Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2010

'LIVE' MKESHA WA MWAKA MPYA UWANJA WA SAMORA

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Dk Mdegella akiendesha maombi maalum jukwaani sasa
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Evarista kalalu akitosa salamu za ufunguzi wa Mkesha ulioandaliwa na umoja wa makanisa Tanzania

Wananchi wakiwa katika mkesha uwanja wa samora usiku huu


Mambo yanaendelea ndani ya uwanja wa samoraKumbuka mtandao huu na redio Overcomers Fm 98.6 tupo Live katika mkesha huu

MEYA MWAMWINDI ASEMA MJI UTAENDELEA KUBORESHWAMSTAHIKI meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi amesema kuwa Halmashauri hiyo imeandaa mpango makakati wa kuhakikisha kuwa mji unaendelea kuwa katika hali ya usafi na wananchi wa mji huo wanaboresha nyumba zao .


Mwamwindi ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya kumpongeza iliyoandaliwa na wazee wakazi wa kata ya Mlandege mjini hapa ,sherehe zilizofanyka katika ukumbi wa CCM kata ya Mlandege.


Alisema kuwa jimbo la Iringa mjini pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) kulipoteza jimbo hilo ila bado CCM yenyewe ndiyo iliyohusika katika kulipoteza jimbo hilo kwa kukata jina la aliyepitishwa katika kura za maoni Frederick Mwakalebela.


"Ukweli hali ya siasa katika mji wa Iringa ilionekana kuchafuka zaidi baada ya kurejeshwa kwa jina la Monica Mbega na kuwa iwapo baada ya kurudi jina la Mbega kama uchaguzi ungefanyika ndani ya siku mbili uwezo wa CCM kupata kura 2000 ungekuwa mdogo......ukweli tumepata wakati mgumu sana na kundi la vijana limetusumbua sana katika uchaguzi huu"alisema

Wao kama CCM wanaamini kabisa kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kupitia mbunge wake mchungaji Peter Msigwa ameazimwa jimbo la Iringa mjini kwa kipindi cha miaka mitano na CCM .

Hivyo alisema kuwa yeye kama mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa ataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote za baraza la madiwani bila ubaguzi na madiwani wote wakiwemo wa CCM na Chadema wanaounda baraza hilo wanapaswa kuhesheshimu kanuni hizo.

Akielezea kuhusu sheria ya wakazi wa mji wa Iringa kujenga maghorofa Mwamwindi alisema kuwa sheria hiyo imeendelea kuboreshwa zaidi ili kuhakikisha kila mmoja anaishi katika nyumba bora na ya kisasa.

Wakati huo huo Mwamwindi amewataka wakazi wa mji wa Iringa kutunza sehemu ya akiba yao ya chakula kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya mvua katika mwaka huu na kuwa upo uwezekano wa mwakani kuwepo kwa hali mbaya ya chakula kutokana na mvua.
MWISHO

'LIVE' SHEREHE YA WAZEE KATA YA MLANDEGE KUMPONGEZA MEYA IRINGA

Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akiwashukuru wazee wakazi wa kata ya Mlandege kwa kumpongeza
Meya Mwamwindi akipokea zawadi toka kwa wazee

Meya Mwamwindi akiwa na wazee


Heshima za kihehe
Wazee wa kabila la kihehe
Pongezi mbali mbali
Wazee wa kihehe wakiwa katika mavazi rasmi
Mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Mhe.Aman Mwamwindi akiwa ukumbi wa sherehe hivi sasa ukumbi wa CCM Mlandege
Wananchi wa Mlandege wakiwa katika sherehe ya kumpongeza diwani wao ambaye ni meya wa manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi

Wazee wakitoa burudani ya kiduo

Madiwani wa kata za jirani waliofika katika sherehe hizi
Video chini
BREAKINGNES .KABURI LA KIYEYEU IRINGA LAHAMISHWA RASMI

Fuvu la kichwa la marehemu Martine Kiyeyeu mkazi wa kijiji cha Mlolo kata ya Mseke wilaya ya Iringa vijijini likitolewa kaburini


