligi ya Taifa ngazi ya mkoa.
Zipo taasisi nyingi za kifedha ndani ya mkoa wa Iringa ila mkakati huo wa MUCOBA ni mkakati wa kipekee ambao unaendelea kuitangaza wilaya ya Mufindi kisoka pamoja na mkoa mzima kutokana na timu hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbali mbali ndani ya mkoa.
Mwalimu wa timu hiyo ya MuCoBa FC Fidelis Kalinga anasema kuwa timu hiyo imeendelea kuwa tishio katika ligi ya Taifa ngazi ya mkoa ,ligi inayoendelea katika mkoa wa Iringa ambapo kila timu ambayo imepata kukutana nayo imekuwa ikipokea kichapo hali ambayo imeifanya timu hiyo kuendelea kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya mkoa.
Anasema kuwa timu hiyo imeendelea kuitangaza vyema wilaya ya Mufindi kupitia kombe la Muungano Mufindi pamoja na mashindano mbali mbali ambayo imekuwa ikijitokeza kushiriki kwa nguvu zote .
Kalinga anasema kuwa jitihada za timu hiyo zinatokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya uongozi wa Benki hiyo pamoja na wanachama wake ambao wamekuwa na imani kubwa na maendeleo ya timu hiyo.
Timu hiyo ya MuCoBa ambayo hadi Jumapili ya wiki iliyopita ilikuwa ikiongoza katika ligi hiyo ya Taifa ngazi ya mkoa kituo cha Samora Iringa chenye timu 6 ikiwemo timu maarufu ya Lipuli FC ambayo imezidi Jumamosi iliyopita ilizidi kuvutwa shati na timu ya MuCoBa baada ya kushinda mabao mawili kwa moja. MuCoBa inaoongoza kwa kuwa na pointi 9 magoli 12 ya kufunga na magoli 2 ya kufungwa huku kwa kituo cha Amani mjini Makambako timu timu inayoongoza ni Mbeya Road ikiwa na pointi 7 magoli 5 ya kufunga na magoli 2 ya kufungwa.
Hata hivyo kwa upande wa kituo cha Samora MuCoBa imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuuwakilisha vyema mkoa wa Iringa katika ligi hiyo ya Taifa ngazi ya mkoa kutokana na mpinzani wake mkubwa Lipuli FC kuwa na pointi 3 magoli 3 ya kufunga na magoli 3 ya kufungwa, pointi ambazo bado hazilingani na MuCoBa FC ambao ndio mabingwa watarajiwa na ligi hiyo kwa mwaka huu.
Mbali ya Lipuli FC kuonekana kuendelea kutupwa mbali na MuCoBa FC katika msimamo wa ligi hiyo ya Taifa ngazi ya mkoa, timu ya Kurugenzi Mufindi inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 3 na magoli 2 ya kufunga na 1 la kufungwa .
Ilula kutoka wilaya ya Kilolo ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 3 magoli 2 ya kufunga na 2 ya kufungwa ,Mshindo ikiwa nafasi ya 5 kwa kuwa na pointi 3 goli 1 la kufunga na 2 ya kufungwa huku timu ya Kidabaga kutoka Kilolo ikishika nafasi ya mwisho katika msimamo huo.
Wakati kwa kituo cha Amani Makambako mbali ya Mbeya Road kuongoza kwa kuwa na pointi 7 magoli 5 ya kufunga na 2 ya kufungwa, timu ya Yono inashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 6 magoli 4 ya kufunga na 1 la kufungwa.
Timu ya Njombe mjini inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 4 magoli 9 ya kufunga na 1 la kufungwa, Livingstone iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 1 goli 1 la kufunga na 1 la kufungwa huku Mbangala FC ikishika nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 1 magoli 4 ya kufunga na 10 ya kufungwa na timu ya JKT Rhino ya Mafinga ikifunga dimba kwa kutokuwa na pointi, goli 1 la kufunga na magoli 4 ya kufungwa.
Pamoja na matokeo hayo kuonyesha uwezekano mkubwa wa kugeuka kutokana na timu kuwa bado na michezo ya kucheza, bado timu ya MuCoBa FC imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuibuka bingwa wa jumla katika ligi hiyo kwa mkoa wa Iringa mwaka 2010.
Timu hiyo inaundwa na jumla ya wachezaji 36 waliopo katika orodha hapo chini
1. Ally Mbwana
2. Nely Mkakilwa
3. Stanley Msangira
4. Stany Kadege
5. Joshua Chatila
6. Rashid Tangai
7. Maka B. Basil
8. August Mshana
9. Nikodem Ben Mfugale
10. Jacob J. Joseph
11. Shaibu Rashid
12. Said Shaban
13. Samwel Juma Mgaya
14. Yohana Kacheche
15. Joshua B. Jimmy
16. Martin Charles
17. Issa H. Nganila
18. Poimen Nelson Macheche
19. Khatib M. Mshana
20. Stany Mussa
21. Hashimu Mbata
22. Rodrick Kibonge
23. Mansuri Abdul Mwango
24. Alex Chura
25. Kenneth John Mkwele
26. Gift Mussa Mwinuka
27. Ibrahim Peter
28. Fukuto Juma
29. Alex Joseph
30. Issa Juma
Alipoulizwa kuhusu sababu ya mafanikio ya timu, Meneja mkuu wa MuCoBa, Danny Mpogole alisema matokeo hayo ni kwa sababu ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya wachezaji, walimu wao, viongozi wa timu na wa benki pamoja na wadau wengine wa michezo. Aliwaasa wananchi wa wilaya ya Mufindi na maeneo mengine mkoani Iringa kuendelea kutumia huduma za benki katika kujiwekea akiba, kupata mikopo, kutuma fedha na kupata huduma za bima ili kuimarisha benki na kuboresha maisha yao .
Timu ya Mucoba kwa sasa imebakiza michezo takribani miwili mbele ambapo michezo yote kwake si migumu ukilinganisha na timu ya Lipuli Fc ambayo imeonyesha kukata tamaa.
Soma habari hii katika gazeti la Mwanasoka Alhamisi wiki ijayo