Mabaki ya mwili wa Kiyeyeu yakiwekwa katika jeneza tayari kwa kwenda kuzikwa upya baada ya eneo la awali kuchimbwa kaburi lake ili kupisha upanuzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya
Jumla ya makaburi nane ndio ambayo yameondolewa katika eneo hilo na hakuna tukio lolote la ajabu lililopata kujitokeza pamoja na kuwepo kwa maneno mengi toka eneo hilo ,habari kamili utaipata

December 29, 2010

BREAKINGNES . KESI YA CHENGE YAFIKIO UKINGONI

Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania ikiwamo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, leo alipona kutupwa jela miaka mitatu baada ya kulipa faini ya sh 700,000 katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.
Rusema alisema kutokana na ushahidi wa watu sita uliotolewa,mahakamani imemhuona na hatia ya makosa manne ambapo alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh 700,000.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake waWili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Habari hii na mdau Issa Michuzi

December 28, 2010

MAUWAJI MENGINE TENA IRINGA

IGP MWEMA
MAUWAJI ya kinyama yazidi kuendelea kuwa tishio kwa wakazi wa mkoa wa Iringa baada ya watu wengine wawili wanaosadikika kuwa ni wanandoa wakazi wa kijiji cha Kiwa wilaya ya Ludewa kukutwa ndani ya nyumba yao wakiwa wameuwawa kinyama kwa kuchinjwa .

Haya ni mauwaji ya pili ya kinyama kutokea mkoani Iringa ambapo mauwaji mengine kama haya yalitokea siku mbili kabla ya sikukuu ya Krismasi baada ya watu wasiofahamika kumchinja kama kuku aliyekuwa mfanyabiashara wa Samaki wabichi katika eneo la Uhindini mjini Iringa Bukuri Mvula,huku na siku ya mkesha wa Krismasi kijana mfanyabiashara Nico Chalale alikutwa akiwa ameuwawa kwa kunyongwa shingo yake.


Pamoja na watu hao kukutwa wakiwa wameuwawa kinyama pia mtoto Justine Sanga (1miezi 6) mkazi wa Kitisi Makambako wilaya ya Njombe amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi na wazizi wake kuteketea kwa moto uliosababishwa na kibatari ambacho kiliwashwa na wazazi wake kabla ya kwenda kumalizia sikukuu ya krsmasi .


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha jana kutokea kwa matukio hayo mbele ya waandishi wa habari na kuwa tukio la kuuwawa kwa wanandoa hao lilitokea Desemba 26 ambapo miili za wanandoa hao Laurent Wiliam (60) na Alphoncia Msanga (55) alipokutwa ndani ya nyumba yao ikiwa imekatwa katwa mapanga .

Alisema kuwa hadi sasa bado waliotenda unyama huo hawajafahamika na jeshi la polisi linaendelea na msako mkali dhidi yao.
MWISHO

MAMA WA KAMBO AMFUKUZA MTOTO WA MIAKA 9 NYUMBANI

Mtoto John Mwangobola (9) mkazi wa Ipogolo mjini Iringa ambaye ni mtoto wa kambo akiwa amefukuzwa na mama yake Farida Mkwawa mwenyeji wa Ipogolo mjini hapa kwa madai kuwa amekuwa na anatakiwa kuanza maisha ya kujitegemea,hapa akiwa stendi kuu ya mabasi akijindaa kujiunga na kundi la watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Hapa msamalia mwema Kasimu Makata (katikati) akimwonyesha mtoto huyo kwa rafiki yake wa karibu Bw Peter,mara baada ya Redio Overcomers FM 98.6 Mhz na mtandao huu kumtembelea mtoto huyo aliyemsaidia

December 27, 2010

MAUWAJI HAYA YATISHIA USALAMA IRINGA MJINI....

Askari kanzu wakikata kamba ili kushusha mwili wa kijana Nico Chalela aliyokutwa amejinyonga kiaina huku akiwa amepiga magoti jambo ambalo halijapata kutokea kwa mtu kujinyonga kama hivi
Wananchi wakishuhudia maiti ya kijana huyo ikitolewa na polisi

Hapa askari polisi wakiwa wameishusha maiti hiyo kutoka katika kamba

Hapa ikiingizwa katika gari ya polisi

Hivi ndivyo alivyokutwa

MAUWAJI ya kinyama yazidi kutishia maisha ya wakazi wa manispaa ya Iringa baada mfanyakazi mmoja wa kituo cha kuziba pacha za magari katika eneo la Mshindo mjini hapa Nico Chalale (28) kukutwa amekufa kifo cha mashaka kwa kunyongwa shingo usiku wa kuamkia sikukuu ya Krismasi ikiwa ni siku moja baada ya kuchinjwa mfanyabiashara wa samaki Bukuri Mvula na watu wasiofahamika jirani kabisa na eneo hilo.

Kijana huyo alikutwa akiwa amefungwa kamba shingoni huku akiwa amepiga magoti hali inayozua maswali zaidi kwa wakazi wa mjini Iringa na kuingia na hofu zaidi ya kuwepo kwa mtandao wa watu wanaojihusisha na mauwaji hayo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakazi wa eneo la Mshindo walisema kuwa kifo cha fundi huyo ambaye wili wake ulikutwa eneo la kazini kwake unawafanya kuingiwa na hofu zaidi na kuliomba jeshi la polisi mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya mauwaji hayo.

Wananchi hao walisema kuwa inasikitisha na kutishia uhai wao kuona watu wakiendelea kunyongwa na kuuwawa kinyama katikati kabisa na mji huo wa Iringa .

Kwani walisema kifo cha Chalale ni tukio la tatu kutokea ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo tukio la kwanza lilikuwa la aliyekuwa kamanda wa kampuni ya ulinzi binafsi ya Force Group marehemu Charlesy Tulo ambaye alikutwa amejinyonga katika mti mfupi unaokisiwa kuwa na futi kama tatu wakati yeye ana urefu wa fupi 5 .

Hata hivyo walisema mauwaji hao hayakuishi hapo kwani siku moja kabla ya Krismasi mfanyabiashara huyo wa samaki Mvulla alikutwa akiwa amechinjwa shingo kama kuku na mwili wake kutelekezwa ndani ya daladala mbovu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .

MWISHO

December 26, 2010

'LIVE' MBUNGE RITTA KABATI AKIHOTUBIA BAADA YA KUWAPA CHAKULA NA MISAADA MBALI MBALI YATIMA WA DBL

Mheshimiwa Ritta Kabati akitoa ahadi zake achangia vifaa lukuki kituo

Viongozi wa CCM mkoa na wilayaVenance Mamoto aliyekuwa mbunge wa Kilolo akiwa na mamake mzazi katikati na mkeweMwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Zainabu Mwamwindi

Ofisa habari mkoa wa Iringa Denis Gondwe akiwa na waalikwa wengine

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Ritta Kabati (wa pili) kushoto) akiwa na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi Meya wa manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi na diwani wa kata ya Mtwivila Victor Mushi

MBUNGE RITTA MOTO KABATI LEO KUSAIDIA YATIMA WA KITUO CHA DAILY BREAD LIFE MKIMBIZI .......MH.Ritta Moto Kabati.
MBUNGE wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Mhe .Ritta Moto Kabati (pichani ) ni mmoja kati ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ameamua kuanza ubunge wake kwa aina ya tofauti ya wabunge wengine kwa kuanza na kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na kumunga mkono mkarandasi maarufu mkoani Iringa Geofrey Mungai ambaye pia ameonyesha mfano mwema kwa jamii ya kitanzania katika kuwakumbuka yatima .

Mbunge huyo leo ameandaa hafla maalum kwa ajili ya kusaidia watoto yatima hao hafla itakayofanyika majira ya saa 7 mchana na kurushwa moja kwa moja na mtandao huu na kituo cha Redio Overcomers FM 98.6 ,sherehe hiyo itafanyika katika eneo la Mkimbizi kilipo kituo hicho wote mnakaribishwa kushiriki kuchangia yatima


Wapo wabunge wengi na wapo makandarasi wengi na matajiri wengi wenye uwezo wa mkubwa ila tujiulize ni wabunge wangapi ama makandarasi wangapi katika jamii yetu ambao wamepata kufirikiria ama kuelekeza nguvu zao kwa yatima?kama wapo basi nitumie nafasi hii kuwapongeza na kama hawapo bado nitumie nafasi hii kuwaomba kuiga mfano huu mwema.

Kama ilivyovumishwa na kuaminika kuwa mkoa wa Iringa ndio unaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuwa na asilimia ya zaidi ya 14 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ndivyo kasi hii inavyozidi kuchangia kuwepo kwa idadi kubwa ya yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu .

Japo zipo taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) nyingi ambazo tumekuwa tukizisikia kuwa zinafanya kazi ya kutunza watoto hao ila bado kwa upande wangu mimi sijaona kazi ya NGOs hizo ama vituo vya kulea yatima ndani ya mkoa wa Iringa dhidi ya walengwa na kama vipo basi ni vichache kama Daily Bread Life Childreans Home cha Mkimbizi Iringa na Nzihi wilaya ya Iringa vijijini, Huruma Center kilicho chini ya kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa , Migori Mtera nacho kilicho chini ya kanisa la Romani na kile Ilula wilaya ya Kilolo na kama vingine vipo basi vimekuwa vikifanya kazi zake maofisini .

Hivyo wakati tukiangalia jinsi ya yatima hao kuendelea kufikiwa na mahitaji yao kupitia vituo hivyo bado mkoa unatakiwa kuanza kufanya tathimini upya ya utendaji kazi wa vituo hivyo na NGOs za yatima katika mkoa wa Iringa ili kuona kuwa vituo vyote vinafanya kazi kama vituo hivyo tajwa na NGOs zote zinafanya kazi kama ilivyo ile ya TAHEA iliyopo chini ya mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Lediana Mafulu Mng’ong’o katika kuwatumikia walengwa na si vinginevyo.

Wapo baadhi ya wabunge ambao katika kipindi kilichopita walipata kujitolea kusaidia yatima kwa kiasi chake na hata jamii kubaki ikiwakumbuka kwa hilo miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Monica Ngezi Mbega ambaye aliweza kufanya vizuri katika jimbo lake la mkoa wa Iringa ,ila wapo wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani ambao pia walipata kuahidi kusaidia yatima ama kuanza kwa kusaidia yatima katika maeneo yao.


Kama ahadi hizo zilikuwepo basi ni vizuri kuanzwa kutekelezwa na kama hazikuwepo basi kuwekwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwani mipango yoyote lazima ingeanzia katika afya za wananchi na waathirika wakuu wa ugonjwa wa UKIMWI ambao ni yatima.

Mhe.Ritta Moto Kabati ambaye ameingia katika nafasi hiyo ya ubunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) kwa mara ya kwanza yeye ameamua kuanza na yatima kwa kuahidi kuandaa chakula cha hisani kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika jimbo la Iringa mjini.

Mhe.Kabati amesema kuwa hafla hiyo imepangwa kufanyika siku ya sikukuu ya Krismas kwa kuwakutanisha watoto wa kituo cha kulea yatima cha Daily Bread Life Childreans Home cha Mkimbizi Iringa na Nzihi wilaya ya Iringa vijijini.

Kwani amesema kuwa amelazimika kuanza kwa kuwasaidia watoto hao kama sehemu yake ya utendaji wa kazi pamoja na kuonyesha mfano kwa vitendo kwa jamii inayowazunguka watoto hao kuwa watoto hao wanahitaji msaada zaidi kutoka kwa jamii nzima ya mkoa wa Iringa .

Pamoja na kuanza kuwasaidia watoto hao pia ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa na wale wanaoishi nje ya mkoa wa Iringa na wasamari wema kujitokeza kwa wingi siku ya Hafla hiyo kwa ajili ya kusaidia misaada yao kwa watoto hao.

Mbali ya kuanza ubunge wake kwa kusaidia jamii hiyo ya watoto yatima ambao wengi wao wamepoteza wazazi wao kwa magonjwa mbali mbali ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI bado aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

Alisema kuwa bado mkoa wa Iringa unakabiliwa na changamoto kubwa ya ugonjwa wa UKIMWI na kuwa ili kupambana na changamoto hiyo jamii haina budi kuelekeza nguvu zaidi katika mapambano dhidi ya UKIMWI pamoja na kuendelea kukemea vitendo vya unyanyapaa kwa wale walioathirika na Virusi vya UKIMWI na watoto yatima.

Mhe.Kabati pia ameahidi kuanzisha kampuni ya usafi katika mji wa Iringa ili kusaidia kutoa ajira kwa vijana wasio na ajira kama njia ya kuwaepusha na vishawishi vya kujiingiza katika makundi ya kiuharifu.

Hata hivyo alisema katika uongozi wake anaamini kabisa maendeleo bila kuangalia yatima na watu wenye shida ni sawa na hakuna hivyo lazima atahakikisha katika jimbo la Iringa mjini na mkoa wa Iringa kwa ujumla unakuwa mfano mzuri katika kuwakumbuka yatima na waathirika wa UKIMWI .


Wakati mbunge huyu akiahidi kuandaa mpango huo wa kusaidia yatima tayari mkandarasi maarufu mkoani Iringa Bw.Geofrey Mungai yeye amejitolea kiasi cha shilingi milioni 1.5 pamoja na sare za watoto wote wa kituo cha Daily Bread Life Childreans Home cha Mkimbizi Iringa na Nzihi wilaya ya Iringa vijijini kama sehemu ya sadaka yake mbele za Mungu dhidi ya yatima hao.

Mkuu wa Makazi na Mratibu wa kituo hicho cha DBL Mchungaji Mpeli Mwaisumbe mbali ya kumpongeza mbunge huyo Mhe.Ritta Moto Kabati kwa kuonyesha upendo wake kwa watoto hao yatima bado anaeleza matatizo mbali mbali yanayokikabili kituo hicho . MATATIZO:-
Kituo chetu kinayo matatizo yafuatayo:-
Michango mashuleni ni mingi na mzigo kwetu pamoja na ushirikiano mdogo sana kwa baadhi ya shule na sio zote, Kutopata michango ya wanachama na wanachi kwa wakati na hivyo kuwa na wakati mgumu kununua mahitaji muhimu na kulipa Ankara mbalimbali, Hakuna ruzuku kutoka Serikalini, Tuna upungufu wa magodoro, yaliyopo yamechakaa 20 zaidi,. Uniform – Mtu amejitolea,. Masweta wakati wa baridi.
Chumba cha maktaba, kinachotumika sasa ni kwa ajili ya Nursery School.
Kujenga Shule ya Sekondari.
Chumba cha Computer na Computers
Mtaji wa shamba na mifugo.

Kituo hicho ambacho kinafanya kazi chini ya shirika la Daily Bread Life Tanzania lenye usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali Namba 12903, chini ya Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi. Huduma hii ya kutunza watoto waliokuwa wanaishi katika mazingira hatarishi na yatima ya DBLCH pia imesajiliwa na Ustawi wa Jamii na kupewa hati ya usajili wa makazi ya watoto Namba 000049995. Shughuli za kila siku za kituo zinasimamiwa na Mchungaji Mpeli Mwaisumbe na mke wake Mchungaji Neema Mwaisumbe.(Waanzilishi na wenye maono hayo) kilianza kujengwa mwaka 2002 na kukamilika mwaka 2004. Kituo hiki kilijengwa kwa msaada wa Mungu chini ya Wachungaji hawa na marariki mbalimbali nje na ndani ya nchi hasa wachungaji wa Marekani.
Tarehe 16/4/2004 kituo kilianza kupokea watoto kumi na wanne(14). Utaratibu unaotumika ni kuwa:- Kituo hiki hupokea watoto kutoka Ustawi wa Jamii kwa utaratibu wa sheria na maamuzi makini kati ya kituo na Ustawi wa Jamii Mkoa kuamua nani anastahili kuwa katika kituo baada ya uchunguzi makini na mahiri watoto hawa wakiwa hapa hupatiwa huduma ya makazi, malazi, chakula, matibabu, huduma ya ushauri, elimu na nyinginezo kwa kadri ya uwezo unaopatikana.


Pia anasema kuwa jumla ya watoto waliopokelewa na kulelewa na kituo hiki sasa ni 51, waliopo sasa ni 34. Kati ya hao wamepata walezi, 7 wapo Sekondari, 1 chuo. Waliopo jinsia ya kiume 16 na jinsia ya kike ni 20, watoto hawa wote kasoro wawili wachanga wanasoma katika Shule za Msingi nne za jirani ambazo ni 1. Ukombozi Shule ya Msingi, 2. Mkimbizi, 3. Mshikama, 4. Star International.

Wakati mafanikio yaliyofikiwa ni pamoja na Jamii kuelimishwa na kuwepo kwa mwitikio wa kujitoa kutusaidia kwa
misaada mbalimbali.

“Tumepata shamba huko kijiji cha Mgera kwa ajili ya kilimo na kujitegemea,Tunalo Bus – Coaster kwa mradi wa kituo,Mradi wa Cherehani pia tumepewa kuendesha kituo cha Inzi chenye watoto “

unamaoni wataka kuwasiliana na mbunge Ritta Moto Kabati ili kusaidia kuchangia yatima Iringa piga simu 0754281188 ama ukiwa ni mbunge ama mtu yeyote wataka kusaidia yatima na unataka kuandikwa hapa piga simu 0754 026299

December 25, 2010

ASKOFU BOAZI SOLLO ASEMA KATIBA MPYA NI UKOMBOZI KWA TAIFA


ASKOFU wa kanisa la Endtime Harvest na mkuu wa kituo cha maombi cha Overcomers Power Sentre mkoani Iringa Boazi Sollo asema kuwa katiba mpya ni ukombozi wa kweli wa mtanzania na kuwataka watanzania kuendelea kudai katiba mpya bila kumwaga damu wala kuingizwa katika machafuko .

Akitoa salamu za Krisamsi leo katika ukumbi wa Sekondari ya Mwembetogwa mjini Iringa mara baada ya kumalizika kwa ibada ya maalumu ya Krismasi ,askofu Sollo alisema kuwa pamoja na watanzania kuendelea kusubiri kwa hamu kubwa mchakato wa katiba mpya bado kuna haja ya kuendelea kuliombea baraza jipya la mawaziri ili kuhakikisha kuwa mawaziri hao wanafanya kazi kwa uaminifu pasipo kujiingiza katika vitendo vya rushwa vinavyoweza kupelekea baraza hilo la mawaziri kukosa imani kwa wananchi na hivyo kuvunjwa.

“Asema viongozi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu na kuepuka kuongoza Taifa kwa mapenzi yao na badala yake wanapaswa kutazama matakwa ya wananchi na kuepuka kula rushwa katika utendaji wao wa kila siku “

Alisema kuwa kila mtanzania anwao wajibu wa kuliombea Taifa pamoja na viongozi wote waliopewa mamlaka za kuwaongoza watanzania hasa baraza la mawaziri lililoundwa na Rais Jakaya Kikwete na Rais wenyewe.

“Ndugu zangu tuna wajibu wa kuendelea kuliombea Taifa letu pamoja na viongozi wake ili waweze kuwajibika kwa kutanguliza hofu ya Mungu badala ya kuendelea kufanya kazi kwa matakwa yao …..sisi kama kanisa pia tuna kituo chetu cha Redio Overcomers Fm (98.6 Mhz) ambapo moja kati ya kazi kubwa ambazo tumekuwa tukizifanya kila siku asubuhi ni kumwombea Rais pamoja na baraza la mawaziri ili kuepuka kuwajibika vibaya katika nafasi zao”

Alisema askofu Sollo kuwa katika mkoa wa Iringa vitendo vya mauwaji ya kinyama vimeendelea kujitokeza pamoja na ugonjwa wa UKWIMI ambao umekuwa ukichafua sifa nzuri ya wakazi wa mkoa wa Iringa.

Hivyo amewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuwa na hofu ya Mungu pamoja na kutamani maisha ikiwa ni pamoja na kuepuka vitendo vinavyoweza kuchangia vifo vinavyotokana na ugonjwa wa UKIMWI.


NIPO 'LIVE' IBADA YA KRISMASI KITUO CHA MAOMBEZI CHA OVERCOMERS POWER CENTRE MWEMBETOGWA SEKONDARI SASA NI MAOMBI

Maombi yakiendelea katika ibada ya krismasi ukumbi wa Mwembegwa mjini Iringa

Askofu Boazi Sollo akiombea wagonjwa

Mtoto ambaye jina lake halijapatikana mara moja akimwombea mama yake
Leah Mnyambwa meneja wa kituo cha Overcomers Fm